William Malecela: Dissaster waiting to happen | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

William Malecela: Dissaster waiting to happen

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Apr 3, 2012.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia

  Hoja zake kubwa ni hizi:

  1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.

  2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .

  3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.

  4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:

  a) Kwa nini iliondolewa in the first place

  b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana

  c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service

  d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake

  5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?

  6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.

  7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?

  Je william anajua:

  a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!

  b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo

  c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?

  d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.


  8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?


  9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.


  10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.


  In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.


  William kama mawazo yako ni hayo then I give up!
   
 2. m

  mharakati JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wewe unataka federation ije 2013 halafu itatunufaisha nini? eti maendeleo ya dunia, hujafafanua economic integration inayoitaka ni ipi? EU model? angalia backaground ya EU toka 1958 mpaka treaty ya 1992, progressively wakiwa wanabadilika taratibu kutokana na mahitaji. EAC inachohitaji ni kuboresha mazingira ya ushirikiano wa kiuchumi na soko huria, labor movement, security sharing etc kabla ya kuwa political federation...nyie ndiyo watz ambao mnaona kila cha nje kinahitaji kuigwa,,na wewe ni hatari zaidi kuliko huyu anayesema federation iende taratibu
   
 3. T

  TanzActive JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 350
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa sasa Tanzania will be losers why?
  1.Mfumo wa Elimu umepolomoka sana na unatoa wahitumu ambao hawataweza shindana na wenzao EA, hii tumeshaanza kuiona kazi nzuri nzuri za IT na banking zimebebwa na wakenya sasa

  2. Arumeru wanalalamikia ardhi, nawajua wakenya wengi tu wanaomiliki ardhi hulo, na ndo kwanA tumeanza

  3. Masoko yetu yamejaa bidhaa za kenya ,lakini nikienda kenya sizioni zetu

  Hapaha EAC kwetu sisi wakulima na wafanyakazi masikini ambao ni 90% bado hatuitaki kwanza
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  EAC to hell
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  tuijadili tunatakiwa tufanye nini
   
 6. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  tunatakiwa tuachane na huo uduanzi wa Eac federation..hatuitaki kwa sasa.
   
 7. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kheri yeye aliyesema twende slow na kutoa sababu zake.Na wewe unayetaka tuharikishe toa sababu zako,
  usikurupuke,EA hatuitaki hatuna ardhi wanayoitamani hawa wenzetu.Mbona ilikuwepo ikatushinda,ndo hii ya
  sasa tutaiweza,damn.
   
 8. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiye mjinga!
  Angalia nchi kama Danmark, Norway. Hazipo kwenye european union na uchumi wake ni makini. Ficha ujinga wako usije ukaropoka na kujaji bila kuelewa duniani kuna nini. Nadhani wewe ndiye upo nyuma sana ki dunia. Huwezi ukazamisha uchumi wa Tz East Afrika na ukategemea tutaibuka. Ni muhimu tujijenge kwanza sisi ndiyo tufikirie kujiunga. Kwa taarifa yao asilimia 99.9999 ya vijana hawataki East africa federation kwani sasa ajila ni shida na hapo bado. Ardhi sasa hivi inamendewa na wageni, na vijana wa tanzania bado wengi ni maskini na wengi ndiyo tumetoka shule sasa huo ushindani tutauweza??
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Asilimia 75 ya watanzania walisema iwe slow kwenye kura za maoni naona yuko sasa ingawa bado namwona ni mtoto wa Obama alitakiwa kurudi mapema Tanzania ili aweze kumudu siasa za ndani ya nchi yake kabla hajaanza kupigania siasa za nje.


  Sina mvuto na vijana wanatoka nje ya nchi na kuja moja kwa moja kushika madaraka napenda wanaotangulia kujijenga kwanza katika siasa wakafahamika.
   
 10. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  nakubaliana na wanaoona process iende taratibu,nikweli sio kosa la wenzetu sisi kuwa nyuma,lakini kuharakisha shirikisho hakutatusaidia pia,bora twende polepole na hatimaye tufikie kuwa na win win situation ndipo tuungane
   
 11. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ..yaani umenichefua sana, nigekuwa MODs ningekulamba BAN ya siku tano ukajifunze madhala ya hiyo federation unayoililia.
   
 12. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  EAC haikwepeki, inamkono wa waendesha dunia. Hivyo suala ni kujipanga na kuondoa sheria na sera mbovumbovu za kijima ili iwe rahisi kwa sisi kwenda kupeleka bidhaa kenya, uganda na sudan ya kusini.
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mi naona yuko right kabisa kwani kuhalakisha hakuna maana kama hatujajiandaa
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tena sio slow tu should be very slow!
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  le mutu le baharia has a point.
   
 16. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hili natofautina na wewe mtoa hoja na nakubaliana na William Malecela, kwanini twende haraka hiyo haraka tunakimbilia nini cha kutunuifaisha kwa sasa tunatakiwa tufanye tathimini toka tumeanza mpaka sasa tunanufaika na nini na tundako tutanuifaika na nini?
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio unamatatizo. wewe binafsi tuambie unataka kwenda kwenye federation ili uexploit opportunity gani? unataka kwenda kufanya nini kenya masikini wewe? hapa nyumbani utakuta hata ardhi hauna will you get it in Kenya? tena sio go slow, ni no federation.
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  william Malecela wengi tunakufahamu tu kupitia jamiiforums lakini watanzania wengi hawajakusikia ungeanza na kujitangaza mapema kama ulikuwa na nia ya dhati ya kuingia kwenye siasa.

  Kutumia short cut kwenye siasa unaweza kuwa unajitenegenezea ajali mbaya ya kisiasa.

  Kumbuka SIYOI SUMARI alipokufa tu baba yake ndipo akataka siasa na wewe mzee wetu John Malecela alipoanguka tu jimboni kwake umechomoza kwenye siasa.

  Hata kama nia yako ni njema umekosea mahesabu ili uweze kukubalika na watanzania wengi ndio maana wengine wanafikiri unatumia jina la baba kama ngao ya kufika juu kwa sababu umeruka baadhi ya ngazi muhimu kwenda juu
   
 19. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Lakini aliomba ushauri humu jamvini, baadhi tulimshauri ila inaonyesha alikuwa amejipanga zaidi. Bado tunanafasi ya kushirikiana naye kimawazo kama atachaguliwa kutuwakilisha. Wahenga walisema, kuvunjika kwa koleo............
   
 20. R

  Renegade JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Huyu Jamaa siyo Mjinga, Ni kweli Tunahitaji EAC, Lakini tunahitaji kwa namna ipi? Sio kitu cha kukurupuka kabisa, tuangalie Strengths zetu na weakness zetu kwanza kabla ya kuingia kwenye Federation. Partners state zote wanataka kutuarakisha kwasababu wanaangalia Opportunities zinazopatikana kwetu na namna ya kuziexploit. Viongozi wetu wako busy kutafuta Posho za Vikao na Safari.
   
Loading...