Yaliyojiri: Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi - Mbeya!

Yaliyojiri: Maadhimisho ya miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi - Mbeya!

mjepo

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
4,913
Reaction score
919
Wakuu chama cha watanzania leo kinaadhimisha miaka 37 tangu kuanzishwa kwake mjini mbeya kwa sasa burudani zinaendelea.

mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais na mwenyekiti wa ccm taifa mh jakaya mrisho kikwete.

viongozi wengene wa kitaifa wa ccm pia wamefika akiwemo ndg nape,kinana ambaye pia ndiye katibu mkuu wa ccm taifa mwanasiasa mwenye huruma sana na watu mwenye kujishusha siku zote kwenye kazi zake.

sherehe hizi pia zinaadhimishwa kote nchini kwa mikoa yote kwa namna tofauti tofauti.
 
kituo cha tbc nao wako live kabisa wakirusha tukio hili muhimu la kichama ili wale ambao hawajafika uwanjani waweze kujionea na kufuatilia vema ni furaha na shangwe uwajna wa sokoine mbeya na watu ni wengi kweli.
 
Tunanufaika na nini umeme juu bei za vyakula juu deni la taifa juu mlala hoi kodi juu. Kwani wewe huyafeel haya maumivu? Acha ulimbukeni unaona kama umeandika kitu cha maana.shwaaaaaain
 
vijana wa uvccm wanaendelea kusherehesha na kuserebuka kila mtu kwa raha zake.
 
katibu mwenezi wa ccm taifa ametoa afa kwa kikundi cha mbozi band kurekodi nyimbo zake kwa gharama ya nape honhera nape kwa kuwaunga mkono vijana wa mbozi viva ccm.
 
kwa sasa dokii ndiye anaburudisha na kibao chake cha njoo kwangu kilichovuma sana mika ile.
 
Tunanufaika na nini umeme juu bei za vyakula juu deni la taifa juu mlala hoi kodi juu. Kwani wewe huyafeel haya maumivu? Acha ulimbukeni unaona kama umeandika kitu cha maana.shwaaaaaain

chakula gani bei juu mkuu soko matola mchele unapata mpaka 1000 kilo kyela ndiyo kabisa tafiti kabla ya kusema jambo utachekwa.
 
Nipo uwanjani hapa kwa kweli nikionacho humu ni muziki tu hakuna sera zaidi uwanja umejaaa watoto wa rika la miaka 5 hadi 15 hawa wengi wao ni wanafunzi wa SANGU, META, IVUMWE, MBALIZ SEKONDARI.

NB; Watu kuvaa kofia kwa mtindo wa kufunika uso ina maana gani.?
 
katibu mwenezi wa ccm taifa ametoa afa kwa kikundi cha mbozi band kurekodi nyimbo zake kwa gharama ya nape honhera nape kwa kuwaunga mkono vijana wa mbozi viva ccm.

ccm imedoda!!! hiki chama lazima kife mwaka huu,hongera lowassa kwa kuliona hilo na kuamua kufanya harakati kivyakovyako!!!
 
kikundi cha ngoma toka kyela nacho kinapata nafasi ya kuburudisha na kudumisha jadi ya watu wa kyela na mbeya kwa ujumla.
 
Mbona uwanja una mapengooo...WATUMISHI wa umma wamekaidi amri....boda boda

mkuu mapengo yako upande gani nambie umekaa upande gani nije tuonane unioneshe mapengo yalipo acha uongo.
 
Back
Top Bottom