Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Mkuu Pasco
Jamaa alkuwa anahofu tu ya kuongea lugha ambayo hakuwa na raha nayo cha msingi ujumbe ulifika na wote waliokuwapo mkutanoni walijua Tanzania imetokana na muungano wa kitu fulani; muhimu ni ujumbe; na isitoshea nina uhakika wajumbe wa mkutano walikuwa na paper hivyo walipata fursa ya kupitia kilichosemwa na Bwana Mulugo.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hivi kaka kwa trend za siasa na hali halisi ya nchi unadhani huo mchemko ungefanywa na kiongozi wa CDM inge make headlines kama ilivyo sasa?

AshaDii dadangu mbona sasa unataka kututoa kwenye mada? hapa tunamzungumzia naibu waziri wa elimu wa JMT, mambo ya vyama vya siasa yanatoka wapi tena? au ndio njia mbadala ya kumnusuru Mulugo na mashambulizi? huyu anatumia kodi zetu kwenda kutuwakilisha kwenye mikutano ya kimataifa watanzania wote sasa akiboronga huko tuna kila haki ya kumshughulikia. Kama unamfahamu kiongozi yoyote ya Chadema aliyeboronga kwenye presentation unaweza kuanzisha thread tumjadili kuliko hivi unavyojaribu kutu divert toka katika hoja ya msingi inayomhusu Mulugo.

Na hata kama kuna viongozi wa Chadema wanaboronga kuongea kiingereza hiyo haiwezi kuwa excuse kwa naibu waziri Mulugo.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani watetezi wa Naibu waziri Mulongo nao kuna jambo wanalikosea...!

Udhaifu wa huyu Mulongo siyo uwezo wake wa "kutamka Kiingereza" wala "kusoma maneno yaliyoandikwa kwa Kiingereza"...!

Udahifu wa Mulongo ni "kutumia ubongo wake kwa ufasaha wakati alipokuwa anasoma ile hotuba" - Kuna shida katika ubongo wake ambayo kwa kiswahili inatafsiriwa kama "ujuzi"...! Mtoto wa miaka mitatu (anayesoma chekechea) ukimpa kitabu asome anaweza kukigeuza "juu chini" na bado akaweza kutambua herufi "a e i o u"...!

Sasa inakuwaje Waziri anashindwa kusoma kilichoandikwa kwenye tarakirishi na kutamka neno lingine tofauti? Na juu ya yote hawezi kutambua kama amekosea au ameteleza ulimi?
 
Mashambulizi ya wadau katika jamii kwa kushindwa kutumia lugha ngeni ya Kiingereza ndio sababu inayofanya Watanzania wengi washindwe kujifunza hio lugha kwa ufasaha kwa woga wa kuchekwa, kebehiwa na hata kusanifiwa ukikosea (mara nyingi hata wakosoaji unakuta pia lugha hawaielewi ila tu bado amcheka mwenzie). Ile sio lugha yake na wala hata makosa katika kukosea... Na ilibidi tu aweke wazi kuwa hio lugha inampiga chenga sababu makosa ni mengi kafanya katika hotuba yake yote.

Hata hivyo hii slip of the tongue ni acceptable kabisa, kosa kubwa lipo kuwa anawakilisha entity ambayo Kimssingi, hairuhusiwi na ni kosa kubwa kutoelewa lugha ya Kiingereza hasa ukizingatia ndio lugha kuu ya maofisini ukiacha Kiswahili. Naamini kwenye 'vipengele husika' vya sifa ya mtu wa ku cover hio nafasi LAZIMA kuna kipengele kinasema mtu awe fluent in English. Sasa sababu serkali yetu inatowa kazi kwa vigezo vya kujuana, connections na upendeleo ndio madhara yake haya...

Katika aibu kwenye conference, katia aibu serkali yake then akatutia aibu na sisi hali tuna watu ni wanastahili hata wangeenda pale wangewakilisha vilivyo.
Dada, majina ya Zanzibar na Zimbabwe ni ya lugha ya kigeni? Kusoma mwaka 1964 kwa lugha ya kiigereza inaweza ikawa tatizo kwa mtu wa lugha nyingine, lakini kusoma majina ya Zanzibar au Zimbabwe kwa mswahili sio tatizo mama!
 
