BAWACHA wamtaka Spika wa Bunge kuwaondoa akina Halima Mdee na wenzake Bungeni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) limemtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kuwaondoa Bungeni Wabunge 19 wa viti maalum wanaodaiwa kuwa wanachama wa CHADEMA, kinyume chake Baraza hilo limetishia kuwahamasisha wanawake Nchini kote kupinga kuendelea kukanyagwa kwa Katiba na matumizi mabaya ya kodi za Watanzania kuendelea kutumika kuwalipa watu wasio na sifa ya kuwa Wabunge kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo leo, Jumatatu Januari 29.2024 imesema kuwa Mahakama Kuu katika hukumu yake ya Desemba 14.2023 imethibitisha kuwa maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika Novemba 27.2020 ambacho kilichukua hatua ya kuwafukuza uanachama wanawake hao 19 yalikuwa sahihi

Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Kaimu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Sharifa Suleiman imeendelea kueleza kuwa, pamoja na hukumu kutolewa na walalamikaji kuwasilisha notisi lakini Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa hajachukua hatua yoyote ya kuwaondoa Bungeni badala yake ameendelea kuwakumbatia kinyume na Katiba ya Nchi jambo ambalo amedai kuwa Mhimili wa Bunge unashindwa kuheshimu maamuzi ya Mhimili wa Mahakama

BAWACHA imesema inatarajia kuona majibu ya Spika Dkt. Tulia Ackson kwa kuchukua hatua mara kikao cha Bunge kitakapoanza Jumanne hii, Januari 30.2024.

20240129_133453.jpg
 
Wanampangia?!
Wanampangia vipi? Katiba iko wazi, hawana uanachama wasiwe wabunge. CCM wenyewe walifurajia bunge kulifanya la Chama kimoja wakasahau sheria za Mabunge kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi wapinzani lazima wawemo, wamekumbuka tayari walishaharibu, Sasa kuionyesha Jumuia ya Mabunge kuwa wanaheshimu sheria, wakawarubuni hawa 19 na leo wanaona aibu kuwatoa. Furaha ya kulifanya bunge liwe la Chama kimoja walisherehekea, Ila kurudi kwenye uhalisia hawataki.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huo ndiyo ukweli mchungu.Kujidai kujua mengi na kutaka kukomoa wengine bila kuishi kwa akili zaidi.Atakayekiri amekuelewa napenda nimfahamu ili nimnunulie bagia za Tsh mia tatu.
 
Mhe. Spika tenda haki. Suala la Wabunge 19 lisije likakuharibia sifa zako. Hukumu tayari ilitolewa na Chama chao kuwavua uanachama. Hawatakiwi kuwa Bungeni.
 
Back
Top Bottom