Nimehakiki laini zangu za simu nimeletewa taarifa sio za kweli kabisa

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,408
1,825
Wanajukwaa salaam

Nimehakiki laini zangu na kuomba taarifa za idadi ya laini zilizosajiliwa kupitia namba yangu ya NIDA nimegundua mapungufu yafuatayo

1: Idadi ya namba nilizoambiwa kama zimesajiliwa kupitia namba yangu ya NIDA baadhi sijawahi kuzisajili

2: Baadhi ya namba nilizoletewa nimezicheki kwa kupitia huduma za fedha mtandaoni nimebaini namba hizo hazijasajiliwa kwa kitambulisho changu hivyo kukoleza hoja yangu kwamba taarifa zao sio sahihi

3: Nimewapigia simu watu wanaotumi namba hizo,nimeongea na mmoja na amenihakikishia laini yake haijasajiliwa kwa kitambulisho
changu. Mmoja amethibitisha kama alipewatu laini na anaitumia kufanyia miamala

4: Ipo namba ambayo nimeisajili mwenyewe lakini kwenye orodha ya namba nilizosajili haimo. Ingawa kupitia huduma zakifedha inasoma jina langu

Kwamaelezo hayo ninayo mashaka makubwa juu ya taarifa za idadi ya laini za simu wanazosema zitafungiwa. Wapo ambao wamesajili kwa vitambulisho vyao watafungiwa na wapo waliogushi na wataendelea kupeta

USHAURI NILIOUTOA KWA ALIYESAJILIWA KUPITIA NIDA YANGU
Nimemwambia ajitahidi atoe fedha zake kabla sijafunga laini hiyo. Kwakweli amenielewa na amenishukuru sana
 
Boss wamesema watafungia kwa siku 30 kwamaana hawatazigawa hizo namba ili kuwapa mwanya watu kama nyie mkazitetee namba zenu baada ya hapo kama hakuna ambayo mtu ataenda ku claim basi ndo watazifungia moja kwa moja
 
Kwa hapa tulipifikia nashauri serikali itoe kandarasi kwa international firms kuja kuliendesha zoezi la vitambulisho vya NIDA, usajili/uhakiki wa laini za simu na mengineyo kwa kushirikiana na serikali. Watusaidie kuunda mfumo thabiti, watoe training na wawasimamie vijana wetu wa IT walau kwa mwaka mmoja.

From there tutakuwa na centralized NIDA, laini za simu, driving license etc etc... Hii itasaidia hata kuboresha daftari la wapiga kura, watoto wanaozaliwa, na huduma nyingine. Haiwezekani sasa ni zaidi ya miaka 7 bado tinahangaika na NIDA na kuhakiki laini, tena wale jamaa zetu wa TUMA KWA NAMBA HII bado wanatesa kama kawa..
 
Halafu Halotel wanaendeleza ubabe wao wa zamani mpaka sasa.

Usipopiga simu miezi3 wanakunyang'anya line bila taarifa na kuiuza kwa mwingine badala ya kuifuta ama kuifunga!

Usajili unakuwapo Nida lakini line moja imesajiliwa kwa zaidi ya mtu mmoja!

Kiufupi ni kwamba, uozo wa kuvuruga mfumo mzima wa usajili wa line za simu, umesababishwa na makampuni ya simu menyewe pamoja na mawakala wao.
 
Ushauri una afya sana mkuu. Naamini wameona ingawa hawataki kukiri mapungufu yao
 
Halafu Halotel wanaendeleza ubabe wao wa zamani mpaka sasa.

Usipopiga simu miezi3 wanakunyang'anya line bila taarifa na kuiuza kwa mwingine badala ya kuifuta ama kuifunga!

Usajili unakuwapo Nida lakini line moja imesajiliwa kwa zaidi ya mtu mmoja!

Kiufupi ni kwamba, uozo wa kuvuruga mfumo mzima wa usajili wa line za simu, umesababishwa na makampuni ya simu menyewe pamoja na mawakala wao.
Ila kupitia laini ya halotel pia napata taarifa nyingi za masangoma eti kama unahitaji tiba uwaone masangoma hao.
Kusema kweli hakuna ujumbe kama huo kupitia laini zangu nyingine

Kwanini haloteli na masangoma na ma freemason?
 
Back
Top Bottom