Da AshaDii,
Heshima yako kwanza kabla sijachangia. Nakuunga mkono kabisa kuwa wziri huyu asilaumiwe sana kwenye lugha. Ila pia nadhani tukiangalia maelekezi ya criticism tutaona kuwa kinachozungumzwa kwenye hili sakata, kimsingi siyo umahiri wa lugha.Tunaangalia kwa mapana dhana ya kuwakilishwa na kiongozi wa level ya juu kama Waziri kwenye international conferences. Kuna makosa ya kawaida ya slip of the tongue na haya hayakwepeki huwa yapo lakini mtelezaji hutarajiwa mara moja kujisahihisha.Kuchanganya Zimbabwe ba Zanzibar siyo kiingereza bali ni kosa dogo but with far reaching implications.Kuchanganya tarakimu kwenye mwaka nalo siyo kosa la lugha.

Shukrani, nimezipokea kwa mikono miwili.... Tausi naomba niwe wazi kuwa siku ya kwanza kusikiliza hio clip my first reaction ilikuwa kucheka (utake usitake haiepukiki!); Ikafuata masikitiko, na nikajisemea kuwa bila pointing this out hata yeye Mulugo asingejua kachemka sababu alikuwa akiongea in a way ambayo inaonesha yeye aliona ni sawa. Hata hivyo la kuchanganya Zimbabwe na Zanzibar ni catastrophe na inatowa picha kuwa hata hio hotuba hakuipitia mapema sababu kama angeipitia asingeweza kosea something that straight forward!

Binafsi nimeweza kuona kuwa kuna makundi mawili ya critics kwenye hii ishu.Kuna watu wanaolalamikia maswala ya kimsingi na pia kuna kundi linalojadili umahiri wa lugha. Kwenye lugha nako kuna vitu vya msingi ambavyo kiongozi wa level ya juu kabisa ya uongozi hatarajiwi kuyafanya.Kwenye mikutano ya kimataifa tunarajia " HIGH QUALITY PARTICIPATION( CONTENT WISE) NA HIGH LEVEL OF REPRESENTATION ( BOTH CONTENT AND TRIMMINGS SUCH AS GOOD COMMAND OF LANGUAGE, PRESENTATION SKILLS, PERSONAL APPEARANCE ETC).Hatupaswi kujali sana swagga na kutema yai kwa maana ya lafudhi kwa maana kwenye hadhira za kimataifa utakutana na lafudhi zote - za kihindi, za kiarabu, za kinaijeria, za kikenya,Kisenegali, kihabeshi, za kiganda, kispaniola, kiitaliano nk).Waziri huyu kwa kweli atuombe radhi watanzania kwa kutokutuwakilisha kwa ufanisi na siku nyingine asing'ang'anie kupanda ndege kabla ya maandalizi.

Upande wa Critics ndio hilo ambalo limenifanya niliongelee.... Observe Tausi, majority ni criticism dhidi ya lugha. Ni wachache ambao wanaongelea namna ilivyo wazi kuwa inaonesha hayupo qualified kwa hio nafasi aliyopo na namna ambavyo ni mfano wa mawaziri ambao kazi yao ni walakini sana kama anawajibika. Kwa mtazamo wangu ile hotuba yake yoote inatowa picha ya nidhamu yake katika kazi (hayupo makini); Yupo chini ya nafasi aliyopo (kama naibu waziri wa Elimu, its un-excusable kutojuwa kiingereza); hana ufikiri, busara wala washauri (maana anazidi kuchemka anavyozidi kuli justfy); hivo at the end of the day tupo pamoja katika hoja yako kuhusiana naye.
 
