Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito: "wanaoua Albino na wenyewe muwaue!" - Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 23, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na Victor Kinambile, Tabora
  KATIKA hali ya isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana aliwaambia wananchi kuwa wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe nao hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.


  "Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena)," alisema Pinda huku akiwaacha watu midomo wazi.

  Pinda anatumia chama chake:-

  "Umoja wa vijana wa CCM mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena," alisema waziri mkuu.

  Waziri Pinda alisema iwapo wananchi wataendelea kuwahurumia wauaji hao ambao wanatafuta viungo vya albino wakitegemea mahakama itatenda haki huku nao wakiongeza kasi ya mauaji kwa Watanzania, watakuwa wanakosea.
  Hivyo alisema kwamba kuanzia sasa mtu yeyote atakayemuona mtu amemkata shingo au mkono mweziwe basi naye auawe papo hapo hii itakuwa ndiyo dawa kwani vingozi wote tumechoka na mauji hayo.
  ---------------------------
  Hivi hapa ni kiongozi wa Chama au wa Serikali na ndivyo Kama Waziri Mkuu alitakiwa kutoa kauli hii ? Je Waziri wa Ulinzi yupo wapi ? Kama mauaji yanaendelea inamaana mkuu wa Jeshi la Polisi,Mkuu wa Upelelezi na Waziri wao hawafai ,hivyo ilibidi wawajibike au yeye Waziri Mkuu awawajibishe na sio kutoa kauli za vitisho na kuwafanya wauaji wawe makini zaidi wanapotekeleza mauaji yao. Na pale aliposema ....Viongozi wote tumechoka..... WaTanzania mnaichukuliaje kauli hii ya Kiongozi Mkuu wa Nchi kutangaza kuwa yeye na wenzake wamechoka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 23, 2009
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Are you sure kauli hii imetoka kwa Waziri Mkuu? Yaani una maana amebariki kujitwalia sheria mikononi, hiyo kali. Kama ni kweli inasikitisha sana. Ningetegemea angetuambia serikali inafanya nini kuimarisha uwezo wake kuwaadhibu na kuwashughulikia watu hawa.
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Yaani nimesioma kauli yake kwenye Gazeti la Mwananchi nikawa siamini-amini. Hili sula inaonekana serikali imeshashindwa kulidhibiti na inaonyesha serikali haina watendaji imara na kwa kweli katika suala la mauaji ya albino siielewi kabisa serikali kwani Vicky Ntetema ameshatoa data ambazo wangemwomba awape majina ya hao wachawi na wakaanzia hapo. Ingekuwa mfano mzuri kwa Wauwaji wenggine lakini tangu taarifa ya BBC wala serikali haikui hukulia tarifa hiyo serious kitu ambacho kinanipa mashakua huenda kuwa wakubwa sana katika serikali ambao wanafaidika na mauaji hayo.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Mimi siamini kuwa maneno hayo yamesemwa na Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mbunge na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae kitaaluma, ni Mwanasheria aliyebobea!. Atakuwa amenukuliwa vibaya!.
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Labda! Tumsubirie akanushe na tuone Gazeti la Mwananchi litasemaje. Mara nyingine hutokea mtu akahamaki na kujikuata anazungumza ambayo hakutarajia.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ila kazi hiyo kusema ifanywe na UVCCM mhhhhhh......
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hii ni ishara tosha kuwa serikali imeshindwa kazi yake. Viongozi wameshindwa kazi yao.
  Hatuwezi kubariki mod justice huku vyombo vya sheria vipo kufanya kazi yake. Ingekuwa ni India huyu waziri mkuu angepigiwa makelele ya kujiuzulu.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa upande mmoja naona Mheshimiwa anataka ushahidi upotee,na wanaowatuma wauaji watakuwa wame "escape' .
  Maana anaemkata kiungo albino ikiwa atakamatwa hai na kutakiwa kutoa ushahidi utakaowawezesha polisi kufuatilia chain nzima ya ukeketaji huo basi wale wanaotiliwa mashaka kuwa ni wahusika wakubwa watakumbwa na aibu na huenda ikawa wamo katika chama Tawala wakiusaka utajiri kama si Uraisi na ubunge.

  Je Mh.Pinda ana wasiwasi wa kukamatwa na kufikishwa katika mkono wa sheria watuhumiwa wa mauwaji wa maalibino ?
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna watu waliokaribu waliwataka waandishi wasiiandike habari hiii lakini ndio hivyo siku hizi habari za kukurupuka ndizo zinazouza magazeti.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chama kuunda Jeshi na Mkuu wa nchi kukiri kwa kuamuru jeshi hilo liingie mzigoni ,sijui vyama vingine kama vinaruhusiwa kuunda jeshi ?
   
