Rais Samia: Katika laini za simu Milioni 61 zilizopo nchini, ni milioni 33 pekee ndizo hutumia Internet

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini (Submarine Cable) wa 2 Afrika na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel tarehe 10 Agosti, 2023 Mbezi Beach Tanki Bovu - Kituo cha 5G ya Airtel.

Nape Nnauye anazungumza
Mkongo huu ni uwekezaji mkubwa, unatazamiwa kuunganisha watu zaidi ya bilioni 3 duniani. Umejengwa kwa teknolojia ya kisasa sana, utakuwa na kasi kubwa.

Mkongo huu utaongeza kasi ya Internet nchini zaidi ya mara 10 na kushusha gharama za Internet nchini, kuvutia makampuni makubwa kama Meta, Google n.k na kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa watanzania.

Kituo cha kutolea huduma ya mtandao huu ndio kitaendeshwa na Airtel walio na ubia na Serikali. Tutaweka free wife kwenye mwendokasi.

Mkongo huu utaifanya Tanzania kuwa kitovu cha mawasiliano ukanda wa Afrika.

Rais Samia anazungumza
Serikali inaendelea na jitihada za kukuza sekta ya mawasiliano ili kujenga uchumi shirikishi wa kidigitali. Uzinduzi wa teknolijia hii ya 5G utaongeza ukuaji wa sekta mbalimbali nchini.

Ujenzi wa minara 758 umeanza ili kupanua wigo wa mawasiliano, watanzania milioni 8 watanufaika. Nilikuwa naona 5G kufika nchini ni kama ndoto, lakini sasa tumeshuhudia lidude kubwa (Robbot) linaleta 5G nchini.

Takwimu za TCRA Machi 2023, kuna laini za simu 61 Milioni, hii ni karibu ya watanzania wote wanatumia simu. Kati ya line milioni 61, ni laini milioni 33 tu ndizo hutumia internet kupitia simu janja na vifaa vingine vya mawasiliano.

Mkongo wa 2 Afrika utaweza kutuunganisha vizuri na dunia kwa sababu u aunganisha mabara ya Asia, Ulaya na Afrika kwa urefu wa kilomita 45,000 na unakisiwa utatumiwa na watu zaidi ya bilioni 3 duniani, Tanzania ikiwemo na sisi ndio tutawapa huduma wenzetu (nchi zisizo na bahari).

Mkongo huu mpya utachochea ushindani wa kibiashara na kufanya gharama za matumizi ya internet zipungue. Itafanya Tanzania iunganishwe na dunia muda wote.

Wizara ya habari na teknolojia ya habari kwa kushirikiana na Wizara zingine ihakikishe mifumo yote ya TEHAMA inayotumika ndani ya Serikali inasomana.

Wizara na taasisi zingine zinazotoa huduma nchini tuanze pia kutumia namba 1 ya mtanzania, tunataka kujuana nani ni nani. Itapunguza pia urasimu wakati wa kutafuta huduma (kubeba barua na nyaraka tofauti kwenye maofisi na taasisi). Kila mtanzania ahakikishe taarifa alizotoa NIDA ni sahihi ili ziweze kutumika. Namba hii inaweza kuanza kutolewa wakati wa kuzaliwa kwa mtoto ili irahisishe taasisi zingine kwenye kukusanya na kutumia taarifa hizo.

Serikalini bado hatujajipanga vizuri kwenye matumizi ya mtandao, tufanye kila linalowezekana serikali ihamie mtandaoni (E Government), tuhame kwenye traditional methods za kufanya kazi.

Wizara ya Habari kwa kushirikiana na TCRA iharakishe mchakato wa matokeo ya utafiti utakao toa mwelekeo wa bei za SMS, data na simu kwa kipindi cha mwaka 2023-2027.

Huduma ya WIFI ya bure itolewe kwenye maeneo muhimu mfano vyuoni ili wanachuo wapate mtandao kwa haraka, wasome vizuri na waweze kukamilisha masomo yao vizuri. Maeneo ya biashara ndogo ndogo (mfano machinga) nao wanahitaji huduma hii.
 
Samia ni shetani.
GENTAMYCINE simkubali Kivile Rais Samia ( japo kuna maeneo mengine anajitahidi Kiutendaji ) ila sijafikia kuwa na Chuki ( kama uliyonayo Kwake ) na kufikia Kumuita ni Shetani.

Sijaishia tu Kusikitika bali nimeumia pia kwa hii Lugha yako. Ni kweli tunakwazika na mengi Maishani ila Watanzania hatuna Lugha na Chuki hii tena kwa Kiongozi ( Rais ) wetu.

Tujifunze kuwa na Adabu kwa Wakuu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini (Submarine Cable) wa 2 Afrika na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel tarehe 10 Agosti, 2023 Mbezi Beach Tanki Bovu - Kituo cha 5G ya Airtel.

Nape Nnauye anazungumza
Mkongo huu ni uwekezaji mkubwa, unatazamiwa kuunganisha watu zaidi ya bilioni 3 duniani. Umejengwa kwa teknolojia ya kisasa sana, utakuwa na kasi kubwa.

Mkongo huu utaongeza kasi ya Internet nchini zaidi ya mara 10 na kushusha gharama za Internet nchini, kuvutia makampuni makubwa kama Meta, Google n.k na kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa watanzania.

Kituo cha kutolea huduma ya mtandao huu ndio kitaendeshwa na Airtel walio na ubia na Serikali. Tutaweka free wife kwenye mwendokasi.

Mkongo huu utaifanya Tanzania kuwa kitovu cha mawasiliano ukanda wa Afrika.
Hizi siasa hizi, mkongo upo huu ni mwaka takribani wa saba! Unaenda kuzinduliwa Leo! Akili, za, maccm shida sana.
 
Haya mahabari yasiyoleta unafuu kwa mlaji wa mwisho, ni trash.
 
Back
Top Bottom