Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Mheshimiwa Lusinde bingwa wa matusi leo anauchapa usingizi? Yeye hakupata nafasi ya kumuuliza maswali huyo mr wako?
 
Katika namna ya kipekee leo Mch C. Mtikila amemuonya mwenyekiti kuhusu kauli kuwa watu wasiotaka muungano watashughulikiwa. Ameuliza jee watashughulikiwa kama Kolimba? Au Dr Mvungi, Ulimboka au kwa namna gani. Ameweka wazi kuwa kwa vile yeye yuko wazi kuwa haungi mkono muungano huu uliopo sasa wa kuipoteza Tanganyika hivyo tishio hilo la kushughulikiwa ni wazi ni kwake yeye. Kama mawazo ya wengine hayasikilizwi bali ya kikundi cha watu wachache (CCM) anafikiria kufungasha virago na kurudi Dar ili kuendelea na shughuli zingine kuliko kushiriki Bunge linaloburuzwa kwa maslahi ya watu wachache. Pamoja na Sitta kuipoza hoja hiyo kwa kusema Mtikila asiwe na wasiwasi, lakini maelezo ya Mtikila yameleta damage kubwa katika uhuru wa uendeshaji wa bunge hilo.
Jee kama kuna kutishana kushughulikiwa inakuwaje kwa wale wajumbe legelege wasio na msimamo thabiti kama Mtikila? Watawezakufanya kazi tuliyowatuma?


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Swala la shule za kina Kayumba/kata inabidi ubora wake usiisitizwe kwenye hii katiba. La sivyo hata wakalimani tutashindwa kuwazalisha.

Hapo sasa ndio wataona umuhimu wa kiwango cha chini cha elimu kwa atakayeomba ubunge kuwa shahada ya chuo kikuu!!! Huwezi kuwa na wabunge wasioelewa kingereza na wewe ukajivuna eti una wabunge; hao wabunge wasioelewa kingereza watakuwa wakina Kayumba tu!!!
 
Japo sipendi ushabiki wa kisiasa naa mini mwigulu yuko vzr, labda useme Sendeka, Lukuvi na wasira hao na shaka nao

Sendeka na Lukuvi hamnaga kitu kabisa, utaona kama sendeka atachangia chochote leo, hapo ngoma ni kwa vijana wa cdm na nccr ndio muda wao
 
Summury: kauli iliyo tolewa na mwenyekiti wa bunge maalumu siku kadha zilizo pita kuwa wachache wanao upinga muungano watashughulikiwa imechuku sura mpya baada ya mchungaji mtikila kutoa msimamo wake kwenye semina inayo endelea bungeni kwa kutoa tahadhari kuwa watanganyika ml48 wenye kutaka maendeleo na mamlaka ya nchi yao Tanganyika hawaogopi CCM (ml2) wanao utunza muungano kwa maslahi yao binafsi na pia amehoji namna ya kushughulikiwa huko akisema "je ni kama alivyo shughulikiwa mh Kolimba Dr mvungi au Dr ulimboka?"

Mtikila ndiye Mtanganyika pekee mwenye ushujaa wa kuiumbua serikali dhalimu na vibaraka wake. Kudos Mtikila
 
Wakati bwana Okao kutoka Kenya akiendelea kuelezea uzoefu wake kuhusu katiba ya Kenya na kutaka watanzania wajifunze kupitia Kenya, mtaalam huyu amekuwa akitoa maelezo hayo kwa njia ya kimombo na baadae kutafsiriwa, baadhi ya wajumbe wamemuomba M/Kiti ili mtaalamu huyo endelee tu kwa lugha ya kimombo kwa vile wengi wanafahamu. wakati Mwenyekiti akihoji kuwa endelee kwa lugha ya kimombo Mh Seif Ali Iddi amepeleka kichwa chake kushoto na kulia akiungana na baadhi ya wajumbe kutaka iendelee kutafsiriwa.,

Sipati picha kwa Mbunge wangu Jah People. Bila shaka moyo umechafuka kabisa.
 
So kumbe mombasa nayo ilikua chini ya sultan wa zanzibar na ndo sababu kenya wakalazimika kukubali mahakama ya kadhi kama mbinu ya kumpoza sultan.
Huku bara wao walijaribu kuimeza zanzibar kimyakimya bila kuaddress ishu ya kilomita 16 za ukanda wa pwani kuwa under the territory of the sultan of zanzibar.
No wonder serikali inang'ang'ania serikali mbili kwa kujua kuwa siku zanzibar ikijitenga wanaweza kudai dar es salaam,tanga,pwani,kilwa.
No wonder pia just in case nyerere aliamua kuhamisha mji mkuu uwe Dodoma badala ya dar,kwani alijua siku yoyote linaweza kubumbuluka.
WE REALLY ARE STUCK BETWEEN A ROCK AND A HARD PLACE.
 
