Chadema nyie mliachwa mkaota mapembe eenhe. Mtoto mtukutu akiachwa akakuwa bila kupunguzwa makali anajihisi na yeye ni baba
 
Dah,huyu Kibatala atamuua Kingai kwa maswali magumu hadi jamaa anapaniki.

Hakuna kesi hapo hata huyo jaji kama ni zoefu atakuwa ameanza kuandaa hukumu hata kabla kesi haijaisha maana anajia kabisa kesi ni ya kupikwa.
 
Yaani unapoteza mudakwa hizo hasirazako hapo hakuna aliyelazimishwa wale walishatoswa na mbowe wakaamua kuusema ukweli kwa maelezo yao polisi baadae mkawalisha maneno waseme waliteswa ndipo kibatala wakili njaa akafungua kesi ndogo ambayo nayo imekama maana ni janja janja tu ili kuwanasua na uhalifuwao unajisumbua tu najuwa unaakili ila kama huna akili endelea kubisha mwisho wa siku nimiaka mingi sana jela wacha tuka mlisi mkewake maana alitaka kuangamiza taifa
kwa namna ulivyoandika maneno ni rahisi mno kujua kiwango cha elimu ulichonacho
 
Hii kesi inaidhalilisha nchi,kama makomandoo 3 wenye bastola1,madawa ya kulevya pamoja na uwezo wa kuzuia magari kwa kupanga miti barabarani wanaweza wakafanya ugaidi na kuwashinda polisi pamoja na jeshi la nchi lenye makomandoo lukuki pamoja na silaha nzito za kivita, basi tutegemee kuwa kuna siku nchi itapigwa na sungusungu wanaotumia mishale na mikuki.
 
Tayari baadhi ya Wadau wa Maendeleo, akiwemo Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada wamewasili Mahakamani.


Hadi saa 3:30 asubuhi hii Watuhumiwa walikuwa bado hawajaletwa Mahakamani.

====

Hatimaye Mbowe na wenzake wameletwa Mahakamani

Jaji Joachim Tiganga ameingia Mahakamani

Wakili wa serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
6. Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo Lake
1. Peter kibatala
2. Jeremiah Mtobesya
3. Michael Mwangasa
4. Nashon Nkungu
5. Dickson Matata
6. Alex Massaba
7. Jonathan Mndeme
8. Hadija Aron 9.
Idd Msawanga

Jaji anaomba Kuwaona Washitakiwa wote 1,2,3 na 4

Wanainuka Kwa kutajwa kwa Namba

Wakili wa Serikali anaomba kesi Kuendelea na Shahidi yupo tayari Lakini Kabla ya Kuendelea anaomba kufuatilia kuhusiana mabadiriko yaliyopalekea mpaka Mheshimiwa Jaji Kuja mwingine kwa mujibu ya kifungu cha 299 CPA (Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai).

JAJI: Upande wa utetezi

Peter Kibatala: hatotatumia Haki ya kumuita tena Shahidi kwa kesi Inayoendelea hapa.

Jaji anaandika.

JAJI: wote mnafahamu na mlikwepo siku ya tarehe 20 mwezi huu na Jaji aliyekuwepo alielekeza Jaji Mwingine atakuja kuendelea na Kesi hii, Na Jaji Mwingine Ndiyo Mimi, kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 Kifungu cha 299.

JAJI: Kwamba Upande wa Utetezi Mnahaki ya a Kumuita tena shahidi kwa kuwa Mmesema hamna nia nitawaruhusu Upande wa Jamhuri Kumuita sasa Shahidi wao tuweze Kuendelea. Mawakili wote Wanainuka ishara ya Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji na Kupokea Maelekezo ya Mahakama.

Wakili wa Serikali anatoka Kwenda Kumuita Shahidi wa leo.

Mahakama ipo Kimya

ACP KINGAI anaingia na Kupanda Kizimbani.

Robert Kidando Wakili wa Serikali anamtaarifu Jaji Kuwa Shahidi amefika.

JAJI: Majina yako Tafadhali

SHAHIDI: ACP Ramadhan Kingai

JAJI: Unakumbuka Uliwahi Kufika Mahakamani, ukaapishwa kutoa Ushahidi, Mahakama inakukumbusha Upo chini ya Kiapo hicho. SHAHIDI: sawa Mheshimiwa

JAJI: Mtakumbuka Mawakili kuwa Siku ya Tarehe 20 Jaji alipokea Kielelezo, baada ya Kupokelewa Kinatakiwa Kusomwa Mahakamani. Naomba Kuanzia hapo Shahidi akabidhiwe Kielelezo aweze Kusoma Kielelezo.

WAKILI WA SERIKALI: Soma Sasa Kielelezo Kuanzia kurasa ya kwanza.

SHAHIDI: Adama Kasekwa anaishi Chalinze Maelezo ya Onyo Chini kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20. MIMI kingai nakuonya wewe Adam Kasekwa

SHAHIDI: Ulazimishwi kusema lolote Pia unaweza Kualika Ndugu, Jamaa au Mwanasheria Kushuhudia utoajo wako Maelezo. Mtuhumiwa akasaini na Mimi nikasaini.

MAJIBU YA ONYO

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo..

MIMI Adam Kasekwa anaonya na Kingai Chini ya Kifungu cha 24 cha Sheria Mwenendo wa Makosa ya Jinai Silazimishwi na yoyote Kutoa Maelezo yangu. Je, Upo tayari Kutoa Maelezo Yako.

Jibu, Ndiyo Nipo tayari.

Shahidi anasoma kielelezo: Maelezo yamechukuliwa Katika Ofisi ya RCO ilala MIMI Adam Kasekwa Nimezaliwa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Ileje... Mwaka 2011 nilijiunga na Recruting Maktopora. Nikachaguliwa Kujiung na Mafunzo Ukomando 92KJ.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Mwaka 2014 niliteukiwa kwenda kituo cha Msangani Kujifunza ulinzi, amani na nikachaguliwa Kwenda DR Congo. Mwaka 2017 nilimaliza Mkataba na kurejea Nilipata malipo na Kumuoa Mke wangu Lilian ambaye naishi naye Mpaka Leo.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Nimepata naye Mtoto Mmoja. Nilirudi nikaa Miezi 6 kazini Nikaugua Ugonjwa wa aKili Nikaachishwa kazi na kulipwa mafao ya Millioni 4 na Laki 6.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Je unamfahamu Luteni Denis? Ndiyo, nilikuwa Mkinga Mawasiliano hayapatikani. Niliporudi nikaambiwa mwenzangu ananitafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Niliporudi nyumbani nilimpigia Simu Mwenzangu Mohammed Ling'wenya Kwamba Kuna kazi ya VIP protection. Akaniambia inabidi twende Morogoro Kumuona Luteni Urio. Tulipoenda akatuambia Kuna kazi ya VIP protection ya kumlinda Freeman Mbowe

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatupatia TSh 21,000 nauli ya Kwenda Moshi. Siku hiyo hiyo tulirudi Chalinze na kuanza Safari ya kwenda Moshi Tulipokelewa na Dereva wake anayeitwa Willy Alitupokea na Pick Up Nyeupe yenye maandishi ya M4C.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tukaenda Mpaka Kwenye Hotel Ya Mheshimiwa Mbowe Huko tulimkuta Khalfani Bwire aliyetutambulisha kwa Mbowe, "Mkuu wale Vijana tuliowaagiza ndiyo hawa hapa." MBOWE akatueleza Kuwa Sabaya anamvuruga sana na anamvuruga wapiga Kura.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba anawatisha Wapiga kura wake kiasi cha Kuhatarisha Kurudi kwake. Na kwamba, akatuelekeza tumdhuru Kwa Njia yoyote. Akatuelekeza Maeneo yake ya Moshi na Arusha.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Tulipanga kumdhuru kwa Spray Spray ya sumu alitafuta Mohammed Ling'wenya

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Siku inayofuata tulikuwa Mimi na Mohammed na wanachana wawili siwakumbuki Majina Baada ya Kufika Dar es Salaam Tulimfikisha Mheshimiwa Mbowe Nyumbani

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Akatukabidhi TSh Laki 2 kwaaajili ya Kununua Nguo. Kwa sababu Kesho yake tulikuwa tunampokea Mheshimiwa Lissu. Na Siku ya tarehe 27 Julai Mbowe alitutumia Kila moja TSh 78 Elfu ya Nauli Ya Kwenda Moshi.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: SIKU ya Tarehe 01 August Tulienda Moshi Tukamkuta Mbowe akiwa na Khalfani Bwire Akatuelekeza Kuwa tufanye ile kazi yake Haraka Akatuelekeza Maeneo anayokaa Sabaya kama vile Milestone PIA Akatuelekeza Tuje DSM, Kuchoma Vituo Vya Mafuta.

