Yesu wa Kenya anaenda kusulubishwa, manabii na mitume wa mchongo wakae kwa tahadhari

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,499
Amani iwe nanyi,

Kazi ya Mungu siku zote ina upinzani mkali. Tumeona Yesu OG, mitume na manabii walivyo uwawa, teswa na kudhihakiwa. Soma maandiko kwa urahisi wa rejea.

Huko jirani, wadau wanataka kumjambisha yule yesu wa mchongo, wanataka kumsulubisha kwa kadiri ya maandiko wakitarajia ufufuko wake siku ya tatu, je sisi tunasubiri nini? Hawa mitume na manabii wa mchongo inabidi wachezee vichapo.

Maandiko yako wazi, hakuna utukufu unaokuja bila mateso.Manabii na mitume walichezea vichapo wakapata utukufu huko kwa baba

Ieleweke, njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba, manabii na mitume chukueni tahadhari.
 
Manabii gani wanakula kuku, wana mashavu yamenona, wana magari ya kifahari. Wanaishi kwenye makasri na ukwasi mwingi kuliko wafuasi wao?

Ukiwauliza maswali wanakujibu mbona ibrahim na suleimani walikuwa matajiri, hawa manabii na mitume wa mchongo wamekuwa wengi mpaka wengine wana vikosi vya ulinzi na usalama kama wa rais.

Eti mtu yuko madhabahuni kajiwekea mabodigadi kumzunguka pande zote, wengine wamevaa sare kama migambo.

Ni vituko vingi mpaka misafara ya magari wanaiga kama wa rais, kuna mijitu imevaa miwani nyeusi na suti huku imenyoa vipara.

Hawa manabii na mitume uchwara wangekuwa hata wanajenga hospitali, shule, maji na barabara wangeonekana wa maana japo wakijenga huduma kama za elimu na afya ni zao binafsi ili kujipatia kipato.

Kwa hiyo nao wakae tayari kusulubishwa kama mwenzao wa kenya
 
Yesu gani huyo anayekimbilia polisi kuomba msaada asisulubiwe? Eti yesu wa bungoma kenya ana mke, huyo ni mkenya tu wa kawaida kama yule mtanzania anayejiita mungu na wafuasi wake wakijiita makerubi.

Kumekuwa na vituko vingi sana kwenye mambo ya imani, huu ni upotoshaji wa imani halisi ya Mungu, ingekuwa ni kwa ile dini nyingine inachezewa hivi bakora zingetembezwa na fatwaa juu yake, wale hawana mizaha na dini yao inaogopwa
 
Yesu wao mwoga sana...hataki kurudi kwa Baba..
MK254
IMG-20230402-WA0002.jpg
 
Manabii gani wanakula kuku, wana mashavu yamenona, wana magari ya kifahari. Wanaishi kwenye makasri na ukwasi mwingi kuliko wafuasi wao? Ukiwauliza maswali wanakujibu mbona ibrahim na suleimani walikuwa matajiri....
Wanapaswa kusulubishwa
 
Yesu gani huyo anayekimbilia polisi kuomba msaada asisulubiwe? Eti yesu wa bungoma kenya ana mke, huyo ni mkenya tu wa kawaida kama yule mtanzania anayejiita mungu na wafuasi wake wakijiita makerubi...
Ngoja wakimpeleka kwa baba baada ya siku tatu tutajua mbivu na mbichi
 
Cha ajabu watu wanawaamini sana wapuuzi hawa. Kuna mmoja hapa wa siloam anajiita majina marefu mpaka na waumini wake wana majina marefu yenye kujipa sifa za kiungu ambazo hawana. Amejirundikia wapuuzi wengi wenye akili mbovu zilizoharibiwa, wakiambiwa wajiteteketeze wako tayari kufanya hivyo. Hawa mitume na manabii feki wakikabiliwa kukutana na changamoto za kuthitisha utume na unabii wao wasikimbilie polisi kuomba msaada
 
Cha ajabu watu wanawaamini sana wapuuzi hawa. Kuna mmoja hapa wa siloam anajiita majina marefu mpaka na waumini wake wana majina marefu yenye kujipa sifa za kiungu ambazo hawana. Amejirundikia wapuuzi wengi wenye akili mbovu zilizoharibiwa, wakiambiwa wajiteteketeze wako tayari kufanya hivyo. Hawa mitume na manabii feki wakikabiliwa kukutana na changamoto za kuthitisha utume na unabii wao wasikimbilie polisi kuomba msaada
Wanatakiwa wapitishwe kwenye tanuru la moto, wafunguliwe Simba, wapigwe mawe kama Daniel, hakunaga free ride ya kwenda mbinguni
 
Back
Top Bottom