Uhalisia wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya

Good Luci

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
370
441
Hello JF,

Karibuni tupate ufahamu wa aliyetuumba sote ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine.Twende pamoja

UFUNGUO
Wakristo kwa Waislamu wanasubiri siku ya kiama au mwisho wa dunia! Wengi wao wakisema mwisho wa dunia wanadhani kuwa ni tanuru la moto ambalo litawaka kama moto wa kuyeyusha chuma kuangamiza watu. Hawadhani kuwa akili kufika mwisho ni suala la wataalamu wote wa dunia kushindwa kutengeneza dawa ya UKIMWI na Corona, ndiyo mwisho wenyewe wa dunia(1Kor. 15:24)!

Mwaka 2000 ilitangazwa Y2K, Manabii wengi waliandaa wafuasi wao kuwa sasa Yesu anarudi Mwaka huo, lakini tayari imeshapita Miaka zaidi ya 20! Madhehebu mengi yaliyokuwa na imani na tumaini hilo, sasa watu wanafanya dhambi kuliko kabla ya kuamini na kutumaini kwa kuwa wamekata tamaa, baada ya kuchoka kusubiri.

Ili ujue kuwa Akili za mtu zimeshafika mwisho, Watawala wa dunia na ulimwengu ambao hawaonekani kwa macho (wakuu wa uweza wa anga-efeso 2:2) wanaosababisha vita, milipuko ya magonjwa, vimbunga vya Katarina na Sunami, hawaongei chochote sasa hivi kwa kuwa akili zao zimefika mwisho kabisa. Watabiri wa hali ya hewa na mambo yajayo nao pia kwa sasa wanatabiri kinyume na matokeo ya utabiri na ubashiri wao

Kwa ufupi, hakuna elimu au ujuzi wa mtu ambao kwa sasa unaweza kutueleza kweli zaidi ya yale yaliyoandikwa katika 1Korintho 15:24-28 kuwa akili ya mtu ikfika mwisho lazima alivekuwepo kabla ya chochote (Yeremia 1:5) akabidhiwe: ufalme,mamlaka, utawala na nguvu ili yeye ndiye awe iuu ya vyote, wote na yote.

Katika Ufunuo 21:1 imeandikwa wazi kuwa Mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vitatoweka na hapo ndipo Aliyeumba kila kitu ataishi katikati yetu juu ya nchi (ikiwa na maana ya kuonekana kwa sura ya kila mmoja wetu). Katika Yeremia 1:5 imeandikwa wazi kuwa, tulijulikana kabla ya kuumbwa. Kipindi hicho kimeandikwa sehemu nyingi katika Kitabu kuwa kikifika kitaitwa Mbingu Mpya na Nchi Мруа.

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
Katika Mistari ifuatayo, suala la Mbingu Mpya na Nchi Mpya limeandikwa kwa uwazi:

•Isaya 65:17;
•Isaya 66:22-23;
•Ufunuo 21:1-3; na
•2 Petro 3:13.

Haihitaji mwenye elimu ya chuo Kikuu kuelewa
maana iliyopo katika mistari hiyo, bali unahitaji ujue kusoma na kuandika tu. Tatizo kubwa, karibu Mabara na nchi zote, hakuna aliyejua kuwa itatokea wakati gani na mahali gani hiyo Mbingu Mpya na Nchi Mpya?

Wamisionari wote waliotangulia kuleta dini na madhehebu mbalimbali huku Afrika na Tanzania ikiwemo, hawakusema kuwa suala hili litatokea Tanzania eneo la Kigoma. Ingawa wao walikuwa wanajua vizuri siri hio. Hata hivyo hata wao walichofichwa ni majira sahihi na nani atakayehusika katika majira hiyo.

A. Suala la Dr. Livingstone kuja Kigoma-Ujiji wakati ule wa Miaka ya 1862, ni suala la kushangaza kwa kuwa kwa wakati ule Kigoma hapakuwa na jina la kumfanya Mtu atoke Ulaya kuja Tanganyika mpaka Kigoma!

Lakini pia suala la yeye kusema kuwa akifa moyo wake uzikwe Kigoma ni suala la kushangaza. Hiyo ina mana kuwa alikuwa anajua Kigoma-Tanzania kutatokea kitu gani.

B. Suala la Waarabu walioweka ngome Ujiji, badala ya Dares Salaam (ingawa walijua pale ni Bandari Salama) ni la kushangaza pia! Ina maana walikuwa wanajua kuwa Kigoma-Ujiji kutatokea kitu gani.

C. Suala la Wajerumani kuweka Makao Makuu ya Germany East Africa Kigoma kwa wakati ule ni la kushangaza, maana Kigoma haikuwa nzuri kuliko Dar es Salaam, Mwanza na sehemu nyinginezo. Unagundua kuwa walijua ni kitu gani kitatokea baadaye. Hata Reli iliyotandikwa kutoka Dares Salaam kuja Kigoma Miaka 100 na zaidi iliyopita, bila kuwepo madini na bidhaa za kuchukua kutoka Kigoma kwenda mbali (wakati ule) ni la ajabu pia. Maana bidhaa iliyokuwepo kwa wakati ule ni ya watu peke yake yaani watumwa waliokuwa wanapelekwa sehemu mbalimbali duniani.

D. Suala la Wamisionari wa kiswidishi waliofikia
Tazengwa-Tabora baadaye wakasema wamekosea ni Bigabiro- Kigoma nalo ni la kushangaza. Ukiangalia kwa haraka unaweza usijue kuwa ni suala la Sauti ya MUNGU BABA iliyosikika Kigoma-Tanzania katika Majira hii.

Kwa ufupi, waliotuletea dini na madhehebu mbalimbali walijua kuwa mambo yanayotokea majira hii yataanzia Kigoma Tanzania,Ila hawakusema. Matokeo yake; Kigoma ikawa ni sehemu ambayo ilikuwa nyuma kuliko sehemu zingine. Watu wa mahali hapo wakawa wanyonge badala ya kuwa mashujaa.

Hiki ndicho Kimechelewesha kuelewa na kupokea ujumbe Wa Hija ya Mungu Baba ambaye ndie Chanzo Halisi kuwa sasa Hija ni Kigoma Tanzania, siyo mashariki ya kati tena kama tulivyozoea katika majira zilizopita.

Kinachoshangaza; hata wenyeji bado hawajapokea moja kwa moja kuwa ndivyo ilivyo pamoja na vithibitisho vingi kama nilivyotangulia kuorodhesha Habari za akina Dr. Livingstone na wengine. Sioni kwa nini tuendelee kutilia mashaka suala hili la Hija ya Chanzo Halisi kuwa Kigoma-Tanzania. Tupokee ili twende mbele kimaendeleo kwa kuwa Hija hii inatupa kuwa na mahusiano mazuri na Aliyetuumba.

MUNGU BABA AMEKUJAJE KUPITIA TANZANIA?

Swali hili wanajiuliza wengi kama si wote. Sababu kubwa ya kujiuliza ni kwamba, kila mmoja alikuwa ha taswira yake binafsi kuhusu MUNGU kulingana na
•Walimu wake (wazazi, mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti, waalimu, mapadre, masheikh na kadhalika)

Imani na matumaini yote, mafundisho mbalimbali Pamoja na maandishi ya vitabu vya watu mbalimbali, huonyesha kuwa Yesu, MUNGU na watakatifu wote ni weupe! Hili nalo limeleta shida kusikia kuwa MUNGU BABA kashukia Kigoma Tanzania! Tena afadhali wangesema maeneo ya Dar es salaam au Arusha, Mwanza, Mbeya, ukisema Kigoma (mahali ambapo miundo mbinu ya kisasa haipo) unaonekana kuwa hauko sawa.

Katika dini na madhehebu karibu yote, hakuna aliyefundishwa kuwa MUNGU BABA aliye chanzo cha kila kitu ni Moyo na ni Sauti! Katika Kitabu imeandikwa wazi kuwa, Muumba wa Kila Kitu alipomtokea Aliyetumwa yeyote alimpaka mafuta kwa Sauti siyo mafuta ya kimiminika kama mawese au Korie. Hili lilijenga taswira kinyume na jinsi MUNGU BABA aliyeumba kila kitu alivyo. Pili, wote waliotumwa kama vile;-

•Kerubi (Ezekiel 28:15)
•Adamu wa kwanza (Mwa.2:15);
•Musa (Kut.3:10);
•Eliva Mtishbi (1Fal. 17:1);
•Yesu (Mdo. 10:38);
•Adamu wa pili (Yoh.9:7).

Hakuna aliyetambulisha Habari za MUNGU BABA katika dunia na ulimwengu. Waliotumwa wote walilazimishwa na dunia kuabudiwa wao ili wawe fidia ya dunia na ulimwengu (Isaya 53 yote). Yesu, alitamani sana kumtambulisha MUNGU BABA kupitia: Yohana 9:29; Yohana 4:23; na Yohana 15:1-15 (kama tunavyoona akiongea naye katika Yohana 17 baada ya kumaliza kazi yake); lakini dunia ilikataa wakataka yeye ndiye aabudiwe.