 11. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Watanzania bado tunayo kazi ya kuondokana na hii dhahama.Kama kweli Mkuu aliyepewa dhamana na wananchi/wapiga kura wake anatoa kauli za aina hii. Au yawezekana ulimi uliteleza kidogo. Manake binadamu tuna mapungu ya hapa na pale. Sasa labda katika kufafanua jambo kwa ufasaa ndio ulimi ukateleza na hayo yalioandikwa yakatoke.
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mh! NAona Kiranja ameumbuka. Naamini alipitiwa tu, Pinda hana desturi ya kukurupuka na kuzungumza pumba tangyu akiwa naibu Waziri, Waziri TAMISEMI hata Waziri Kiranja; Pinda penye ukweli hukiri madhaifu tofauti na Wakulu wengine. Kama imemkuta hii basi ujue serikalini hali ni ngumu kupita maelezo na Serikali nzima inabidi ibomolewe na tuunde Serikali mpya kabisa tena ya Kitaifa na si ya Kisiasa kama hii ya CCM.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Samahani wakuu,fikiria mdogo wako ni albino na ghafla mko sebuleni kwenu pale mnaangalia ze comedy,mara kaingia mtu na kuukata mkono wa mdogo wako albino na kuanza kutimua nao. Mungu bariki wewe na ndugu zako mkamkimbiza na kumtia mikononi huko bondeni,wewe na jamaa zako mtamfanyaje huyo jamaa?
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na yeye tutammaliza na kumnyofoa kiungo kimoja kimoja na sio kwa kumkata bali tutanyofoa kama unaenyofoa magoya ya kuku baada ya kumwaia maji ya moto.

  Ila kwa hili kiongozi mkuu hakutakiwa kuwakilisha adhabu ya kifo ,kama unakumbuka mauaji ya vibaka kwa kuwachoma moto huku wamevalishwa matairi ,serikali ilikuja juu na kusema watu wasijichukulie hatua mikononi mwao,Je kwa Waziri Mkuu kusema watu wasingojee sheria ichukue mkondo wake ndio ametoa kauli kuwa sasa ni huria watu kujichukulia hatua mikononi mwao ? Kumbuka maalbino ni watu nao vilevile wanaweza kutumika kumwangamiza mtu asie na hatia ,ikiwa tu atatiliwa kitita cha feza na kwenda kujigandamiza kwa mlengwa akidai anataka kumkata mkno na watu wasiojua kinachoendelea wakamvamia mtu na kumua ,sijui uminielewa? Kiasi cha kuiona hatari iliyopo kwa kauli ya Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda !!!
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tutawasha moto na tumtengene GRILL.

  NB: Haya matatizo ya mawaziri wanachaguliwa na Rais ndiyo upuuzi wao. Masha kashindwa kazi na Pinda wala hawezi kumsema neno maana wote wamechagulia na Muungwana. Muungwana ndiyo majukumu kibao. Afufue ATCL, Bandari, kufuatilia pesa za EPA, Kiwira, Safari za nje, kuoza wanae, migomo ya kila siku, afufue reli, ajenge shule, akague maendeleo nk nk Hii ni kazi kubwa kwa mtu mmoja mchapa kazi, sasa itakuwa inapokuja mtani wangu Mkwere? Alahhh, Wakwere ni wanetu, siwezi watania :)
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wanasema kimtokacho mtu ndo kilicho mjaa moyoni.Kwamba muuaji wa albino kwa sasa(wengi wetu) tungependa naye auawe. Tatizo linakuja pale ambapo wote tunaukataa ukweli uliomo ndani ya mioyo yetu. Waziri mkubwa amesema hayo(mawazo yangu) pengine kutokana na ukweli kuwa hawa jamaa wanatuumiza sana vichwa Watz wote. Mtu ni albino anaishi kwa taabu tena akiwa na mikono miwili,mtu kwa tamaa zake anaondoa mkono,albino huyo aishije? Upande wa pili Waziri mkubwa kaona adhabu zetu ni laini mno na hazitekelezeki haraka ktk mahakama zetu,bora kuisaidia mahakama(maoni yangu pia) ua pale pale. Hofu ni kwamba wabaya wanaweza kuitumia hali hiyo ya sheria mkononi kwa manufaa binafsi. Rejea kijana wa Morogoro aliyefungwa maisha kwa kusingiziwa kuwa kabaka bibi, kumbe ugomvi wa shamba kijijini kwao.
   
 17. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ilikuwa ziara ya kichama au kiserikali? Katika kikao cha bunge kilichopita, Mh. Zitto aliwahi kumuhoji Mh. Pinda kuhusiana na swala la kutumia ziara za serikali kufanya shughuli za chama. Na kama hakufanya shughuli za chama, basi hakuwa na sababu ya kuwapa assignment UVCCM pekee. All in all, kauli yake ya "kuruhusu" wananchi wachukue sheria mikononi mwao ndio ya kuiangalia zaidi hapa !!
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Pinda huenda aliteleza ulimi na sasa yaani anaijutia kauli yake!
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...safi sana, ila tahadhari; hii ina apply kwa MUUAJI ATAYEONEKANA tu ...i.e caught red handed na shoka/panga lake na mkono wa albino...

  Revenge has no more quenching effect on emotions, than salt water has on thirst.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Utanitumia audio ya Waziri Mkuu Pinda akitangaza operesheni "jino kwa jino" ambapo inadaiwa alitoa kibali kwa UVCCM kushiriki katika mauaji ya watu wanaoamini kuwa ndio wauaji wa maalbino. Kama unayo sehemu ya hotuba hiyo wasiliana nami haraka iwezekanavyo.

  Wa kwanza kutuma ndiye atakayepata kifuta jasho hicho: Hata kama iko kwenye tape za kawaida.

  Wasiliana nami: mwanakijiji@mwanakijiji.com
   
  Last edited by a moderator: Jan 26, 2009
Loading...