Shahidi anaendelea kusoma kielelezo: Kwamba yeye anatachochea maandamano ILi Serikali ionekane Imeshindwa Kuandaa Uchaguzi. Tulienda Maeneo ya Boma Ng'ombe Njia ya kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kumfuatilia.

Siku ya terehe 03 tulienda Maeneo ya RAU madukani kwa ajili ya kubana Matumizi. Kwa sababu Mheshimiwa alituachia Pesa Laki Moja na Nusu kwa ajili ya kukaa, isingetosha. Tulienda Kukaa kwa Dada yake kukaa kwaajili ya Kubana Matumizi.

Swala la Kupanga Ugaidi ni la kweli Na swala la a kukutwa na Silaha ni la kweli Wakati Polisi wananikamata pia walinikuta na Heroine Baada ya kuchukua Vitu hivyo Askari walisaini na Mimi nikasaini na Polisi walichukua Vitu hivyo kwenda Central

Baada ya Maelezo hayo Adam Kasekwa akasaini Na Mimi Kingai nikasaini Baada ya Kuchukua Maelezo hayo Muda ulikuwa ni saaa tatu.

Wakili wa Serikali: ACP Kingai Kutokana na Maelezo uliyoyasoma hapa mahakamani Yeye alikuelza nini Kutokana na Maelezo Uliyoyasoma Mahakamani Shahidi: alikiri kuwa anamfahamu Luteni Urio. Alikiri Kupewa Maelekezo ya kazi kutoka kwa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Alikiri Pia alipewa Maelekezo ya kazi Kutoka akwa Mbowe Kupitia Kwa Luteni Deni Urio. Alikiri Pia kuwapo Moshi tarehe 24 Mwezi wa 07, 2020

Shahidi: Alikiri Pia kuwapo Moshi na wenzake Mohammed Ling'wenya na Mwenzake aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe. Baada ya Ufutailiaji tukamfahamu ni Moses Lijenje. Alikiri Pia kufanya Mkutano yeye na wenzake wanne.

Yeye Mwenyewe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya, Moses Lijenje (Aliyemtaja Kwa Jina la Kakobe) Khalfani Bwire na Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: kwa Mujibu wa Mkutano huo nini kiliendelea. Shahidi: Mbowe alitoa Maelezo kuwa Sabaya anamfanyia Vurugu, (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai)

Wakili wa Serikali: kitu gani Kingine alikueleza Shahidi: Mtuhumiwa alikiri Kupewa Pesa 150,000/= kukidhi Mahitaji kipindi watakapokuwa hapo Moshi.

Wakili wa Serikali: tueleze Shahidi kuhusiana na kilichofuata Shahidi: Alikiri Kuwa Siku ya Tarehe 01 Mwezi wa Nane saa 11 Alfajiri kabla ya Safari ya Kuja DAR ES SALAAM Aliwaelekeza wamdhuru Ole Sabaya.

Shahidi: Akawaonyesha Picha ya Ole Sabaya Kupitia Simu yake ya mkononi Aliwapa Maelekezo Kufanya kazi hiyo na Kwamba baada ya hapo atawataka warudi Dar es Salaam. Alipanga kuwapa kazi ya kwenda Kulipua Vituo Vya Mafuta. Alipanga kufanya Vurugu kwenye masoko.

Mtobesya: OBJECTION Naomba Shahidi ajielekeze Kwenye kikichoandikwa kwenye Statement Mambo ya Kituo cha Mafuta na Masoko havijatajwa.

Jaji: Kwahiyo a some?

Mtobesya: ajielekeze kikichoandikwa hata kama ana Rudia Kuelezea, Sheria inasema Statement itajielezea Yenyewe.

JAJI: Upande wa Mashitaka

Wakili wa Serikali: Sahihi Mheshimiwa tutarekebisha.

Wakili wa Serikali: Alikueleza Lengo ilikuwa ni nini

Shahidi: Lengo ni Serikal ionekane imefeli Alikiri Pia kukamatwa na Polisi Siku ya tarehe 05 Mwezi wa 08, 2020 akiwa Rau Madukani.

Alikiri Pia kukamatwa na Pistol aina ya Ruvern ikiwa na Risasi 03.

Shahidi ACP KINGAI: Alikiri kukamatwa na Kete 58 za Madawa aina ya Heroine.

Wakili wa Serikali: baada ya kuwa umeandika Maelezo hayo, yeye ulimpeleka wapi kwa Siku hiyo.

Shahidi ACP KINGAI: ilikuwa Siku ya tarehe 07 Mwezi wa 08, 2020 nilimrudisha Mahabusu.

Wakili wa Serikali: Shughuli gani Nyingine ili endelea baada ya Shughuli hii

Shahidi ACP KINGAI: tuliendelea na Upelelezi ya Kuwatafuta watuhumiwa wengine. Maeneo ya Chang'ombe tulimkamata Khalfani Bwire.

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma Gani

Shahidi ACP KINGAI: Kwa tuhuma hizi hizi za Kula Njama kutenda Matendo ya Ugaidi.

Wakili wa Serikali: nini kiliendelea

Shahidi ACP KINGAI: nikimtaka Khalfani Bwire aandike Maelezo yake

Wakili wa Serikali: elezea Kuhusu Kumkamata kwake

Shahidi ACP KINGAI: baada ya a kuwasiliana na Askari aliyekuwa kwenye Pointi akiwa kwenye gari, tukielekeza Gari iingie Kituo cha polisi Chang'ombe. Tukawa tumeingia pale na Inspector Mahita na ASP Jumamne.

Jaji: ASP nani? Shahidi: Jumanne

Wakili wa Serikali: baada ya Kumkamata Mlimpeleka wapi

Shahidi: tuliekeza Superitendent Lukangira wa hapo hapo Chang'ombe. Hii ni baada ya Mtuhumiwa kutuelekeza hana Makazi hapa Dar es Salaam ni Mkazi wa Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Nia ya Kuuliza kwake ni wapi ilikuwa ni ya nini

Shahidi: nia ilikuwa kufanikisha Shughuli za kiupepelezi

Wakili wa Serikali: baada ya Lukagingira kuandika Maelezo yake nini Kilifuata

Shahidi: Tukawa tunaendelea Kufuatilia Makazi yake, Tofauti na Taarifa alivyokuwa ametoa yeye kwakuwa tulijua haiwezekani awe kila Siku anaenda Ngerengere.

Wakili wa Serikali: Wakati Unapata Taarifa ana makazi Wilaya ya Temeke, elezea Sasa Maelezo yalikuwa yanaandikiwa wapi

Shahidi: Maelezo yalikuwa yanachukuliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe na Mimi niliweka Bass Central polisi (Ilala).

Wakili wa Serikali: baada ya Kutoa Maelekezo Hatua Kuchukua Maelezo Isimame, nini kilifuata

Shahidi: tulipata Taarifa Mtuhumiwa anakaa Temeke Makangarawe, Tuliungana na Detective John wa Temeke na RCO kwa ajili ya kwenda Kumpekua Makazi yake.

Wakili wa Serikali: Mlienda sehemu ipi haswa huko Mkangarawe

Shahidi: Ule Mtaa Jina Limenitoka

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kuutambua sasa

Shahidi: tukielekezwa na Watu hadi Nyumba alipokuwa amepanga Mtuhumiwa.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa hiyo Shughuli ilifanyikaje na Khalfani Bwire alikuwa wapi.

Shahidi: Tuliongozana na Mtuhumiwa, Tukamtafuta Mwenyekiti wa Ule mtaa, Tukamkuta na Mwenye nyumba aliyempangisha Khalfani Bwire na hata Mke wake alikwepo.

Wakili wa Serikali: huyu Mwenyekiti ni wanini?

Shahidi: Ni Mwenyekiti wa Mtaa

Wakili wa Serikali: Nini Kilifuata

Shahidi: Nilimuelekeza ASP Jumanne Kwa Kushirikiana na Detective John Kutoka Ofisi ya RCO Temeke na kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mtaa na hata Mke wake.

Wakili wa Serikali: Elezea sasa Katika Upekuzi huo Mlikuta nini?

Shahidi: Vitu mbalimbali vilipatikana kama Uniforms za JWTZ, Masharti ya JWTZ, Tshirt za JWZT, name tags za kwake za JWTZ.

Wakili wa Serikali: baada ya Kupata Uniforms na Vifaa Mbalimbali nini Kilifanyika baada ya Kupata Vitu hivyo.

Shahidi: Viliorodheshwa katika Hati ya Uchukuaji Mali. Wakati wa Upekuzi tulikuta Kidaftari kilichokuwa na Ramani na Majina ya Vituo Vya Mafuta.

