Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Wanabodi,

Kumekuwepo kwa thread mbali mbali za kumshutumu, kumbeza hadi kumkebehi Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Phillip Mulugo kwa kauli yake ya Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba!.

Naomba kujitokeza kumtetea huyu jamaa "It was only a slip of a tongue!. Yaani aliteleza tuu ulimi!.

Tumhukumu mtu kwa utendaji wake na sio kwa "Sleep of a tongue"!.
Pasco.


Sawa yeye ilikua slip and sleep of a tongue, na wewe je?? ni hiyohiyo slip au sleep of hand or head???
 
Kajitetea tena kwa kuweka 'CV' yake, kwamba ni mwalimu wa muda mrefu wa Historia na Uchumi! Tena wa kiwango cha shahada! Na bado hajashtuka kwamba Zanzibar inamaanisha Pemba na Unguja!
Nadhani labda alikua anaiwazia Zimbwabwe walati alipotaka kutamka Zanzibar...yaani akitoka SA anapitia Zimbwabwe, hadi Zanzibar!

Hahaha, jamaa kadiri anavyojitetea ndivyo anavyochanganya. Na hata Clouds FM hawakushtukia hili, karudia yaleyale.
 
Mkuu Pasco
Jamaa alkuwa anahofu tu ya kuongea lugha ambayo hakuwa na raha nayo cha msingi ujumbe ulifika na wote waliokuwapo mkutanoni walijua Tanzania imetokana na muungano wa kitu fulani; muhimu ni ujumbe; na isitoshea nina uhakika wajumbe wa mkutano walikuwa na paper hivyo walipata fursa ya kupitia kilichosemwa na Bwana Mulugo.

Chama
Gongo la mboto DSM
Hapo kwenye red ndipo alipo aibika kwa sababu alikuwa anaongea tofauti na kilichoandikwa kwa kutokujua au kwa kutokuwa makini.
 
Sisi wanafunzi wake tunamfahamu sana Mulugo alipokuwa mwalimu wetu, tulikuwa tukiigiza broken zake darasani na hata pronuncition yake huwa ni mgogoro. Acha kutetea upuuzi usiokuwa na mantiki, heshima yako inashuka mkuu.

Hahahaha mwanafunzi wa Mulugo umenifurahisha sana..... ila sikulaumu kwasababu hizi ni athari za kufundishwa na mwalimu kama huyo!
 
Kaka DC,

Sijakataa kuwa jamaa kafanya kosa na kachemka... Ukinisoma upya hapo utakuta kuwa nimesema ni kheri angekuwa wazi na kusema kuwa lugha hiyo inamsumbua. Hio statement ingemletea heshima kwa kuwajibika na kusema kweli kuwa HAWEZI badala ya kujitetea ambako kunafanya mambo yawe worse!

Hili la kukosea kama wananchi tupo hodari sana! Na hio ndio down fall yetu Watanzania, huwa tunajuwa sana kukosoa lakini sio kutenda wala kufanyia kazi pale ambapo tunaweza!

Hivi kaka kwa trend za siasa na hali halisi ya nchi unadhani huo mchemko ungefanywa na kiongozi wa CDM inge make headlines kama ilivyo sasa? Ama unadhani kuwa huyo Mulugo angekuwa muwajibikaji to the extend anajulikana kwa kazi nzuri anayofanya katika nafasi yake kuna watu wangemcheka kwa hilo? AU tu unadhani kuwa CCM wasingekuwa na makashfa yoote yaliyopo toka nepotism, ufisadi na mambo kibao yasio hesabika angekuwa judged vibaya?

Hapa issue ni kuwa tayari ni wazi kuwa Mawaziri wa JK kwa kiasi kikubwa na failures, hivo kosa lolote lile analofanya hata kama la kibinadamu hata dogo vipi ni LAZIMA ashambuliwe na jamii sababu jamii IMECHOKA. Lakini bado hio hainipi sababu ya mimi kulichokulia kama mwanajamii aliyechoka bali tu kama mwanadamu. Na narudi pale pale kuwa sio kosa lake kukosea lugha thou kosa kubwa ni yeye kuwepo katika nafasi ambayo hastahili kuwepo...

Kwa mtazamo wangu huu ukosoaji ni halali kabisa kwa sie wananchi, ila ni vizuri tukifanya hivyo for the right reasons...
AshaDii,

Kwa hapo tu umenifanya nishindwe kuendelea na hoja nyingine...

