Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Nimeshangaa sana baada ya Rais kubadili Maelekezo yake. Mwanzoni alikiri kuwa ni vigumu usajili kukamilika kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa lkn jana ameelekeza kuwa kufikia Tarehe 20 Januari 2020 usajili huo uwe tayari. Nikaangalia nilipo mimi huku Idukilo - ukitaka kukutana na NIDA mpaka uende Kishapu, nafuu mie nina kabaiskeli. Nikiangalia kaya kama 792 huku Idukilo wenye vitambulisho vya NIDA au namba za NIDA hawazidi 200 (hizi ni kaya zenye uelewa kidogo). Kati ya kaya hizo 792 kaya kama 500 hivi wanamiliki simu - ingawa nyingi zao ni za tochi. Sasa hawa 500 ambao pengine wanaweza kusajili laini zao kwa Vitambulisho vya NIDA ni kama hao 200 niliosema. Kwa maana hiyo kufikia Tarehe 21 Januari 2020 kijijini kwetu laini za simu zisizopungua 300 zitakuwa disabled kupata mawasiliano. Hebu chukua kijiji kingine na kingine. Yawezekana Chato, Darisalama na Dodoma hali hii isiwepo lkn kwa Tanzania nzima vitambulisho au namba za NIDA hazijawafikia wengi sana.
Maelekezo aliyoyatoa Rais kama yametoka kwa kupitia kwa washauri wake basi siamini km hawakujua ni ushauri unaoelekea kumjengea chuki Rais na wanachi wa hali ya chini ambao siku zote amesimama kidete kuwatetea. Angeweza kueleweka vizuri Rais pengine angeeleza pia ni kwa nini kabadili kauli yake ya mwanzo au angeelekeza basi usajili utumie hata utambulisho mwingine kama vile barua za watendaji, vitambulisho vya kupigia kura au namna yeyote ile wakati wananchi husika wakifuatilia vitambulisho vya NIDA. Zaidi ya yote Rais angeweza kuongeza muda usiopungua miezi minne na kuwaelekeza NIDA wafike hadi vijijini. Kwa kweli maelekezo yenye dalili za ubabe kutoka kwa Rais yanazidi kujenga chuki na yanaweza kufanya Uchaguzi ujao watu wakawa wameshazoea ubabe na wakakubaliana nao na kura wakambania kabisa.