either tuamue kuamini ushahidi ni wauongo au ushahidi niwaukweli.....Je tunajuaje ushahidi ni wauongo au waukweli?..... huyo Urio aliyetajwa naye yupo kwenye kutoa ushahidi?,

Figure za hela zinazotajwa wahusika kupewa mbona hazilingani na kazi tunayoambiwa walipewa?..

Sijaona mahala popote wahusika wanapewa kazi kwa makubaliano fulani, Je wahusika waliahidiwa nini baada ya hiyo kazi ya hatari?...hivi mtu anaweza tu kufanya kazi ya hatari kama hiyo bure?...maswali ni mengi ngoja tuendelee kujiuliza..
Wewe ni mnafiki sana, comment yako ya mwanzo umeisahau mara hii? Ngoja nikukumbushe mwanzo umeandika hivi ... "hii kesi imemkalia vibaya mwamba...."

Hapo juu unauliza huna uhakika kama huu ushahidi ni wa ukweli au wa uongo, Sasa kilichokufanya uandike kesi imemkalia vibaya mbowe ninini? Acha unafiki!
 
Mbowe kishakaangwa na watu wake ambao walipokuwa ndani yeye akiwa nje aliwatelekeza kumbe walishaga toa ushahidi mzuri tu juu yake sasa mambo hazarani maovu ya mbowe yanajulikana sasa waliokuwa wanamuona kama malaika hakosei waanze kufumba midomo yao wa kwanza erythrocyte
Acha mihemko, mmeshikilia mtuhumiwa muda wote huo, mmekamata moshi mkampeleka mpaka Dar, halafu baadae mnakuja na ushahidi wa maneno yaliyoandikwa eti ndio maelezo aliyotoa mtuhumiwa.

Ninini hasa kitatufanya tuamini huo ushahidi ni kweli umetolewa na mtuhumiwa? na Je hajateswa na kulazimishwa kusaini hayo maelezo?

Mawakili wanawauliza maswali ya msingi, lakini kwa uzuzu wenu mmeshindwa kuelewa lengo la maswali hayo, kwa mwenendo wa kesi nzima, mbowe alitakiwa kuwa mshtakiwa namba moja, je ni kwanini si mshtakiwa namba moja?

Mnadai hamkumkakata sababu upelelezi juu yake ulikuwa haujakamilika, je upelelezi juu ya hawa wengine ulikamilika lini hadi wakakamatwa? Na kama upelelezi juu ya watuhumiwa watatu ilikuwa umekamilika, huyu mliyemuacha nje anazurura hadi anaenda nje ya nchi ni upelelezi wa aina gani mlikuwa mnaufanya juu yake, ambapo matokeo ya upelelezi huo ni yapi (ushahidi) yakawafanya mumkamate? Eleweni maswali ya mawakili yanalenga kutoa picha gani.

Kama maswali hayo ni magumu achana nayo usinijibu kimihemko na hoja za kiuvccm.
 
Mbona mnahaha sana? Huyu ndiyo kwanza shahidi wa 1 upande wa serikali, kuna wengine 19 wanakuja, subirini!!
Sasa kama shahidi wa kwanza anayetarajiwa kupigilia msumari katika kesi ushahidi wake ni huo wa kakipande cha karatasi, amekiri kabisa hana Fingerprints, wala DNA, hao mashahidi wengine 18 watakuja na vielelezi gani kama sio kutupotezea muda tu?

Pelekeni kesi haraka mtoe hukumu acheni kutupotezea muda. Mpelelezi mwaka mzima unakuja na kielelezo hiki kama ushahidi? oneni aibu!
 
Back
Top Bottom