Yaliyojiri: Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi - Mbeya!

Yaliyojiri: Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi - Mbeya!

Hivi lowasa mwenyewe yupo hapo mbona somuoni?
 
Chama kimefanya kazi yake, serikali itaendelea kuchukua hatua
 
Katibu mkuu ni mtu wa field, sio wa kukaa ofisini
 
jk anamwaga sifa kwa kinana kuwa ni mtu wa watu anayeweza kukaa na watu na kula nao hakika ametimiza jukumu la kuwa katibu mkuu wa chama safi ndugu yangu kinana.
 
Nimeonaa watu wanagawana Tshirts za friends of Lowassa Bagamoyo
 
umbea huo mbona hajataja mtu, ukiwa mzee utakuwa mchawi,
mimi niko uwanjani lakini sijaona jk kumgusa lowasa,
je,kwa macho yako kamgusa wapi begani au mikononi?
tatizo lako una macho lakini huoni, una masikio lakini hayasii, tatizo inaonekana ni matunda ya shule za kata!
 
naona jk ameshaanza kumnanga lowasa, haa haa

Sijui neno "kumnanga" kwako linamaanisha nini. Kwa Kiswahilisafi neno "kumnanga" mtu ni kumpamba zaidi ya kiasi. Mfano ukisema bi harusi "wamemnanga" ina maanisha kapambwa mpaka ana chusha. Ukisema mbona mna "mnanga" nkongu kwa maneno, inamaanisha unasifiwa kwa maneno zaidi ya sifa unazostahiki mpaka inakera.

Jee, ulipoandika ulimaanisha nini? Au Kiswahili ni lugha uliyoijulia ukubwani na unaokoteza maneno bila kujuwa yana maana ipi, mradi fulani aliliandika nawe unakurupuka nalo bila kujuwa lina maanisha nini.

Pole kama nimekuudhi lakini naona ni wajib wangu kukupa ilm usiokuwa nayo na natumai kuanzia sasa utalitumia neno hilo kiufasaha zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Tunaboresha shule zetu za msingi na sekondari
 
Mbeya haiko hivyo pic sijuwi umeitowa wapi kichaa ww!!
Hii picha km hawa watu wapo wanashuka sidhan km wanashukia Mbeya mjn sijawahi ona mahali km hapo mbeya mjn.
Lakn km wapo wanapanda hilo lori hayo maeneo ni km ya Chimala.
Mtoa picha ni vema akatupatia ukweli vingnevo tukubaki jf itakuwa inaendelea kuingiliwa na watu wasio.
 
Mwigulu anasema -Mtaji wa kisiasa wa CCM ni mafanikio ya watanzania, mtaji wa CHADEMA ni umaskini wa watanzania, anasema CHADEMA wanajifanya wazalendo lakini kwenye maandamano watoto wao hawaji, matokeo yake watoto wa watu wengine ndio wanakufa. Kanichekesha sana aliposema bendera ya CHADEMA imefanana na SANDA.
Yani haya ndio maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha naibu waziri???

Hii ni sherehe ya kutoa stress kwa vijembe au?
 
Back
Top Bottom