Wakili wa Serikali: baada ya kuorodhesha kitu gani kilifanyika

Shahidi: baada ya Kuwa Viliorodheshwa yaliandikwa Majina ya walioshuhudia Upekuzi huo. Pia wakasaini Hati ya Uchukuaji Mali. Mtuhumiwa pia alisaini Hati ya Uchukuaji Mali na aliyepekua alisaini Hati hiyo.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Hati ya Uchukuaji Mali, Kitu gani Kiliendelea

Shahidi: Nilikuwa nimeelekeza Mashahidi walioshuhudia waandikwe Maelezo pale pale

Wakili wa Serikali: baada ya Kukamilisha

Shahidi: Tulichukua Vitu tulivyo orodhesha na Mtuhumiwa akarudishwa a kituo Cha Polisi.

Wakili wa Serikali: Kituo gani cha Polisi Shahidi: Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Baada ya kumrudisha Kituo cha Polisi Chang'ombe Kitu gani pia Kiliendelea.

Shahidi: Mtuhumiwa tulimkamata na Kidaftari chenye Ramani ya Vituo Vya Mafuta Dar es salaam, Soko la Kilombero Arusha.

Tukachukua Sampuli za Miandiko ya Watuhumiwa wote. Lakini pia tuliendelea na hatua ya kuwatafuta watuhumiwa wengine

Wakili wa Serikali: watuhumiwa gani wengine Mlikuwa mnawatafuta

Shahidi: Watuhumiwa wengine tuliokuwa tunawafutilia ni Mtu alikuwa anaitwa Gabriel, Lijenje, Malima, Khalid na Jamaa Mmoja anaitwa Kaaya.

Wakili wa Serikali: nini hatima ya hao mliokuwa mnawafuatilia

Shahidi: Ukimuondoa Mtu Mmoja anaitwa Malima, Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani.

Wakili wa Serikali: vipi kuhusu moses Lijenje Shahidi: bado hatujafanikiwa Kumpata

Wakili wa Serikali: Hapa Mahakamani kuna Washitakiwa Wanne inakuwa je hao wengine hawapo Mahakamani kama Walifumgukiwa Mashitaka

Shahidi: walifutiwa Mashitaka baada ya Kuonekana Ushahidi hakuwa wakutosha ukilinganisha na wenzao.

Wakili wa Serikali: ACP kingai katika Ushahidi wako tangu Mwanzoni umezungumzia kukamatwa Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Khalfani Bwire Vipi ukamatwaji wake Mshitakiwa wa Nne.

Shahidi: Freeman Mbowe alikamatwa 21 July 2020 akiwa Mwanza

Wakili wa Serikali: Kwa tuhuma gani

Shahidi: Kwa tuhuma hizi hizi

Wakili wa Serikali: Wakati Unatoa Ushahidi wako Ulizungumzia kukamatwa hawa wengine Mwaka 2020 na huyu 2021 elezea Ilikuwa je hapa Mahakamani.

Shahidi: Tulikuwa tunajirishisha haswa uhusika wake. Tulikuwa bado tunaendelea Kufuatilia mawasiliano Na Uchunguzi wa Forensic ambao ulikuwa unahusiana na Shauri hili

Wakili wa Serikali: Sababu ukamataji ulifanyika 21 July Mwaka 2020, ni lini taarifa zilifahamika rasmi.

Shahidi: Zilifahamika Mwanzoni July 2020

Wakili wa Serikali: wakati anakamatwa Upelelezi ulikuwa umefikia Hatua gani

Shahidi: Upelelezi wetu kwa muda huo tunamkamata ulikuwa umekamilika.

Wakili wa Serikali: Upelelezi wa aina gani ulikuwa unaendelea kwa Mshitakiwa nne

Shahidi: Tulifanya Forensic na Divices za Kieletronic tuliokuwa tunafuatilia Kujiridhisha dhidi yake na Tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Wakili wa Serikali: wakati Unatoa Ushahidi wako Mwanzoni ulisema Ulielezea Kuwa Umelekeza kufungua Jalada la Tuhuma za Kigaidi.

Shahidi: Kulingana na Taarifa ambazo tulikuwa tumezipata kwa Luteni Urio na aina Ya Vitendo vilivyokuwa Vimepangwa na Watuhumiwa Ilikuwa ni Kudhuru Viongozi wa Serikali, kufanya Vurugu sehemu zenye watu wengi, Kulipua Vituo Vya Mafuta, Hata Miti kwenye highway kukatwa Kuzuiwa Magari yasipite, Hasa katika Barabara ya Morogoro kwenda Iringa.

Wakili wa Serikali: Ukatafsiri ni Vitendo gani

Shahidi: Vitendo vyenye kuleta hofu kwa Wanachi Kujiona hawapo salama, Ni Vitendo vinavyoleta Tafsiri la Shitaka la Ugaidi

Wakili wa Serikali: ulisema katika Taarifa ya Luteni Urio ulisema walipanga Kuonyesha kuwa Nchi haitawaliki.

Mtobesya: OBJECTION kaka yangu Wakili Msomi ajielekeze Kwenye fact siyo Opinion Maana huyo ni Shahidi wa Fact, He is doing too Much Sasa Maana Mwanzo tulijua ameteleza.

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji nitaomba nijielekeze sawa Sasa.

Wakili wa serikali: Vitendo hivi vilipangwa Vifanyike wapi

Shahidi: Mwanza, Moshi, Dar es Salaam na Arusha

Wakili wa Serikali: Vilikuwa Vifanyike Lini

Shahidi: Kabla ya Uchaguzi wa Mwaka Jana

Wakili wa Serikali: ni hayo tu Kwa sasa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Upande wa utetezi

Mtobesya: Asante Mheshimiwa Jaji nitaomba niendelee kwa Niaba ya Mshitakiwa wa kwanza.

Mtobesya: ni sahihi Shahidi wewe ulikuwa ni sehemu ya waliokuwa wanahusika na upelelezi wa Kesi hii

Shahidi: ni sahihi

Mtobesya: ni sahihi kuwa Baada ya kupokea Maelezo kwa DCI BOAZI mkafungua Jalada

Shahidi: Ni sahihi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni lini Mlifungua Jalada

Shahidi: Yalikuwa Majalada Mawili la upelelezi na Kesi

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Lilifunguliwa Jalada la Uchunguzi

Mtobesya: Uchunguzi au Upelelezi

Shahidi: yote ni yale yele labda useme unataka Jalada gani

Mtobesya: wewe Ndiye unayetoa Ushahidi

Shahidi: Sawa Mwanzo Lilifumguliwa Jalada la Uchunguzi wa Kula njama. Ilikuwa July Mwaka Jana.

Mtobesya: yote Mawili Mlifungua kwa Pamoja au Tofauti

Shahidi: Kuna Utaratibu wa Kiupelelezi labda kwa sababu ujawa mpelelezi Ndiyo Maana Unahangaika Kuna Jalada la Awali la Uchunguzi lakini unapopata Taarifa unafungua Jalada la Kesi ya kula njama Lilifunguliwa na Mkaguzi wa Polisi Msaidizi anaitwa Swila

MTOBESYA: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kabla hamjawakamata Watuhumiwa Mlikuwa mmekusanya Taarifa zipi kwa wakati huo

Shahidi: Taarifa za kutaka kuwadhuru Viongozi wa Serikali, Kufanya Maandamano ya siyo na Kikomo, Taarifa za Kukata Miti na Kufanya Uporaji Magari yasipite na Kutaka Nchi isitawarike

MTOBESYA: kwa hiyo hizo Taarifa ndiyo zilitengeneza Kosa la Kula Njama

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji hizo Taarifa Mlizipata kabla au Baada ya Kumchukua Maelezo Mshitakiwa wa Pili

Shahidi: Kabla

MTOBESYA: kabla ya Kesi Ndogo unakumbuka ulisema Urio aliwapatia Taarifa kuwa Vijana wamepatikana, Unakumbuka ulisema tarehe Ngapi.

Shahidi: Ilikuwa tarehe 04 Mwezi wa Saba Mwaka Jana

MTOBESYA: wakati unaelezea (Kusoma) unakumbuka Kielelezo ulipata wasaa wakujua Urio alishiriki Vipi katika swala hili?

Shahidi: sijaelewa Vizuri

MTOBESYA: Statement hii ambayo unasema uliandika unakumbuka Urio alishiriki namna gani?

Shahidi: naomba Jaji anisomee anapoparejea

Jaji: labda tuweke, Ushiriki wa urio ulikuwa Vipi

Shahidi: Urio ameshiriki kwa kuwatafuta Vijana, ameshiriki kuwapatia nauli na ameshiriki Kutafuta Vijana waliofukuzwa Jeshi

Mtobesya: Umesema kwenye Maelezo alifanya hayo Tarehe ngapi

Shahidi: Sikumbuki tarehe

MTOBESYA: sasa nije kwenye Maelezo uliyoyachukua, kwa ajili ya Kumbukumbu Unakubaliana na Mimi Kuwa kuna namna tatu za Kuchukuliwa Maelezo. moja, Kwa Anateyetaka Kuchukuliwa Maelezo kuomba Karatasi na kalamu na kuandika Mwenyewe. Pili, kwa anayehojiwa kuongozwa Tatu, kwa njia ya Maswali na Majibu Wewe ukichagua Njia gani?

Shahidi: Mimi nilitumia Maswali na Majibu

Mtobesya: naomba niishie hapa

Wakili Malya: naomba Kielelezo (Statement) Mahakama inampatia John Malya

Wakili Malya: Unasimu ya mkononi

Shahidi: Ndiyo

Wakili Malya: unaweza kututajia EMEI namba ya Simu yako

Shahidi: Hapana Siwezi

Wakili Malya: kwanini..?

Shahidi: Sijaamua kuishika

Wakili Malya: Una ya mtu yoyote wa Karibu yako unayoikumbuka

Shahidi: Hapana

Wakili Malya: sasa Katika maelezo Adam alikutajia EMEI namba Kutoka wapi

Shahidi: Alikuwa na kikaratasi

Wakili Malya: Ulizungumza kwamba Mshtakiwa alikuwa na kikaratasi?

Shahidi: Sikuzungumza

Wakili Malya: ni sahihi unapoandika Maelezo unaandika kwa usahihi kabisa

Shahidi: Sahihi Kabisa

Wakili Malya: kwa uelewa wako Unapotaja Sheria, kwa Mbele Mwaka Unatajwa, Maana ya Kuwa na Miaka katika Sheria.

Shahidi: Mimi siyo Mwanasheria

Wakili Malya: Nafahamu wewe siyo Mwanasheria ila Umeandika Mwenyewe Vifungu Vya Sheria ili Mtu ajue Haki yake

Shahidi: Ndiyo nafahamu. Sasa Unatoa somo

Wakili Malya: Kwa hiyo wewe Unaweza kuandika Mwaka wowote tu.

Shahidi: am not aware of It

Wakili Malya: kwa hiyo wewe Unaweza Kuandika Sheria na Mwaka ukaweka Wowote tu

Shahidi: Hapana naweka na Sheria

Wakili Malya: na Mwaka kama imefanyika amendment Zake? Sasa Kwa Maelezo hayo uliyoyashika Tusomee hapa.

Shahidi: Cap 20 REV 2018

Wakili Malya: sasa hiyo Sheria Hakuna. Wewe umechukua Maelezo ya Onyo kwa Sheria ambayo haipo, Unasemaje kwa hilo

Shahidi: Hiyo ni Typing Error kwa sababu imechapwa. Ile niliyoandika kwa Mkono wangu huenda sikuandika hivi.

WAKILI mallya: wakati unaisoma hapa Mahakamani Ulisema hapa kwamba hii siyo au ulikariri ukawa unaisoma tu Hapa

Shahidi: kwenye eneo hili Onyo Chini ya Kifungu Cap Rev 2002 badala Ya kusomeka 2018.

Wakili Malya: kwa hiyo ulipaswa Kusomeka Vinginevyo siyo hiyo

Shahidi: Ndiyo

MALYA: ushawahi Kusikia Kiongozi wa Polisi Liberatus Barrow aliuwawa

Shahidi: Ndiyo Wakili Malya: aliuwawa?

Shahidi: Ndiyo WAKILI

Mallya: waliomuua Walikamatwa Ndiyo

Shahidi: Ndiyo

WAKILI mallya: walishitakiwa na Makosa gani?

SHAHIDI: mauaji

WAKILI mallya: Lakini Kumdhuru Sabaya ni Ugaidi?

Shahidi: kuleta Vurugu kwenye Masoko, Kukata Miti Barabara, Kuzia Magari yasipite ni Vitendo vingeleta hofu na Wasiwasi Vitendo hivi Vinaashiria ni Vitendo Vya Ugaidi.

Wakili Mallya: umerudi Viongozi sana Ukimtoa lengai Ole Sabaya Kiongozi Mwingine nani..?

Shahidi: ni Maelezo ya Adam Kasekwa, Siyo ya kwangu

Wakili Mallya: ulipomkamatia Adamoo Moshi na Kilichokufanya usichukue Maelezo Moshi ni sababu zipi

Shahidi: Sababu za Kiupelelezi

Mallya: wakati Unatoka Moshi ulipitia Njia ipi ya Chalinze au Bagamoyo

Shahidi: Msata

Mallya: ulitoka Msata kwenda Central Njia kuna Mbweni na Oysterbay kwanini uliamua kwenda Central

Shahidi: Sababu za Maelezo na Pili Ndipo kesi ilipofunguliwa

Wakili Mallya: Wewe kwa sasa ni RPC KINONDONI Je unafahamu kuwa Kinondoni inajitegemea

Shahidi: Ndiyo, zikiwa Chini ya Kanda Maalum Dar es Salaam

Wakili Mallya: ulieza Mahakama Kwanini Huyu achukuliwe Maelezo Temeke Mkoa Mwingine wa Kipolisi na kwanini hakusafirishwa kama wenzie kuja Mkoa wa Ilala

Shahidi: Hapana sikueleza

Wakili Mallya: umesema Yalifunguliwa Majalada mawili

Shahidi: Ndiyo

Wakili Mallya: nani alifungua hayo Majalada Shahidi: Inspector swila

Wakili Mallya: Umemtaja Sabaya, Alikuwa Mkuu wa Wilaya wa wapi Vile?

Shahidi: Hai

Wakili Mallya: je pale Hai Pana Ofisi ya Mkuu wa upelelezi?

Shahidi: Ndiyo

WAKILI: mallya Je Kilimanjaro Kuna Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Mallya: Ni hayo tu

JAJI: naomba Tubreak Kwa Lisa limoja Tutarudi hapa Saa 7 na Dakika 20

Jaji anatoka

Mpaka sasa saa saba na nusu, Jaji hajaingia.

Mahakama imerejea

Wakili Robert Kidando anaomba Kumtambulisha Wakili Nasorro Katuga

Jaji: nilipo Break tulikuwa tumemaliza Maswali ya Dodoso ya Wakili wa Mshitakiwa wa Pili, Nipo sahihi..? Wawakili wa Pande zote Mbili wanaitikia, NDIYO

Jaji: namruhusu Wakili wa Mshtakiwa wa tatu aendelee,

WAKILI MATATA

Matata: Shahidi Ni sahihi kwamba Maagizo ya Kushughulika na Kesi hii ulipewa na DCI

Shahidi: Ndiyo

Matata: Ni kweli kwamba Urio ndiye aliyekupa Taarifa kuwa kuna Makomandoo amewatafuta kuwapeleka kwa Mbowe, kusaidizana naye kutenda Uhalifu. Shahidi: Kweli

Matata: Urio huyo huyo ndiye alikupa Taarifa kwamba alikuwa anatoa fedha za Kuwawezesha Makomandoo

Shahidi: Ndiyo

MATATA: na Ukasema Mambo hayo yote yangefanyika Mwaka Jana Kuanzia Mwezi wa Saba.

MATATA: nitakosea Nikisema Mbowe Kuwapa Fedha Makomandoo Yalifanyika Mwaka Jana

Shahidi: Kweli

Matata: Utakubaliana na Mimi Mbowe amekamatiwa Mwaka huu Mwezi wa Saba Shahidi: Kweli

Shahidi: Ndiyo

Matata: amekamatwa akiwa Mwanza

Shahidi: Ndiyo

MATATA: Mbowe alishiriki Uchaguzi Mwaka Jana akigombea Jimbo la Hai?

Shahidi: Kweli

Matata: Kwa Nyakati tofauti Mbowe amekuwa nchini

Shahidi: Kweli

Matata: Leo Umeeleza Mahakama Kwamba hamkumkamata kwa sababu mlikuwa Mnafanya Upelelezi na Uchunguzi wa Ki-Forensic

Shahidi: Kweli

MATATA: Utakubaliana na Mimi kwamba huo Uchunguzi Umeisha lini

Shahidi: Nimeeleza Mahakama

MATATA: Utakubaliana na Mimi Kwamba huo Uchunguzi wa Kiforensic Ulikuwa Unahusu nini

Shahidi: nimeeleza

Matata: Wakati unahojiwa na Wakili umeeleza huo Uchunguzi wa Kiforensic ulihusisha nini

Shahidi: Nilieleza Kwamba ni Vifaa Vya Electronics

MATATA: nikisema Mbowe Mmemkamata Mwanza 21 July 2020 kwa sababu ya kutaka Kufanya Kongamano la Katiba nitakuwa Nimekosea

Shahidi: Si kweli, Utakuwa Umekosea

MATATA: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu

Jaji: Wakili wa Mshtakiwa wa Nne

Peter Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Shahidi Katika Statement Uliyosoma kuna Mambo yanamgusa Mshtakiwa wa Nne

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwanini huwa tunataka Kifungu Mahususi kinacho mpa Haki zake Mshitakiwa katika Caution Statement.?

Shahidi: Ni takwa la Kisheria

Kibatala: kwa hiyo unafahamu kuwa kuna matakwa yake ili zoezi likamilike kuwa la Kisheria

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu Kuwa unapokosea Kifungu cha Sheria Jambo Lote linakufa.

Shahidi: Inategemea

Kibatala: Ukikosea Sheria yenyewe?

Shahidi: inaweza kuwa Fatal

Kibatala: Sheria katika Kielelezo P1 imepatiwa au Imekosewa

Shahidi: slip of the pen

Kibatala: hiyo Slip of the pen Mpaka Mawakili wanakuongoza Kwa Mujibu wa "Oxygen Principle" kwamba turekebishe hata kwa pen

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Kuwa Kukiri Kwa Mshitakiwa kunapaswa Kuongozane na Vitu Vingine

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je umetaja hapa Mahakamani vielelezo gani Vingine kama vinaunga Mkono Kukiri Kwa Mshtakiwa wa Pili?

Shahidi: Maelezo yake

Kibatala: ndiyo hayo Maelezo Yanatakiwa yafungwe Mkono na Premises zingine tuorodhesheee

Shahidi: Maelezo ya Luteni Denis, Kuhusu Kukata Miti na Kutaka Kufanya Vurugu.

Kibatala: Umemueleza Jaji sehemu yoyote kwamba ulienda huko Morogoro Mpaka Iringa Kuona Miti iliyotakiwa kukatwa.?

Shahidi: Hapana Wala sijaenda

Kibatala: Umetaja Maandamano yalitakiwa kufanyika wapi hadi wapi

Shahidi: Hapana sijasema

Kibatala: Kuhusu Mwanza Pia Maandamano yalitakiwa yaanze Point gani hadi Point gani tarehe fulani?

Shahidi: Sijamwambia

Kibatala: Kuhusu Kilimanjaro ulitaja sehemu yoyote?

Shahidi: Hapana sijamwambia

Kibatala: Umemtaja Mheshimiwa Jaji Maandamano yalitakiwa kuanzia wapi hadi wapi na ajenda ya maandamano

Shahidi: nilisema ili Kuonekana Nchi haitawaliki

Kibatala: Kuna sehemu umemwambia Jaji tarehe ya Maandamano

Shahidi: Hapana

Kibatala: Umezungumzia kuwa alipanga kuwepo yeye personally

Shahidi: Sikusema

Kibatala: ulitaja Vituo vilivyotakiwa Kuchomwa

Shahidi: Ndiyo nilivitaja

Kibatala: ndiyo Mwambie Mheshimiwa Jaji ulitaja wapi na wapi

Shahidi: Nakumbuka nilitaja Big Bon Kariakoo, Big Bon Sinza na Total Morroco

Kibatala: Unakumbuka Upo Chino ya Kiapo, Maana kazi yangu ni Kuuliza Maswali swala la Uongo au La! wanajua watu wengine

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je baada ya planning Huko Moshi Je washitakiwa walifanikiwa Kuja Dar es Salaam Kuja kutekeleza hilo

Shahidi: Walikuwa Baada ya Kuwakamata

Kibatala: Nauliza Mshitakiwa wa Nne alitoa Maagizo Moshi akaja Dar es Salaam Kuja Kutekeleza hayo Maagizo

Shahidi: Dar es Salaam tuliwakamata kabla hawajatekeleza.

Kibatala: Mliwakamata na nini ambacho Mtu anaweza Kukihusisha na Ulipuaji wa Vituo Vya mafuta

Shahidi: kwa Upande wa Kuchoma Vituo Vya Mafuta sikuwakamata na Kitu chochote

Kibatala: Uliwakamata na Kifaa gani kinachohusisha Kukata Miti

Shahidi: Sikuwakamata na Kifaa chochote

Kibatala: Mshitakiwa wangu wa Nne ulimkamata na Kipeperushi cha Maandamano?

Shahidi: Hapana

Kibatala: we Polisi Mzoefu Miaka 18 ya Upelelezi Kazini, najua Siyo Mwanasheria ila Unasimamia Sheria je Unafahamu Mtu anapokiri anatakiwa kukiri Kila Kipengele anachoshitakiwa

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ulizungumza Chochote Kuhusu Mshitakiwa Mbowe kuwapo Morogoro kati ya Tarehe 1 May na 20 August 2020

Shahidi: Sikuzungumza

Kibatala: Ulizungumza Katika ya Tarehe 01¬May 2020 na 20 August 2020 kuwa washitakiwa watatu walikuwa Arusha

Shahidi: Ndiyo nilizungumza ila siyo Leo

Kibatala: kwa ufahamu wako kama Mpelelezi Mkuu umewahi Kugundua kuwa Freeman Mbowe na Watuhumiwa wenzake Mkoani Morogoro

Shahidi: na Mbowe Hapana

Kibatala: Waliwahi Kukutana Mkoa wa Arusha

Shahidi: Sijafahamu

KIBATALA: Waliwahi Kukutana Mkoani Dar es Salaam

Shahidi: walikuja Dar es Salaam, walikuwa Pamoja Tarehe 26 July 2020.

Kibatala: hayo yapo katika maelezo ya Kukiri uliyoyasoma?

Shahidi: Yapo Ndiyo

Kibatala: Naomba Mahakama nimkabidhi P1 anitafutie eneo hilo

Jaji: tutajie kurasa

Shahidi: "Kesho yake tulirudi Dar es Salaam, Tukiwa na Mheshimiwa Mbowe na wanachana Wengine ambao sikuwafahamu" That Means walikutana

Kibatala: Sitaki tafsiri yako, Tusomee ambao Mshtakiwa amesema walikutana

Jaji: nafikiri kuna sehemu hamkutani, nafikiri anatafsiri kuwa kuna Wakati walikuwa wote Dar es Salaam, We unamaanisha nini?

Kibatala: "Hati ya Mashitaka inasema walikuwa wamekaa Kikao, Nitafutie alipokiri kuwa walikaa Kikao"

Shahidi: hiyo specifically Kikao sikueleza

Kibatala: ooohhhh Sasa Umeelewa

Kibatala: Sheria inayounda Shitaka Unatakiwa kuitamka kikamilifu ili haki za Mshitakiwa ziwe zimekamilika, Unafahamu..?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je unafahamu sub section mbili zote zinazozungumzi hilo

Shahidi: hiyo ni Mpaka Niperuzi

Kibatala: aahhhhhh Sawa Ngoja nimpatie Sheria

JAJI: anacheka, Sasa atafahamu Vipi kuwa yenyewe

Kibatala: nawapa kwanza Kaka zangu Mawakili wa Serikali waithibitishe

Wakili wa Serikali: Ndiyo yenyewe

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Iwapo Maelezo ya Onyo ulitaja Kifungu cha Sheria cha Kwanza na Cha Pili (Subsection)

Shahidi: Subsection Sikutaja

Kibatala: Kwa ufahamu wako wewe Kutokutaja Subsection zinakuja zimeathirika au hazijaathirika

Shahidi: Hiyo ni Curable Irregularity

Kibatala: ulitoa ufafanuzi huo Kwa Jaji ili afanye hiyo CURE

Shahidi: sikutoa Kibatala: Hawa Washitakiwa 2 wanashitakiwa Kushiriki Vitendo, Mkutano wa Kuongea Vitendo Vya kigaidi Ndiyo Hati ya Mashitaka inavyosema.

Shahidi: Sahamani naomba Niione

Kibatala: Ooh Sawa hii hapa

Kimya Kinatawala Shahidi anasoma

Wakili wa Serikali: Sahamani Mheshimiwa Jaji na sisi kabla ajajibu tunaomba tuione

Kibatala: Ooohh sawa Mheshimiwa Jaji wanahaki hiyo

Wakili wa Serikali: Ndiyo yenyewe Mheshimiwa

Jaji Shahidi: Ndiyo yenyewe

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa Iwapo alishiriki Mkutano, Ugaidi ilikuwa sehemu ya Maelezo yako ya Onyo.

Shahidi: Nilimuonya kwa Vitendo

Kibatala: Ulimuonya kwa Meeting au hukuonya

Shahidi: Si Kumuonya

Kibatala: Terrorists Meeting ni Shitaka Namba ngapi

Shahidi: 4

Kibatala: Ndiyo ambalo hukumuonya Adamoo

Shahidi: Ndiyo sikumuonya

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulimuonya kwa Kupatikana na Mali

Shahidi: Kwa Vitendo Vya kigaidi

Kibatala: Twende Shitaka la Tano, kwa Kupatikana kwa hiyo Mali, Si bado tunakubaliana kuwa kunapaswa Kuungana na Mambo Mengine si Tuna kubaliana

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ulifanya Forensic ya DNA au Finger Prints kuwa ni Kweli ilikuwa Chini ya Umiliki wake

Shahidi: hapo unazungumzia kumilili..?

