Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Kila mtu anakazi yake kama mimi kazi yangu ni kulima mpunga ili wewe ule.... basi wewe kama mwanahabari inabidi unipatie habari zote bila chenga nikizitaka.... Siku ukikosa mpunga basi njoo unilaumu.
Achana nae alitaka abembelezwe kuleta taarifa akiwa kwenye mdahalo, sasa hakuna aliyembembeleza kanuna ana kisasi.
 
kwa kweli ni majukumu tu ya kijamii yaliyonifanya nishindwe kwenda nyumbani UDSM kushuhudia na kushiriki moja kwa moja japo asante ITV Nimeshiriki kwa kuona tu..ila mchakato umeanza vizuri,kwa hari kubwa na wachangiaji wameonesha changamoto nyingi za kupambana nazo katika kufikia mabadiliko ya kikatiba.na nilipenda sana ushauri wa Dr.kitila kwamba mchakato uende bila nguvu ya msukumo wa vyama vya siasa mana wao wako katika mbio za kijiti za kupolana madaraka hivo wanaweza wakawainflunce watu kwa itikadi na maslahi ya chama chao na sio Taifa.pia vivi ITV kwa kutusaidia kupata matangazo moja kwa moja.
 
Nadhani bado kuna watu wenye mawazo hayo bungeni! lakini pia itatu-expose kwenda kwenye hali kama ya kenya ya kusubiri maumivu badala ya kuzuia! Let's weigh
 
Ninawapongeza wasomi wa Chuo Kikuu cha Dsm kwa mjadala wa leo juu ya Katiba mpya. Wamedhihirisha kuwa wao ni taasisi muhimu kwa mustakabli wa nchi hii. Ninatoa wito kwa taasisi nyingine zinazofanana nayo kufanya hivyo bila woga.
 
Ninawapongeza wasomi wa Chuo Kikuu cha Dsm kwa mjadala wa leo juu ya Katiba mpya. Wamedhihirisha kuwa wao ni taasisi muhimu kwa mustakabli wa nchi hii. Ninatoa wito kwa taasisi nyingine zinazofanana nayo kufanya hivyo bila woga.
UDOM nao inabidi wabadilike kwakeli!waige mfano huo!
 
Hivi alipewa kazi ili atikise viberiti..... Tena ingebidi ajiuzulu... kama ni kutikisa viberiti hata mimi naweza....

Jenerali Ulimwengu alimaliza pale pale aliposema "...inafika mahali mtu anateuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkoa... kwa sababu ni hawala yake..., mteliwa huyo wananchi wakimpelekea malalamiko anawajibu hovyo hovyo atakavyo kwa sababu tu hawezi kuwajibishwa na hawala yake..! Watu ukumbini walishangiliaje, inaonekana kama ilimgusa mtu pale!

Jenerali alipendekeza wakuu wa wilaya na mikoa wachaguliwe na wananchi wa eneo husika ili awajibike kwao moja kwa moja na umma uwe na sauti ya mwisho katika matumizi ya rasilimali za eneo lao. Nili ipenda sana hoja hii! Big up Ulimwengu!
 
It was great indeed and I believe we're in the right course as a country
 
Shivji yuko sahihi 100% haya maccm huwa hayana aibu kuwadhulumu na kuwaonea wanyonge kama kitumbua chao kiko hatarini. Lazima uelewe unapobadili katiba kuna watu nafasi( 0pportunity ) za kujinufaisha zinaondolewa
 
Jamani wana JF Prof Shivji ameongea kwenye kongamano leo kwamba kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni ni hatari kwani CCM watachukua advantage ya uwingi wao bungeni kuikwamisha,does it make sense,kweli bado tuna bunge la watu wa kujali maslahi ya chama,naomba michango kwa hili.
Ni kweli katika hali ya kawaida ccm wangeizuwia..
Lakini mbona mwenyekiti wao amesema kwa uwazi mbele ya wanaJamhuri wote kuwa katiba mpya haiepukiki, na ni wakati muafaka kujadiliwa, na ameahidi kuunda kamati ya upembuzi wa awali..
Sioni ccm-bungeni watakuwa na courage gani ya kumbishia mkuu wao!
 
"...ili tupate katiba nzuri inabidi tupeleke bungeni muswada upitishwe ili iwe guidelines ya kuandika katiba mpya, yawekwe maadili ya Taifa kama yaliyokuwepo enzi za Mwl. JKN ...ndiyo yawe mwongozo wa kuanza mchakato wa kuundwa katiba mpya..." Alisema Mzee Kaduma!
 
Je kuna mtu anaweza kutuwekea hapa links za huu mjadala kama alivyofanya jana kwenye mjadala wa Dowans? Wengine huku tumechelewa kuamka na mjadala ITV ulikuwa umeshamalizika.
 
Very useful post! shukrani wadau wote waliorusha na waliochangia, sisi tulio mbali tumepata highlights za kutosha.
 
shivji yupo sahihi kabisa. CCM will take advantage of their majority in the parliament to make decisions in their favour.....
 
Ndio yale yale aliyoyasema julius mtatiro. Naibu katibu mkuu wa cuf-tanganyika. Chadema hawana uelewa wakutosha ndio maana mnyika akakimbilia bungeni kujipatia umaarufu. Nyie chadema na siasa tokea lini?
 
Kutokana na dhamira ya Mnyika kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, mtoa mada wa leo Prof. ISSA SHIVJI amewaonya CHADEMA kuwa suala hilo wasilipeleke bungeni kwani hatari yake ni kuwa suala hilo litatekwa na CCM kwa vile wao ni wengi na kuamua walitakalo. Alisema ya kwamba CDM wafikirie zaidi ya jambo hilo kuliko hivi sasa ambapo wanaonyesha wanajadili mambo ya katiba kwa jazba na kishabiki

Ahsante Shivji kwa kuwa mkweli.
 
Back
Top Bottom