Yanayotokea Muhimbili ni kweli?

Yanayotokea Muhimbili ni kweli?

Mkuu The Boss, japo hili sijalifuatilia ila nilisikia wamebinafsisha huduma zote kwa wale wanaokwenda Muhimbili by choice ambao sio referral. Wanautumia mtindo wa CCBRT wenye pesa walipe, na wasio na pesa wataendelea kuhudumiwa bure na kwa kuchangia. Kuna wagonjwa kibao wa rufaa za mikoani au accident victims wanaotibiwa bure 100%. Wagonjwa wenye ndugu waletewe chakula wenye, pesa walipe chakula, dawa na matibabu, wasio na pesa, wasio na ndugu kila kitu ni bure.

Kitu ambacho sijajua ni kriteria tuu. Mimi nilipopata ajali ya piki piki nililazwa Moi Private by choice unalipia kuanzia room, chakula, service charges ya services zote, consultations, madawa, vifaa tiba, na kila kitu, tena wakati huo CT Scan name MRI zilikuwa mbovu hivyo unalipa 1.M Regency, ambulance 100,000 per trip, and that was 8 years ago name kulipia ilikuwa ni by choice sasa ambapo ni lazima sijui hali itakuwaje.

Paskali.

Paschal hiki ndiyo kinanifanya nikupende sana, huna upande wowote wewe unapenda kusema ukweli bila kulalia upande wowote, safi sana Paschal.
 
haswa hivyo ndivyo ilivyo muhimbili kwa sasa ni juzi kati tu hapa tulikua na mgonjwa pale baada ya siku mbili akafariki maiti yake ilizuiwa ikidaiwa hizo siku mbili alizo lazwa yaani tumefika patamu haswa
 
ICHF hii kadi inachangamoto zake kubwa sana, inatakiwa uchague hospital mbili mfano Kaloleni na Mount Meru, shida ukiwa mbali na hizo hospital huwezi pata huduma na kuna kuwa na orodha ya majina. Nashauri serikali iboreshe iwe ni kwa hospitali zote.
 
Hakuna tena Huduma za afya bure,kuchangia ni lazima na ukitaka exception mzunguko ni mrefu balaa so kama huna bima ya afya kakate tu!acha kulialia by the way jifunzeni home remedies kinga ni Bora Saudi!
Labda hii ndiyo itapelekea kila Mtanzania kujuwa umuhimu wa kujichukulia bima ya afya.
 
Halafu huoni aibu umeweka "Maoni ya wadau wengine"!!! Maoni ya watu wawili katika katika Taifa/Mkoa wenye watu milioni+.
 
Labda hii ndiyo itapelekea kila Mtanzania kujuwa umuhimu wa kujichukulia bima ya afya.

Bima ya afya haitakuwa na maana kama garama za matibabu zikipanda sana. Bima huwa wanapunguza "benefits" au wanaongeza "premiums" wakiona wanajikuta wanalazimika kukulipia fedha nyingi kwa matibabu yako. Hapo garama bado inarudi kwa mgonjwa. Labda hii ipelekee familia za Kitanzania kujifunza kupanga uzazi na kuepuka matumizi holela. Watu waanze kujua kwamba mke wako, mtoto wako ni wa kwako siyo wa serikali.
 
Tareh 21 October mwaka huu nilipata rufaa Lugalo kwenda Muhimbili baada ya wakunga wa hospital ya Kadinali Rugambwa Ukonga kumvunja mtoto mguu wakati wanamsaidia wife kujifungua, wife na mtoto wa siku 3 walilazwa siku 8 pale Maternity, bili iliyokuja haikufika elfu 12, na sina kadi ya bima wala nini, so hizo gharama kiukweli mnazosema mimi binafsi sijakutana nazo kabisa.
 
hao uliowataja hapo ndo wanauwezo wa kukudadavulia au hata wengine kama wana taarifa ?
 
bavicha mna kazi kweli kila siku taarifa za kuchonga,kama kweli hali ingekuwa hivyo si malalamiko yangekuwa ya kiwango cha lami
 
Mkuu The Boss,

Sijajua vipimo vingine, lakini nataka nitoe ufafanuzi kwenye vile nilivyothibitisha.

Upande wa Ct Scan, ni uongo. Mdogo wangu alikuwa anatatizo moja hivi tukaenda kucheck pale, Gharama yake ni Tsh. 150.000 (Hiki kipimo kunakipindi niliona Ikonda ni Sh 270.000 sijui kwa sasa) Tena hapa alifanya Ct Scan ya kichwa.

Kwa upande wa M.R.I mimi mwenyewe nilikuwa (mpaka sasa) na tatizo moja hivi, Nimeenda kupima juzi kati hapo hata mwezi haujaisha. Gharama yake ni Tsh. 250.000. Hivyo ndivyo vipimo nilivyo na uthibitisho navyo.

Kinachokuza Gharama,

Pale Muhimbili panamsongamano mkubwa wa Wagonjwa na ukizingatia ukubwa wa Hosptitali yenyewe. So kwa wale wenye uwezo huwa hawataki kufuata utaratibu uliowekwa na hosptali hivyo huwatafuta "Madalali" Hawa ni wajuzi wa Hospitali hii, Madaktari na Vitengo vyake kulingana na Ugonjwa wa Mgonjwa mwenyewe.

Kwahiyo hawa usipokuwa makini ndio wanaokuza gharama pasipo wewe kujua... Unakuta kipimo fulani ni Shilingi 10.000 mf, Yeye anakwambia Laki moja..!! Wewe kwasababu hauelewi a wala be, na hautaki usumbufu unajikuta unalipa gharama hizo..!!

Halafu pia, Pale Muhimbili kuna huduma zinatolewa kama Private (kwa mahitaji ya mgonjwa mwenyewe) Gharama za Private haziringani na gharama za kawaida, ingawaje hazijapishana ile sana.

Hii ndiyo inawakuta watu wengine wanaopenda Wake zao wajifungue kwa huduma ya Private. Ninachojua, huduma ya Uzazi kwa kina mama ni bure, ingawaje kunagharama kidogo unachangia kama mkeo kafanyiwa Operation.

Hicho ndicho kidogo ninachojua..!!

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom