dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,130
- 49,391
... kati ya waovu wengi hawakosekani wachache wenye haki! Kwani katika majiji ya Sodoma na Gomora hapakuwa na watatu, watatu tu, wenye haki kati ya maelfu?Ila yule koplo alikuwa na ubinadamu sana.
Fikiria amekutana na mtuhumiwa wa ugaidi kwa mara ya kwanza hapo selo tena katika mazingira ambayo askari wenzake wanamtesa, anamuulizaanatokea wapi! jamaa anamjibu anatokea Mwanza na alikuwa askari.
Koplo anamwambia hata yeye ameshawahi kukaa Mwanza, na anatoa siri kuwa kuna wajeda wenzake pia wapo hapo selo. Na kuanza hapo anajenga urafiki, anapitia kumsalimia kila siku. Na anampatia biskuti kila akipata nafasi wakati ambapo akina Kingai hawampi chakula.
Kumbe katika hawa polisi, wapo wenye roho nzuri pia.