Naona kama CCM na wafuasi wake wamejenga chuki kubwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi, tatizo ni nini hasa? Je, wanaelewa umuhimu wa kundi hili?

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Wandungu, siyo siri naamini nanyi mmeona kuwa chuki dhidi ya watanzania waishio nje ya nchi imeongezeka sana kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli. Kama huamini jaribu kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo humu ndani hasa kuhusu mada zinazohusu siasa na watanzania waishio nje ya nchi, utaona chuki imejengeka kuelekezwa kwa ndugu wanaojitafutia mali nje ya nchi.

Ushuhuda upo wazi kuwa CCM na wafuasi wake wamekuwa wakiwaita watanzania waishio nje ya nchi mawakala wa mabeberu, mashoga, wabeba boksi, wanaishi maisha duni na waosha vikongwe. Zaidi utawasikia ama kuwasoma wakitoa wito eti rudi nyumbani kumenoga.

Hali ya chuki imezidi kuongezeka sana hasa kipindi hiki tukielekea kwenye uchaguzi mkuu.

Hali hii inakera sana, hasa kwetu sisi tunaoujua umuhimu wa raia wa taifa lolote lile kuishi nje ya nchi yao. Hapa napenda kutoa somo kidogo kuweka mambo sawa.

KWANZA
Hakuna mtanzania yeyote aliyeko nje ya nchi anayeichukia nchi yake bali anachukia matendo ya kikundi kidogo cha watu wanajiita serikali dhidi ya watanzania wengine kisa tu wako vyama vya upinzani. Hivyo siyo kila anayepinga uovu ambao kwa sehemu kubwa mataifa hasa ya magharibi nayo yanapinga basi ni wakala wa mabeberu.

PILI
Siyo kila mtanzania aliyeko nje ya nchi ni shoga hata kama anatetea haki ya mashoga kuishi, pia si kila mzungu anawapenda mashoga, zaidi ya yote mashoga wapo kila mahali ikiwemo Tanzania, wapo maofisini na mitaani, wengine wameoa na wana watoto lakini pia wanagongwa ama kugonga wanaume wenzao, wanafanya siri kubwa. Kuna wasagaji pia. Tofauti ya nchi zilizostaarabika na Tanzania ni kuwa zinalinda uhuru wa mtu na haki yake ya kuishi haijalishi awe shoga ama wa kawaida kwa kuweka sheria imara.

TATU
Siyo kila mtanzania aliyeko nje ya nchi anabeba boksi ama kuosha vikongwe. Lakini hata hivyo ikiwa utaringanisha maslahi ya mtanzania anayebeba box ama kuosha vikongwe nje ya nchi ni zaidi ya maafisa wa juu wanaofanya kazi serikalini huko Tanzania. hapa naongelea mshahara. Ni hakika ikiwa mbeba boksi wa Ulaya (hapa naongelea Ulaya magharibi) atakuwa na mkataba wa kudumu kwenye kampuni yoyote ile mshahara wake kwa mwezi ni zaidi ya Tsh milioni 7 kwa mwezi.

Achana na wale ambao wanafanya kazi kupitia mawakala wenye mikataba ya muda mfupi lakini nao mashahara wao si haba. Muosha vikongwe naye anaheshimika sana, kazi hii haifanywi hovyo hovyo tu kama wengi mnavyofikiria. Inafanywa na wataalam wa ustawi wa jamii.

Lakini Ulaya ni Ulaya tu, umeme wa uhakika, usafiri wa uhakika, internet ya uhakika kila mahali (hakuna kununua bando), barabara nzuri na za kudumu kila mahali, waweza tembea nchi nzima usikanyage udongo labda upende. Kila mahali pamewekwa vigae. Maji ya kunywa hununui ni kwenye bomba tu. hata kwenye choo cha umma unapata maji ya kunywa safi na salama. Huyu mbeba boksi ana uwezo wa kumiliki gari zuri ikiwa atapenda. Lakini wengi wanaamua kutokuwa na magari kwa sababu usafiri wa umma ni wa uhakika na bus, treni, tram viko kila mahali na vinaenda kwa muda.

Ukitafuta google map unaona mpaka muda bus litakapofika. Makazi kiukweli ni gharama ila unaweza kumudu. Ikiwa una milioni 2 za Tanzania kwa mwezi waweza pata nyumba (apartment) nzuri ya kuishi. Wengine nimeona wanabeza kuhusu apartment residence. Ulaya ndiyo utaratibu. Ukisikia apartment haimaanishi zile za NHC, bali ni nyumba zilizojengwa vizuri na zinatoa privacy ya uhakika. Chakula ndiyo usiseme, vipo kwa wingi na bei utakayoimudu.

Huduma za afya za uhakika. Ikiwa utaugua kampuni utaendelea kukulipa. Ikiwa huna kazi serikali itakulipa kiwango cha fedha za kumudu maisha kila mwezi mpaka utakapopata kazi. Ifahamike kwamba pia kuna watanzania wanafanya kazi professional kabisa na wala siyo kubeba box ama kuosha vikongwe.

NNE
HAKUNA MTANZANIA MWENYE DOCUMENT HALALI ANAYEISHI MAISHA DUNI ULAYA HILI MFAHAMU, MAISHA YAKE NI BORA MARA NYINGI SANA ZAIDI YA BOSI WA TANZANIA.

UMUHIMU WA RAIA KUJITAFUTIA MAISHA NJE YA NCHI
Ukichunguza kwa makini utagundua siyo Rais Magufuli, serikali yake na watanzania wengi wanafahamu umuhimu wa watanzania wengi kuishi nje ya nchi. Licha ya kwamba hawawezi kuajiri watu huko nyumbani. Wengi huwaona watanzania walio nje ya nchi kama vile wasaliti na wasioipenda nchi yao. HII SIYO KWELI. DUNIA NI MOJA NI HAKI YA KILA MTU KUISHI AONAPO FURSA.

Hakuna kundi la watanzania linaloipenda Tanzania kama waishio nje ya nchi.

Sina takwimu za BOT kuhusu Tanzania lakini tukitazama takwimu za utumaji hela nyumbani kutoka watu waishio nje ya nchi zao kwa nchi za kusini mwa Afrika kwa mujibu wa Bank ya Dunia ni kwamba mwaka 2018 watu waishio nje ya eneo la nchi ya SADC walituma jumla ya $46 billion, soma zaidi hapa Record High Remittances Sent Globally in 2018. Ni wazi kwamba watanzania walio nje nao hutuma nyumbani, ikiwa kutaletwa takwimu za uhakika naamini kiasi kitakuwa kikubwa.

Fedha hizi ni nyingi sana kwa maendeleo ya watu kwa maana mara zote hutumwa kwa familia kusaidia gharama za elimu, chakula na malazi moja kwa moja. WENGI HAWAONI UMUHIMU HUU.

YAANI SERIKALI YA RAIS MAGUFULI INGEJUA UMUHIMU WA WATANZANIA KUISHI NJE YA NCHI INGETOA PASSPORT KWA RAIA WAKE WOTE ILI IKIWA WATAKOSA AJIRA NYUMBANI BASI WAKAJITAFUTIE NJE YA NCHI. LAKINI KWETU UTASIKIA RUDI NYUMBANI KUMENOGA KISA UJENZI WA MADARAJA YA JUU. SHIDA KWELI KWELI.

NIMALIZIE KWA KUWAULIZA WANDUGU, ILI NAYI MJAZILIZIE, KWA NINI CHUKI DHIDI YA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI IMEONGEZEKA HASA KIPINDI CHA AWAMU YA TANO? JE RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE WANATAMBUA UMUHIMU WA RAIA KUISHI NJE
 
Kwani ni lazima nchi ikubali kuwa na uraia pacha? Hao waliopo nje hakuna mtu aliyewakataza kushiriki siasa na uchumi wa hapa nchini waje tu wawekeze mbona JK alikwenda US kuwachukua Sullivan kwa nini asiwalete na hawa wetu. Tanzania bado ni nchi changa ngoja kwanza ijenge uchumi imara alafu mengine yatafuata
 
Loooo!! kumbeeee!! wewe hujui mleta Mada!!....Miafrica imejawa na chuki kufuruuuu!!...ndo ilivo hata ufanyejeeee!! wewe kazia hapo hapo!!! chuma uchumavyo!! somesha wanao!! sana!! shikamana na anaye kushika mkono!!

lkn ukijifanya eti kurudi sababu tu! wanuka vikwapa wanasema eti kumenoga mweee!!.......... hako ka-fly over kachafu!! ka mfugale ndo kakurudishe??? .....kulee watakudedisha tu!! kwanza ujue tu kuwa kuchomoka mikoani tu! kwenda jijini Dar es salaam!!


Utavunjwa moyo ni ile mbaya kama siyo kurogwa usipate hamu tena!! Si unaonaga ukienda Mikoani huko kuzika watu wanavo jipendekeza kupata connection!!! wameshindwa yaani wewe ukienda mikoani ni km gold hasa kam unavinyamanyama hujachoka??

wakisema wabeba Box!! kamwee!! usiumie!! wao wenyewe hao wanatamani Hilo box walipate wapi??? hayo ni maneno ya kukosa achana nao!! Rais wao mwenyewe ana zomewa sembuse weye!!...kazia hapo hapo weweeee!

hata hapo bongo ukiwa na maisha safi flani hivi!!! wa chini yako wanaumia sana! hasa mliotoka nao sehemu moja yaani ukimuangalia usoni ivi unaona kabisaa huyu analilia moyoni huyu!!! bora huko huko mnafanana!!

na hii iko kwa ndg na hata marafiki, na hata ukirudi hapo then ukapigika!!! ni hao hao wata kufanya uishi kwa stress!!!! cha msingi ukichomoka chomoka tuuuuuuu!! toa hela zako kwa akil utarogwa hayaaaaa!
 
Back
Top Bottom