Kutumia mitishamba na material things kuponya kwa jina la Yesu si dhambi kibiblia

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,418
7,032
Ni uzi wa pili huu naushusha kwa leo, roho yangu inafurukuta sana kuufumua ukweli ambao wengi hawaujui kwenye maandiko. WaTZ tuache uvivu wa kusoma maandiko. Tusiwe watu wa kutafuniwa tafuniwa kila kitu na mapadre na hawa manabii, tuumize vichwa vyetu 'why' tunakuwa wavivu wavivu wa kusoma maandiko?

Kuwa kwetu wavivu ni mitaji kwa watumishi na manabii wa mchongo wasio wa kweli. Tuumize vichwa, no pain no gain jamani. Yaani wengi mnakuwa watu wa Yes Sir kama mrenda? Yaani majinga mengi nina mashaka yapo huku Tanzania kwa Afrika nzima hii na dunia.

Haya tuanze na kisa hiki,
Yesu alipotema mate chini akachanganya na udongo na kutengeneza tope kisha kumpaka kipofu juu ya kope za macho kisha kumuambia aende akanawe Bwawa la Siloamu, alitumia materials halali.

Mate yake(Yesu), na udongo= tope ni materials yaliyotumiwa na Yesu na kumponesha kipofu. Kisa cha pili ni cha wale walioletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwa mtume Paulo na pepo wachafu wakawatoka wakilia kwa sauti kuu, na magonjwa yao yakaponywa.

Haya yangefanyika leo hii kama baadhi ya mitume na wanavyofanya, waTZ wangepiga kelele na kusema ni nguvu za shetani, kwa sababu hawatumii jina la Yesu basi ni nguvu za kuzimu. Wakisahau kuwa haya yote yanafanyika kwa imani katika Kristo Yesu.

Sawa hatukatai kuwa wanaweza kuwepo watumishi wa uongo nao wakafanya ishara hizi kwa jina la Kristo Yesu, ila kuwahukumu kwa kisingizio cha kuwa wanatumia vitu(material things) badala ya jina la Yesu siyo sahihi, tafuteni sababu zingine. Siyo dhambi kabisa kubariki material things na kuzitumia kwa imani ya jina kuu la Yesu kuwaponya wagonjwa na kutenda miujiza.

Siyo dhambi kubariki mafuta kwa jina la Yesu na kuyatumia kuponya, siyo dhambi kubariki keki halikadhalika na kula kwa imani ya jina la Yesu. Tusipotoshane hapa! Mradi tu ni kwa jina la Yesu vitu hivyo vinabarikiwa na kutumiwa.

Tukija kwenye suala la mitishamba, ni dhambi kuagua(kwenda kwa mganga wa jadi/mchawi na kuomba kujulishwa kwa undani kuhusu tatizo husika kwa njia za kipepo). Ndiyo, ni DHAMBI KWENDA KWA MGANGA WA KIENYEJI KUAGUA AU KUTAFUTA SOLUTION YA TATIZO LOLOTE LILE. Ila,
Kutumia mzizi wa mti wowote lets say mpapai au majani ya mpera kutibu kuharisha au ugonjwa wa tumbo siyo dhambi, kwa sababu miti imeumbwa na Mungu na siyo najisi. Ila kuagua TU ndiyo dhambi.
#TutumieMitishambaKwaUtukufuWaMungu

Kuna watu madhehebu ni kama mzigo mzito kwenu;
una dhehebu, unatoa sadaka na kuhudhuria ibadani, ila bado mwilini mwako una chale zaidi ya 100 sasa hilo dhehebu linakusaidia nini si uachane nalo tu watu wajue moja upo upande upi.
una dhehebu lako lets say Mroman Catholic etc ila bado unakwenda kwa mganga kuizindika nyumba yako na kuuzindika mwili wako. Wewe ni mjinga ikiwa unafanya haya kwa kutojua. Ila kama unafanya haya kwa kujua, wewe ni taahira na huna akili nzuri.

Tunategemea unapokuwa katika dhehebh fulani basi unufaike ikiwa ni pamoja na kupata ulinzi kutoka kwa Mungu wako. Hii ni kusema kuwa, WA MADHABAHUNI ATAKULA VYA MADHABAHUNI, case closed.

Natumai nimeeleweka kwa uchache kwenye hivyo vipengele viwili, vya mitishamba na 'material things'. Tusome tuache ulelemama jamani, dunia siyo rafiki sana hii.

Mimi si mkamilifu, naruhusu criticism, wote tunajifunza.
 
Koma kabisa ku generalize mambo, sema kuna waTZ wengine
Tafadhali kama wewe na majirani zako na family yako ni mambumbu hawataki kusoma basi ni nyie tu walahi!
Maana mimi nimezungikwa na professors kila kona ya maisha yangu, vijana wanakwenda kwenye universities za hali ya juu nchini kwetu na nje!
Sasa nyie kama ni idiots ni nyinyi wenyewe makora
Unasikia mtoto mdogo rudi shule ndio utanielewa, imbecile
 
Koma kabisa ku generalize mambo, sema kuna waTZ wengine
Tafadhali kama wewe na majirani zako na family yako ni mambumbu hawataki kusoma basi ni nyie tu walahi!
Maana mimi nimezungikwa na professors kila kona ya maisha yangu, vijana wanakwenda kwenye universities za hali ya juu nchini kwetu na nje!
Sasa nyie kama ni idiots ni nyinyi wenyewe makora
Unasikia mtoto mdogo rudi shule ndio utanielewa, imbecile
Samahani kwa kujumuisha waTZ wote. Nimekosa!
 
Back
Top Bottom