Mbunge Zaytun Swai: Utekelezaji wa Programu Endelevu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Itawasaidia Sana Akina Mama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

MBUNGE ZAYTUN SWAI: PROGRAMU ENDELEVU YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI ITAWASAIDIA SANA AKINA MAMA

Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha tarehe 11 Oktoba, 2023 ameshiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Utekelezaji wa Programu Endelevu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kwa kutumia Utaratibu wa Malipo kwa Matokeo (Program for Results-PforR) mkoani Arusha na kusema Program kwa Upande wa akina Mama itawasaidia sana.

"Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua kero za wananchi hususani zile zinazogusa mwananchi moja kwa Moja. Tarehe 11 Oktoba, 2023 Mkoa wa Arusha tumezindua rasmi programu endelevu ya Maji Vijijini ambao utagharimu takribani Bilioni 4.8" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.

"Mradi wa Uzinduzi wa Utekelezaji wa Programu Endelevu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kwa kutumia Utaratibu wa Malipo kwa Matokeo (Program for Results-PforR) mkoani Arusha utakuwa ni msaada mkubwa hususani kwa Wilaya za pembezoni ambazo zinachangamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji" - Mhe. Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha.

"Shughuli kubwa ya wananchi wengi ni Ufugaji na Kilimo ambacho kinategemea sana upatikanaji wa Maji ya uhakika kwa Maisha yao kama binadamu lakini hata kwa Mifugo na shughuli za Kilimo. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuamua na Arusha kuwa sehemu ya Programu hii ni jambo kubwa sana la kumshukuru" - John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Mama Yupo Kazini! Maji Bombani ni Lazima!
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.08.jpeg
    27.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.03.02.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.03.02.jpeg
    29.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.12.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.12.jpeg
    43 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.09(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-12 at 15.00.09(1).jpeg
    32.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom