Wimbi kubwa la wazee na wanawake wa miaka 45+ kuongezeka kwenye kamari (kubeti) tatizo ni nini?

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,992
Habari za asubuhi wana JF,

Kuna wimbi kubwa mtaani la wazee na wanawake kujiingiza kwenye kamari (kubeti), tatizo umasikini au ndio maendeleo ya soka nchini?

Nakumbuka World Cup last year kila mtu ni kubeti tu, ukikutana na wazee, wanawake wa mtaani wanataka uwafundishe kubeti na wakisikia fulani kashinda mkeka wanachanganyikiwa, na wao wanajitahid kubeti kwa nguvu ili washinde. Unakuta familia nzima wanabeti!

Viongozi wa dini nao wanabeti kisirisiri, nilishawahi kumshitukia mmoja. Mnajifanya wema Sana kukataza,na tuwe mbali na dhambi ya kamari kumbe na nyie mpo addicted na kamari.

Na wastaafu wengi wakiona tu hela inakaribia kuisha nao wanajiingiza kwenye kubeti, mwisho wa siku hela imekata wanakuwa addicted na kamari, kazi kupiga vizinga watu ili wakabeti.

Vijana tupambane na life ili tusitumie uzee wetu kwenye kamari, kubeti ni kama burudani sio kazi.

Naomba kuwasilishaa.
 
Chanzo cha haya yote ni ajira.....nina mwanangu tulikuwa watu wa mikeka sana hizi jackpot za mbet na spotpesa tumezicheza sana. Mwaka jana kapata kazi akabetbeti kidogo akaona vipigo vimezidi na mshahara anao sahvi kaacha kubeti kabisaa.
 
Hawa wanawake wana bahati sana mimi ni mpenzi wa spin pale premier bet kuna dada namkutaga na nikifuata upepo wake nabutua balaa sijamuona muda sasa ila mara ya mwisho aliondoka na over 300k kwenye spin akaaga anaenda kupumzika mpka ajifungue mimba ilikua kubwa tu nahisi ashashusha mfuasi mpya wa kubet mtaani😆😆
 
Hawa wanawake wana bahati sana mimi ni mpenzi wa spin pale premier bet kuna dada namkutaga na nikifuata upepo wake nabutua balaa sijamuona muda sasa ila mara ya mwisho aliondoka na over 300k kwenye spin akaaga anaenda kupumzika mpka ajifungue mimba ilikua kubwa tu nahisi ashashusha mfuasi mpya wa kubet mtaani
 
Moja kati ya shida kubwa iliyoibuka Africa- Tanzania ni hizi betting, akili za watu zimekuwa dormant hakuna kingine Cha kuwaza. Nilikuwa mkoa flani nikashangaa kuona mpaka wazee watu wazima wanaelekea kuzeeka lkn wako na makaratas mengi na wako busy sana. Inasikitisha, Mzungu anajua kuivuna Africa Kwa stail nyingi. Hakuna Tena ubunifu Mawazo yamekuwa ni kubashiri tu, licha yaa rasilimali zinazopatikana TZ.
 

Attachments

  • images (14).jpeg
    images (14).jpeg
    41 KB · Views: 16
Itakua huijui kabisa betting,huko ulaya vilabu vya kandanda vinaangalia uwezekano wa kutoweka tangazo la betting kwenye jezi zao,maana wazungu wanabet balaa kiasi inawaletea umasikini, marekani ndiyo usiseme,ni kukosa kazi,ukiwa na kazi kubet ni nadra au hakuna
 
Moja kati ya shida kubwa iliyoibuka Africa- Tanzania ni hizi betting, akili za watu zimekuwa dormant hakuna kingine Cha kuwaza. Nilikuwa mkoa flani nikashangaa kuona mpaka wazee watu wazima wanaelekea kuzeeka lkn wako na makaratas mengi na wako busy sana. Inasikitisha, Mzungu anajua kuivuna Africa Kwa stail nyingi. Hakuna Tena ubunifu Mawazo yamekuwa ni kubashiri tu, licha yaa rasilimali zinazopatikana TZ.
Ukibeti halafu unazalisha huduma au Mali

Ila kama unabeti na huzalishi chochote basi hatari ya nchi kuyumba ni mkubwa

Usipozalisha na upate fedha,basi utaiba Ili ubeti
 
Ma Afisa ubashiri tunalipa Kodi Kwa Kila mkeka kwa takribani 18%-20% kwenye Kila mkeka.  Ma Afisa usafirishaji (bodaboda) hawalipi kiasi hicho. IfIke hatua makampuni ya bima yatutambue.
Aahaaaa

Afisa Ubashiri

Nimelipenda hili neno

Mkuu Hawa maafisa kima Cha chini Cha mishahara yao ni tsh ngapi Kwa mwezi!!
 
Back
Top Bottom