Habari zenu tena wooteee mnaosoma uzi huu,
Ilikuwa ijumaa hii iliyoisha, Yahaya kama kawaida alikuja mida ya lunch tukapata chakula cha mchana pale city retaurant kisha nikarudi endelea na kazi. Yhaya huyu amekuwa mkarimu mnoo na mcheshi na amekuwa akinijulia hali kila leo tangu asubuhi hata saa ya kulala. Yahaya amekuwa akinipeleka fukwe za bahari kupunga upepo pale agakhana na tunakula wote madafu kisha ananirudisha nyumbani pasi giza kuingia.
Sasa jumamosi hii Yahaya sikumuona wala jumapili hii kwani pia tangu nifahamia na Yahaya amekuwa akifika hata kanisani ninakosali na huwa tunasabahiana baada ya ibada kisha kila mtu na njia yake, ila jumapili hii Yahaya hakuwepo kanisani nikasubiri na ibada ya pili labda atatokea hadi mwisho wa ibada sikumpata. Yahaya hapatikani kwenye simu ya kiganjani wala mtandaoni, kote naambiwa message not delivered.
Sasa nawaza Yahaya atakuja kesho ofisini, sijui atanipigia kunieleza lipi lilimpata, najiuliza hivi maana muda wote nimefahamiana na Yahaya sijui anaishi wapi wala anafanya shuhuli gani, marafiki zake siwajui wala sijui nitampataje ..............
Yahaya kanizoesha vibaya na sasa napata tabu, Yahaya unaishi wapi nije nikusabahi labda umegonjweka walau nikuletee panadol. Yahaya huyu nilikutana nae kwenye foleni ya kuchukua road license ofisi za TRA samora miezi kadhaa nyuma mwaka huu. Natamani kesho niende TRA niulizie road license zote zenye jina la Yahaya cha kushangaza hata u bin wake siujui, yaani sijui anaitwa Yahaya nani msinicheke jamani nisaidieni kumtafuta Yahaya.
Nimekuja huku maana katika maongezi yetu wlau siku moja alinitajia kuwa ni memba wa JF ila hakunitajia ID yake hivyo sijui Yahaya anatumia ID gani JF .........................
Yahaya unaishi wapi??? ntakupataje mie Mkunde. looh!!!
Sitaki kujuta kukufahamu maana nina matumaini kuwa utanitafuta kesho, usiku mwema Yahaya.