KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Wenyewe wanaoifahamu vyema kesi hii wanakwambia hivi:Heshima kwa wote.
Nafuatilia hii kesi ya Mbowe na wenzake watatu najikuta nacheka na kusikitika kwa wakati mmoja.
Mosi Magaidi wanampango wa kwenda kulipua vituo vya mafuta na kukata Miti hawana Mabomu wala mapanga au Cheingso.
Pili katika hati ya mashtaka hakuna ushahidi kwamba walikuwa na mkutano au kulikuwa na ushahidi wa kilichopangwa na kupangika.
Tatu kulikuwa na mpango wa kumdhuru Sabaya lakini hakuna aina yoyote ya silaha iliyokamatwa kama kielelezo
Aina hii ya kesi ipo Tanganyika pekee yake yaani Polisi anaweza kukamata na kuandaa mashtaka bila ushahidi wenye mashiko na ukakaa mahabusu muda wa kutosha.
Ipo haja Police wetu kurejea upya darasani na kujifunza namna bora ya kuandaa mashtaka, kupeleleza na hatimaye kupelekea kesi Mahakamani, kinyume chake ni kupoteza fedha za walipa kodi buuure.
1. "Mbowe siyo Malaika", wakionyesha wanajuwa mengi yaliyopangwa na Mbowe na wenzake, yatakayowashangaza watu yatakapotolewa mahakamani.
2. Mwingine katangazia dunia kabisa, kwamba "washiriki wenzake tayari yalishahukumiwa na wanatumikia vifungo vyao. Mbowe pekee yake hakuhukumiwa kwa vile alikimbia na kwenda kujificha Nairobi." Kwa hiyo ni zamu yake Mbowe kupata haki yake mahakamani!
Na ushahidi wenyewe utakaomweka hatiani, ndio huo ambao umewasilishwa mahakamani na shahidi wa kwanza wa Jamhuri.
Hawa watu wote hawaoni hata haya, soni, aibu mbele za watu wengine wenye akili timamu, wenye uwezo wa kufikiri. Hivi kweli inahitaji mtu ajue sheria kama msomi wa fani hiyo kuweza kuona yanayoendelea kwenye mahakama hii?
Tukiweka pembeni uovu wa matakwa yao, tunaloweza kusema hapa ni jinsi nchi yetu ilivyoporomoka, hata katika ule uwezo wa kutunga uongo tu unaoweza angalau kuonekana kama una ukweli ndani yake.
Lakini hawa wakubwa hili siyo tatizo kwao, maadam wanao uwezo wa maguvu, kufanya lolote wanalojisikia wanaweza kulifanya.
Ikiwapendeza, Mbowe anaweza kuendelea kukaa ndani kwa muda wote wakati hawa wakiendelea kuwa madarakani kwa nguvu.
Wakati huo huo, tusiwasahau wahusika kama DCI, ambaye anaruhusu kesi kama hii kwenda mahakamani!
Nchi hii tumefika pabaya sana sasa!