Kwani huyu Mulugo (kama mtu binafsi na kiongozi, tena wa wizara nyeti) analaumiwa kwa makosa yapi?

Labda tuanzie hapo...ingawa nimeona mdau mmoja, Edson kataja baadhi kwenye post #68....
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini aitumie??

Mie naona alijimini na siku zote huko nyuma alijuwa kua anajua kiingereza. Hasa tokana na tabia yetu Watanzania kuwa wakarimu na kumkosoa mtu wa karibu unaona ngumu. Sidhani kama kuna mtu aliwahi mwambia kuwa kiingereza chake ni kibovu... Lol.

Naibu waziri wa elimu ni lazima awe ni mtu anayejimudu katika sekta ya elimu. Na lugha ya kiingereza ikiwa ni lugha rasmi ya kufundishia kuanzia shule za sekondari hadi vyuo vikuu, ikiwa ndio lugha rasmi ya mawasiliano ya serikali, naibu waziri analazimika kuifahamu vizuri, na katika hili sioni sababu ya kumtafutia visingizio vya kumsua na aibu hii aliyotuletea watanzania wote.

Tunapokubali watu dhaifu waendelee kutuongoza tusitarajie matokeo mazuri, wakati tunapolalamika kwamba elimu yetu inazidi kushuka kiwango cha ubora na somo la kiingereza likiwa ni mojawapo ya masomo ambayo watoto wetu wanafanya vibaya hatuna sababu ya kusema ulimi ulimteleza au namna nyingine ya kumtetea. Tukikubali huo utetezi rahisi rahisi tutakuwa tunakubali akili ndogo iongoze akili kubwa.

Mbona mawaziri wengine waliofanya presentation katika mkutano huo ndimi zao hazikuwateleza? na hapa usisahau kwamba cv yake imesomwa na kuletwa hapa JF mara nyingi na bila kumung'unya maneno Mulugo hakustahili hata kidogo kuwa naibu waziri katika wizara yoyote achilia mbali wizara nyeti kama ya elimu.

Mimi binafsi hata akijitetea kwa kiwango gani bado hawezi kunishawishi kwamba ulimi ulikuwa unateleza kila mara. Kwani huo ulimi wake una nini hadi uteleze tangu mwanzo hadi mwisho wa speech. Mimi mwenyewe si mzuri sana katika kuongea lugha ya kiingereza lakini kwenye kusoma hapo utanipenda tu. Akili ya kawaida tu inakusaidia kugundua baadhi ya makosa ya kiuchapaji kama kichwa chako wewe mwenyewe kiko vizuri, lakini kama ni mweupe hata yale yaliyoandikwa vizuri wewe utayasoma kwa kuyakosea.


Kaka Maranya,

Hii post sijajuwa kua ulikuwa unanieleza kwa zaidi ama kuwa unadhani kuwa nipo tofauti.

Hapo in blue post yangu ya kwanza ulo ni quote naomba isome upya... Nishasema pia kuwa hafai. Na kwamba yupo katika nafasi ambayo sio saiz yake. Na nimegusia pia kuwa HASA ukizingatia kuwa 'entity' anayowakilisha ni vema akajua kiingereza.

Hapo in red noted. Nakubaliana na wewe. Hapo nilipo bold hata mimi pia huwezi nishawishi tupo pamoja. Nisome upya, NIMESEMA kuwa bora akili kuwa lugha inampiga chenga, anavyozidi kujitetea anazidi kuharibu.
 
Katika aibu kwenye conference, katia aibu serkali yake then akatutia aibu na sisi hali tuna watu ni wanastahili hata wangeenda pale wangewakilisha vilivyo.

Bora hata angefanya kosa hilo humu ndani ya nchi. Huko nje anatufanya Watanzania tuaibike, aisee
 
Vipi na ile one nineteen sixty four? Na yenyewe ni kuteleza kwa ulimi?

Hiyo ameifafanua kua awali alitaka kuutaja mwaka kwa kutamka single digits, then akachange akaona ataje kwa mkupuo!
Akatoa mf. Ni kama vile utake kumwambia mtu "nitakuja mwaka kesho"
but ukajikuta ukisema "nitakuja mwaka (then pause) mwaka kesho"
hivyo neno mwaka ukalirudia mara mbili . ndiyo hiyo "one nineteen sixty four"
one kaitanguliza then akairudia kuichanganya kwenye nineteen.
 