Kibatala: Ulizungumzia Kuhusu kwamba Umefanya Uchunguzi wa Finger Prints

Shahidi: Hapana Siku fanya Finger Prints

Kibatala: hii Kesi tangu ianze kuanzia kuwakamata na Muanze Upelelezi ni muda gani

Shahidi: Miezi 08

Kibatala: Kwa hiyo kwa Miezi 08 hamjawahi Kufanya Finger Prints

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa DNA ni Njia ya Kisasa Ya kuthibitisha Umiliki, na Jinai

SHAHIDI: ndiyo

KIBATALA: Umezungumzia Chochote Kuhusu DNA analysis

Shahidi: Hapana Mheshimiwa

Kibatala: Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Adamoo amepata wapi hii Bunduki

Shahidi: Adamoo hakusema

Kibatala: Nikiangalia Kielelezo Cha Mahojiano nitaona Hilo swali?

Shahidi: Hapana Nilimuuliza Kama Mimi tu

Kibatala: Wakati anakamatwa Adamoo alikwambia walikuwa na Moses Lijenje, Je alikwambia wakati wa Mahojiano ya Kisheria au Nje Ya Kisheria

Shahidi: kivipi

Kibatala: Uliipata baada ya Kumuhoji Adamoo..?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulimuhoji kwa mdomo AU kwa Maandishi

Shahidi: kwa Mdomo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwamba hilo kitendo cha Kumuhoji Adamoo hutakiwi Kukifanya kwa Mujibu wa Sheria

Shahidi: nilikuwa namuhoji Kupata upelelezi

Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwa Mujibu PGO ulipaswa kwanza Umpe haki zake Mshitakiwa wa 2 wakati Mpo Moshi

Shahidi: Usichanganye Vitu

Kibatala: Miye nakuhoji unachosema wewe, Kwamba Unakubaliana kuwa kuna Mahojiano Yalifanyika Moshi

Shahidi: Ndiyo nilifanya Mahojiano ya Mdomo

Kibatala: lakini Mliwasafirisha kutoka Moshi Kuja Dar es Salaam Kuja Kuwahoji.?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ilikuwa Muda gani

Shahidi: Muda uleule

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji pia kama Ulimuhoji Mohammed Ling'wenya Akiwa Moshi kuhusu Moses Lijenje

Shahidi: Ndiyo nilimuoji pia na Maelezo ni yaleyele

Kibatala: nimesikia kuwa Leo Umemtaja Kakobe kuwa ndiyo Moses Lijenje

Shahidi: kwa Maelezo yao Ndiyo WAMESEMA hivyo.

Kibatala: Shahidi nakukabidhi Maelezo hayo ya Kielelezo ya P1 kuwa Adamoo anasema KAKOBE ndiyo Moses Lijenje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sikumbuki kama niliandika

JAJI: Kibatala Umemwambia atumie muda Mwingi iwezekanavyo kutafuta hilo, nakukumbusha Muda ni wa Mahakama.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji samahani sana nilipigiwa, Kama ningekuwa mwangalifu ningesema Kwa Ruhusa ya Mahakama

Kibatala: Nitafutie sehemu katika Maelezo kuwa Mshitakiwa wa Pili amekiri Bastola ni ya kwake

Shahidi: Hakuna Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Nitafutie katika Maelezo ambayo Mshtakiwa amekiri kuwa Bastola hiyo alitaka kutumia kumdhuru Sabaya, Kutumia kwenye Maandamano au Kutumia Kukata Miti

Shahidi: Hilo Mheshimiwa Jajo hakuna

Kibatala: Nitafutie Mstari au haya yoyote ambayo Mshtakiwa wa pili anasema kuwa uniform za JWTZ walitaka kuzitumia kwa ajili ya Ugaidi

Shahidi: Hakuna kwa sababu Mshitakiwa sikumkuta na Uniforms

Shahidi: Uliza Maswali Sensible Bwana

Mawakili wa Utetezi Wote wananyanyuka

KIBATALA: No No No No Kaeni Mwacheni

Kibatala: Nataka Useme kama Kuna sehemu katika maelezo kuna sehemu umesema kuhusu Uniform

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nina Swali la Lijenje kijinga ila Nivumilie Je kuna sehemu kuna Maelezo ya Nyongeza? Kuhusu Kuchukua Sampuli za Miandiko

Shahidi: Hatukua na haja hiyo

Kibatala: Kwa hiyo Mshitakiwa wa Pili hakuna anapozungumza kuhusu Mwandiko

Shahidi: Hakuna

KIBATALA: Naona Umeokoa muda sasa

Kibatala: Iliwachukua muda gani Kuwashitaki wakina Malima Mpaka Mkagundua kuwa hapakuwa na Ushahidi wa kutosha.

Shahidi: Tuliwashitaki Mwishoni Mwa Mwaka Jana

Kibatala: Ikumbushe Mahakama Mteja wangu tangu Mumkamate anamuda gani Vile

Shahidi: Kama Miezi 4

Kibatala: Fedha zilitumwa katika Ushahidi wa Mshitakiwa wa Nne kwenda kwa watu wengine

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Rekodi za SMS za Mshitakiwa zipo sehemu ya Ushahidi? Nazungumzia Mshitakiwa wa Nne

Shahidi: Hapana hakuna

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ulichukua Device za Watoto wa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Ndiyo nilichukua Kibatala: Mpaka Leo Unazo

Shahidi: walizidai nikatoa Maelekezo

Kibatala: Mpaka Leo unaongea Wamerudishiwa au bado?

Shahidi: sijui nilitoa Maelekezo

Kibatala: lakini wewe Ndiyo Mkuu wa Uangalizi

Shahidi: Kwa sauti ya Hasira anasema SIYO MUANGALIZI

Kibatala: Umeeleza Makamani Kuhusu Kumtaarifu Sabaya

Shahidi: Hiyo sikusema

Kibatala: Je hapa Mahakamani Umetoa Taarifa kuwa Uliwapa Taarifa kuwa Kuna Jambo Zito kama hilo Kwenye Kamati za Ulinzi na Usalama

Shahidi: Hapana Sikuwapa

Kibatala: Je, wewe Binafsi umeshawahi Kumuhabarisha Rais Samia Suluhu kuhusu Kesi hii

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je unataarifa kwamba Washitakiwa wameshafungwa na Kuchukuliwa hata kabla ya Kesi Kuanza

Shahidi: Unamaana gani Kuuliza swali Kama hilo

Kibatala: Maana najua Mimi, We Jibu swali

Shahidi: Sijui

Kibatala: Umeongelea hapa Kuhusu ya Battle Confusion

Shahidi: Mimi siyo Practitioner

Kibatala: Wewe Mpaka unamuhoji Mshitakiwa ambaye anarekodi ya Kuumwa Ugonjwa kama huo

Shahidi: alikuwa ananijibu Vizuri na Kwamba alikuwa ameshapona.

Kibatala: umesema akiwa anaondoka Chalinze yeye akijua anaenda Moshi kufanya VIP PROTECTION

Shahidi: Mheshimiwa labda sasa tusomewe

Kibatala: anasoma "Nilienda hadi Nyumbani nikaambiwa Kuna Kazi ya VIP protection, ambayo anajua zaidi Luteni Urio"

Shahidi: Ndiyo lakini siyo Maelezo yote.

Kibatala: Tafuta Katika Statement hiyo Mshtakiwa anapo Sema Kuwa Urio alikuwa anamtafuta Kwa Vitendo Vya Ugaidi

Shahidi: Hakuna Sehemu ambayo Adamoo amesema hayo

Kibatala: hata Huko Mbele kuna sehemu amesema Urio alimtafuta kwa ajili ya Kutenda Vitendo Vya Ugaidi?

Shahidi: Hapana lakini walikutana na Mbowe

Kibatala: Sijakuuliza kuhusu Mbowe nimekuuliza kuhusu Urio

Shahidi: Sasa Usinibane Kuniuliza Maswali ambayo siwezi Kutoa Maelezo Alikuwa anaficha ficha

Kibatala: Wewe ndiye Umesema Urio alikuwa Willing Informer Leo amekuwa Mtu wa kuficha ficha tena.?

Shahidi: Usiniulize kuhusu URIO mimi

Kibatala: Kwanini sasa Nisikuulize Kuhusu URIO, Wewe Ndiye umemleta Urio Mahakamani.

JAJI: kibatala Unamchanganya sana Shahidi, Kumleta maana pia Kumbeba

Kibatala: sahamani Mheshimiwa Jaji kama kaelewa hivyo

Kibatala: Unakubaliana na mimi, Mpaka wanaenda Moshi Mlinzi wa Mheshimiwa Mbowe alikuwa ni Willy

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mshitakiwa wa Pili ameenda Moshi 26 /07 /2020. Wakati Mashitaka yenu yanasema tangu Mwezi 05 alikuwa ameshiriki Vitendo Vya Ugaidi

Shahidi: Miye sijui hayo

Kibatala: Unakubaliana na Mimi kwamba Mpaka Mshitakiwa wa pili anaenda Moshi alikuwa hajui Mambo ya Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: kuna sehemu inayosema kwamba tulienda naye kwenye Kikao Cha Chama wakarudi. Je kuna sehemu inafafanua kuwa walirudi wapi?

Shahidi: Hapana hakuna, ila Mwenye akili timamu anajua walirudi wapi

Kibatala: Miye sina Akili timamu

Kibatala: kitendo cha Mkuu wa Wilaya kushusha Bendera za Chadema inaruhusiwa Kisheria?

Shahidi: Hapana hairuhusiwi

Kibatala: Kwamba Kufanya Preventive measures kwa Kuzuia Mtu kushusha Bendera za Chadema ni Ugaidi huo

Shahidi: Nimeshatoa Maelezo kuwa Jinai haiwezi Kuzuiwa na Jinai

Kibatala: Jibu swali Langu, Sasa swali langu halikuwa hivyo

Kibatala: Je Kitendo cha Kuzuia kwamba wasishushe, Mbele ya Mungu ni Ugaidi

Shahidi: halikuwa hivyo

Kibatala: hapa kuna Maelezo kuwa "Ametisha Wapiga Kura, amefanya hujuma na Kutisha Wapiga kura, ikiwemo Kuiba Kura" haya Umeyaandika wewe Je uliyaamini au huyaaamini Haya Maneno

Shahidi: Mimi sijui Sasa
inaweza Kuwa sijaamini

Kibatala: tutatakiwa Kuhoji wengine kama wewe uliyeandika Maelezo huyaaamini wao wametoa wapi Nguvu ya Kuleta Mahakamani

Shahidi: Mheshimiwa Sijazungumzia

Kibatala: Huyo ambaye alikuwa ampatie Ling'wenya Spray ya Sumu umezungumzia hapa, huyo Mtu

Shahidi: sijamzungumzia, Lakini upelelezi Unaendelea

Kibatala: kwa hiyo kuna Siku unaweza Kutuletea Mtuhumiwa Mwingine

Shahidi: Ndiyo inawezekana

Kibatala: Okey Mwenye Mahakama anasikia unachosema

Kibatala: Kuna sehemu inasema "Baada ya Kumfikisha Mheshimiwa Nyumbani Kwake" katika hiyo Statement Uliyorekodi ametajwa au hakutajwa

Shahidi: huyo atakuwa ni Mheshimiwa Mbowe

Kibatala: Nakuuliza hapo Kwenye Statement huyo Mheshimiwa ametajwa?

Shahidi: hajatajwa

Kibatala: tulikuwa na Mohammed Je hapo kwenye Statement Mohammed ametajwa kuwa ni Mohammed Nani

Shahidi: sijataka

Kibatala: Kitendo Cha kwamba tulipewa pesa Kwenda Kununua Nguo ili Kumpokea Tundu Lissu, Je kutumia hizo pesa Kununua Nguo ni Kosa la Jinai

Shahidi: Lengo halikuwa hilo

Kibatala: Mimi sitaki Lengo nauliza Mlichoandika hapa

Shahidi: Lengo haswa lilikuwa ni Kufanya uhalifu, hii ilikuwa Kama incentives

Kibatala: hiyo incentives ndiyo walipanga Kununua Nguo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna sehemu ambayo amekiri kwamba Hiyo pesa ilikuwa kwa ajili ya Kutenda Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: "Kesho tukaenda Kumpokea Lissu, Mimi na Mohammed Je huyo Mohammed ametajwa ni nani?

Shahidi: Sikutaja ila atakuwa ni Mohammed Ling'wenya

Kibatala: Ndiyo ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Uligundua kuwa ni Mohammed Ling'wenya.?

Shahidi: Hapana sikusema

Kibatala: na hii 78,000 ya nauli inajumuishwa kama pesa ya kufadhili Ugaidi..?

Shahidi: Inawezekana ikawemo

Kibatala: Wewe Upelelezi wako Uligundua nini

Shahidi: Imo

Kibatala: Kuna Mahala Mshitakiwa anasema pesa ilitumika Kwenda Kununua Spray ya Sumu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna Mahala popote Mshitakiwa anasema alipewa Pesa na Mbowe kwa ajili ya Kufadhili Maandamano

SHAHIDI: Hapana

Kibatala: Kuna Mahala Popote Mshitakiwa alikiri Kuwa alifika Arusha..?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna Mahala Popote kwamba Mshitakiwa anakiri alipewa Pesa Kwenda Kumdhuru Sabaya

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna Mahala Mshitakiwa wa pili amekiri kuwa alishawahi Kwenda Arusha

Shahidi: Kwenye Maelezo haya Hakuna Sehemu kama hiyo

Kibatala: Katika Maelezo Mshitakiwa alikuwa na Kete za Madawa ya Kulevya 52 Je yanatosha Humu?

Shahidi: Sikutaja 52

JAJI: tujielekeze Katika hii Kesi

Kibatala: Katika hayo Madawa DNA analysis ilifanyika

Shahidi: Hapana Kibatala: finger prints ilifanyika.?

Shahidi: haikufanyika

Kibatala: Huyu Moses Lijenje yupo wapi? tunapomzungumzia leo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: hata Kama amekufa hufahamu

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Mpaka wakati huu unapozungumza hujawahi kuhangaika Kujua yupo wapi?

Shahidi: Hapana sijahangaika

Kibatala: Ulishawahi Kuuliza Jeshi Kuhusu Uwepo wa Moses Lijenje

Shahidi: Sasa Mtu kafukuzwa, Jeshi litajuaje?

Kibatala: ndiyo Ni Jibu swali Langu hata Kama la kijinga

JAJI: halipaswi Kuwa swali la Kijinga, anaweza Kilipuuza au Mimi nisiandike likija la Kijinga

Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji ni la Msingi

Kibatala: Shahidi Uliwashirikisha Jeshi Kuhusu Lijenje

Shahidi: Ndiyo tuliwashirikisha

Kibatala: Nimeona umezungumzia kuhusu Uniforms Za Jeshi, Una utaalamu wa Kujua Uniform za Jeshi?

Shahidi: hata Nikiona naweza Kujua hili Jeshi la Wapi, Yemen, Nepal au India.

Kibatala: Je unafahamu Kuwa Nguo za Jeshi zimetungiwa Kanuni

Shahidi: hilo sifahamu

Kibatala: Kama hufahamu Kanuni unajua wapi Mambo ya Nguo za Jeshi

Shahidi: Kwa Kuona

Kibatala: kwa kuwa Leo Upo Ngoja Nikuulize, Je unajua kuwa Mtuhumiwa wa Kwanza alitekwa Kwenye Daladala akiwa na Maafisa wa zamani wa Jeshi Nyuma yake na Mbele yake akawekwa Mtu Kati, Yeye akaomba wasimdhuru wala wasimpige wakayamalize Polisi.

Shahidi: hayo ya kwako

Kibatala: umesema mara ya kwanza Mshitakiwa wa Kwanza alichuliwa Maelezo akiwa wapi.?

Shahidi: Chang'ombe

Kibatala: Unafahamu nini Kuhusu Kupeleka Mshitakiwa Tazara

Shahidi: Miye Mambo ya Tazara siyajui

Kibatala: kwa hiyo tukienda Kwenye Detention Register tunaweza Kuwa na Kuwa alikuwa Chang'ombe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Detention Register ili iwe Genuine Unatakiwa ionekane Vipi nje na Ndani

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Kwanini hufahamu na wewe ni Afisa wa Polisi kwa Muda wa Miaka 18.

Shahidi: kuna Maswali unataka Kunibana na Mimi nakwepa.

Kibatala: mimi kazi yangu Kuuliza Maswali tu, Wenyewe walikaa wataamua, tumeambiwa tukuulize kila kitu kwa sababu hatuna Uhakika kama utakuja tena

Shahidi: Ndiyo basi Unilishe maneno

Kibatala: Wewe Kwa uzoefu wako Kuna Kesi yoyote ile ambayo mnataarifa jambazi anataka Kuvamia Benki A, B, C na Mkamuacha Jambazi azurure Mtaani? ipo?

Shahidi: Ndiyo Ipo

Kibatala: umeitolea Ushahidi hapa Mahakamani?

Shahidi: Hapana

Kibatala: kabla ya Kumkamata Mbowe katika Kongamano la Katiba Mwanza, mlikuwa mnajua kuwa Mbowe anasafiri Nje ya Nchi.

Shahidi: Ndiyo tulikuwa tunajua

Kibatala: Wewe Mtu Mzima Inaingia akilini Mtu ana kesi ya Ugaidi mnampeleleza Mkamruhusu asafiri Mpaka arudi Mwenyewe

Shahidi: Ndiyo inawezekana tulikuwa tuna Mpelelezi Ndani na Nje ya Nchi.

Kibatala: Ulishawahi Kutaarifu Mamlaka zingine nje ya Nchi kuwa anayekuja Ni Gaidi

Shahidi: Hapana hakuwa Flight Risk

Kibatala: umesikiliza Mahojiano ya BBC na Rais Samia

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Rais wa Nchi amesema alipokuwa BBC kuwa Freeman Mbowe alichelewa Kukamatwa kwa sababu alikimbia Nje ya Nchi

Shahidi: Naomba Jaji aniruhusu Kujibu hilo swali.

Kibatala: Mimi nahitaji hilo Jibu, Labda Mahakama inizuie, Lakini Mimi nataka Unijibu.

Wakili wa Serikali: OBJECTION, Mheshimiwa Jaji naomba tuangalie Sheria kama zinaruhusu au Kutubana.

Wakili wa Serikali 02: MAJIBU anayotaka ni Kuhusu Mahojiano, aulizwe Maswali ambayo yeye yanamhusu.

JAJI: Peter kwa hoja hizo Unasemaje Kibatala: Mheshimiwa Jaji samahani Sana, Tulifungua Kesi ya kikatiba namba 21 ya Mwaka 2021 Wakalamikiwa walikuwa DPP, na Mwanasheria Mkuu. JAJI mgeta akasema hivi; Mahakama yake inafungwa haiwezi Kuingilia Kesi hiyo, na Kama kuna hoja anaomba Ziwasilishwe katika kesi ya Jinai inayoendelea Katika Mahakama Kuu.

Jaji: Sasa huyu amekuja Kama Executive Order au Kama Shahidi

Kibatala: Ikumbukwe Mahakama ipo Majaribuni pia kwamba sasa Rais ameshasema

Jaji: Naona Shahidi unamtreat kama Shahidi anayekuja Kuwakilisha Muhimili, Wakati tumemuapisha kuja Kutoa Ushahidi Kwenye Jambo alilolifanya

Kibatala: Kama hutojali uamuzi Ule tumekatia Rufaa, Mimi ukiniambia hapa Siyo Mahali pake nitatumia hiyo Statement.

Jaji: Mengine yote unaweza Kumuuliza, lakini tusimuilize Swali ambalo kasema Mtu Mwingine.

Kibatala: Nauliza kama Forum hapa Ikifungwa tukienda Kwingine wasisiseme hatukulileta hapa.

Jaji: Hatuwezi Kusema kwa hii Trial Mlango pia Umefumgwa, Nafahamu kwamba mnamashahidi mnaweza Kuwaleta mkawahoji kuhusu Kauli hizo.

Kibatala: Je Shahidi Unafahamu kuwa Freeman Mbowe alikimbia Nchi kwa Kukwepa tuhuma za Ugaidi

Shahidi: Hilo si fahamu Kibatala: Unakubali kuwa ulikwepo wakati Mnampekua Freeman Mbowe

Shahidi: Mi nilikuwa Nje tu zoezi lilisimamamiwa na Superitendent Mwakabonga

Kibatala: ilikuwa saa ngapi.? Shahidi: ilikuwa saa 3 Mpaka saa 4

Kibatala: kwa ufahamu wako Sheria Inasemaje Kuhusu Kupekuliwa Usiku.

Shahidi: Nikuulize wewe Kibatala:

Kibatala Shahidi Mbona swali lipo Fair

Shahidi: Tunaruhusiwa kupekua hata Usiku.

Kibatala: uliwahi Kumkamata na Kumpekua Mbowe Kabla

Shahidi: Hapana Kibatala: kwa hiyo ni Mwaka Mmoja

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ile situation Report ambayo Makamanda wanabadilishana Taarifa na Makamanda wengine Kipolisi inaitwaje

Shahidi: Situational Report

Kibatala: Sasa tuambie kuwa Mpaka Kamanda Wa Mwanza anamkamata Mbowe

Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Busy, Sikuwa najua kilichotokea Mwanza

Kibatala: kwa hiyo Kibona Hakukwambia lolote kuhusu tulio la Mwamza

Shahidi: kwanza sisi tuna riport kwa IGP siwezi Kujua kinachotokea kwa Mkoa Mwingine.

Kibatala: Maelezo hayo uliyatoa Kwenye Ushahidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwanini ulimtamkia Mshitakiwa Freeman Mbowe kuwa "wewe si Unajifanya Unajua Sana Katiba Mpya, Sasa tunakupa Kesi ya ugaidi Safari hii hutoki"

Shahidi: Hayo ni Maneno wameyapanga kwa Maslahi yao wenyewe kama Unavyosema Nipo Chini ya Kiapo, hapa Pia Quran ipo.

Kibatala: Kiongozi gani Mwingine wa Upinzani Ushawahi Kumkamata

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Lissu Je

Shahidi: Sijawahi Kumkamata ila Niliwahi Kushughulika n a kesi zake

Kibatala: Ngapi.?

Shahidi: Mbili

Kibatala: ni hayo tu Mheshimiwa jaji

Mndeme: Shahidi Unafahamu kuna Sheria ya Vyama Vya siasa

Shahidi: Nafahamu

Mndeme: unafahamu kuwa inaruhusu Mkutano na maandamano

Shahidi: Nafahamu

MNDEME: unafahamu Maandamano ni Kosa au Siyo Kosa

Shahidi: Yakiwa na Kibali siyo Kosa

Mndeme: utakubaliana Kutofautiana Kisiasa Siyo Kosa la Jinai

Shahidi: Ndiyo

Mndeme: Kutoipenda Serikali ni Maoni ya kisiasa.

Shahidi: ni Maoni ya Mtu Binafsi

Mndeme: kwa hiyo hatakuichukia Serikali ni Maoni Binafsi

Shahidi: Inategemea na Mtu

Mndeme: ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Wakili wa Serikali: Naomba Tuahirishe hadi Kesho Asubuhi Saa 3 ilituweze Kumalizia

Jaji yupo Kimya Na Mahakama Ipo Kimya kidogo Bado shahidi Yupo Kizimbami

Jaji: Upande wa Utetezi mnasemaje

Kibatala: Hatuna Pingamizi lakini tunaomba Kesho Waje na Shahidi Mwingine kwa kuwa Re examination hata Ikiwa ndefu haitozidi Masaa 2 tukianza Saa 3 Asubuhi

Jaji: sawa, ikiwezekana mje na Shahidi Mwingine.

Jaji: basi Maombi ya ahirisho yamekubaliwa kama ambavyo yameombwa na Upande wa Jamhuri na hayajapingwa na Utetezi. Basi tunahairisha Mpaka kesho saa tatu tutakapo endelea na Shahidi Namba Moja na baada ya Shahidi namba Moja tunategemea Kuendelea na Shahidi namba 2.

Jaji: Washitakiwa wataendelea Kuwa Ndani Mpaka hapo Kesho.

Jaji: ananyanyuka.
Kumbe walevi wa kuwasukuma bado wapi?
 
Yaani Samia apoteze muda wake kuja kuhojiwa na wakili kilaza kama Kibatala? Samia huyu huyu mnayempigia magoti kila siku kuomba kuonana naye? Unaota...
tunachoomba kukutana nacho ni mamlaka ya Urais tu , lakini Samia ni wa kawaida sana , usijisahau utachekwa , angalia picha hii halafu waulize wanaokulipa kwamba ilikuwaje .

Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
 
CCM wakishirikiana na kina kingai wameitunga hii kesi na ndiyo maana ina mapengo mengi mno.

Ukiwa Jaji wa haki kabisa hakuna haja na kusikiliza hii kitu, wastage of country resources.
Zipo tetesi kwamba baada ya wiki 2 jaji huyu naye atajiuzulu
 
tunachoomba kukutana nacho ni mamlaka ya Urais tu , lakini Samia ni wa kawaida sana , usijisahau utachekwa , angalia picha hii halafu waulize wanaokulipa kwamba ilikuwaje .

View attachment 1987762

Nyie ni wajinga!

Mbona mkiambiwa Rais katoa bilioni kadhaa huwa mnahoji kwani zake?

Kwani hilo la mamlaka ya urais yapo kwenye kukutana na wapinzani tu?
 
Back
Top Bottom