Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Huyu jamaa ni kilaza fulu,alifundisha pale northen hilands,kazi kubwa ilikua ni kutembea na wanafunzi wa kike n a kichapo kwa wavulana,hakua na taaluma yoyote ile darasani alikua haeleweki na ole wako umkosoe utajuta kuzaliwa.shule anayomiliki ilikua ya gabachori mmoja akamletea zengwe na yule mdosi akatoroka nchini basi jamaa ndio mpaka leo kaimilik.akiulizwa sasahivi umejenga au umenunua kwa nani hatoweza kukupa maelezo ya kutosha zaidi ya umbulula wake.anywayamshukuru sana MWANJELWA kwani lile pande alilompigia DHAIFU ndilo linalomfanya aleshavu sasahivi.
 
AshaDii,

Kwa hapo tu umenifanya nishindwe kuendelea na hoja nyingine...

Kwani huyu Mulugo (kama mtu binafsi na kiongozi, tena wa wizara nyeti) analaumiwa kwa makosa yapi?

Labda tuanzie hapo...ingawa nimeona mdau mmoja, Edson kataja baadhi kwenye post #68....


Binafsi namlaumu kwa haya;


  1. Inaonesha kuwa hayupo makini na kazi yake! Yeye kama naibu waziri akiwa anaenda kuwakilisha nchi nzima kwa kutoa hotuba ilitakiwa aandae hio hotuba na aombe ushauri kwa wenzie pia ambao anajuwa wapo vizuri katika hio sector (kuelezea sifa ya nchi vilivyo na lugha pia); Kusoma kwake ile hotuba inaonesha kuwa aliiandaa mwenyewe (maybe kwa kujiamini mno) sababu angeandaa mwingine makosa angesahihisha wakati kwa kujieleza (refer to Zimbambwe Vs Zanzibar).
  2. Kwa aliye tazama ile clip inaonesha kuwa hayupo that comfortable pale mbele.... Kana kwamba ni mtu ana 'stage fright' sasa kwa yeyote ambaye unajua una tatizo hilo swala la kuwakilisha nchi ni lazima ujiandae na kama huwezi eleza mapema SIO tu kwa kuangalia maslahi binafsi kuwa unasafiri na unapata malupu lupu!
  3. Namlaumu kwa kuzidi kushemsha! Ingawa inazidi kutoa picha ni mtu wa namna gani... Yeye hataki kukosolewa na no wonder lugha inamsumbua. Alikuwa hata haya ya kuenda clouds na kulichukulia hili swala ki wepesi! IMO ilitakiwa aite hata press conference na AKUBALI udhaifu wake sio kutaka kuufunika! Unaweza vipi kuwashawishi wasomi wa Tanzania kuwa ume slip kutamka 1964?
  4. Pia analaumiwa kwa kuwa mbinafsi... anajuwa kuwa hawezi ila kwa malahi yake na sababu zake binafsi kujifanya anaweza.

Kubwa kuliko nalaumu hio serkali ya CCM kwa kututia aibu kwa meengi... hata yale ambayo yanawezekana kabisa kuepukika. Hii ni product yao; inaonesha wazi na kutowa picha namna gani nafasi za juu zimekaliwa na wasio weza.

Simlaumu kutumia vibaya kiingereza sababu ni wazi kuwa HAWEZI! Na wala hana sababu ya kujitetea, anazidi kutia aibu.
 
one nineteen sixty four!!!??? na indian ocean ni nchi pia?
Tunategemea nini hapa kwa elimu ya watoto wetu?
 
Hivi huyu Mulugo si ndio huyu alifundisha Southern Highland school, ambapo kuna siku wakaguzi wa elimu walipita na kummtolea nje kuwa hana sifa wala vigezo vya kuwa mwalimu? ndipo akaenda kujiunga Open University kwa degree. Tena yalikuwa makosa makubwa kufundisha bila kupita chuo chochote cha elimu. Leo hii yeye ana ubavu wa kuwazukia wenzie na kuwafukuza eti hawana sifa....loh!

Taarifa zake pale wizarani, mara nyingi kama ana ugeni wa nje ya Tz hufanya juu chini kukutana nao peke yake, hataki maafisa kuwepo kwa kutojiamini kwake na lugha. Mulugo kachemka - full stop!
 
Upande wa Critics ndio hilo ambalo limenifanya niliongelee.... Observe Tausi, majority ni criticism dhidi ya lugha. Ni wachache ambao wanaongelea namna ilivyo wazi kuwa inaonesha hayupo qualified kwa hio nafasi aliyopo na namna ambavyo ni mfano wa mawaziri ambao kazi yao ni walakini sana kama anawajibika. Kwa mtazamo wangu ile hotuba yake yoote inatowa picha ya nidhamu yake katika kazi (hayupo makini); Yupo chini ya nafasi aliyopo (kama naibu waziri wa Elimu, its un-excusable kutojuwa kiingereza); hana ufikiri, busara wala washauri (maana anazidi kuchemka anavyozidi kuli justfy); hivo at the end of the day tupo pamoja katika hoja yako kuhusiana naye.

AD kama utakumbuka vizuri Mulugo alishajadiliwa hapa JF tangu mwaka 2011 mara tu baada ya uteuzi wake wa kuwa naibu waziri wa elimu. Hiyo thread bado ipo na hata hiyo video ilipoletwa hapa JF kwa mara ya kwanza ilitupwa kwenye uzi huo huo kabla ya kuanza kushambuliwa kwa style tofauti tofauti. Tangu wakati huo watu tulisema waziwazi kwamba Mulugo haqualify kuwa naibu waziri wa elimu kwakuwa elimu yake mwenyewe ilikuwa ya mashaka mashaka, na wengine wakaenda mbali zaidi wakasema hata cheti anachotumia si chake kwakuwa alichemka mtihani wa form six.

Nachotaka kukukumbusha ni kwamba critics wanaoonyesha kwamba Mulugo hana sifa za kuwa naibu waziri ni wengi sana na hii ya lugha ni kitu kimekuja tu "ku spark" moto ambao ulikuwa umeanza kufifia. Nadhani ukisoma kwa makini comments za watu wengi hapa wana relate udhaifu huu wa lugha moja kwa moja na uwezo wake mdogo kielimu.
 
KWELI ALITELEZA BANA NA KUNA ALIPOSEMA“FROM WORK BADALA YA FLAME WORK“ jamaa anateleza kweli kama kwenye mlenda au ganda la ndizi
 
Embu tuwe makini lakini na pia tujiulize yafuatayo ( Nwe jiulize yafuatayo)

1. Ni kwanini Mulugo hakufuata aliyoandikiwa na kupewa katika ppt hadi atoe kichwani mwake?? alitaka ule umma umueleweje?? kuwa anajua sana na haitaji kusoma au??

2. Yeye kama mdau na mwenye dhamana ya elimu nchini kwetu alitaka kuutangazia nini ule umma wa dunia??

Makosa MAKUBWA kuliko hata lile la yule mtoto aliyekojolea kuran!!

A. Kusema Tanzania " was formed in ONE NINETEEN SIXTY FOUR" yaani 11964!!! (huyo ndiye waziri ambaye pia alikuwa mwalimu!!)

B. Kusema Tanzania was formed...by UNIFYING islands of ZIMBABWE and PEMBA!!! ( yaani visiwa vya Zimbabwe na Pemba. Eti "unifying"!!! hiki ndio nini??

C. Kusema Tanzania tuna "Pre primary school ya miaka miwili" huu ni uongo dhahiri shahiri!! Hatuna kitu kama hiki!!

D. Kusema NACTE inatoa Masters na Doctorate degree!!!

Hivi ni baadhi tu ya yaliyomo katika presentation yake na bado tunasema ni "SLEEP OF A TONGUE"

Tunahangaika kumpeleka MTOTO aliyekojolea Kuran, wakati kuna MIBABA inatuharibia nchi na tunaiacha!!

Hivi Mugabe akisikia itakuaje??


Enzi za mwalimu, huyu wakati anarudi tu na kutua Airport DIA...moja kwa moja alikuwa anakwenda UKONGA/SEGEREA au KEKO baada ya kula viboko kumi na viwili wakati anaingia na kumi na viwili wakati wa kutoka akamuoneshe mke wake!!
 
ulimi wake una utelezi sana aisee

hadi leo kasema tena pemba, zanzibar na tanzania bara

Halafu badala ya kusema ilikuwa ERROR kasema ilikuwa HERROR. Hata kama ni kuteleza ulimi kwa suala sensitive kama hilo linalohusu taifa angeshtuka na kurekebisha lakini wapi. Ni aibu kubwa sana kwa taifa, yaani Mulugo katoa reflection ya hali halisi ya viongozi wetu.
 
Kama hiyo ni ulimi kuteleza mbona makubwa,
Kwani ni kweli Tanzania ni Muungano wa visiwa vya Zanzibar na Pemba? Au usahihi ni Unguja na Pemba pamoja na Tanganyika?
 
Msisahau hii lugha sio yake ya kwanza...sasa angekosea lugha ya kwanza na ya pili manake kiswahili ndio tungemlaum sana...
 
Hivi Pasco, mtu unapozunguka mashuleni kufanya kazi ya school inspector ndio unapiga kazi ????


Je amekaa kwenye desk lake akapitia sera mbalimbali za Elimu?

Uwezo wake ni kufanya kazi ambayo inafanywa na mainspector sema hawako makini sana, na kila akienda anachukua wanahabari kama nyie ili ku unleash madudu....hivi kuna innovation yoyote au la ajabu katika madudu hayo husika au ni ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji shule kwa mujibu wa wizara, ni kazi ambayo school inspectors na kitengo cha kaguzi kinatakiwa kiimarishwe kifanye hayo,

Yeye akae apitie mitaala ya mashule maana kila shule inatoka kivyake, lakini nadhani uwezo wake umeishia kwenye kushout orders tu hahahah
 
hii mada ningeiona ina mantiki lkn kwavile alieileta hapa nae ndio walewale wakuteleza ulimi "i doesn't matter":becky: na mzee wa kukurupuka kutoka usingizini na mfuasi wa lowassa ..a.k.a PASCO...huyu ni galasa kama ni katika mchezo wa karata
 
Pasco huyu Mlugo amekuwa akidaiwa na watu wengi kwamba ananunua sana paper ili kufaulisha mitihani katika shule yake na shule yake ilishawahi kuadhibiwa kwa hilo, pia akiwa mwanasiasa kuna taarifa kwamba anajitahidi sana kununua waandishi wa habari, usitake niamini kwamba nawewe amekununua pia maana umekuja na utetezi mwepesi sana kiasi ambacho naamini hata wewe huamini katika utetezi wako ila njaa inakusumbua. Ingekuwa Mlugo kakosea hilo tuu tungesema kweli kateleza ulimi lakini ukiwa makini katika hotuba yake kuna makosa zaidi ya uliyotolea utetezi, Mfano mbona hujatoa utetezi wako kuhusiana na kusema Muungano wetu ulikuwa mwaka 1,1964? au mbona hujazungumza lolote aliposema NACTE wanaofa Masters na PHD? Nawachukia sana waandishi njaa jamii ya Pasco
 
Hazifani kabisa, huyo elimu ni lazima ni ya wasi wasi, hata kama lugha inasumbua huweze soma 1964 namna alivyosoma yeye... Ni ngumu sana.



Point taken Maranya... Nimerudi kwenye mada kaka... Nisamehe buree...
AshaDii,

Kwa watu wanaofuatilia mambo ya elimu, wanajua kuwa hali yetu kama nchi ni mbaya sana......

Juzi juzi nilikuwa nangalia kipindi cha Masoud Kipanya wakati anasaili vijana, nilibaki najishangaa....Kuna kijana kamaliza form 4 (may be kama Mulugo), anasema kuwa binadamu ana maini mawili, figo mbili na firigisi mbili!!

Kuna dada mwingine (ex form 4) huyo alishindwa kueleza maana ya biology......

Tatizo letu ni kubwa sana na ndiyo maana wengine tungependelea kuwa tufike mahali tuwe na zero tolerance kwenye mambo ya taaluma. Kiongozi ambaye uwezo wake uko chini ya viwango apigwe chini akatafute kazi nyingine.. Na hapa tusisitize kuwa wanaotafuta umilionea kwenye uongozi wamekosea njia....uongozi unatoka ndani kabisa ya mtu na siyo nafasa ya kujijaza mafedha!!
 
Last edited by a moderator:
Watu wenye uzoefu wa kimataifa wa public speaking huwa wanafanya practice kabla ya kupanda jukwaani kuongea. Japokuwa public speaking ni janga la kitaifa Tanzania lakn yeye waziri hana excuse kwa hili kwa kuwa inaonyesha hakujiandaa kabisaa.
 
1. membe aliwahi kuchemk sana kule arusha kwenye kikao cha sullivan mwaka 2008 ilikuwa balaa....

2. hawa ghasia nae one day pale mnazi mmoja aliwahi kuchemka sana

3.mkuu wa nchi kule davos na wakati anahojiwa na kituo cha MSNBC alichemka sana...pale davos ile ''manufacturing of teachers'' ilitamkwa na mkuu..akimaanisha tuzalishe walimu wa kutosha

4. siku ya mazishi ya prof saitoti pale Nairobi waziri nchimbi nae alichemka sana wakati anasoma salamu toka kwa rais.

5. Mulugo nao kachemka vilivyo

6. juzi tu wizara imeandika barua kwa papa Benedicti xvi wakimshukuru ...barua hiyo imo humu jf imejaa makosa ya kufa mtu na aliyeandika hajui kaandika nini...

7..ni membe nae si amesaini mkataba bila kusoma majuzi kati hapa!!!....



ni shida tupu hawa viongozi......mulugo asijitete kuwa aliteleza kwa kifupi hajui kusoma vizuri kwa lugha hii ya malkia....
 
kwakweli ndo maana tunasema mtoto anamaliza darasa la saba hajui kusoma wala kuandika kumbe sababu walimu wao ni kama huyu ex-teacher ambaye ss ni waziri
Mungu tuondolee hili janga la kunyemelewa na kizazi kisicho na elimu
 
Back
Top Bottom