1. mulugo hajui kusoma kwa kutumia lugha ya kingereza

2. elimu yake ni ya mashaka sana

3. hajiamini anapokuwa mbele ya hadhara

4. wala asijitetee kuwa aliteleza ni upuuzi tu........tangu lini mtu makini anayejua kusoma presentation akawa anasoma mstari kwa mstari?!!.....

Well said! uwezo wake ni mdogo mno jamani! elimu yake pia ni ya mashaka achilia mbali maswali yanayoweza kuulizwa hivi aliteuliwaje kuongoza wizara kitivo cha maarifa - Elimu??? Kama unawasilisha kwa kutumia power point ni dondoo tu ambazo Mulugo angekuwa anazielezea in details tena bila kusoma, wakati mwingine hizo dondoo ni kama talking notes. Mulugo alikuwa anasoma mwanzo mwisho kwa lafudhi na makosa makubwa!

Hivi atajitetea vipi kwenye 1-1964 (one ninteen sixty four, Tz imepakana na nchi 8 ikiwemo "Indian Ocean", NACTE wanatoa degree??? hana uelewa wowote wa mtiririko mzima wa speech yake. Introduction aliyotoa was poorly written. Hotuba zinapowasilishwa huhitaji kuwasomea watu heading kama alivyofanya, angetiririka tu kama kweli ana uwezo. Kutokujua lugha si tatizo, tatizo ni pale unapotaka kutumia lugha usiyoimudu hata unachowasilisha kinakosa ladha. Anahitaji kupatiwa public presentation skills na speech writing/presentation skills!
 
Wanabodi,

Kumekuwepo kwa thread mbali mbali za kumshutumu, kumbeza hadi kumkebehi Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Phillip Mulugo kwa kauli yake ya Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba!.

Naomba kujitokeza kumtetea huyu jamaa "It was only a slip of a tongue!. Yaani aliteleza tuu ulimi!.

Ukiangalia ile video kwenye U-Tube utaona ni PPT Presentation kupitia Over Head Projector kila neno alilotamka pia limeandikwa na kuonyeshwa na ile projector screen.

Japo ni kweli aliitamka neno Zimbabwe lakini screen ya projector ilionyesha neno Zanzibar!. Hivyo hilo neno Zimbabwe, was a sleep of a tongue tuu yaani aliteleza ulimi ni kosa la kawaida la kibinaadamu!.

Kufuatia kosa hilo dogo tuu, kitendo cha Clouds Redio kumkomalia hana nzima sio cha kistaarabu na sio kumtendea haki!.

Watu sasa wameanza hata kuhoji elimu yake!. Watanzania sasa tumekuwa wagonjwa wa "paper qualifications" watu humu sasa wanamkomalia kuhusu elimu yake!. I doesn't matter jamaa ni jembe kweli!. Nimemshuhudia akipiga mzigo wa kufa mtu!. Akifanya ziara za kikazi popote, hufanya 'surprize visit" kwenye mashule au vyuo na kuibua madudu!.

Tumhukumu mtu kwa utendaji wake na sio kwa "Sleep of a tongue"!.
Pasco.


Yaani Mkuu Pasco pamoja na kuwa na "Premium Member" ila naona unataka kuanza kudharauliwa!!! Embu tuwe makini lakini na pia tujiulize yafuatayo ( Nwe jiulize yafuatayo)

1. Ni kwanini Mulugo hakufuata aliyoandikiwa na kupewa katika ppt hadi atoe kichwani mwake?? alitaka ule umma umueleweje?? kuwa anajua sana na haitaji kusoma au??

2. Yeye kama mdau na mwenye dhamana ya elimu nchini kwetu alitaka kuutangazia nini ule umma wa dunia??

Makosa MAKUBWA kuliko hata lile la yule mtoto aliyekojolea kuran!!

A. Kusema Tanzania " was formed in ONE NINETEEN SIXTY FOUR" yaani 11964!!! (huyo ndiye waziri ambaye pia alikuwa mwalimu!!)

B. Kusema Tanzania was formed...by UNIFYING islands of ZIMBABWE and PEMBA!!! ( yaani visiwa vya Zimbabwe na Pemba. Eti "unifying"!!! hiki ndio nini??

