Wizara ya Fedha: Tanzania ipo kwenye viwango vizuri vya kuendelea kukopesheshwa kati ya nchi chache

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1709704021951.png

Madeni ya nchi nyingi za Afrika yanakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa viwango vya riba na kubadilisha fedha duniani na kusababisha kushuka kwa thamani ya fedha za ndani.

Hayo yamebainishwa Mjini Victoria Falls, Zimbabwe, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati wa Mkutano wa 56 wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi kutoka nchi za Umoja wa Afrika unaoratibiwa na Kamisheni ya Uchumi chini ya Umoja wa Mataifa (UNECA)

Bw. Mwandumbya alisema kuwa awali ukuaji wa deni ulikuwa unaendana na ukopaji lakini kwa sasa imebainika kuwa kuna sababu zingine zinazochochea kuongezeka kwa deni hilo ikiwa ni pamoja na mabadiliko makubwa ya viwango vya kubadilisha fedha na riba hivyo kuzifanya nchi za Afrika kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto hiyo.

Alisema kuwa katika kulihudumia deni “dept service” lililoongezeka, kumekuwa na changamoto kubwa kwa sababu nchi nyingi bado hazina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha kuweza kugharamia huduma mbalimbali.

“Sisi Tanzania tunashukuru kwa kuwa kupitia Taasisi za Kimataifa za Moody’s na Fitch zinazojihusisha na ufanyaji tathimini kwa nchi ili kujua uwezo wake wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, wamethibitisha kwamba nchi yetu ipo kwenye viwango vizuri vya kuweza kuendelea kukopesheshwa miongoni mwa nchi chache”, alisema Mwandumbya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, alisema kuwa dhumuni la mkutano huo wa 56 ni kubadilishana mawazo na hasa kwenye kauli mbiu inayosema Financing the Transition to Inclusive Green Economies in Afrika inayotoa hamasa na kutafakari njia ambazo zinaweza kutumika kufadhili Uchumi na kufanya uwekezaji ambao unazingatia mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo wa 56 unaoratibiwa na UNECA ni Jukwaa ambalo limeanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kuzisaidia nchi za Afrika kufanya mijadala na tafiti mbalimbali ili kuzalisha na kufanya ubunifu utakaokuza uchumi hivyo kutengeneza fursa ya kujadiliana na kuhakikisha ushauri unaotolewa unaendana na mazingira halisi.
 
Hiyo sio kauli ya kusema.
Tunapaswa kujua hiyo mikopo Inafanya shughuli gani hasa. Hesabu zake ni zipi?
Mfano mkopo A umefanya shughuli B kwa ukamilifu na gharama ni hizi
 
Makamu wa Rais, Dr Mpango anasemaje yeye, ukizingatia alikuwa waziri wa fedha awamu ya Tano?
 
Siku ningemsikia baba angu mzazi anatamba mtaani kwamba bado anakopesheka kwenye duka la mangi pale mtaani walahi ningemlamba makofi
 
Makamu wa Rais, Dr Mpango anasemaje yeye, ukizingatia alikuwa waziri wa fedha awamu ya Tano?
Kutegemea mikopo sio sifa nzuri kwa nchi ambayo ina uwezo wa kujitegemea kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha!! Ni aibu iliyoje.
 
Hawa viongozi wanatuona mataahila! Hawana aibu! Madeni kibao, matokeo kiduchu, afu jamaa anabwajaja tu anadhani sisi ni manyani!
 
Hiyo sio kauli ya kusema.
Tunapaswa kujua hiyo mikopo Inafanya shughuli gani hasa. Hesabu zake ni zipi?
Mfano mkopo A umefanya shughuli B kwa ukamilifu na gharama ni hizi
Kwanza kuwa na uwezo wa kukopa siyo sifa ya kujivunia. Hii inaonyesha viongozi wetu walivyo mbumbumbu na huwaza kukopa kila muda.
 
Kwahio tunaendelea kukopa mpaka pale tutakaposhindwa kukopesheka ?; Sio kwamba tujitahidi na sisi tuanze kukopesha...
 
Back
Top Bottom