Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

Mimi nilisikia sehemu ndogo tu ya aliyokuwa anasema. Ni kweli pengine kauli aliyoitoa ni kama vile inasupport 'sheria mkononi'. Hata hivyo nadhani critics wake wanajaribu kuyatoa manano yake kwenye context ili kummaliza kisiasa.

Pinda katika kukemea mauwaji ya albino na kuonesha possible immediate conseqences za kuua albino alitoa mfano akijaribu kujiweka katika nafasi ya kama mmoja wa wanakijiji.

Sina uwezo wa kukumbuka neno kwa neno (inawezekana nimepunguza au kuongeza) lakini ile context yake ilikuwa kama hivi:

"Umeua albino, kukata viungo vyake na nakukimbia navyo. Tunakufukuza na kukukamata, je tukupeleke polisi tusubili uhukumiwe na mahakama? Hatutaweza kusubiri, tutakuuwa tu!"

bado hili halijibu swali: Hivi majuzi hapa Detroit afisa mmoja wa jiji alilazimika kujiuzulu baada ya kuiita mahakama ya hapa kuwa ni "Ghetto court"; huko nyuma mtangazaji Imus alilazimika kuacha kibarua chake baada ya kuwaita wachezaji wa timu fulani hivi kuwa wana "snappy hair" na kutumia jina la "hore" Hivi majuzi Prince Harry amelazimika kuomba radhi kwa jamii ya wahindu baada ya kuelezea kilemba cha singasinga alichovaa mwanajeshi mwenzake kuwa ni "rag" (tambala).

Mifano ya matumizi ya maneno na jinsi watu wanawajibishwa kutokana kwayo ipo mingi. Kwanini? Kwa sababu maneno yana nguvu mno. Tumeshuhudia nguvu ya maneno katika mauaji ya kimbari kule Rwanda na jinsi gani waliokuwa madarakani kwa maneno ya mzaha mzaha hivyo walichochea mauaji hayo kwa kuwaita wale waliowakusudia kuwa ni "cockroaches".

Kwa wengine maneno ya Waziri Mkuu ni "alimaanisha" nini. Siku chache zijazo tukisikia kuna watu wameuawa Shinyanga "wakiaminiwa" kujihusisha na mauaji ya Albino tutashindwa kabisa kuelewa ni kwanini. Hata hivyo, sisi wenyewe (baadhi yetu) hatuoni ubaya wa kumwadhibu mtu kwa sababu "tuna ushahidi" kashika mkono wa Albino ameunyofoa na "anakimbia nao". Kwetu sisi huo ni "ushahidi wa wazi".

Mawazo haya ndiyo yanayowafanya vibaka watiwe viberiti kwa sababu wamekutwa wakimchomolea mtu na mtu kamkamata sasa ushahidi wa nini? Katika mawazo ya namna hiyo tutaona kuwa mahakama haiitajiki.

Dalili zote naamini hayo ndiyo mawazo ya Waziri Mkuu. Niko tayari kusahihishwa kwa mtu kuweka hadharani kile hasa alichosema Waziri Mkuu.

Kuna wanaotaka tuamini kuwa Waziri Mkuu alinukuliwa nje ya maudhui ya alichokuwa anazungumzia. Hilo linaweza kuthibitishwa kwa urahisi kweli.. toeni rekodi ya hotuba hiyo ya Waziri Mkuu, uncut and unedited kama walivyoisikia wale warugaruga!
 
Mwanakijiji,

Umeamua kuendeleza jambo lisilo na ukweli wowote.Nilikuonya asubuhi ila unaendelea tena kwa staili mpya,ulitaka kutumia pesa kupata habari ukashindwa..kwa faida ya nani sasa.?tujadili inshu za maana na siyo hili jambo lisilo na manufaa

Kuna tatizo la waandishi wetu tulio nao nyumbani.wanakurupuka wakisikia neno moja tu .

Mhe. Pinda hakusema maneno ya gazeti la Mwananchi
 
alisema nini?
 
alisema nini?
Waziri mkuu alisema kuwa ili kukomesha mauaji ya Malbino unaweza tumia sheria Mkononi bila kusubiri mahakama.Sheria mknoni siyo kuua mtu ila hata kumkamata mtu ni kujichukulia sheria mkononi.

Naungana na maneno ya Mkapa aliyowahi kuyasema siku moja,Tanzania ya sasa imejaa watu wanopenda siasa za chuki,wanaweza eneza jambo fulani ili mtu flani achukiwe na Jamii hata akiwa ni mwema.

Na siku zote nimekuwa nikionya kuhusiana na Hili.Mwanakijiji na wewe unatak kukubali kutumika kwa hili kama mtaji?Na hii ndiyo sababu kubwa ya Watanzania kutochagua wapinzani hata kama CCM imewachosha..

Habari hiyo ukiipata kwa pesa nyingi itakusaidia nini?Una lengo gani?na kwa faida ya nani mpaka utumie pesa nyingi kuiasi hicho?ina mana Huwa unanunu Habari?
 
Mwanakijiji,

Hiyo pesa mchangie tu Maxenco kwa ajili ya JF.Au ipeleke Nyumbani.

unataka kusema kuna mpango flani umeandaliwa?
 
irrelevant.

Nikipata alichosema Waziri Mkuu na kumsikia kwa masikio yangu nitaamua alimaanisha nini then naweza kuform my well informed opinion. Kutumia pesa kununua habari siyo jambo geni duniani au kwenye vyombo vya habari. Habari nayo ni bidhaa inanunuliwa na kununulika. Kama unayo hiyo clip nitumie hata bure basi.
 
Mzee Mwanakijiji,

KWa taarifa nilizo nazo ni kuwa Mwananchi na TAnzania Daima walimnukuu vibaya Waziri Mkuu,I mean wameelewa vibaya kauli aliyosema nakwa maana nyingine walikimblia kusema jambo la kufikirika kwanza.

hata mimi nitaarifa hizo hizo, tatizo hakuna mtu aliyeweka hadharani alichosema Waziri Mkuu so the questions still linger.

Waziri mkuu alisema kuwa ili kukomesha mauaji ya Malbino unaweza tumia sheria Mkononi bila kusubiri mahakama.Sheria mknoni siyo kuua mtu ila hata kumkamata mtu ni kujichukulia sheria mkononi.

weka kauli yake ilikuwa ipi hasa kutokana na taarifa ulizonazo. kusema "alisema".. haitoshi. Kama hujui alichosema si vibaya kumuacha mtu mwenye kujua aseme. Tatizo ni nini, au hatutakiwi kuhoji alichosema Waziri Mkuu kwa vile ni "Waziri Mkuu"?
 
Mwanakijiji,

Hiyo pesa mchangie tu Maxenco kwa ajili ya JF.Au ipeleke Nyumbani.

unataka kusema kuna mpango flani umeandaliwa?

umefikia mahali pa kunipangia fedha yangu niitumie vipi. dau limepanda kufikia dola 200 kwa yeyote atakayenipatia hotuba ya Waziri Mkuu Pinda huko Shinyanga, uncut and unedited. Kama JF itaiweka hotuba hiyo nimeshasema nitawapatia kiasi hicho.

Kwa vile unayo hiyo hotuba kwanini usiiweke hapa ili nitoe kiasi hicho kwa JF?
 
Kwa siku kadhaa sasa hivi kile ambacho alisema Waziri Mkuu kuhusu wauaji wa Albino kinabakia kuwa siri kubwa. Kumekuwa na jitihada za makusudi kabisa kuficha alichosema Waziri Mkuu.

Huu ulikuwa ni mkutano wa hadhara, wewe muandishi wa habari huwezi kusema alichosema Waziri Mkuu kinafichwa! Kituko!

Huwezi kutegemea, huwezi kusubiri, Ofisi ya Waziri Mkuu ikupe nakala ya hotuba, offcourse wataifanyia ukarabati!

Ni sawa na kusema waandishi na wabunge wanasubiri Ikulu itoe nakala ya hotuba ya Rais bungeni. Kwani alipoisoma alikuwa amejifungia chumbani na familia yake???? I mean, how preposterous is that?

Mkutano kuhusu the most pressing issue at the time, mauaji ya albino halafu hakuna press person hata mmoja aliyekuwepo, au aliyekuwa na ki-recorder. Makampuni ya uandishi Bongo yanashindwa kuwa na ki-SONY recorder cha dola 40 cha Best Buy?

Crummy crummy crummy press!

Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Exactly what I was fearing. I mean, I knew these could not be seasoned press people. Absolutely impossible. Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all.

Hakuna anaejua Pinda katamka nini Mwanza. Hakuna anaejua Mkapa katamka nini Zanzibar with this "kakiri makosa" story. Hakuna anaejua Mwakyembe katamka nini Mbeya juzi akiwacharura wapinzani. Matokeo yake ndio inabidi ukamuulize Mwakyembe mwenyewe "eti ulisema hukusema"? Offcourse atakuyeyusha, atakupa tafsiri mpya kama anavyojisikia, utamuitikia itikia hapo wee, halafu anakuona hujui lolote anakupa sasa mpaka tafsiri za Pinda wakati yeye mwenyewe hakuwepo, na wewe na mimi msikilizaji wote hatukuwepo, na yeye unaemuuliza anasema hajui kilichosemwa. But he is good enough kukutafsiria. Labda sasa tuwaombe kina Shekhe Yahaya wawe wanatuambia yanayosemwa popote pale kwa kutumia some telepathic means or something. Nobody knows nothing. Press yetu masikini weee!

"Kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu..."!

Such cheesy press!
 
Kwa siku kadhaa sasa hivi kile ambacho alisema Waziri Mkuu kuhusu wauaji wa Albino kinabakia kuwa siri kubwa. Kumekuwa na jitihada za makusudi kabisa kuficha alichosema Waziri Mkuu.

Jana katika taarifa ya habari ya saa mbili (za usiku) TBC ilizungumzia jinsi NCCR ilivyotoa tamko la kulaani mauaji ya Albino. Wao wakaongezea na kusema kuwa Waziri Mkuu alisema kuwa wale wanaohusika na mauaji ya Albino "washughulikiwe kwa mujibu wa sheria".

Nimepata nafasi ya kuzungumza na watu wengi weekend hii kupata hasa alichosema Waziri Mkuu karibu wote wanazungumzia kile "alichomaanisha". Nimegundua hakuna anayesema hasa kile "alichosema".

Je ni kweli Waziri Mkuu alitoa kauli hizi kama zilivyonukuliwa na Mwananchi?:

na hii hapa kuhusu UVCCM kushiriki katika kukomesha mauaji ya albino, labda kwa kuangalia (a) hapo juu.

Naamini hakuna "maelezo" au "taarifa kwa vyombo vya habari" ambayo inajibu swali la nini hasa Waziri Mkuu alisema.

Kuna njia moja tu ya kuamua kwa haki kauli ya Waziri Mkuu ilikuwa ni ipi hasa maana uwezekano kuwa Waziri Mkuu wetu akizungumza kwa niaba ya "viongozi wote" na kwa jina la serikali kwamba amewaambia watu wa kijijini kuwa wanaweza kuua with impunity inatisha. Hofu yangu siyo kwa wasomi wa kisheria na watu ambao wanaweza kuelewa "alichomaanisha" bali wale watu ambao walikuwa wanamsikiliza walisikia nini hasa.

Sisi wengine wanaweza kutuzuga kuwa alimaanisha nini lakini wale Sungusungu, na wanakijiji kule Shinyanga walivyomsikia watakuwa na utata wowote wa kuelewa alichomaanisha?

Mimi nilisikiliza mahojiano kati ya mbunge wa viti maalumu (albino) aliyekuwa ameaambatana na PM siku hiyo akihojiwa na mwandishi wa habari wa Radio Wapo FM kuhusu kauli ya PM na yeye alirudia kauli ya 'Jino kwa jino' huku akisema, 'Nami naunga mkono wanaoua albino wauawe. Tumechoka na watu wa namna hii,' alisema huyo mbunge.

