Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Kwenye lugha ya kidhungu kutoeleweka kwa watz wwngi nani haswa alaumiwe? Ni shidaaaa sana kwakweli
 
Nimefurahi kusikia kwamba kutoka kwa Mwanasheria Mstaafu wa Kenya, Amos Wakko kwamba Kenya nafasi nyingi mfano: Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu, Wakuu wa Taasisi zote za Umma, wanaomba ajira kama wafanyakazi wengine wowote wale. Na Interview kwa nafasi muhimu mfano Jaji Mkuu hufanywa kwenye TV Live. Hii ni jambo muhimu sana, tunahitaji kuwa nalo maana rushwa na wizi wa rasilimali utapungua katika Ofisi za Umma. Kila mtu yuko huru kufanya kazi kwa utaalamu bila kuogopa aliyemteua...

Ni jambo la msingi sana hilo, watu waombe nafasi na wapigiwe usaili kama watumishi wengine
 
kumbe janga la kizungu ni kubwa sana hata hapa JF hakuna Updates ya mambo yanayoendelea bungeni.wengine hatuna TV tulitegemea hapa kama ilivyosiku zote.! ya leo kali.
 
Wana jf punde tu msemaji alikuwa anatoa semina kwa kiingereza nilichoona utulivu ulikuwa asilimia 100 sasa ishu imegeukia kiswahili fujo zimeanza.sasa napata wasiwasi je lugha ya kiingereza ndo kiboko ya wasumbufu bungeni au
 
Muda huu Mtikila amewaambia wanaccm wasitishe watanzania juu ya muungano kwani naye wamemshwawi arudi dar amekataa imefikia sasa wanatamka kumshughulikia.Mh Sitta kasems atalindwa kwa mujibu wa sheria
 
Wanajamvi.

Mtikila anamchana live Mh. Sitta kwa kauli yake ya nitawakomesha wale wote wanaopinga muungano. Mch. Mtikila amesema mengi ila kubwa ni jinsi gani na namna gani atashughulikiwa. Anauliza atashughulikiwa kama Dr. Ulimboka, Dr. Mvungi, Mwangosi au mwingine aliyeteswa na CCM.
 
Mbona hueleweki sasa jazia nyama nasie tuliombali tujue huyo Mtanganyika kaongea nini
 
WanaJF,

Katika hali ya kushangaza bungeni, mch Mtikila ametokea kukurupuka na kuingizia mambo ambayo hayahusiki katika mjadala unao endelea bungeni kwa sasa ambao ni kuhusu semina ya uzoefu wa nchi ya Kenya katika kuandaa katiba yao.

Mchungaji Mtikila bila ya aibu ametokea kuingizia mijadala mingine kabisa ambayo haina mahusiano ya kile ambacho kinajadiliwa bungeni na kupelekea kutokea kwa hali ya taharuki miongoni mwa wajumbe wa bunge maalumu. Jambo ambalo limemdhalilisha sana Mtikila.

Kubwa ambalo Mtikila alikuwa anang'ang'ania ni kupigania Tanganyika bungeni eti akidai kuwa kuna vitisho kutoka kwa mhe Sitta vya kuwashughulikia wale watakao ipigania Tanganyika kama ambavyo Dr Ulimboka, Dr Mvungi na Kibanda walivyo shughulikiwa. Jambo ambalo limepingwa vikali na Mhe Sitta kwa kumwambia yeye kama Mwenyekiti atatumia kanuni za bunge na sio vinginevyo katika kushughulikia hoja.

My take,

Mhe rais Kikwete amefanya makosa sana kuteua watu ambao vichwani mwao haijulikani kama ni wazima ama lah.

Hivi huyu Mtikila anashindwa kuelewa kuwa kuna mjadala wa semina na pia kuna mgeni!? Tanganyika nani anaitaka? Kama sio yeye na CHADEMA tu?
 
Wanajamvi.

Mtikila anamchana live Mh. Sitta kwa kauli yake ya nitawakomesha wale wote wanaopinga muungano. Mch. Mtikila amesema mengi ila kubwa ni jinsi gani na namna gani atashughulikiwa. Anauliza atashughulikiwa kama Dr. Ulimboka, Dr. Mvungi, Mwangosi au mwingine aliyeteswa na CCM.
Swali zuri sana,Sitta amesahau kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na si Mwenyekiti wa Bunge Maalum la CCM la Katiba,
 
Back
Top Bottom