Wimbo mpya wa Israel Mbonyi uitwao "Nitaamini" umejawa upako na matumaini

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,294
17,136
Wakuu,

Bila shaka mmewahi kuusikia Wimbo wa 'Nina siri na Yesu', ukiimbwa na mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili kutoka nchini Rwanda mwenye asili ya Congo, Israel Mbonyi.

Sasa siku kadhaa zilizopita alitoa wimbo wake mpya ukienda kwa jina 'Nitaamini'. Ni wimbo mzuri mno, lakini napenda sana Kiswahili fasaha wanachotumia Wanyarwanda.

Tangu umewekwa katika mtandao wa YouTube, ndani ya siku tano tu ilifikisha views zaidi ya Million moja.

Wimbo huo wenye dakika 13:04, hauchoshi kuusikiliza. Umejawa utukufu na sifa kwa Mungu.

Unatuasa hata tukimuomba Mungu hata asipotujibu, tuendelee kuamini kwa sababu hata hapo kabla Mungu alishatenda makubwa zaidi.

Sehemu ninayoipenda zaidi ni pale anapoimba kuanzia dakika ya 4:45.

Si mara ya kwanza kunitoa katika magumu, nina ushuhuda zaidi ya moja, wewe ni mwaminifu, nina historia maalum wewe ni Chemchem ya Uzima.

Ewe ndugu yangu, unaweza ukawa unapitia katika kigumu sana. Iwe katika afya yako, uchumi, familia, ama lolote lile. Tafadhali nakusihi endelea kumuamini Mungu kuwa atayafanya. Huenda anakupima imani yako, usinung'unike. Yatafakari yale makubwa ambayo tayari Mungu alishakutendea.

Unaweza kuusikiliza hapa chini, weka sauti ya juu. Sikiliza ujumbe murua

Lakini pia, unaweza kuangalia Youtube katika akaunti ya Israel Mbonyi.

View: https://youtu.be/iwcjcSEmw60?si=S9NtymhZ5bUHGHjQ

Ubarikiwe sana.
 
Juzi tulikuwa bar waheshimiwa wanywaji waliruka sana wimbo wa nina siri sijui.
 
Back
Top Bottom