Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,006
Mimi nilisikia sehemu ndogo tu ya aliyokuwa anasema. Ni kweli pengine kauli aliyoitoa ni kama vile inasupport 'sheria mkononi'. Hata hivyo nadhani critics wake wanajaribu kuyatoa manano yake kwenye context ili kummaliza kisiasa.
Pinda katika kukemea mauwaji ya albino na kuonesha possible immediate conseqences za kuua albino alitoa mfano akijaribu kujiweka katika nafasi ya kama mmoja wa wanakijiji.
Sina uwezo wa kukumbuka neno kwa neno (inawezekana nimepunguza au kuongeza) lakini ile context yake ilikuwa kama hivi:
"Umeua albino, kukata viungo vyake na nakukimbia navyo. Tunakufukuza na kukukamata, je tukupeleke polisi tusubili uhukumiwe na mahakama? Hatutaweza kusubiri, tutakuuwa tu!"
bado hili halijibu swali: Hivi majuzi hapa Detroit afisa mmoja wa jiji alilazimika kujiuzulu baada ya kuiita mahakama ya hapa kuwa ni "Ghetto court"; huko nyuma mtangazaji Imus alilazimika kuacha kibarua chake baada ya kuwaita wachezaji wa timu fulani hivi kuwa wana "snappy hair" na kutumia jina la "hore" Hivi majuzi Prince Harry amelazimika kuomba radhi kwa jamii ya wahindu baada ya kuelezea kilemba cha singasinga alichovaa mwanajeshi mwenzake kuwa ni "rag" (tambala).
Mifano ya matumizi ya maneno na jinsi watu wanawajibishwa kutokana kwayo ipo mingi. Kwanini? Kwa sababu maneno yana nguvu mno. Tumeshuhudia nguvu ya maneno katika mauaji ya kimbari kule Rwanda na jinsi gani waliokuwa madarakani kwa maneno ya mzaha mzaha hivyo walichochea mauaji hayo kwa kuwaita wale waliowakusudia kuwa ni "cockroaches".
Kwa wengine maneno ya Waziri Mkuu ni "alimaanisha" nini. Siku chache zijazo tukisikia kuna watu wameuawa Shinyanga "wakiaminiwa" kujihusisha na mauaji ya Albino tutashindwa kabisa kuelewa ni kwanini. Hata hivyo, sisi wenyewe (baadhi yetu) hatuoni ubaya wa kumwadhibu mtu kwa sababu "tuna ushahidi" kashika mkono wa Albino ameunyofoa na "anakimbia nao". Kwetu sisi huo ni "ushahidi wa wazi".
Mawazo haya ndiyo yanayowafanya vibaka watiwe viberiti kwa sababu wamekutwa wakimchomolea mtu na mtu kamkamata sasa ushahidi wa nini? Katika mawazo ya namna hiyo tutaona kuwa mahakama haiitajiki.
Dalili zote naamini hayo ndiyo mawazo ya Waziri Mkuu. Niko tayari kusahihishwa kwa mtu kuweka hadharani kile hasa alichosema Waziri Mkuu.
Kuna wanaotaka tuamini kuwa Waziri Mkuu alinukuliwa nje ya maudhui ya alichokuwa anazungumzia. Hilo linaweza kuthibitishwa kwa urahisi kweli.. toeni rekodi ya hotuba hiyo ya Waziri Mkuu, uncut and unedited kama walivyoisikia wale warugaruga!