AshaDii Nadhani tatizo la Waziri sio kutomudu kutumia lugha vema, ila tatizo kubwa hana uwezo wa kufanya presentation.. Na kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama hicho ni aibu kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Habari wana jf
naomba mod hii kitu iacheni hivi
msiichangane na maada ya kosa lake

Ikiwa anaojiwa na pj wa cloud fm, wazir huyu amekili kosa kuwa alichanganyikiwa kwani alikuwa anatumia powerpoint na wazir aliyetoka baada ya yeye kuongea ni waziri wa elimu wa zimbabwe nakatika akili yake hakawa bado anafikila naye na then kusema ni kuteleza kwa ulimi tu

Kuhusu mwaka pia amekili ni kosa alivyosema 1~19 6 4 kwenye 19 alimaanisha 9 tu

Lakini sasa kaulizwa je jibu nilipi akasema tanzania ni muungano wa zanzibar, pemba na tanganyika ndio kosa lingine ili kwani ata class one anajibu zuri tu kuwa ni ZANZIBAR ( unguja na pemba) na TANGANYIKA

MY TAKE
Waziri jaribu kudeal sana na watanzania wenzako zaidi, mambo yanayohusu lugha ya nje, n.k muachie doctor K ayafanye

Bado tusubiri
~steven masele
~janeth mbena n.k

V
SENGEREMA

hata mimi naona
 
i know the guy back in 2002,jamaa alkuwa mkuu wa shule pale southern highland mbeya ye ndo alikuwa mwiz namba moja wa mitihan kujipendekeza na usalit ndo vilimpa mashavu
 
Umepewa sh. Ngapi za kuja kumtetea hata aibu huna! Tatizo cc watanzania tunaficha sana udhaifu wetu na hatupendi kujikosoa na kusema ukweli, hainiingii akilini hata kidogo kwa mtu anaye mtetea labda awe ni chizi

Kwa mfano, huwezi ukaniambia ni kosa la kibinadamu wakati udhaifu upo kuanzia kusoma hadi kukosa kujiamini, yeye kama kiongozi hakuonyesha umakini na kujiamini, na kumbuka yeye ni mwalimu sifa kubwa za mwalimu ni kujiamini na kuwa makini.

Huwezi ukawa waziri/naibu waziri ukaongea yale halafu(pemba, zimbabwe na tanganyika) ushindwe hata kujikosoa halafu useme it was a slip of the tongue, kwani aliapa kwa jamhuri ipi?

lazima tukubali viongozi wetu wengine uwezo wao ni mdogo, kama tatizo ni lugha za kigeni watumie kiswahili na kuwepo na mkalimani.
 
Namna Waziri anavyotamka maneno ya kiingereza naona kama alifaa sana kushiriki kwenye lile tangazo la haki Elimu la THIPIUUUU na Pie chart , ni full comedian hakuna cha utetezi hapa, jaribu kufikiri kuwa waziri kama huyu ndio anaenda kutetea maslahi ya Nchi kimataifa sia atabaki anaunga mkono hoja tu hana skills za kujadili hoja kwa kiingereza
 
naomba kuweka angalizo kidogo, wakubwa wamezoea kuandaliwa kilakitu hotuba PPT nk. nimefanya kazi wizarani kwa miaka 9, na tatizo kama hili limejitokeza sana. Lakini mh mulugo hana uzoefu katika kuwasilisha mada mbele za wataalam jamani
 
Kumbe na wewe unadanganyaga ,kama hujjadanganya basi inaelekea hujui vyema
1.Ofisi zipi unazozungumzia kuwa lugha kuu ya mawasiliano ni kingereza !!!!!
2.Ofisi hizo ambbazo lugha kuu ya mawasiliano ni kingereza kikifuatia kiswahili zinawahudumia wanajamii wapi(wanaozungumza na kuelewa lugha gani?)?
3.Sio kweli kuwa kigezo cha kuajiriwa serikali ni kujua kuongea kingereza fluent (Hapa unataka kutuaminisha kuwa kujua kuongea kingereza fluent ndio kipimo cha ufanisi).Fuatilia usahili unafanywa kwa lugha gani. Afisa Ushirika anayeenda kufanya kazi Muleba anaenda kuwasiliana kwa lugha gani na hao anaokwenda kuwahudumia mpaka kigezo kiwe kuongea kingereza fluent..