C. Kusema Tanzania tuna "Pre primary school ya miaka miwili" huu ni uongo dhahiri shahiri!! Hatuna kitu kama hiki!!

D. Kusema NACTE inatoa Masters na Doctorate degree!!!

Hivi ni baadhi tu ya yaliyomo katika presentation yake na bado tunasema ni "SLEEP OF A TONGUE"

Tunahangaika kumpeleka MTOTO aliyekojolea Kuran, wakati kuna MIBABA inatuharibia na tunaiacha!!

Enzi za mwalimu, huyu wakati anarudi tu na kutua Airport DIA...moja kwa moja alikuwa anakwenda UKONGA/SEGEREA au KEKO baada ya kula viboko kumi na viwili wakati anaingia na kumi na viwili wakati wa kutoka akamuoneshe mke wake!!
 
Haya ni matokeo ya kukiuka kanuni ya msingi ya kuchagua au kuteua viongozi na badala yake undugu, kujuana, urafiki, fadhila, rushwa n.k vikachukua nafasi.
 
Dada, majina ya Zanzibar na Zimbabwe ni ya lugha ya kigeni? Kusoma mwaka 1964 kwa lugha ya kiigereza inaweza ikawa tatizo kwa mtu wa lugha nyingine, lakini kusoma majina ya Zimbabwe au Zimbabwe kwa mswahili sio tatizo mama!

Hazifani kabisa, huyo elimu ni lazima ni ya wasi wasi, hata kama lugha inasumbua huweze soma 1964 namna alivyosoma yeye... Ni ngumu sana.

AshaDii dadangu mbona sasa unataka kututoa kwenye mada? hapa tunamzungumzia naibu waziri wa elimu wa JMT, mambo ya vyama vya siasa yanatoka wapi tena? au ndio njia mbadala ya kumnusuru Mulugo na mashambulizi? huyu anatumia kodi zetu kwenda kutuwakilisha kwenye mikutano ya kimataifa watanzania wote sasa akiboronga huko tuna kila haki ya kumshughulikia. Kama unamfahamu kiongozi yoyote ya Chadema aliyeboronga kwenye presentation unaweza kuanzisha thread tumjadili kuliko hivi unavyojaribu kutu divert toka katika hoja ya msingi inayomhusu Mulugo.Na hata kama kuna viongozi wa Chadema wanaboronga kuongea kiingereza hiyo haiwezi kuwa excuse kwa naibu waziri Mulugo.

Point taken Maranya... Nimerudi kwenye mada kaka... Nisamehe buree...
 
"Fikira sahihi huja kwa lugha sahihi".... hili ndio lilikua tatizo kwa jamaa lugha ALIOKUA AKIITUMIA PENGINE NDIO ILILETA KIGUGUMIZI BT haikua kuteleza kwa ulimi "WOGA WA KUONGEA KWA LUHA YA KIGENI MBELE YA WENYE LUGHA YAO"
ni sawa ukiswalisha huku ukijua nyuma yako wako mashekhe wakubwa waliokuzidi elimu.
 
Nimesononeka sana moyo hadi leo nimeshindwa kuisikiliza hiyo clip kwa zaidi ya sekunde hata 20 maana naona aibu.

Kila nikifungua pale anapoanza roho inaniuma sana na mwili unanisisimka!
 
Kumekuwepo kwa thread mbali mbali za kumshutumu, kumbeza hadi kumkebehi Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Phillip Mulugo kwa kauli yake ya Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba!.Japo ni kweli aliitamka neno Zimbabwe lakini screen ya projector ilionyesha neno Zanzibar!. Hivyo hilo neno Zimbabwe, was a sleep of a tongue tuu yaani aliteleza ulimi ni kosa la kawaida la kibinaadamu!.[
QUOTE]

Kama hivyo ndivyo bado kuna tatizo, Tanzania si muungano wa Zanzibar na Pemba, tusitetee makosa, kakosea jamani na akubali kukosolewa, Kha, utaendaje kwenye media huku una hangover bhana, hujui kuwa unaiwakilisha nchi? au alikua anawazia Perdiem na kinywaji? Mbona yeye anakomalia walimu hivyo? kuna Teacher alikutwa na earphone class basi kamkomalia kinoma haya sasa leo kwake sasa...
 
Back
Top Bottom