Ishara 10 za manabii na mitume feki waliotapakaa Tanzania

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
13,992
20,283
1. Wapo tayari kuungana katika kutetea kazi za usanii wanaoufanya ndani ya majengo ya makanisa. Lakini hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kutawalika kwa mwingine! Kila mmoja anataka amtawale mwenzake.

2. Huwa wanafanya kazi zao kwa muundoo wa ku-copy & paste. Mfano wakiona kuna Nabii mwenzao ametoa Mapepo kwa kupuliza Upepo Mic na wengine watafanya hayo hayo!

3. Hawafanyi kazi ya Unabii bila Pesa Mkononi. Mhitaji akienda Awe na Pesa ya kumuona Nabii, Awe na Pesa ya kwenda Kusafishiwa Nyota, Pesa ya kutabiria! Unabii wao ni kwa ajili Maisha ya watu tu. Hawana Unabii kwa Taifa wala Ulimwengu kwa ujumla.

4. Ni waoga wa kufa kuliko raia (watu) wanaowahudumia. Imefikia wakati hata Ulinzi wa Nguvu za Mungu hawauamini! Wamekuwa na Walinzi wa Kimwili zaidi. Huwa wana VITISHO sana kwa watu wanaowakosoa kiutendani! Wapo tayari Kushambulia kwa maneno au kushambulia kwa Vitendo, Kupiga mtu, Kutishia watu maisha na hata kutoa kauli za kumuua mtu!

5. Wananena kwa Lugha kwa staili ya maneno yale yale ya KUKARIRI yasiyozidi Kumi (10), yaani Lugha yetu wanayonena haipanuki kimaneno, maneno ni yale yale yaliyopo Dsm, Mwanza, Dodona na Morogoro, hayazidi zaid ya hapo! Na hawajui maana ya yale maneno wanayotamka!

6. Wanaongoza KUSENGENYANA wao kwa wao, lakini wakikutana pamoja ni kama wana Umoja wa Kazi ya Mungu na kumbe ndani yao ipo shida kubwa! Wanapenda Sifa sana, Kusifiwa, Kunyenyekewa na Kuabudiwa kuliko hata Mungu mwenyeqe. Hupenda kila wanalolifanya waonekane na watu! Hata akimsaidia mtu msaada wa nauli ya daladala ya Tshs 1,000/= wanataka Wamchukue picha (Selfee). Wakienda huko Maporini (Mlimani) kwa ajili ya kile wanachokiita Maombi ya Mlimani ndiyo usiseme! Hakuna maombi huko ni Vurudu za picha na Clip za shot Video. Hakuna Mungu huko zaidi ya maingizo ya maombi!

7. Wanapenda kunyang'anyana Waumini ndani ya majengo ya Ibada na hasa pale wanapoalikana Kihuduma. Wanapotoka hapo walipoalikwa kuhudumu huchukua namba za simu za Waumini wa eneo husika ili kuwahamisha na hasa wale wenye kuonekana wana Kipato kifedha! Hupenda sifa zaidi hata Waandishi na Mafarisayo kuwawafikii Mitume na Manabii wa zama hizi kwa sifa. Hupenda mashindano ya kuvaa Masuti ya gharama, Hushindana kula vyakula ya bei mbaya na bila kujua hapo mtaani kwake anapohudumu kuna watu ni Maskini wa kutubwa na wanalala na njaa. Hupenda zaidi kujionyesha kwa watu na hasa pale wanaponunua Magari ya kutembelea.

8. Wengi wao wana vinywa Vilivyojaa matusi na maneno Makali ambayo huwezi kumdhania. Wapo tayari kurusha picha za NGONO au mtu anayekata mauno! Halafu utamsikia mrushaji akisema "JAMANI ANGALIENI HAPA NDIPO DUNIA ILIPOFIKIA" na kumbe yeye ndiye anayependa mambo hayo na yamejaa kwa simu yake! Ukiwa nao na kuwaangalia ni Dakika 10 wanaweza kujifanya wapo Kiroho, lakini dakika chache wanakuwa watu wa Kimwili. Na wapo tayari kwenda kwa WAGANGA WA KIENYEJI ili kukuza Kundi la Watu.

9. Mahubiri yao Mitume na Manabii yameegemea zaidi kwenye AGANO LA KALE na hasa Vitabu vya MALAKI (Fungu la Kumi), ZABURI (Misingi ikiharibika), Urejesho wa nyota, Mafanikio wakimnukuu Ibrahimu Baba wa Imani. Bila kujua kwamba Ibrahimu yeye alishakuwa na mali nyingi kwa sababu ya Juhudi zake. Bali Mungu alichokifanya pale ni kumuongezea tu. Zaidi ya hapo hakuna mahubiri zaidi! Labda hapo yatafuata mahubiri ya Kichwani ya Kufoka (Kukoroma) pasipo na maandiko!

10. Wengi wao hawajui nini maana ya Utume Ki-Biblia wala hawajui maana ya Unabii Ki-Biblia. Hata ukimuuliza juu ya Yesu anaweza hata kukujibu kwamba Yesu siyo Mungu! Ndiyo maana kwa hapa Tanzania Mitume wengi na Manabii ndiyo wamekuwa ni Wachungaji wa Kanisa.
 
Manabii na mitume wamegeuzwa maadui kuliko wachawi na waganga waliotapakaa kila mtaa. Wanashambuliwa kuliko majambazi na vibaka . Wanachukiwa kuliko wauaji wa maalbino, kisa ni nini?

Udhaifu wa mwanadamu usiwe sababu ya kuipinga kazi ya Mungu. Mitume na manabii sio malaika bali wanadamu. Wewe unawahukumu kama nani ? Mwenye kazi ni Mungu na siku ya hukumu atafanya tathimini na kutoa hukumu ipasavyo!
 
Umesahau moja. Hawahubiri juu ya habari ya kuokoka na kumjua Mungu.

Wanasema tu juu ya mambo ya utajiri, kupandishwa cheo, kupata mume, kusafisha nyota, kuimarisha biashara.
 
Manabii na mitume wamegeuzwa maadui kuliko wachawi na waganga waliotapakaa kila mtaa. Wanashambuliwa kuliko majambazi na vibaka . Wanachukiwa kuliko wauaji wa maalbino, kisa ni nini? Udhaifu wa mwanadamu usiwe sababu ya kuipinga kazi ya Mungu. Mitume na manabii sio malaika bali wanadamu. Wewe unawahukumu kama nani ? Mwenye kazi ni Mungu na siku ya hukumu atafanya tathimini na kutoa hukumu ipasavyo!
Usihalalishe kisicho haki et kwaasabab vingne vinafanywa mkuu....ukiwa logicaly correct na kichwan zimo zile za kwel si za kukariri huwez sikiliza wanachohubiri na kuongea hao jamaa hata kwa dk 10..utaboreka na kuondoka..

Mi gf wangu alikua anasali huko kwa prof nan sjui makongo juu..ni sect ya major 1..yule bushiri.huko ni wanasal matajir tu..

Nilienda nikakaa dk 30 kwa tabu sana kumskiliza jamaa yule..na sikurud teeena

Mahubir yao yako cheap sana kwa intelligent mind.
 
Usihalalishe kisicho haki et kwaasabab vingne vinafanywa mkuu....ukiwa logicaly correct na kichwan zimo zile za kwel si za kukariri huwez sikiliza wanachohubiri na kuongea hao jamaa hata kwa dk 10..utaboreka na kuondoka...
Ni sawa... Tumepewa akili tupime hizo nabii... Lakini kuhukumu sio kazi yetu. Ukiona mafundisho yake hayakufai kaa pembeni. Kuna mwingine kwa mafundisho hayo dhaifu atapata hapo neno litakalomgeuza na kumnusuru na jehenamu !!!
 
Hivi Ulaya hamna manabii? Mbona hatuwasikii, maana huku kwetu wamekuwa wengi mno, kila mkoa sasa hivi kuna Nabii au Mtume.
Kidhungu mnakijua? Ukiweka mhubili hapo watu si watajua anaimba kinageria ?
 
Kwani wapo manabii na mitume wa ukweli?? Hata hao mnaojifanya mnawajua toka huko mbali ni fake tu
 
Manabii na mitume wamegeuzwa maadui kuliko wachawi na waganga waliotapakaa kila mtaa. Wanashambuliwa kuliko majambazi na vibaka . Wanachukiwa kuliko wauaji wa maalbino, kisa ni nini? Udhaifu wa mwanadamu usiwe sababu ya kuipinga kazi ya Mungu. Mitume na manabii sio malaika bali wanadamu. Wewe unawahukumu kama nani ? Mwenye kazi ni Mungu na siku ya hukumu atafanya tathimini na kutoa hukumu ipasavyo!
Mleta uzi kagonga mlemle! Mnayo nafasi ya kuachana na hayo mambo yaliyoainishwa na mleta mada, muwe authentic ktk kazi ya Mungu. Kwa sasa primary objective yenu ni kupiga hela si kumtangaza Mungu. Mnachukiwa kuliko vibaka ksb mnatumia neno la Mungu kuhalalisha dili la kupiga pesa kutoka kwa waumini wenu.
 
Go and try !!!
 
Who is authentic and what is authenticity in this field ,?!!
 
Manabii na mitume wamegeuzwa maadui kuliko wachawi na waganga waliotapakaa kila mtaa. Wanashambuliwa kuliko majambazi na vibaka . Wanachukiwa kuliko wauaji wa maalbino, kisa ni nini? Udhaifu wa mwanadamu usiwe sababu ya kuipinga kazi ya Mungu. Mitume na manabii sio malaika bali wanadamu. Wewe unawahukumu kama nani ? Mwenye kazi ni Mungu na siku ya hukumu atafanya tathimini na kutoa hukumu ipasavyo!
Wapiga ramli tu hao hakuna manabii wala mitume, wapo kwa ajili ya kutafuta utajiri wa Mali kwa kuwatapeli maskini, Mungu anasingiziwa sana eti
 
Who is authentic and what is authenticity in this field ,?!!
Kubali kujirekebisha mtu wa Mungu, kwani unapungukiwa na nini. Achana na ubishi usio wa lazima. Hayo mambo aliyoainisha ni kweli tupu,ndivyo mnavyofanya,je? Kwa utashi wako unadhani mambo hayo yanampendeza Mungu?.
 
Manabii na mitume wamegeuzwa maadui kuliko wachawi na waganga waliotapakaa kila mtaa. Wanashambuliwa kuliko majambazi na vibaka . Wanachukiwa kuliko wauaji wa maalbino, kisa ni nini? Udhaifu wa mwanadamu usiwe sababu ya kuipinga kazi ya Mungu. Mitume na manabii sio malaika bali wanadamu. Wewe unawahukumu kama nani ? Mwenye kazi ni Mungu na siku ya hukumu atafanya tathimini na kutoa hukumu ipasavyo!
Mchawi na mganga ni rahisi kumhubiria na kuokoka tofauti na "anayejiita nabii na mtume" ambaye anajua maandiko lakini ameyageuza na ni sikio la kufa huku akiwapotosha na kupoteza wengi, akina kibwetere, ngwizuu, na wengine wengi hapa anzania
 
Kajaribu kuwahubiria . Kuna wachawi wangapi uliwahubiria wakaokoka na kuna manabii wangapi uliwahubiria wakagoma ?
 
Back
Top Bottom