Nilisikitika sana! Yaani, kuondoa uovu kwa kufanya uovu mwingine na kujiona kuwa kufanya huo uovu mwingine ni sahihi kabisa au kunatofautiana na ule wa kwanza?
 
Huu ulikuwa ni mkutano wa hadhara, wewe muandishi wa habari huwezi kusema alichosema Waziri Mkuu kinafichwa! Kituko!

Huwezi kutegemea, huwezi kusubiri, Ofisi ya Waziri Mkuu ikupe nakala ya hotuba, offcourse wataifanyia ukarabati!

Ni sawa na kusema waandishi na wabunge wanasubiri Ikulu itoe nakala ya hotuba ya Rais bungeni. Kwani alipoisoma alikuwa amejifungia chumbani na familia yake???? I mean, how preposterous is that?

Mkutano kuhusu the most pressing issue at the time, mauaji ya albino halafu hakuna press person hata mmoja aliyekuwepo, au aliyekuwa na ki-recorder. Makampuni ya uandishi Bongo yanashindwa kuwa na ki-SONY recorder cha dola 40 cha Best Buy?

Crummy crummy crummy press!

Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Exactly what I was fearing. I mean, I knew these could not be seasoned press people. Absolutely impossible. Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all.

Hakuna anaejua Pinda katamka nini Mwanza. Hakuna anaejua Mkapa katamka nini Zanzibar with this "kakiri makosa" story. Hakuna anaejua Mwakyembe katamka nini Mbeya juzi akiwacharura wapinzani. Matokeo yake ndio inabidi ukamuulize Mwakyembe mwenyewe "eti ilisema hukusema"? Offcourse atakuyeyusha, atakupa tafsiri mpya kama anavyojisikia, utamuitikia itikia hapo wee, halafu anakuona hujui lolote anakupa sasa mpaka tafsiri za Pinda wakati yeye mwenyewe hakuwepo, na wewe na mimi msikilizaji wote hatukuwepo, na yeye unaemuuliza anasema hajui kilichosemwa. But he is good enough kukutafsiria. Labda sasa tuwaombe kina Shekhe Yahaya wawe wanatuambia yanayosemwa popote pale kwa kutumia some telepathic means or something. Nobodies knows nothing. Press yetu masikini weee!

"Kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu..."!

Such cheesy press!

Amen Amen!JF kuna vichwa vinachambua kama karanga!
 
Huu ulikuwa ni mkutano wa hadhara, wewe muandishi wa habari huwezi kusema alichosema Waziri Mkuu kinafichwa! Kituko!

cover up inawezekana mahali popote. Soma taarifa ya awali ya Mwananchi utaelewa nazungumzia nini. Kuwa ni mkutano wa hadhara haina maana haiwezekani kujaribu kuficha habari hiyo kufika kwenye hadhara kubwa. Hujawahi kusikia Jaji mmoja aliyeta waandishi wazime kamera alipokuwa anazungumza kwenye hadhara moja, na baadaye akawaomba radhi? Siyo geni kuwa linalosemwa kwenye hadhara ndogo, likajaribu kuzuiliwa kufikia hadhara kubwa.

Kwa mchambuzi uliyebobea inashangaza hulijui hilo.

Huwezi kutegemea, huwezi kusubiri, Ofisi ya Waziri Mkuu ikupe nakala ya hotuba, offcourse wataifanyia ukarabati!

Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo wazungumzaji wa Waziri Mkuu. Ni wao kwanza wanaotakiwa kuzungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu. Ni wao ndiyo wanatarajiwa kutoa taarifa sahihi bila kukarabati. Sasa kama hawafanyihilo, hilo ni suala jingine.

Hujui watu wakitaka habari za White House wanaenda kwa msemaji wa Ikulu hiyo? Hili wewe kutolijua, nalo inashangaza.
Ni sawa na kusema waandishi na wabunge wanasubiri Ikulu itoe nakala ya hotuba ya Rais. Kwani hiyo hotuba alipoitoa alikuwa amejifungia chumbani na familia yake???? I mean, how preposterous is that?

Hii inashangaza kwa mtaalamu wa vyombo vya habari kama wewe. Ulitegemea nani atoe hotuba ya Rais kwa waandishi, idara ya ugavi wa umeme? Katika demokrasia au nchi inayojaribu kujenga demokrasia nikitaka hotuba ya Rais naipata toka Ikulu. Huko kwingine ni kulinganisha tu. Zaidi ya yote sitarajii idara ya serikali kupindisha kile alichosema Rais au Waziri. Hili kutolifahamu nalo inashangaza.

Mkutano kuhusu the most pressing issue at the time, mauaji ya albino halafu hakuna press person hata mmoja aliyekuwepo, au aliyekuwa na ki-recorder. Makampuni ya uandishi Bongo yanashindwa kuwa na ki-SONY recorder cha dola 40 cha Best Buy?

Kwa jinsi ambavyo unazungumza kwa uhakika kuwa "hakuna press person hata mmoja" inadai ukweli. Unataka watu waamini kuwa hakuna mwenye recorder n.k Hili ndilo tatizo la uchambuzi wako. Waziri Mkuu alirekodiwa na ukisoma taarifa ya awali, ilifanyika juhudi ya wazi ya kuzuia waliorekodi kwenda na hotuba hiyo. Allirekodiwa na ofisi ya Waziri Mkuu na waandishio wa habari. Kama umesikiliza BBC siku ile ungesikia clip ya hotuba toka kwa Eric Nampesya sasa unafikiri ilirekodiwa kwenye muwa?

Crummy crummy crummy press!

No sir, this is crummy crummy crummy pseudo-analysis!

Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Exactly what I was fearing. I mean, I knew these could not be seasoned press people. Absolutely impossible. Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all.

Well, hii kama imani yako ndiyo hiyo ni wazi kuwa tukiangalia uchambuzi wa vyombo vya habari ndiyo shoddiest of all. Mwakyembe hakusema "waandishi ni watoto wa shule". Inashangaza jinsi gani kwa mchambuzi uliyebobea kushindwa kupata alichosema Mwakyembe. Sikiliza vizuri alichosema.

Hakuna anaejua Pinda katamka nini Mwanza. Hakuna anaejua Mkapa katamka nini Zanzibar with this "kakiri makosa" story. Hakuna anaejua Mwakyembe katamka nini Mbeya juzi akiwacharura wapinzani.

ndiyo maana watu wanauliza maswali, vinginevyo tusingeuliza. Kuuliza mtu alichosema au kutafuta kilichosemwa siyo kosa au ubaya. NI sehemu ya jukumu la kutafuta ukweli.

Matokeo yake ndio inabidi ukamuulize Mwakyembe mwenyewe "eti ilisema hukusema"? Offcourse atakuyeyusha, atakupa tafsiri mpya kama anavyojisikia, utamuitikia itikia hapo wee,

Tatizo ni kuwa unafikiri kutafuta clarification ya alichosema mtu kutoka kwa mtu mwenyewe ni makosa. Kama alinukuliwa na sisi tunamuuliza alinukuliwa sahihi kosa liko wapi?

halafu anakuona hujui lolote anakupa sasa mpaka tafsiri za Pinda wakati yeye mwenyewe hakuwepo, na wewe na mimi msikilizaji wote hatukuwepo, na yeye unaemuuliza anasema hajui kilichosemwa. But he is good enough kukutafsiria.

Bila ya shaka ningekuwa mtu wa kuridhika ningeridhika jana na majibu ya Mwakyembe. Unafikiri mimi si kunote hicho na ungesikia nilichomuuliza ni kwamba kama ikijafahamika kuwa Waziri Mkuu alisema anachodaiwa kusema kama atabadili maoni yake (tafsiri yake). Jibu lake lilikuwa nini?

Labda sasa tuwaombe kina Shekhe Yahaya wawe wanatuambia yanayosemwa popote pale kwa kutumia some telepathic means or something. Nobodies knows nothing. Press yetu masikini weee!

Sasa wale wachambuzi wanaojua wenyewe tuwaweke kundi gani kama wanashindwa kujua vitu vidogo kama hivi tunavyovizungumzia?

"Kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu..."!

Such cheesy press!

Kwamba kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu kufikia hadhara kubwa halina shaka. Such cheesy and shallow analysis of the media.
 
Na siku zote nimekuwa nikionya kuhusiana na Hili.Mwanakijiji na wewe unatak kukubali kutumika kwa hili kama mtaji?Na hii ndiyo sababu kubwa ya Watanzania kutochagua wapinzani hata kama CCM imewachosha.

Mbona unakimbia kivuli chako?
 
Mods!naomba thread niliyoanzisha regarding the same issue ihamie humu!
 
Amen Amen!JF kuna vichwa vinachambua kama karanga!

Amen Amen, Kuna vichwa na vichwa katika uchambuzi. Lakini kiukweli kuna kichwa ambacho ni zaidi ya vichwa; kwani siku zote huchambua kama karanga. Mungu abariki tumbo lililobeba kichwa hiki !
 
Huu ulikuwa ni mkutano wa hadhara, wewe muandishi wa habari huwezi kusema alichosema Waziri Mkuu kinafichwa! Kituko!

Huwezi kutegemea, huwezi kusubiri, Ofisi ya Waziri Mkuu ikupe nakala ya hotuba, offcourse wataifanyia ukarabati!

Ni sawa na kusema waandishi na wabunge wanasubiri Ikulu itoe nakala ya hotuba ya Rais. Kwani hiyo hotuba alipoitoa alikuwa amejifungia chumbani na familia yake???? I mean, how preposterous is that?

Mkutano kuhusu the most pressing issue at the time, mauaji ya albino halafu hakuna press person hata mmoja aliyekuwepo, au aliyekuwa na ki-recorder. Makampuni ya uandishi Bongo yanashindwa kuwa na ki-SONY recorder cha dola 40 cha Best Buy?

Crummy crummy crummy press!

Hata Mwakyembe jana ame vindicate ninacho ki-guess kila siku humu kwamba waandishi ni watoto wa shule. Mwakyembe kasema mwandishi wa MwanaHALISI aliyemnukuu juzi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Nyegezi. Exactly what I was fearing. I mean, I knew these could not be seasoned press people. Absolutely impossible. Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all.

Hakuna anaejua Pinda katamka nini Mwanza. Hakuna anaejua Mkapa katamka nini Zanzibar with this "kakiri makosa" story. Hakuna anaejua Mwakyembe katamka nini Mbeya juzi akiwacharura wapinzani. Matokeo yake ndio inabidi ukamuulize Mwakyembe mwenyewe "eti ilisema hukusema"? Offcourse atakuyeyusha, atakupa tafsiri mpya kama anavyojisikia, utamuitikia itikia hapo wee, halafu anakuona hujui lolote anakupa sasa mpaka tafsiri za Pinda wakati yeye mwenyewe hakuwepo, na wewe na mimi msikilizaji wote hatukuwepo, na yeye unaemuuliza anasema hajui kilichosemwa. But he is good enough kukutafsiria. Labda sasa tuwaombe kina Shekhe Yahaya wawe wanatuambia yanayosemwa popote pale kwa kutumia some telepathic means or something. Nobodies knows nothing. Press yetu masikini weee!

"Kuna jitihada za kuficha alichosema Waziri Mkuu..."!

Such cheesy press!

Sikubaliani na wewe kabisa kwa hoja hii "Journalism in Tanzania is the shoddiest profession of all." Ila ninachojua you are arguing from ignorance of what journalism is and what it entails! Kama unayosema kuhusu waandishi wa habari ni kweli basi viongozi wetu wengi (au tu Watz wengi) wangekuwa kwenye taaluma ya uandishi wa habari kwa kuona namna wanavyowajibika au ripoti kuhusu matukio fulani fulani kwenye sehemu zao za kazi!

Mwandishi wa habari anaweza kuripoti ukweli fulani lakini ukakanushwa kwa makusudi na kwa bahati mbaya ukikanushwa kwa namna hiyo, huyo mwandishi wa habari ataonekana mwongo. Lakini anayekana ukweli ataonekana yuko sahihi.

Mwandishi wa habari anaweza akakatazwa kuripoti tukio fulani kwa vile linagusa maslahi ya watu fulanifulani au hata kama ataripoti owner wa gazeti anamwambia editor wake kuwa stori fulani isitoke kwenye gazeti lake au kama ikitoka anapewa nakala tofauti na ile ya mwandishi wa habari. Haya yanafanyika! Baadhi ya viongozi wana waandishi wao na hawataki mwandishi mwingine yeyote na kabla ya kuripoti kitu wanaambiwa kitu gani waandike.

Na ujue mwandishi wa habari anapoleta stori kwa editor siyo yeye (mwandishi wa habari) tena anayeamua hiyo stori itoke hivyo au ibadilishwe. Je, wewe ungekuwa mwandishi wa habari katika mazingira hayo ungefanya nini - yaani ulichoandika hakitoki vile na kama kikitoka unakuta kimebadilishwa baadhi ya 'contents' zake?

Hivi unakumbuka alivyosema ex-Waziri Mapuri wakati waandishi wa habari walipopigwa na askari magereza hapa Dar miaka michache iliyopita? Mambo yalipopamba moto Mapuri alikanusha na kusema alikaririwa vibaya na vyombo vya habari - namna tu ya 'defence mechanism'.

Unakumbuka pia wakati ugongwa wa Mafua ya Ndege au Rift Valley (sikumbuki vizuri ulikuwa ugonjwa gani nimesahau) ulivyotesa muda fulani Dodoma na vyombo vya habari viliripoti, lakini baadaye waziri fulani alikanusha na kusema ni uongo? Ila mambo yalipoendelea kuharibika waziri huyohuyo alitangaza ugonjwa huo kuwa 'janga la kitaifa'.

Unakumbuka pia kulitangazwa kuna njaa Singida au Arusha (sikumbuki vizuri pia ni mkoa gani kati ya hiyo 2) miaka michache iliyopita na kwamba mtoto mmoja alifuka kwa kukosa chakula lakini waziri fulani akakanusha na kusema alikufa kwa 'malnutrition' na siyo njaa? Yaani yeye alijidai anajua kilichomwua mtoto kuliko hata mama mzazi aliyekuwa hana chakula nyumbani.

Siku moja nilipita kituo fulani cha polisi hapa Dar na kukuta askari wa kike amemkaba bwana mmoja shingoni akimtolea lugha chafu na kusema 'leo utanikoma'. Kwa vile dirisha lilikuwa la vioo na nilikuwa karibu niliona kilichokuwa kinafanyika.

Huyo bwana alikuwa akiomba radhi lakini huyo askari wa kike alisema tu 'leo nimekwambia utanikoma'! Askari wadogo walijitahidi kusuluhisha lakini aliwakemea akiwaambia wao ni askari wadogo tu hawawezi kumwambia kitu. Hivyo aliendelea kumwonyesha huyo bwana uwezo aliokuwa nao juu yake.

Na watu wengine pia walikuwepo na nilienda pale kituoni kuuliza kama kuna kitu kama hicho. Askari wa zamu alinijibu kila kitu kilikuwa swari na hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa amekabwa vibaya na askari. Pia alisema kama nikitaka maelezo zaidi niende kuuliza Central Police Station kwa vile pale kituoni hawakuona kitu chochote. Hivyo nilishindwa kupata habari yoyote ya huyo (bwana harusi mtarajiwa aliyekuwa ameenda kwenye kikao cha harusi karibu na kituo cha polisi na kuangukia pabaya).

Uandishi wa habari ni taaluma sawa na taaluma zingine lakini ni taaluma taofauti pia. Mtu anaweza kuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na akawa mwandishi wa habari na mwingine akawa profesa mwenye zaidi ya PhD 10 na asiwe mwandishi wa habari.

"... But one thing is common to the job of all journalists: they are all communicators. They are gatherers and disseminators of information, eager to share their knowledge and insight with members of the public thirsting for understanding... [a journalist] is an explorer, venturing where we sometimes fear to go - places of danger and splendor... When necessary journalists act as shapers of opinion - as the moral conscience of the nation - expressing general public outrage over injustice, cruelty or stupidity by those in power... " (Journalism Notes - The Writers Bureau College of Journalism, Manchester - UK).

Jounalists ni watu wanaojituma sana na wanafanyakazi kwenye mazingira magumu mno. Lakini sisi Watz tumejazwa tu na 'prejudice' kuhusu hawa watu na kwa bahati mbaya wakiripoti kitu ambacho ni sahihi na baadaye kikikanushwa na wakubwa kwa sababu fulanifulani za kisiaza tunaona wao ndio hawajui - hawana elimu!

Kwani kusema PM Pinda kasema hivi au vile kuhusu albinos unahitaji uwe na digrii ngapi au uwe mwaka wa ngapi chuoni? Mbona sources wenyewe wa habari wanaweza hata wakawa watoto wa chekechea, shule ya msingi nk?

However, kunaweza kuwa na 'factual errors' katika reporting, pengine kwa sababu watu waliotakiwa kuthibitisha walificha baadhi ya information. If that happens haina maana kwamba basi hii taaluma ni bure kabisa - 'shoddist of all professions'.
 
Magobe....well said,

i couldn't agree with you more than what you wrote above,........however, experience ya watu wengi hapa kuhusu waandishi inatufanya tuangukie mitego ya ku-undermine taaluma hii ya uandishi wa habari........wakati mwingine tukisoma taarifa kutoka magazetini tunaogopa ku-comment.....simply bse facts ni ndogo kuliko "rhetorics" in a way.........

vinginevyo......nakubaliana na wewe......pple don't underestimate hii fani ya uandishi wa habari.........
 
Pinda anapaswa kujua kuwa kila analotamka linachukuliwa kwa uzito mkubwa maana ni PRIME minister,,kawaida neno likishatamkwa halirudi na huwa na impact kubwa katika jamii.So nashauri umakini kwa huyu pm wetu
 
Ilibidi ieleweke raisi wetu alikuwa katika ziara hiyo kichama au kiserikali
kama ni chama basi chama chake kupitia msemaji wake wangetoa maelezo ya
ziada kutokana na kauli hizo za raisi na kama ni serikali basi tujue ule
ndio msimamo wa serikali na iwekwe kwa njia ya maandishi kwamba serikali ya
jamhuri ya muungano wa tanzania msimamo wake ni huo

inatia uchungu sana unapoona viongozi wetu wakuu wanavyokuwa na kauli za
ajabu ajabu kama hizi na ambazo vyama vyao wala serikali haijutii kauli hizi
wala kuja mbele ya vyombo vya habari kutolea maelezo ya ziada

mimi naona kiongozi anapokuwa katika shuguli za kiserikali kama ilivyokuwa
kwa yeye kikwete asiruhusiwe kabisa kujihusisha na vijembe au kufanya
shuguli za kichama pale ameenda kutumikia wananchi wa jamhuri ya muugano wa
tanzania ambao serikali yao haina dini wala kabila .

Kama wataendelea na kauli hizi basi wawe na wasemaji wao ambao ndio kazi yao
hiyo

--
 
Tumeona wiki iliyopita viongozi wetu wakuu wa nchi wakitoa kauli ajabu ajabu
ambazo wananchi wakiamua kuzifuata basi baadhi ya maeneo hayatakalika na
amani kuvunjika sehemu hizo husika

kwanza ni kwa mhe kikwete alivyokuwa katika ziara ya visiwani alipoapa
kutokugawana madaraka na chama cha cuf hadi mwaka au labda mpaka atakapotoka
yeye madarakani

ilibidi ieleweke raisi wetu alikuwa katika ziara hiyo kichama au kiserikali

Back
Top Bottom