ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,785
View: https://twitter.com/WBTanzania/status/1724805228581781607?t=rIJGgp2j31MJan_0GHtG-w&s=19
Tanzania imetajwa kuongoza Duniani kwa upelekaji wa huduma ya maji ya bomba Duniani kupitia program ya Lipa kwa Matokeo.
Kupitia programu hiyo jumla ya miradi 1,500 imetekelezwa vijijini na inafanya kazi na kuwezesha upatikanaji wa maji kwa vijijini imefikia 78%.
Mambo kama haya yanawachukiza sana Machadema.
Kazi iendelee 👇
--
Akiongea na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Maji Jumaa Aweso nchini Ethiopia, Makamu wa Rais Kwakwa amesema Tanzania ni mfano bora katika utekelezaji wa Programu ya PforR na ameiomba itoe uzoefu wa mafanikio yake kwa Nchi zaidi ya 23 kutoka kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika zinazoshiriki mkutano wa maji na usafi wa mazingira (WASH Leadership Summit).
Amesema awali Tanzania ilipata Dola za Kimarekani milioni 350 katika miaka mitano lakini ndani ya miaka mitatu ya kwanza ilikuwa imefikisha maji kwa zaidi ya Watu wapya millioni 4.7 vijijini katika mikoa 17. Kufuatia mafanikio hayo, kulingana na matokeo hayo, Benki ya Dunia imeiongezea Tanzania Dola za Marekani milioni 300 na hivyo kupanua wigo wa utekelezaji kufikia mikoa 25, kwa sasa shillingi milioni 970 zimepelekwa katika kila Halmashauri kwa ajili ya kuanza utekelezaji.
Wizara ya Maji imesema mafanikio haya yamefungua rasmi milango ya uendelevu wa programu hii ambayo inafikia ukomo Julai 2025 na kufuatia hoja ya Tanzania ya kuwa na PforR Awamu ya Pili, Benki ya Dunia imeonesha utayari wa kuwa na PforR Awamu ya Pili katika kipindi cha 2025-2030.
Millard