Wanabodi,
Declaration of Iterest.
Mimi ni mhanga wa ajali mbaya ya pikipiki na kutibiwa Muhimbili, ila nilitibiwa private na kuhudumiwa kama mfalme hivyo ushuhuda wangu huu uko based kwenye Private na sio Public.
Jee wajua kuwa huduma zinazotolewa na hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni huduma the best zenye gharama ndogo kuliko hospitali nyingine zozote? .
Uthibitisho kuhusu gharama za Muhimbili kuwa ni the best na cheapest, umetolewa leo na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Algaisha kufuatia hoja zilizoibuliwa humu Jf katika bandiko hili la Mkuu The Boss likihoji
https://www.jamiiforums.com/threads/yanayotokea-muhimbili-ni-kweli.
Bandiko hili lilimuibua Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw.Aminiel Algaisha.
Kitendo cha mwana Jf The Boss kuibua hoja yenye concerns kwa jamii, ni cha kupongezwa ila pía Kitendo cha Afisa Uhusiano wa Muhimbili kujibu ni cha kuungwa mkono na kupongezwa kwa sababu uongo ukisemwa na kuachwa bila kukanushwa kunapelekea watu kuuamini huo uongo, hivyo PRO wa Muhimbili amefanya vyema kujibu, ila asiishie kujibu tuu bali sasa ajiunge JF ili kukitokea uongo mwingine wowote, unajibiwa pale pale ila pia kwa vile JF inawanachama wengi, then sio vibaya Muhimbili ikiitumia JF katika uelimishaji masuala mbalimbali ambayo ni muhimu kwa umma.
Hizo ndio gharama za kutibiwa Muhimbili. Kama kuna yeyote aliyetibiwa hospitali nyingine yoyote yenye madaktari wa ubingwa kama wa Muhimbili na zenye vifaa kama vya Muhimbili, ajitokeze.
Ila pia kama kuna mtu alilipishwa viwango zaidi ya hivi vilivyoonyeshwa hapa na kupewa risiti, pia ajitokeze, ila kama umelipishwa zaidi na hukujali kuhusu risiti, naomba nikupe pole yako kwa sababu wale watumishi wa Muhimbili, nao pia ni binaadamu na sii malaika.
Nilipotibiwa Moi, Muhimbili miaka 8 iliyopita CT scan na MRI zilikuwa mbovu hivyo ikabidi nipelekwe Regency kwa vipimo hivyo, kila kimoja ni 500,000. Lakini leo MRI Muhimbili ni 210,000, CT Scan 150,000, Ultra Sound 25,000, X Ray 18,000, zunguka ukikuta popote huduma hizo ni nafuu kuliko Muhimbili, tujulishe tukimbilie hapo.
Baada ya Muhimbili nilikwenda Apollo India, nikilinganisha vifaa vya kule Apollo na vile vya Moi, kiukweli Moi wanavifaa bora kuliko Apollo. Kipimo cha pressure Moi ni cha umeme, Apollo nI kile cha kubonyeza. Vitanda Moi ni vya umeme, Apollo ni vile vya kunyonga, etc hivyo kiukweli tuna kila kitu ila basi tuu.
Tofauti pekee kati ya Muhimbili na Apollo ni customer care services, kule unahudumiwa kwa kunyenyekewa kama mfalme, jinsi manesi wanavyokuchangamkia na kukusmile, mgonjwa unajisikia nafuu na baadhi ya mgonjwa madogo madogo yanajiponea yenyewe.
Wenzetu kule wanafanya biashara ya tiba, huku tunatoa tuu huduma za tiba.
Hivyo hatua za Hospitali za umma kutoza gharama za kuchangia matibabu zina lengo jema la kuiwezesha Muhimbili kuboresha huduma zake. Yule nesi kule India anayekusmilea hadi kuchanganyikiwa, anakuwa alipata mlo asubuhi, anakula vizuri, anaishi mahali pazuri, ana usafiri wa uhakika na analipwa vizuri, kwa nini wasi smile hadi jino la mwisho?, vivyo hivyo huko kuchangia gharama kutawafanya wahudumu wa Muhimbili kusmile.
Hivi hiki wanachotufanyia Muhimbili Hospital ni haki kweli?
Paskali