Anaogopa nini na yeye ni jasiri kuliko wanasiasa wote tz
 
WanaJF,

Katika hali ya kushangaza bungeni, mch Mtikila ametokea kukurupuka na kuingizia mambo ambayo hayahusiki katika mjadala unao endelea bungeni kwa sasa ambao ni kuhusu semina ya uzoefu wa nchi ya Kenya katika kuandaa katiba yao.

Mchungaji Mtikila bila ya aibu ametokea kuingizia mijadala mingine kabisa ambayo haina mahusiano ya kile ambacho kinajadiliwa bungeni na kupelekea kutokea kwa hali ya taharuki miongoni mwa wajumbe wa bunge maalumu. Jambo ambalo limemdhalilisha sana Mtikila.

Kubwa ambalo Mtikila alikuwa anang'ang'ania ni kupigania Tanganyika bungeni eti akidai kuwa kuna vitisho kutoka kwa mhe Sitta vya kuwashughulikia wale watakao ipigania Tanganyika kama ambavyo Dr Ulimboka, Dr Mvungi na Kibanda walivyo shughulikiwa. Jambo ambalo limepingwa vikali na Mhe Sitta kwa kumwambia yeye kama Mwenyekiti atatumia kanuni za bunge na sio vinginevyo katika kushughulikia hoja.

My take,

Mhe rais Kikwete amefanya makosa sana kuteua watu ambao vichwani mwao haijulikani kama ni wazima ama lah.

Hivi huyu Mtikila anashindwa kuelewa kuwa kuna mjadala wa semina na pia kuna mgeni!? Tanganyika nani anaitaka? Kama sio yeye na CHADEMA tu?

Wewe na mtikila nani yupo vizuri kichwani? Mwenzio kaenda shule anjiamini na anachokiongea yupo tayari kukijengea hoja.
 
Ajabu ni kuwa alijipendekeza mwenyewe kwenye orodha ya wajumbe wa bunge la katiba iliyopelekwa kwa rais, hiyo ilikuwa ishara ya kukubaliana na mchakato mzima. aache mikwara kama anajitoa aondoke awaachie wengine wenye mapenzi mema na nchi
 
Sitta ni ndumila kuwili ni hatari kubwabungw kuongozwana mtu aina yake . hatufiki mbali
 
Huyu jamaa wanamsemaga chizi sababu ya ujasiri na misimamo yake, ila wengine huwa tunamkubali ya kuwa ni kati ya majembe machache ya Tanganyika yaliyobakia.
 
Katika namna ya kipekee leo Mch C. Mtikila amemuonya mwenyekiti kuhusu kauli kuwa watu wasiotaka muungano watashughulikiwa. Ameuliza jee watashughulikiwa kama Kolimba? Au Dr Mvungi, Ulimboka au kwa namna gani. Ameweka wazi kuwa kwa vile yeye yuko wazi kuwa haungi mkono muungano huu uliopo sasa wa kuipoteza Tanganyika hivyo tishio hilo la kushughulikiwa ni wazi ni kwake yeye. Kama mawazo ya wengine hayasikilizwi bali ya kikundi cha watu wachache (CCM) anafikiria kufungasha virago na kurudi Dar ili kuendelea na shughuli zingine kuliko kushiriki Bunge linaloburuzwa kwa maslahi ya watu wachache. Pamoja na Sitta kuipoza hoja hiyo kwa kusema Mtikila asiwe na wasiwasi, lakini maelezo ya Mtikila yameleta damage kubwa katika uhuru wa uendeshaji wa bunge hilo.
Jee kama kuna kutishana kushughulikiwa inakuwaje kwa wale wajumbe legelege wasio na msimamo thabiti kama Mtikila? Watawezakufanya kazi tuliyowatuma?


Sent from my iPad using JamiiForums

anachosema mtikila ndicho wengi wanachokishangaa muungano gani wa upande mmoja?yaani Tanganyika kujiita Tanzania,lakini Zanzibar iko palepale na serikali yake,rais wake na katiba yake na mbaya zaidi katiba ya zanzibar inasema wazi kwamba Zanzibar ni nchi. watu wenye akili timamu lazima washangae na kuona wanaelezwa kisicho ilezeka. la msingi hapa ni kutueleza kwanza huu muungano ukoje? maana kila anayesema azungumzii haya.ebu wana JF niwekeni wazi na mimi nielewe
 
Back
Top Bottom