Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

Sasa PM ameshaomba msamaha..watu bado mnamkolia hivi? He is just a gentleman!

Kwani ni nani msafi kati yetu ambaye hajawahi kukosea ktk kauli...mbona mmamnyooshea hivi kidole?
 
ameomba msamaha kwa kitu gani? au unasikia kaumba msamaha na wewe unasema "nimemsamehe".

Nikikupiga kibao halafu nikaomba msamaha kwa wewe "kukwazika" utakubali msamaha wangu?
Mwana kjj, kwa hili hatuko pamoja,

pamoja na matatizo waliyo nayo watawala lakini ukatili wanaofayiwa albino hauhitaji kufuata mkondo wetu wa kisheria ukizingatia rusha iliyo jaa kwenye mahakama zetu. Kumbuka wahusika wa haya mambo ni mafisadi wenye pesa wanaweza kununua uhuru wao.

Naungana na Mh. Pinada; tukiwakamata red-handed ni kuwahukumu palepale!
 
Dear Mwanakijiji,
I do respect your views, but I beg to disagree with you on this matter of the PM's resignation. Why don't you assume that the PM has been overwhelmed by the ongoing killings of the Albinos and that’s what led him to that statement. I have tried to imagine if one of us had a close family member who happened to be an Albino and suddenly disappeared? How would you retaliate if you catch a person on the process of trying to kidnap your family member? I rarely post articles on this forum, but I felt compelled to add my few cents. I am worried sometimes how the opposition parties react to some issues. Their solution is always for one to resign, but instead of accepting it as a human error and lay down their solution to the problems. Any caring citizen who believes in humanity would react the same way the PM did. I would rather accept his apology and unity to find solutions to this problem, which is becoming a national crisis.
I think there is a need of declaring a national crisis that requires collective efforts to fight the perpetrators. This is not a time to gain political leverage on the expense of the Albinos. All interest stakeholders have to come together and find a solution. I would have been so impressed if Dr. Slaa himself would take initiative and host some albinos from his own constituency. At least Waziri Mkuu has adopted a child who might have become a victim and another number. Resignation would not solve the problem. I am not defending his statement, but the statement does not require his resignation. We should bear in mind resignation is also costly for our nation.

Tatizo law enforcement bodies such as the police are cuaght on this nonsense belief.

Lets put our political interests aside and put constructive suggestions on how the victims could be protected.

Ciao
 
Mwanakijiji;

Inaonyesha mzee unapata raha sana viongozi kujiuzulu... hili la Mh. Pinda... andika maandiko unayoandika mara 1000 lakini sidhani utaweza fanikiwa kama ulivyofanikiwa kwa Mh. Edward Lowassa.

wrong! naona raha viongozi wabovu, wenye kutumia nyadhifa zao vibaya, kujinufaisha kwa fedha za walipa kodi, wenye kutumia utawala wa vitisho na unyanyasaji, wanaotangaza wazi watu wavunje sheria au wao wenyewe wakizivunja wakijiuzulu. No apologies there. Sina raha hata kidogo kiongozi mzuri, mzalendo wa kweli, mtetezi wa watu, mwenye kuheshimu sheria na maslahi ya taifa akijiuzulu!

Tunaiishi kwenye dunia ya viumbe dhaifu.. makosa kama hayo yatakuwepo na mengi tu... hata mahakamani wanaangalia ulitoa tamko gani? ukiwa kwenye hali gani? Na mazingira gani?

Ndio maana kuna mada case, na man slaughter ingawa zote ni kuua.

This could go down in history as the lamest attempt at excusing incompetence, defending corruption, and rewarding mediocrity!
 
Hapo sijaelewa chochote.

Kwa vyovyote nitakavyong'ata maneno Magobe, fani ya uandishi wewe mwenyewe unakubali indirectly kwamba imeingiliwa (kama ulivyotaja kwenye post yako iliyotangulia. Wengi wa waandishi hawajali ubora wa kazi, zaidi ya kutoa habari (prestige au mshiko).

Waandishi wa habari wa Tanzania wana kiwango cha chini sana sio tu cha kuripoti, bali hata knowledge wa wanachoripoti. Tueleze background ya habari na tupashe ipasanyo.

Kama unaona circumstances zimekunyima kupata actual information at that particular time and place, subiri na endelea kutafuta habari kamili. Sio kudesa one to one mwishowe unajikuta umelishwa kasa.

Ingieni kwenye news outlets kubwa duniani, angalieni wenzenu wanavyohabarisha. Elimu ni bahari, hivyo videgree vya IJMC, SAUT na Times kudesa ili kufaulu mtihani ndio vinavyowaangusha bandugu.

Kuna ukweli kwenye hoja uliyochangia. Lakini nadhani umeenda mbali mno. Lazima tu'acknowledge' kuwa siyo waandishi wote ambao uandishi wao uko chini au wanaokubali mshiko ili wabadili mwelekeo wa habari. Kwa kawaida 'waandishi-mishiko' wanajulikana hata kwa waandishi wengine - wanaweza kukiuka maadili ya uandishi wa habari kutokana na maslahi binafsi.

Habari zao zinasomwa tu kufata 'facts' fulani lakini siyo kupata ujumbe wake. Hawa wanajulikana sana na baadhi yao hawana aibu; wanataja kabisa hela wanazopewa wanapokuwa na vigogo wanaowafadhili. Wengine kutokana na hela hizo wameweza kujenga nyumba, kununua magari na hata kusomesha watoto kwenye shule za gharama. Hawa bwana huwa wanaamini kabisa 'anayemwoa mama ndiye baba'.

Kwa upande mwingine, hivi unajua kuwa baadhi ya waandishi Tz wanaandikia hizo 'news outlets kubwa duniani'? Kwa hiyo, usidhani Tz hakuna waandishi wenye vichwa; wapo wengi sana ila wanakuwa 'frustrated' na mazingira ya kazi kwenye local media houses, ambazo nyingi ni biashara na siyo kujenga taaluma au kutumika kama political propaganda.

Ndiyo maana nasema mazingira ya Tanzania, of course, yanaweza kuathiri uandishi, yet kuna waandishi ambao wanalinda nidhamu na maadili ya uandishi wa habari. Yes, kuna wale wanaotumiwa na vigogo fulani na hawa wanajulikana. Kwa vile hawa wanatumiwa, haina maana kuwa waandishi wa habari wote wanatumiwa.

Nilichokuwa nimejearibu kueleza ni circumstances zinazo'affect' upatikanaji wa habari. Na pia nimeeleza jinsi mara nyingine unakuta habari ni kweli kabisa na inakanushwa na serikali au viongozi fulani, then watu wanafikiri ni mwandishi aliyechemka. Hivyo, ni vizuri pia kusoma habari na kujiuliza maswali.
 
Machozi ya Pinda yalowesha wabunge

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifuta machozi wakati akielezea mauaji ya Albino alipokuwa akijibu swali Bungeni kuhusiana na kauli yake aliyoitoa hivi karibuni katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Hoja ya wapinzani kumtaka ajiuzulu yayeyuka

Leon Bahati

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameangua kilio bungeni kuonyesha uchungu alio nao dhidi ya vitendo vya mauaji ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), hivyo kuyeyusha hoja ya wabunge wa upinzani waliokuwa wamepania kumbana, ili ajiuzulu kwa madai kwamba, alitoa amri ya kuua wauaji ambayo ni kinyume na katiba ya nchi.

Hali hiyo ilitokea jana bungeni, wakati Pinda akielezea yaliyomfanya atoe kauli hiyo tata kikatiba na misingi ya haki za binadamu.

Pinda alisema alipokuwa katika ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alipata taarifa za kusikitisha kuhusu mauji ya albino na mara kesho yake habari zikatoka kwenye vyombo vya habari kwamba, albino mwinge kauawa.

"Jamani jamani taarifa za matukio hayo kibinadamu zinatia uchungu sana na kumfanya mtu ashindwe kujizuia….," mara akaanza kutokwa machozi na kukatisha maelezo yake akatoa miwani na kujifuta huku wabunge wakiwa kimya.

Waziri Mkuu alisema hayo baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, kumtaka atoe ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni akiwa katika ziara Kanda ya Ziwa, kuwaruhusu wananchi kuwaua watu watakaokutwa wakimchinja albino.

Hamadi alisema katiba ya nchi inamlinda mtu kupewa nafasi ya kujitetea, hivyo akamtaka waziri afafanue maana ya kauli yake, kwa kuwa ni kinyume na taratibu ambazo nchi imejiwekea katika kuhakikisha haki inapatikana.

Pinda alisema mtu anaposikia au kusoma taarifa za mauaji ya albino, hawezi kupata hisia juu ya mateso wanayoyapata, sawa na anayewasikiliza watu walionusurika kufa au walioshuhudia vitendo hivyo vikitendeka.

"Mimi walinihadithia, aah! Samahani," alisema kwa masikitiko Pinda huku akiwataka radhi wabunge kwa kushindwa kuendelea kueleza kwa jinsi alivyoguswa na matukio hayo. Mara akaanza kububujikwa na machozi na baada ya sekunde kama 15, alichukua kitambaa chake akajifuta.

Aliendelea kuelezea jinsi maalbino wanavyouawa kikatili, akisema wengi walikufa kwa kushindwa kupata huduma mapema ya kuzuia damu baada ya ama kukatwa mikono ama miguu na majitu hayo katili yenye imani potofu kwamba, viungo hivyo vinaweza kumpatia mtu utajiri.

Alisema alielezwa kuwa, wauaji wanachokifanya ni kumshambulia albino na kumkata kiungo wanachokitaka kwa kutojali hali wanayomuacha nayo kama ni mateso, kufa au kupona hivyo alipatwa na uchungu kiasi cha kujikuta anatamka kuwa, watu wanaokutwa wakitenda hayo nao wanapaswa kuadhibiwa papo hapo.

Alifafanua kuwa wakati akiwa kwenye ziara hiyo iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kukemea na kupanga mikakati ya kukabaliana na vitendo hivyo, idadi ya maalbino waliouawa walikuwa 30 na baada ya kukemea vitendo hivyo, ghafla akapewa ripoti ya kuuawa wengine wawili, jambo ambalo lilizidi kumuudhi na kumchanganya.

Waziri Pinda aliwaomba radhi watu walioudhika kutokana na matamshi na pia akimuomba Mungu amsamehe iwapo amewakosea.

"Kama mnaona kile nilichofanya ni makosa naomba mnivumilie. Naomba Mungu anisamehe kama nimewakosea," aliomba Waziri Mkuu na kuongeza kuwa serikali imechukizwa sana na mauaji hayo ya kikatili.

Alisema Tanzania imekuwa ikiheshimika sana katika jumuiya ya kimataifa, lakini mauaji ya albino na ya vikongwe katika eneo hilo yameitia doa.

Alielezea pia kuhuzunishwa zaidi na tamko la Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) la kulaani mauaji hayo, kana kwamba wao wanaguswa sana na suala hilo kuliko Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema kuwa katika ziara hiyo, ambayo iliwahusisha pia baadhi ya mawaziri, wabunge, viongozi wa polisi, viongozi wa dini na kisiasa, waliahidi kushirikiana kuhakikisha kuwa wanakabiliana na kulimaliza tatizo.

Isitoshe alisema aliwataka viongozi wa vijiji kurejesha ulinzi wa jadi, maarufu kama sungusungu ili kukabiliana na wauaji.

Pinda alisema kuwa serikali ipo tayari kupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali, yanayoweza kusaidia kupata mbinu ya kukomesha kabisa mauaji hayo, ili kuiokoa jamii hiyo ya albino.

Alisema katika kumbukumbu za serikali, hadi mwishoni mwa mwaka jana vikongwe 2,866 walikuwa wameuawa kwa imani potofu kuwa ni wachawi.

Alisema serikali imeliagiza jeshi la polisi kutumia maarifa yake, hata kama itabidi kutumia gharama kubwa, ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na mauaji hayo.

Wapinzani pia walimtaka Pinda atoe maelezo yanayodaiwa kuwa yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete kisiwani Pemba kwamba, aliwashangaa wakazi wa eneo hilo kuwachagua watu ambao hawawezi kuunda serikali na ambao watachukua muda mrefu kupata nafasi hiyo.

Pinda alisema anapata taabu kujibu swali hilo, kwa sababu hawezi kuyatolea maelezo mambo yaliyozungumzwa na bosi wake na wala hajui kama ni kweli rais alisema kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Mbunge wa Konde, Dk Ali Tarab Ali (CUF) alimtaka Pinda aeleze kama kitendo cha Rais Kikwete kutumia magari ya serikali kisiwani Pemba na kuonekana akifanya shughuli za chama ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Pinda alimjibu akisema kuwa, ni vigumu rais kutofautisha vyombo vya usafiri anavyovitumia wakati akifanya ziara za kisiasa ama za kiserikali na kutoa mfano kwamba, hata rais wa Marekani hutumia ndege aina ya Air Force one bila kuchagua kuwa ni shughuli ya kisiasa au kiserikali.

Wakati hayo yakitokea bungeni, baadhi ya viongozi wa dini nchini, wamemtaka Waziri Pinda kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam, Sheikh Ramadhan Sanze alisema Pinda alifanya kosa la kiufundi kwa kuwa yeye ni mtendaji mkuu wa serikali, hivyo hakupaswa kusema jambo linalopingana na msimamo wa serikali, sheria na katiba ya nchi.

"Kwa vile kauli hiyo haijaleta madhara mpaka sasa Waziri Mkuu ana uchochoro wa kupita ili kujisafisha. Cha msingi ni kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi" alishauri Sheikh Sanze.

Alisema, hajafuatilia vizuri kuhusu hoja za kambi ya upinzani bungeni na kwamba, kujiuzulu inaweza isiwe suluhisho la tatizo hilo kwa kuwa, hata kama atajiuzulu kauli haitafutika na tatizo litabaki palepale.

"Nchi hii haina dini na kwa hiyo haingozwi na sheria za dini bali inaongozwa na sheria za nchi, kwa hiyo Pinda alipaswa kuangalia sheria ya nchi kwanza kabla ya kutoa agizo lake," alisema Sheikh Sanze.

Alifafanua kuwa, Waziri Pinda ametengeneza mazingira ya uchafuzi na uchochezi, kutokana na kauli yake hiyo kwani baadhi ya watu wanaweza kuitumia vibaya kwa kumuua mtu kwa sababu ya chuki tu baina yao.

Alisema, athari ya kauli kama hizo zinaweza kusababisha migogoro kati ya dini na dini nyingine, kabila moja na jingine au dhehebu moja na jingine kama wananchi watautumia wito huo.

Alisema vita dhidi ya mauaji ya albino imekuwa ikitumika kisiasa zaidi kuliko kitaalamu na kuongeza kuwa, mamlaka husika ziliangalie tatizo hilo kitaalamu badala ya kuliacha likitumika kisiasa.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa alisema kauli ya Pinda ya kutaka aliyeua albino auawe si sahihi kwa sababu mtu akimuua aliyeua ni muuaji na ana kosa kisheria.

Mauaji ya albino yamekuwa yakitikisa nchi na hasa katika eneo la Kanda ya Ziwa, licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu, vyama vya walemavu na watu binafsi.

Source:Mwananchi
 
Machozi ya Pinda yalowesha wabunge

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifuta machozi wakati akielezea mauaji ya Albino alipokuwa akijibu swali Bungeni kuhusiana na kauli yake aliyoitoa hivi karibuni katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Hoja ya wapinzani kumtaka ajiuzulu yayeyuka

Leon Bahati

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameangua kilio bungeni kuonyesha uchungu alio nao dhidi ya vitendo vya mauaji ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), hivyo kuyeyusha hoja ya wabunge wa upinzani waliokuwa wamepania kumbana, ili ajiuzulu kwa madai kwamba, alitoa amri ya kuua wauaji ambayo ni kinyume na katiba ya nchi.

Hali hiyo ilitokea jana bungeni, wakati Pinda akielezea yaliyomfanya atoe kauli hiyo tata kikatiba na misingi ya haki za binadamu.

Pinda alisema alipokuwa katika ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alipata taarifa za kusikitisha kuhusu mauji ya albino na mara kesho yake habari zikatoka kwenye vyombo vya habari kwamba, albino mwinge kauawa.

"Jamani jamani taarifa za matukio hayo kibinadamu zinatia uchungu sana na kumfanya mtu ashindwe kujizuia….," mara akaanza kutokwa machozi na kukatisha maelezo yake akatoa miwani na kujifuta huku wabunge wakiwa kimya.

Waziri Mkuu alisema hayo baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, kumtaka atoe ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni akiwa katika ziara Kanda ya Ziwa, kuwaruhusu wananchi kuwaua watu watakaokutwa wakimchinja albino.

Hamadi alisema katiba ya nchi inamlinda mtu kupewa nafasi ya kujitetea, hivyo akamtaka waziri afafanue maana ya kauli yake, kwa kuwa ni kinyume na taratibu ambazo nchi imejiwekea katika kuhakikisha haki inapatikana.

Pinda alisema mtu anaposikia au kusoma taarifa za mauaji ya albino, hawezi kupata hisia juu ya mateso wanayoyapata, sawa na anayewasikiliza watu walionusurika kufa au walioshuhudia vitendo hivyo vikitendeka.

“Mimi walinihadithia, aah! Samahani," alisema kwa masikitiko Pinda huku akiwataka radhi wabunge kwa kushindwa kuendelea kueleza kwa jinsi alivyoguswa na matukio hayo. Mara akaanza kububujikwa na machozi na baada ya sekunde kama 15, alichukua kitambaa chake akajifuta.

Aliendelea kuelezea jinsi maalbino wanavyouawa kikatili, akisema wengi walikufa kwa kushindwa kupata huduma mapema ya kuzuia damu baada ya ama kukatwa mikono ama miguu na majitu hayo katili yenye imani potofu kwamba, viungo hivyo vinaweza kumpatia mtu utajiri.

Alisema alielezwa kuwa, wauaji wanachokifanya ni kumshambulia albino na kumkata kiungo wanachokitaka kwa kutojali hali wanayomuacha nayo kama ni mateso, kufa au kupona hivyo alipatwa na uchungu kiasi cha kujikuta anatamka kuwa, watu wanaokutwa wakitenda hayo nao wanapaswa kuadhibiwa papo hapo.

Alifafanua kuwa wakati akiwa kwenye ziara hiyo iliyokuwa maalumu kwa ajili ya kukemea na kupanga mikakati ya kukabaliana na vitendo hivyo, idadi ya maalbino waliouawa walikuwa 30 na baada ya kukemea vitendo hivyo, ghafla akapewa ripoti ya kuuawa wengine wawili, jambo ambalo lilizidi kumuudhi na kumchanganya.

Waziri Pinda aliwaomba radhi watu walioudhika kutokana na matamshi na pia akimuomba Mungu amsamehe iwapo amewakosea.

"Kama mnaona kile nilichofanya ni makosa naomba mnivumilie. Naomba Mungu anisamehe kama nimewakosea," aliomba Waziri Mkuu na kuongeza kuwa serikali imechukizwa sana na mauaji hayo ya kikatili.

Alisema Tanzania imekuwa ikiheshimika sana katika jumuiya ya kimataifa, lakini mauaji ya albino na ya vikongwe katika eneo hilo yameitia doa.

Alielezea pia kuhuzunishwa zaidi na tamko la Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) la kulaani mauaji hayo, kana kwamba wao wanaguswa sana na suala hilo kuliko Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema kuwa katika ziara hiyo, ambayo iliwahusisha pia baadhi ya mawaziri, wabunge, viongozi wa polisi, viongozi wa dini na kisiasa, waliahidi kushirikiana kuhakikisha kuwa wanakabiliana na kulimaliza tatizo.

Isitoshe alisema aliwataka viongozi wa vijiji kurejesha ulinzi wa jadi, maarufu kama sungusungu ili kukabiliana na wauaji.

Pinda alisema kuwa serikali ipo tayari kupokea maoni kutoka kwa watu mbalimbali, yanayoweza kusaidia kupata mbinu ya kukomesha kabisa mauaji hayo, ili kuiokoa jamii hiyo ya albino.

Alisema katika kumbukumbu za serikali, hadi mwishoni mwa mwaka jana vikongwe 2,866 walikuwa wameuawa kwa imani potofu kuwa ni wachawi.

Alisema serikali imeliagiza jeshi la polisi kutumia maarifa yake, hata kama itabidi kutumia gharama kubwa, ili kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na mauaji hayo.

Wapinzani pia walimtaka Pinda atoe maelezo yanayodaiwa kuwa yalitolewa na Rais Jakaya Kikwete kisiwani Pemba kwamba, aliwashangaa wakazi wa eneo hilo kuwachagua watu ambao hawawezi kuunda serikali na ambao watachukua muda mrefu kupata nafasi hiyo.

Pinda alisema anapata taabu kujibu swali hilo, kwa sababu hawezi kuyatolea maelezo mambo yaliyozungumzwa na bosi wake na wala hajui kama ni kweli rais alisema kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Mbunge wa Konde, Dk Ali Tarab Ali (CUF) alimtaka Pinda aeleze kama kitendo cha Rais Kikwete kutumia magari ya serikali kisiwani Pemba na kuonekana akifanya shughuli za chama ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Pinda alimjibu akisema kuwa, ni vigumu rais kutofautisha vyombo vya usafiri anavyovitumia wakati akifanya ziara za kisiasa ama za kiserikali na kutoa mfano kwamba, hata rais wa Marekani hutumia ndege aina ya Air Force one bila kuchagua kuwa ni shughuli ya kisiasa au kiserikali.

Wakati hayo yakitokea bungeni, baadhi ya viongozi wa dini nchini, wamemtaka Waziri Pinda kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam, Sheikh Ramadhan Sanze alisema Pinda alifanya kosa la kiufundi kwa kuwa yeye ni mtendaji mkuu wa serikali, hivyo hakupaswa kusema jambo linalopingana na msimamo wa serikali, sheria na katiba ya nchi.

"Kwa vile kauli hiyo haijaleta madhara mpaka sasa Waziri Mkuu ana uchochoro wa kupita ili kujisafisha. Cha msingi ni kukiri kosa, kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa mamlaka za kisheria, Bunge na Wananchi" alishauri Sheikh Sanze.

Alisema, hajafuatilia vizuri kuhusu hoja za kambi ya upinzani bungeni na kwamba, kujiuzulu inaweza isiwe suluhisho la tatizo hilo kwa kuwa, hata kama atajiuzulu kauli haitafutika na tatizo litabaki palepale.

"Nchi hii haina dini na kwa hiyo haingozwi na sheria za dini bali inaongozwa na sheria za nchi, kwa hiyo Pinda alipaswa kuangalia sheria ya nchi kwanza kabla ya kutoa agizo lake," alisema Sheikh Sanze.

Alifafanua kuwa, Waziri Pinda ametengeneza mazingira ya uchafuzi na uchochezi, kutokana na kauli yake hiyo kwani baadhi ya watu wanaweza kuitumia vibaya kwa kumuua mtu kwa sababu ya chuki tu baina yao.

Alisema, athari ya kauli kama hizo zinaweza kusababisha migogoro kati ya dini na dini nyingine, kabila moja na jingine au dhehebu moja na jingine kama wananchi watautumia wito huo.

Alisema vita dhidi ya mauaji ya albino imekuwa ikitumika kisiasa zaidi kuliko kitaalamu na kuongeza kuwa, mamlaka husika ziliangalie tatizo hilo kitaalamu badala ya kuliacha likitumika kisiasa.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa alisema kauli ya Pinda ya kutaka aliyeua albino auawe si sahihi kwa sababu mtu akimuua aliyeua ni muuaji na ana kosa kisheria.

Mauaji ya albino yamekuwa yakitikisa nchi na hasa katika eneo la Kanda ya Ziwa, licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu, vyama vya walemavu na watu binafsi.

Source:Mwananchi
 
Dear Mwanakijiji,
I do respect your views, but I beg to disagree with you on this matter of the PM's resignation. Why don't you assume that the PM has been overwhelmed by the ongoing killings of the Albinos and that's what led him to that statement. I have tried to imagine if one of us had a close family member who happened to be an Albino and suddenly disappeared? How would you retaliate if you catch a person on the process of trying to kidnap your family member? I rarely post articles on this forum, but I felt compelled to add my few cents. I am worried sometimes how the opposition parties react to some issues. Their solution is always for one to resign, but instead of accepting it as a human error and lay down their solution to the problems. Any caring citizen who believes in humanity would react the same way the PM did. I would rather accept his apology and unity to find solutions to this problem, which is becoming a national crisis.
I think there is a need of declaring a national crisis that requires collective efforts to fight the perpetrators. This is not a time to gain political leverage on the expense of the Albinos. All interest stakeholders have to come together and find a solution. I would have been so impressed if Dr. Slaa himself would take initiative and host some albinos from his own constituency. At least Waziri Mkuu has adopted a child who might have become a victim and another number. Resignation would not solve the problem. I am not defending his statement, but the statement does not require his resignation. We should bear in mind resignation is also costly for our nation.

Tatizo law enforcement bodies such as the police are cuaght on this nonsense belief.

Lets put our political interests aside and put constructive suggestions on how the victims could be protected.

Ciao

Don't wait for Dr Slaa to host an albino, just take that initiative yourself and then others will emulate you. What PM said (tit for tat) was not something to be proud of. Although he was moved by an increase in the number of albino killings, his statement had adverse implications on all of us - appeal for mob justice on albino killers.

It is good to show compassion or sympathise with the victims but not to the extent of promoting or implying mob justice - it is extremely important to show good judgement too. If critics demanded his resignation, it was purely on his misleading statement on albino killers.

Kauli tatanishi ndiyo huwa zinaleta maafa makubwa. Kwa hiyo, PM anapaswa asiwe miongoni mwa watu wanaotoa kauli tatanishi kama hiyo aliyosema. Kama akisema kwa makosa, atakapogundua kosa au kuonyeshwa hilo kosa aseme alikosea. Wote tunafanya makosa lakini haya makosa yasiwe 'justified'.
 
Last edited:
Unajua, Magobe, unaposema "bila kujua mazingira yalikuwaje" unakubali kwamba waandishi na kazi zao ni dhaifu, na sababu ni mazingira ya kazi.

Kwa hiyo chochote kile utakachosema kuelezea sababu za udhaifu, iwe mazingira, iwe mshahara mdogo, iwe wanapokea rushwa, iwe wanacheleweshewa mshahara wao, iwe uongozi mbaya, iwe umaskini wa makampuni yao, mwisho wa siku umekubali kwamba waandishi na kazi yao ni dhaifu. Hizo unazoeleza wewe ni sababu za udhaifu. Kwa hiyo unakubaliana na mimi kwamba kazi yao ni dhaifu. Nukta.

Mkuu,

Sasa kumbe unakubali umekosea, na umesema uliposhtuliwa umerekebisha, sasa badala ya kuuchuna unanilaumu mimi kwamba nimefanya "scathing attacks on Tanzanian journalists...rightly or wrongly" wakati uliyoambiwa umekubali yamefanya usahihishe makosa. Sasa kosa langu nini hapo?

Halafu kama nimesema kitu "rightly or wrongly" basi huwezi kunilaumu kwa hilo maana inawezekana nimekisema rightly.

Kuhani, unachosema kina ukweli fulani. Lakini siyo waandishi wote ni dhaifu. Kitu ninachokataa ni sweeping statement - kudhani kuwa uandishi wa habari 'is the shoddist of all professions'. Statement hii haiwezi kuthibishwa na aliyeisema.

Hii ndiyo ilikuwa 'context' ya yale nilyoandika na ndiyo maana nilionyesha hayo mazingira uliyoyataja. Lakini kwa ujumla waandishi wa habari wanajitahidi sana ukilinganisha na mazingira waliyomo na kazi wanayoifanya.

Hizo 'sweeping statements' zinatokea wakati mwandishi fulani ameibua hoja controversal halafu serikali au vigogo fulani wakaipinga.

Hali hii hufanya baadhi ya watu wadhani kwa vile habari fulani imepingwa basi siyo sahihi. Siyo kweli. Mfano, halisi ni kauli ya PM. Mwandishi ali'narrate' PM alichokisema lakini baadhi ya watu walianza kutilia mashaka umakini wa huyo mwandishi katika kuripoti kilichosemwa. Waliona PM hawezi kusema hivyo ila mwandishi wa habari anaweza kusema uongo. Lakini si umeona PM mwenyewe kakiri alisema (ingawa hakutaka kurudia the 'exact words')?

Ila ni kweli pia kuwa kuna waandishi wa habari wanaotumiwa kwa maslahi binafsi na hawa wanaeleweka na waandishi wengine. Kwa hiyo, 'We should not just water down journalism because certain reporters/journalists do not adhere to professional ethics. Let's acknowledge the reporters/journalists who do their work boldly and responsibly and these are not weak.'

Mahali pa kutoa changamoto kwa vyombo vya habari tutoe na mahali vyombo vya habari vinapofanya kazi nzuri tuone pia. Kwa hiyo, siyo kweli kuwa 'journalism is the shoddist of all professions'. Na ukiangalia hata huyo aliyesema haya hana argument yoyote isipokuwa hisia tu. Na mtu huwezi kujenga hoja kutokana na hisia tu.
 
Hivi yale mauaji ya Shinyanga yaliyomfanya Waziri wa Mambo ya ndani ya wakati huo, Mh. Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu, yalikuwa makubwa na ya kutisha kuliko haya ya Maalbino - maanake hapa hatusikii mtu anajiuzulu. Sana sana watu wanaishia kumwaga machozi na kukurupuka na matamshi yasiyo na kichwa wala miguu.

Tunajifunza nini hapa - ni kuwa tuna uongozi lege lege. Uongozi wa juu ukiwa lege lege huzaa viongozi wa chini wasiowajibika wala kuwajibishwa na huishia kumwaga machozi wanapoelemewa. Duh, sina zaidi.
 
Back
Top Bottom