Yaani Rais anafitinishwa hivi hivi - Usajili wa laini simu usilete chuki

Tila-lila2

Senior Member
Joined
Oct 20, 2019
Messages
129
Points
250

Tila-lila2

Senior Member
Joined Oct 20, 2019
129 250
Nimeshangaa sana baada ya Rais kubadili Maelekezo yake. Mwanzoni alikiri kuwa ni vigumu usajili kukamilika kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa lkn jana ameelekeza kuwa kufikia Tarehe 20 Januari 2020 usajili huo uwe tayari. Nikaangalia nilipo mimi huku Idukilo - ukitaka kukutana na NIDA mpaka uende Kishapu, nafuu mie nina kabaiskeli. Nikiangalia kaya kama 792 huku Idukilo wenye vitambulisho vya NIDA au namba za NIDA hawazidi 200 (hizi ni kaya zenye uelewa kidogo). Kati ya kaya hizo 792 kaya kama 500 hivi wanamiliki simu - ingawa nyingi zao ni za tochi. Sasa hawa 500 ambao pengine wanaweza kusajili laini zao kwa Vitambulisho vya NIDA ni kama hao 200 niliosema. Kwa maana hiyo kufikia Tarehe 21 Januari 2020 kijijini kwetu laini za simu zisizopungua 300 zitakuwa disabled kupata mawasiliano. Hebu chukua kijiji kingine na kingine. Yawezekana Chato, Darisalama na Dodoma hali hii isiwepo lkn kwa Tanzania nzima vitambulisho au namba za NIDA hazijawafikia wengi sana.

Maelekezo aliyoyatoa Rais kama yametoka kwa kupitia kwa washauri wake basi siamini km hawakujua ni ushauri unaoelekea kumjengea chuki Rais na wanachi wa hali ya chini ambao siku zote amesimama kidete kuwatetea. Angeweza kueleweka vizuri Rais pengine angeeleza pia ni kwa nini kabadili kauli yake ya mwanzo au angeelekeza basi usajili utumie hata utambulisho mwingine kama vile barua za watendaji, vitambulisho vya kupigia kura au namna yeyote ile wakati wananchi husika wakifuatilia vitambulisho vya NIDA. Zaidi ya yote Rais angeweza kuongeza muda usiopungua miezi minne na kuwaelekeza NIDA wafike hadi vijijini. Kwa kweli maelekezo yenye dalili za ubabe kutoka kwa Rais yanazidi kujenga chuki na yanaweza kufanya Uchaguzi ujao watu wakawa wameshazoea ubabe na wakakubaliana nao na kura wakambania kabisa.
 

Musundi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
916
Points
1,000

Musundi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2016
916 1,000
Naweza kukuamini. Kwa idadi ya watu waliobaki kusajiliwa kwa mujibu wa TCRA hawatamalizika ndani ya siku hizi 23 zilizobaki. Na hata watakaojisajili kipindi hiki hawapati namba papo hapo. Haileti mantiki kumfungia mtu laini wakati hajapata namba hiyo japo alishajiandikisha tayari!
Niamini mimi hawatasitisha....Nida ni zoezi endelevu kwanini usajili uwe na kikomo
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Musundi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
916
Points
1,000

Musundi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2016
916 1,000

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
3,099
Points
2,000

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
3,099 2,000
Ni mwaka wa uchaguzi na wanataka kuangalia habari za watu. Itakuwa ngumu kuliko wanavyofikiria. Kuna gharama kubwa sana kufuatilia watu lakini kuna watu usalama wa taifa wanaona ni mradi wao na watatumia hii kuingiza kampuni zao za uangalizi bila pesa ya budget na kupata ulaji.
 

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
2,391
Points
2,000

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
2,391 2,000
Basi waamue mtoto akizaliwa apate cheti cha kuzaliwa chenye alama za vidole kabisaaa!
Yaani hata chekechea bila alama za vidole huingii!
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Messages
4,162
Points
2,000

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2011
4,162 2,000
Toka hapo unaonaje baina ya rais na wananchi ? Kwanza kuna mafuriko na serikali yake haikuleta, wako busy
 

obakunta

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2018
Messages
226
Points
250

obakunta

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2018
226 250
Mtu unayemiliki simu hauwezi kushindwa kufuata kitamulisho, acheni uzushi rais anafanya jitihada za kulinda watu wake dhidi ya matapeli.
Hata muda ukiongezwa miaka kumi bila kuwa mkali bado mtaendelea kusuasua.
 

Tila-lila2

Senior Member
Joined
Oct 20, 2019
Messages
129
Points
250

Tila-lila2

Senior Member
Joined Oct 20, 2019
129 250
Mtu unayemiliki simu hauwezi kushindwa kufuata kitamulisho, acheni uzushi rais anafanya jitihada za kulinda watu wake dhidi ya matapeli.
Hata muda ukiongezwa miaka kumi bila kuwa mkali bado mtaendelea kusuasua.
Sio kila anayemiliki simu amenunua yeye. Mwenyewe mama yangu,na ndugu wengine kadhaa nimewanunulia mimi zile simu za tochi!

Mama anaweka credit ya shilingi elfu 2 kwa mwezi. Leo unataka atoke Idukilo kwenda Shinyanga mjini au Kishapu kwa ajili ya kuwatafuta NIDA!?

Na anaweza akaenda siku ya kwanza asifanikiwe. Kuwa na uhakika kukamilisha zoezi lote hilo ni lazima aende mjini mara mbili hadi tatu hivi. Kumbuka hilo hakuwa kalipanga pia halina bajeti.

Kinachobaki ni Rais kufitinishwa tu kwa watu hawa! Anyway labda atabadili tena statement yake kwa kurudia ile ya kwanza.
 

Forum statistics

Threads 1,390,952
Members 528,310
Posts 34,067,645
Top