- Well, nimesoma yote na kwa makini sana I mean kwanza naomba kusema hivi:
1. Mleta mada kwa kutumia picha hii kuna a misguided understanding, ni kwamba nilipokuwa ninaishi New York City, USA nilikuwa STAR wa kipindi maarufu sana cha Growing UP African TV Realty Show, sasa kitaalamu ukiwa muhusika wa TV show kama nilivyokuwa, unapangiwa namna ya kuvaa na the whole appearance yako na PRODUCERS wa kile kipindi cha TV, kwa hiyo ndio maana kwenye picha zangu nyingi nikiwa US utakuta nimevaa kwa ridhaa za watayarishaji wa kipindi. I mean nilitaka kusawazisha hilo kwamba sio tabia yangu kuvaa namna hiyo isipokuwa ni moja ya kazi zangu kule US za kuwa mchezaji wa TV Show ndio maana nilikuwa ninavaalishwa Chain, Fulana, na nguo za aina mbali mbali ili kukizi matakwa ya watayarishaji wa kipindi, au waajiri wangu.
- Kuhusu mengine yote niliyoyasema kwenye mahojiano na Skype/Radio World, UK ninayasimamia kwa 100% ndio msimamo wangu na ninaamini unapaswa kuwa msimamo wa Taifa langu, kwamba:
- EAC ilivunjwa na Kenya Mwaka 1977 baada ya kudumu kwa Miaka 10 tu, ilipovunjika sisi Tanzania ndio tulioumia sana hasa nyanja za Airline na Railways ambazo mpaka leo hatuja-recover, leo Tanzania tuna Ardhi inayomilikiwa na Serikali kisheria wakati Kenya hakuna sheria kama zetu, sasa tunaingiaje kwenye One Currency na Political Federation bila ya kuwa makini na kutafakari kwanza? Ninasema kwamba tuwe makini sana kabla ya kuingia huko kichwa kichwa, sasa kama kwa kuwa na msimamo huu ni kuwa a disaster in waiting so let it be! Lakini given a chance nitarudia tena na tena kwamba ndio msimamo wangu na ninaamini kwamba unatakiwa kuwa msimamo wa Taifa letu!
- Kuhusu JKT: Kama nilivyosema ninasema tena hivi Serikali yetu ni muhimu sana ikarudisha JKT kwa sababu mimi binafsi imenifundisha sana Uzalendo, mpaka kweza kuishi nje miaka yote niliyoishi bila kubadili Uraia wangu, again ninasema JKT irudishwe it was a very good thing kwa Taifa.
- Moja ya mafanikio yangu makubwa on Community Organizing ilikuwa kuwakusanya wa-Tanzania karibu 300 mjini New York na kushirikiana nao kutayarisha Sherehe kubwa ya kumpokea Naibu Katibu Mkuu wa UN, DR. Asha-Rose Migiro na pia kuwaunganisha Wa-Tanzania kama Chama kwenye Community ya New York, na pia mimi ndiye muasisi wa tawi jipya la CCM, New York City, USA: Now let me say this kama wewe msomaji unaamini kwamba anybody can have this skills za kuweza kufanya hayo niliyoyafanya, then forget about it lakini mtumzima yoyote mwenye akili timamua anyeijua New York City, anajaua kwamba it takes a lot of skills za uongozi kuyafanya hayo niliyoyafanya na infact I am proud of it!
- Otherwise, ninaomba kusema hivi this is me, siwezi kujifanya something I am not kwa sababu nitakwua a pretender au fake, EAC imekuwepo kwa miaka mingapi hebu sema ni lini uliwahi kusikia Mbunge wetu wa EAC akisema anything? iwe huko bungeni au popote pale nchini? You know that wont be the case with me, kwanza nataka wananchi wote wa Tanzania wajue kwamba kuna hilo bunge na sisi ni mwanachama wa Bunge hilo, pili sitathubutu hata siku moja kuamua maamuzi mazito bila kuongea na Bunge letu la Jamhuri for their approval, kama na wao hawaelewi na ninaona ni ishu yenye faida kwa Taifa letu hasa wananchi, nitaichukua kesi yangu kwa Wananchi, waamue wanataka nini hasa baada ya kuwaelimisha on the ishu!
- Kwa hayo machache ndugu zangu, naomba kurudi kwenye kuendelea na michakato ya kampeni yangu na mihimu tukasaidiana maana taifa ni letu wote!
MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA AIBARIKI JF!
William.