Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Watu wanapiga pesa ndefu kujifanya wanapeleleza
 
Je sheria inakataza kushitaki kampuni inayoishi mkoa A kushitakiwa katika mkoa b ambako ndipo ilipoingia makubaliano?katika mkoa b
 
Mi naomba kuuliza,kwa nini kesi za Aridhi katika mabaraza ya Aridhi zinachukua muda mrefu sana!?
 
Ni ipi mipaka ya kiutendaji kati ya wizara hii na zingine kama ya mambo ya ndani au habari, utamaduni na michezo? Maana ni mara kadhàa tumeona waziri wa wizara hii akisimama na kutoa kauli ambazo zingefaa kutolewa na wizara zingine? Mf. Kuzuia usambazaji wa habari flani n.k
 
Kati ya wizara zilizo but, wizara yenu inaongoza. Mapungufu mengi ya kusheria yametokea mkiwa kimya, eg rais kuzuia uuzaji wa bia mchana huku sheria ya vileo ipo wazi, wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka watu sero, wakuu wa wilaya na watendaji kuwaweka sero walio kosa hela kulipa vitambulisho vya wajasiria mali. Ni mengi mno lakini hata mara moja hamjawahi sikika mkitoa japo ufafanuzi.
 
Ni maoni mazuri. Hata hivyo, sheria inampa nafasi ya kufungua kesi ya madai ili kulipwa fidia. Ni haki yake kisheria na atapatiwa stahiki zake akifuata utaratibu huo.
Wapo walio thubutu kufungua hayo madai, lakini hawakuwahi fika tena mahakamani mpaka kesi zinafutwa. Siku moja kabla ya siku ya kesi mhusika anashikwa na kuwekwa mahabusu! Kinadharia mfumo wetu wa sheria ni mzuri, kiuhalisia haufai.
 
Mmezingatia Kweli suala la ukosefu wa Ajira na Upana wake kwa Tanzania?
 
Hakuna wajanja kama wanasheria. Wamejivua majukumu yote na kulipa sheri. Hakimu anahukumu vibaya kwa kupokea rushwa, akishinda rufaa, anaambiwa hakimu wa mwanzo aliongozwa vibaya na sheria(s/he was mislead by the law!)
 
'mapanya wengi hawachimbi shimo likaenda' idadi ya wajumbe wa bunge la katiba ilikuwa kubwa mno kufanikisha lolote la maana. Muda mwingi ukatumika kutunga kanuni.
 
Hakuna wajanja kama wanasheria. Wamejivua majukumu yote na kulipa sheri. Hakimu anahukumu vibaya kwa kupokea rushwa, akishinda rufaa, anaambiwa hakimu wa mwanzo aliongozwa vibaya na sheria(s/he was mislead by the law!)
Hata baada ya kuonekana imem-mislead hakimu, bado sheria hiyo inayomislead mahakimu haibadirishwi..!!
 

Kwanza asanteni kwa kuanzisha huu uzi hapa ni jambo jema.

Majibu yenu kwa mdau ( man dunga ) yanaleta maswali mengi zaidi kuhusu sheria ya mafao. Kwanza, Je ni kweli Selikari na wizara haina taarifa kuwa kuna tatizo kubwa la ajira Tanzania? Mifano ni mingi sana na mojawapo ni zile nafasi za ajira zilizotangazwa na TRA mwaka jana nafasi ni moja wanaomba watu zaidi ya 1000 au zaidi, sasa kama kuna tatizo la ajira na ni kubwa kwanini mseme mwenye taaluma ana nafasi kubwa ya kuajiriwa, hao waliopo mtaani na wakakosa ajira hawana taaluma?

Swali lingine, Je kila mwenye taaluma anihitaji kufanya kazi hadi uzeeni (hili pia limeulizwa na DeepPond )? ni lini mlifanya utafiti mkagundua kuwa watanzania wanahitaji kufanya kazi mpaka wawe wazee ndio muwalipe mafao yao?

Kingine hamuoni kuwa huu ubaguzi unapunguza uwezekano wa kufunguliwa kwa biashara endelevu, maana kama utampatia mtu mwenye taaluma mafao yake angali bado ana nguvu za kufikiria na hali ya kufanya kazi (akiwa kijana) uwezekano wa yeye kuwekeza kwa kuanzisha biashara ni mkubwa hivyo kuongeza nafasi za jira na mapato katika nchi na kuleta ukuaji wa uchumi. Sasa kwa sheria hii ni wangapi wanashindwa kufanya hivyo na badala yake mmewafanya wawe watu wa kutegemea ajira?
 
Swali: kwanini faini za barabarani ni sawa kwa vyombo vyote vya usafiri? mfano pikipiki ni elfu 30 sawa na 113 scania, kwanini faini isiwe kulingana na ukubwa wa gari? hii kitu inachochea rushwa sababu bodaboda atatoa wapi fedha za kulipa faini na badala yake ana amua kutoa rushwa
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

YAANI KAJIPATIA BIL309 ISIVYO HALALI FAINI BIL29
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…