KUBOMOA NA KUJENGA MUHIMBILI.
April 10, 2026 nimewasikia CCM katika kusanyiko lao haramu wakisema wanakwenda kujenga hospitali mpya ya Taifa ya Muhimbili (Muhimbili National Hospital (MNH) na watatumia TZS 1.2 Trilioni ambao ni mkopo.
Serikali katili ya CCM imeeleza kwamba ujenzi utatumia mkopo wa TZS 1.2 Trilioni, lengo ni kuwa na hospitali bora, sasa imeshindwa kupata ithibati kutokana na majengo kusambaa na kutumia eneo kubwa.
Akasisitiza, Mpango huo ni mahsusi kwa ajili ya kujenga Muhimbili mpya yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 1,300, pamoja na ujenzi wa majengo na usimikaji wa mitambo yote, na itatekelezwa kwa awamu saba.
January 24, 2022; Waziri wa Afya, akiwa ni Ummy Mwalimu, alisema Serikali itajenga ‘upya’ (MNH). Akasema MNH haiendani na mabadiliko ya sayansi & teknolojia katika utoaji huduma bora za matibabu.
Ummy Mwalimu akasema, Muhimbili National Hospital (MNH) imeandaa mpango wa matumizi ya ardhi mpango unaogharimu TZS 500 Bilioni kuboresha miundombinu ya kutoa huduma ikiwemo ujenzi wa majengo.
August 12, 2023; Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Profesa Mohammed Janabi akatoa ufafanuzi akasema, Serikali imechukua mkopo EXIM BANK CHINA, kiasi cha TZS 600 bilioni ili kujenga Hospital ya Taifa – Muhimbili
Prof, Mohammed Janabi, alisema mradi huo wa ujenzi wa Muhimbili National Hospital (MNH) ni kati ya miradi mikubwa saba ya Serikali iliyoidhinishwa na kutengewa fedha, kwamba itabomolewa na kujengwa upya.
February 16, 2024; Prof. Mohammed Janabi, alikutana na timu iliyokuwa inafanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na ushauri elekezi (consultancy services) wa ujenzi, kuashiria kuanza kwa mchakato.
Prof, Mohammed Janabi akiwa Mkurugenzi Mtendaji MNH alisema mradi wa Hospitali mpya ya Taifa ya Muhimbili (MNH) utajengwa kwa awamu (Phase-based Construction) na kugharimu TZS 700 bilioni.
Mei 14, 2024; Aliyekuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alilieleza bunge wanatarajia kutumia TZS 500 Bilioni kujenga upya miundombinu ya MNH ikiwa ni kubomoa majengo yaliyopo na kujenga upya.
Mei 30, 2024; Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Albert Chalamila, wakati wa mjadala mkubwa wa ziara za nje za Rais, alisema Rais amekwenda Korea Kusini kuomba mkopo wa TZS 560 Bilioni za ujenzi wa MNH
Walipa kodi, hatukuelewa, pesa hizo ni mkopo kutoka katika Serikali ya Korea Kusini au EDCF (Economic Development Cooperation Fund) au mkopo wa The Export-Import Bank of China (EXIM Bank China).
Muhimbili (MNH) walijenga Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila, ambayo inapatikana Kwembe, Ubungo (nje kidogo ya mji, kando ya barabara kuu ya kuelekea Morogoro). Serikali haijaridhika na viwango vyake?
Hospitali ya Yaifa Muhimbili – Mloganzila ni hospitali ya rufaa ya ngazi ya juu (superspecialized). Hili ni tawi la kisasa la MNH lililolenga kupunguza msongamano MNH Upanga na kutoa huduma za kibingwa zaidi.
Muhimbili – Mloganzila kuna eneo kubwa ambalo lingeweza kutosha ujenzi huo na kupunguza mrundikano wa wagonjwa kampasi ya Upanga na kuifanya (MNH-Mloganzila) Hub ya kimataifa ya tiba.
Kwanini zitumike fedha nyingi za mikopo ambayo tutalipa kwa gharama kubwa kubomoa na kujenga hospitali katika eneo ambalo ipo sasa? Serikali timamu ingewekeza nguvu ujenzi wa ‘Muhimbili’ mikoani.
Tanzania kuna mikoa 31, halmshauri 185. Kwanini hiyo fedha inayokwenda kutumika katika kubomoa majengo na kuyajenga upya, isigawanywe kwa utaratibu mzuri na ipelekwe kujenga hospitali za kisasa na vifaa tiba?
Serikali ya CCM ilitenga TZS bilioni 4 bajeti 2023/24 ujenzi wa Hospitali ya Rufaa – UKEREWE, Mwanza. Kama Sh4 bilioni zinajenga hospitali ya Rufaa, TZS 1.2 Trilioni zingejenga wastani wa hospitali za rufaa 300.
Kila halmashauri ingepata hospitali yenye hadhi ya RUFAA. Mikoa yote 31 ingelipata hospital za kisasa hadhi ya rufaa na zingebaki fedha za hospital 84. Fedha zingetosha kununua vifaa tiba vya kisasa pia.
MNH majengo baadhi yanahitaji ukarabati na unadhifu siyo kubomoa na kujengwa. Wizara ya afya haielewi nini vipaumbele vyake. Wizara inakwenda kama gari mbovu ambalo linaweza kuwaka katika gia ya reverse.
Badala ya kubomoa majengo ambayo wao wanasema hayana ithibati kwa sababu yamesambaa eneo kubwa, watumie adaptive reuse (kuboresha jengo la zamani kwa matumizi ya kisasa) huokoa fedha nyingi
kuna ukosefu wa mpango mkakati (strategic planning). Miradi inapangwa kwa ajili ya kuonekana kwa macho (optical politics) badala ya kutatua kero za msingi za mgonjwa anayekaa saa sita kusubiri daktari.
Kabla ya kubomoa, wafanye utafiti. Ukarabati vs. Ubomoaji (Cost-Benefit Analysis). Unadhifu na mazingira safi ni hitaji la msingi la afya, halihitaji bajeti ya mabilioni ya ujenzi, bali usimamizi madhubuti.
Kabla ya kubomoa, iwepo ripoti ya wazi inayoonyesha kwanini ukarabati hauwezekani. Upimaji wa hali ya majengo (structural integrity audit). Wataalamu wa afya na watumiaji wa huduma waeleze nini kero yao.
Kuna maeneo nchi yetu hii, hayana hospitali kabisa, huko zipelekwe fedha zikajengwe hospital zenye hadhi sawa na MUHIMBILI. MNH – Upanga, iboreshwe kwa kupewa vifaa tiba vya kisasa na dawa za kutosha.