Baada ya Majira kufika ya kuja MUNGU BABA, ninachoeleza hapo juu ndicho kimesababisha
kuchelewa kupokea ujio wa MUNGU BABA.

Aliyeshukia Tanzania kwa Sauti, kwanza Kama Nafsi ya Kwanza Mwaka 2017 na sasa akiwa Moyo Halisi 2020. Ukisoma Zekaria 14:9 ujumbe ni wazi kuwa anayesemwa pale siyo Mwana bali ni Chanzo Halisi, lakini dunia ilifundisha tofauti kwa malengo yao maalumu.

SABABU ZA DUNIA KUKATAA UJIO WA MUNGU BABA.

Ukisoma Mwanzo 1:1 utagundua kuwa MUNGU
BABA, ambaye ni Moyo au chemchem ya mema na mazuri yote, aliachilia Utajiri na Heshima kupitia ule Moyo wa Mwanzo(uliokasimiwa uumbaji) ambao ndiyo Mbingu ya Kwanza na Nchi ya Kwanza (Mithali 3:10).

Kupitia Ufunuo 12:1, utagundua kuwa kuna chipukizi ambalo kwa jina sahihi ni nafsi ya uvamizi lilichukua huo utajiri na heshima yote ndani ya huo Moyo wa Mwanzo. Katika huo moyo wa mwanzo, Kulikuwemo kila kitu kinachofanana na alivyobaki navyo Chemchem ya mema na mazuri tu.

Kila aliyekubali ishara ya kwanza, ya pili na ya tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9), ndiye aliyepata heshima na utajiri. Hao Ishara tatu ndio waliounda kitu kinachoitwa dunia na ulimwengu badala ya mbingu na nchi zilizoachiliwa katika Mwanzo1:1. Aidha, hao ishara tatu mbinguni, ndio wanaomwambia Mwana, katika Luka 4:5-9 kuwa yote viko mikononi mwao (ingawa wewe pale unaona imeandikwa ibilisi)! Kumbuka siku zote kuwa shetani, ibilisi ni mdogo sana kwa kulinganisha na hizo ishara tatu mbinguni.

Majeshi vote ya uharibifu katika Efeso 6:12 ni ya hizo ishara tatu mbinguni. Kuzimu na ujinini pia ni majeshi ya hizo ishara tatu mbinguni.

Waliotumwa wote katika majira zote saba, walikuwa chini ya hizo ishara tatu mbinguni. Hakuna dini, dhehebu au Huduma chini ya jua iliyowahi kuwa juu ya hizo ishara tatu mbinguni katika Ufunuo 12:1-9!

Pia, hakuna chuo wala shule iliyowahi kufundisha kuwa kuna zaidi ya Mwanzo1:1 au Ufunuo 12:1 aliyevamia Moyo wa Mwanzo, maana wote walikuwa chini yake, lakini wengi kwa kutokujua.

Hicho ndicho kimesababisha kuchelewa kupokea ujio wa MUNGU BABA juu ya nchi kupitia Tanzania. Mafundisho yote kutoka kwenye ufahamu ulioanzia Mashariki ya kati kwenda Ulaya, Amerika, kurudi Ulaya na kisha Afrika na kwingineko, yalikuwa yanaonyesha kuwa mambo yote ni Israeli na mecca ya kule Mashariki ya kati na si penginepo.

Kila mwanatheolojia, anasahau swali aliloulizwa
Yesu kuwa, yale aliyoeleza katika Mathayo 24 yote, kuhusu siku ya mwisho yatatokea lini? Alisema kuwa yeve wala Malaika wa mbinguni (kwa wakati ule) hakuna aliyekuwa anajua zaidi ya Baba yake.

Aidha, wanatheolojia wanasahau kile alichosema Yesu katika Mathayo 24:22 kuwa kama siku zisingefupishwa, yaani ile Miaka elfu Moja katika Ufunuo 20:6, hakuna ambaye angeokoka. Pia, wanatheolojia wanasahau alichosema Yesu katika Mathayo 21:43 kuwa ilikuwa ni lazima ufalme uhame kutoka Mashariki ya kati kwenda katika Taifa lingine, ambalo Chanzo Halisi anaona kuwa linamzalia Matunda.
 
Back
Top Bottom