.......


Mwakalinga hapo namba 1 kuna mambo mengine sio lazima ya ainishwe... Inaweza kuwa haijaandikwa popote lakini hio ni common knowledge kuwa office nyingi nchini lugha ya Kiingereza ni mbadala kwa asiyejua Kiswahili hasa mjini.

Hio ya 3 naona unachukulia kila kitu literally, sijasema hayo in blue... Ila nimesema kuwa 'moja ya' (zingatia tofauti tafadhali..)

Hio paragraph ya mwisho nakubaliana na wewe, na hio inanifanya niwe na wasi wasi kama kweli umelielewa vema bandiko langu, sijamtetea Mulugo kwa lolote zaidi ya kusema kuwa yeye kukosea ni kosa la kibinadamu.

Pia niligusia kuwa kachemka na ilitakiwa awe wazi kusema haelewi lugha na pia nimegusia kuwa hayo ni matunda ya utendaji mbovu wa serkali kwa kuchagua kwa vigezo vya undugu na connections.
 
Hakuna excuse kwenye hili. Mfano ingekuwa ni mtihani wa Uraia,nchi ya Tanzania ilitokana na muungano wa nchi zipi na mwaka gani? Jibu liwe ilitokana na Tanganyika iliyoungana na visiwa vya Bahari ya Hindi vya Pemba na Zimbabwe mwaka 11964 wasahihishaji wangesema kalamu imeteleza? Kosa ni kosa tu hakuna cha utelezi. Viatu alivyovalishwa havimtoshi.
 
kuna mambo ambayo hata kwa kijana makini wa darasa la saba yanatakiwa yawe kwenye finger tips. Pemba na Zimbabwe hazina kawaida ya kutamkwa kwa pamoja (tafuta maandishi yoyote popote). Lakini vilevile labda kama waziri wetu haelewi tafasri ya kiswahili ya aliyokuwa akiyasoma kwa kiingereza. Kwa sababu hakuonekana hata kushtuka kwa lolote, na kama anaelewa tafasri ya aliyokuwa akiyasoma yalikuwa na maana gani kwa kiswahili basi huyo Waziri inawezekana alikunywa kidogo ili kutafuta confidence bandia kumbe kapitiliza. Kwa hivyo suala la kuteleza hapa halipo, LAZIMA KUNA TATIZO.

Lakini pia suala la elimu ya Waziri nalo si la kupuuza unless tuseme elimu haina maana yoyote katika nafasi za kisiasa. Ni kweli kwamba si kila mwenye elimu anaweza kuwa kiongozi, tunachopaswa ni kutafuta walio viongozi na ambao wameelimika kwa namna yoyote tuijuayo. Inawezekana ni mchapa kazi kama anavyotaka kutuaminisha mtoa hoja, lakini ni muhimu vile vile awe mzuri katika ku-communicate.
 
Ama kweli duniani kuna WATU na VIATU! Yaani GAFFE ya Mulugo kwamba Tanzania ni Muungano wa Viswa vya Pemba Zimbabwe na Tanganyika bado wewe unasema ni SLIP OF TONGUE! Tena VIATU hivyo ni vya Kichina.

Hata kama angesema kwamba Tanzania ni Muungano wa visiwa vya Pemba, Zanzibar na Tanganyika bado angekuwa amekosea achilia mbali hiyo Zimbabwe.

Watu huwa tunafanya rehersal kabla ya presentation, inaelekea yeye alitokea CASINO na kwenda kwenye podium bila kufanya rehersal. Nchi za wenzetu makini huyu angekuwa fired immediately baada ya kumaliza presentation kwani makosa aliyofanya ni kibao.
 
It's a human error. Kwangu sikuona issue kubwa, ingawa always natamani watumie lugha ya kwetu. Mbona viongozi wengi wa mataifa makubwa wanatumia lugha za kwao (sio kizungu)...! Ameshatoa ufafanuzi na kuomba radhi nadhani watanzania tuelewe hivyo pia.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom