Angellah Kairuki: Ma DAS wamekuwa wakianzisha mivutano na wakuu wa wilaya kwa kisingizio kuwa na wao ni wateule wa Rais

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Ungedhani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuwaonya wateule wake kuhusu kuendekeza migogoro kazini, hali hiyo pengine ingekoma. Lakini hali sivyo ilivyo.

Migogoro isiyokwisha ya makatibu tawala wa wilaya na wakuu wa wilaya kwa baadhi ya wilaya nchini, imeibua hasira ya Serikali iliyotoa onyo la mwisho kwa watakaobainika kuendeleza hali hiyo.

Hali ya kuwapo kwa migogoro hiyo ambayo viongozi wa juu serikalini wamekuwa wakiikemea mara kwa mara, ilibainishwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Angellah Kairuki wakati wa mafunzo ya siku tatu kwa makatibu tawala wa wilaya zote za Tanzania Bara jijini Dodoma.

Alisema kuna migogoro na kesi nyingi ambazo amekuwa akisuluhisha kwa vigogo hao wa wilaya.

Kairuki alisema uvumilivu na kuwanyamazia sasa itakuwa basi na kwamba kuanzia sasa watakaobainika, watapelekwa kwa mamlaka ya uteuzi kwa uamuzi.

Rais Samia Juni 6, 2023 alifanya uteuzi wa makatibu tawala wapya 72, na kuwabadilisha vituo vya kazi 51 na 11 kuachwa katika vituo vyao vya kazi.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kairuki alisema baadhi ya makatibu hao ama kwa makusudi au kutojua, wamekuwa wakianzisha mivutano na wakuu wa wilaya kwa kisingizio kuwa na wao ni wateule wa Rais.

"Kuanzia sasa watakaoshindwa kubadilika, nasema kuwa siwezi kuwavumilia, tutakwenda kushauriana na mamlaka zilizowateua. Tumechoka kusuluhisha migogoro yenu, tunaangalia akaunti zenu kwenye mitandao pia hamfanani kama viongozi, kwani mnazungumza vitu vya ajabu kabisa, maadili na tabia lazima ziakisi nafasi zenu," alisema Kairuki.

Waziri huyo alisema mara nyingi anatembelea akaunti za viongozi na kile anachokutana nacho siyo mambo ya maendeleo, bali kila wakati anaona wanavyoendeleza malumbano yasiyokuwa na msingi mzuri wa kimaendeleo na ndiyo maana waliamua kuwaita ili wawape mafunzo.

Kingine aliwaagiza kwenda kufanya kazi ya maofisa masuhuli wakisimamia kila mchango utakaokuwa unaingia au kutoka kwenye halmashauri ili wawe na taarifa sahihi za kila kinachoendelea.

Migogoro ya watendaji

Kauli ya Waziri Kairuki imekuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu Rais Samia alipoeleza sababu ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Kabidhi Wasii Mkuu, Angela Anatory na kumteua Frank Kanyusi, akisema ni ugomvi usiokwisha ulioshusha utendaji kazi katika ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Pia Rais Samia alimteua Irene Lesulie kuwa Naibu Kabidhi Wasii Mkuu, akichukua nafasi ya Lina Sanga.

“Kabidhi Wasii Mkuu na naibu wako nimewateua baada ya kuwaondoa viongozi wote wawili waliokuwepo pale, nilikuwa nategemea wananchi wapate huduma za kuridhisha ndani ya ile ofisi, lakini kilichokuwa kinatokea ilikuwa ni ugomvi.

“Nikasema labda kwa kuwa wote walikuwa kinamama ndiyo maana kulikuwa na ugomvi mkubwa, lakini ukiangalia kwa ndani kulikuwa na kutokutekelezeka kwa kazi vizuri, mwingine akisema huyu anakasirika, mwingine akirekebisha mwingine anachafua, kwa hiyo nikaamua kuwaondoa wote wawili watapangiwa kazi nyingine, sasa nendeni ninyi,” Rais aliwaagiza wateule wapya.

Ugomvi wa wateule wa Rais katika halmashauri pia ulijitokeza katika utawala wa awamu ya tano na miongoni mwao ni ule wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde na aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Wende Ng’ahara.

Akiwa ziarani Mkoa wa Kagera Februari 20, 2019, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwataka wamalize tofauti zao.

Chanzo: Mwananchi
 
Vyeo vya uteuzi ni vingi mno pasipo sababu za msingi. Ni wazi hata majukumu wanaingiliana ndiyo sababu wanatunishiana misuli.
 
Ni kweli ndiyo kuwa wao ni wateule wa Rais, kwani uongo??
Suluhisho pekee na sahihi kwa migogoro ya kiutawala kama hii ktk Serikali ya Tz ni kufanya Mabadiliko Makubwa kabisa ya mfumo wote wa utawala hapa nchini (General Government Overhaul and Restructuring). Mabadiliko yaguse mifumo yote ya Serikali, Bunge na Mahakama pamoja na taasisi zote kabisa zilizopo katika mihimili hii yote ya dola juu ya namna ya utekelezaji wa majukumu yake. Na njia pekee ya kufanikisha Mabadiliko haya ni upatikanaji wa Katiba Mpya itakayotokana na mawazo au maoni ya watu wengi zaidi ktk nchi, pamoja na Kufanyia Mabadiliko au Maboresho ya Sheria zote za nchi hii. Hili ndio suluhisho pekee katika kutatua tatizo hili pamoja na mengine mengi kama haya.
Kwa hiyo, suala la Upatikanaji wa Katiba Mpya nvhini Tanzania kwa sasa ni jambo lisiloepukika(in short, The New Constitution in Tanzania is an INEVITABLE, whether we like it or not).
 
Vyeo vya uteuzi vipunguzwe , hasa huku chini. Watu wafanye application wafanye interview then selection.

Uteuzi uteuzi ndio haya matatizo yanapo tokea
 
Back
Top Bottom