Yaani Rais anafitinishwa hivi hivi - Usajili wa laini simu usilete chuki

Sera zinazoenda na wakati ziko Chadema usitegemee CCM kuja na jipya la kumuonea huruma Mwananchi

Ndugu zangu Watanzania uchaguzi 2020 ndio wakati wa kuiadhibu CCM
China Nchi iliyoendelea sana hakuna usumbufu huo kule ukisajili line kama huna kitambulisho chochote unapigwa picha yako na unapewa line wanafanya biashara ndiyo maana uchumi wao unakua haraka, Tanzania kwa visingizio vya ajabu wanaenda kuziletea hasara kubwa kampuni za simu ni hatari kwa uchumi wa Nchi
 
Acha kuwa mtumwa wa kifikra,hatufanyi jambo kwa ajiri ya waafrika kusini au China wao wana mechanism nyingi za kiulinzi ila sisi tunatumia fingerprint na NIDA ili kuboresha usalama wa watumiaji,kuna muda tufikiri kabla ya kujudge mkuu,na hizi Siasa mnazoendekeza ndio zinaua taifa
Nchi zilizoendelea kama China South Africa na sehemu nyingi Duniani hawana Sheria za hivyo kule unanunua line kwa kitambulisho cha aina yeyote na ukitumia unatupa ukitaka ingine unanunua tena, Sheria zingine ni ni Sheria zisizo na Tija kwa Taifa mda wa kutosha ndiyo nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa sana baada ya Rais kubadili Maelekezo yake. Mwanzoni alikiri kuwa ni vigumu usajili kukamilika kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa lkn jana ameelekeza kuwa kufikia Tarehe 20 Januari 2020 usajili huo uwe tayari. Nikaangalia nilipo mimi huku Idukilo - ukitaka kukutana na NIDA mpaka uende Kishapu, nafuu mie nina kabaiskeli. Nikiangalia kaya kama 792 huku Idukilo wenye vitambulisho vya NIDA au namba za NIDA hawazidi 200 (hizi ni kaya zenye uelewa kidogo). Kati ya kaya hizo 792 kaya kama 500 hivi wanamiliki simu - ingawa nyingi zao ni za tochi. Sasa hawa 500 ambao pengine wanaweza kusajili laini zao kwa Vitambulisho vya NIDA ni kama hao 200 niliosema. Kwa maana hiyo kufikia Tarehe 21 Januari 2020 kijijini kwetu laini za simu zisizopungua 300 zitakuwa disabled kupata mawasiliano. Hebu chukua kijiji kingine na kingine. Yawezekana Chato, Darisalama na Dodoma hali hii isiwepo lkn kwa Tanzania nzima vitambulisho au namba za NIDA hazijawafikia wengi sana.

Maelekezo aliyoyatoa Rais kama yametoka kwa kupitia kwa washauri wake basi siamini km hawakujua ni ushauri unaoelekea kumjengea chuki Rais na wanachi wa hali ya chini ambao siku zote amesimama kidete kuwatetea. Angeweza kueleweka vizuri Rais pengine angeeleza pia ni kwa nini kabadili kauli yake ya mwanzo au angeelekeza basi usajili utumie hata utambulisho mwingine kama vile barua za watendaji, vitambulisho vya kupigia kura au namna yeyote ile wakati wananchi husika wakifuatilia vitambulisho vya NIDA. Zaidi ya yote Rais angeweza kuongeza muda usiopungua miezi minne na kuwaelekeza NIDA wafike hadi vijijini. Kwa kweli maelekezo yenye dalili za ubabe kutoka kwa Rais yanazidi kujenga chuki na yanaweza kufanya Uchaguzi ujao watu wakawa wameshazoea ubabe na wakakubaliana nao na kura wakambania kabisa.
Mimi naona huo muda ni mkubwa sana,nimeshachoshwa na zile SMS za ile pesa itume kwa hii namba xxxxxxxxx jina litakuja mwanaidi mwakatope

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kweli tatizo ni hilo, kwanini hukutumia akili kuliondoa hilo tatizo na unatumia nguvu nyingi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa sana baada ya Rais kubadili Maelekezo yake. Mwanzoni alikiri kuwa ni vigumu usajili kukamilika kwa kutumia Vitambulisho vya Taifa lkn jana ameelekeza kuwa kufikia Tarehe 20 Januari 2020 usajili huo uwe tayari. Nikaangalia nilipo mimi huku Idukilo - ukitaka kukutana na NIDA mpaka uende Kishapu, nafuu mie nina kabaiskeli. Nikiangalia kaya kama 792 huku Idukilo wenye vitambulisho vya NIDA au namba za NIDA hawazidi 200 (hizi ni kaya zenye uelewa kidogo). Kati ya kaya hizo 792 kaya kama 500 hivi wanamiliki simu - ingawa nyingi zao ni za tochi. Sasa hawa 500 ambao pengine wanaweza kusajili laini zao kwa Vitambulisho vya NIDA ni kama hao 200 niliosema. Kwa maana hiyo kufikia Tarehe 21 Januari 2020 kijijini kwetu laini za simu zisizopungua 300 zitakuwa disabled kupata mawasiliano. Hebu chukua kijiji kingine na kingine. Yawezekana Chato, Darisalama na Dodoma hali hii isiwepo lkn kwa Tanzania nzima vitambulisho au namba za NIDA hazijawafikia wengi sana.

Maelekezo aliyoyatoa Rais kama yametoka kwa kupitia kwa washauri wake basi siamini km hawakujua ni ushauri unaoelekea kumjengea chuki Rais na wanachi wa hali ya chini ambao siku zote amesimama kidete kuwatetea. Angeweza kueleweka vizuri Rais pengine angeeleza pia ni kwa nini kabadili kauli yake ya mwanzo au angeelekeza basi usajili utumie hata utambulisho mwingine kama vile barua za watendaji, vitambulisho vya kupigia kura au namna yeyote ile wakati wananchi husika wakifuatilia vitambulisho vya NIDA. Zaidi ya yote Rais angeweza kuongeza muda usiopungua miezi minne na kuwaelekeza NIDA wafike hadi vijijini. Kwa kweli maelekezo yenye dalili za ubabe kutoka kwa Rais yanazidi kujenga chuki na yanaweza kufanya Uchaguzi ujao watu wakawa wameshazoea ubabe na wakakubaliana nao na kura wakambania kabisa.
Idadi ya kura haitegemei wananchi kujitokeza au la ....go figure
 
Huduma ni lazima nakazia lazima iwafuate wananchi walipo
Hela zipo na usafiri upo kwanini wafanye ugumu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sera zinazoenda na wakati ziko Chadema usitegemee CCM kuja na jipya la kumuonea huruma Mwananchi

Ndugu zangu Watanzania uchaguzi 2020 ndio wakati wa kuiadhibu CCM
Be serious please !
Screenshot_20191101-085446.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom