- Hakuna Diplomasia kwenye Historia
Historia gani unayoizungumzia wewe isiyo diplomasia? Au ndiyo unatutaarifu mapema kwamba utaenda kutu-Lusinde huko kwa kusema mambo bila diplomasia?
ndio maana tumekalia Diplomasia wenzetu wanatuzidi akili,
Kufikiri kwamba diplomasia haiwezi kufanywa kwa akili ni kukosa akili. Yaani wewe ushaona choice hapa ni either diplomacy or brute force, and diplomacy is foolish, brutish speech is admirable.
Sasa wewe unaweza kuniambia kwamba una tofauti na Lusinde wewe zaidi ya severity of words tu? Kwa nini nisiamini kwamba unaweza kuingia bungeni siku moja ukatupa diplomasia zote za kibunge na kuanza kubwabwaja ovyo?
sina mpango wa kuwa Mbunge wa namna hiyo hata siku moja,
Huyu bwana anatutangazia mapema kwamba hana mpango wa kuwa mbunge anayefuata diplomasia hata siku moja. Watu kama hawa ni hatari hasa katika uhusiano wa kimataifa. Lusinde anaweza kubwabwaja mambo yakaishaia ndani, akienda kubwabwaja huyu bunge la Afrika ya Mashariki akikutana na mpuuzi mwenzake anayemjibu ovyo nchi zinaweza kupigana vita.
hatuwezi kujenga Jumuiya ambayo ni unbalanced kwa sababu tu tunataka tuonekane tunajua Diplomasia
Sijasema tujenge jumuiya unbalanced kwa sababu tunataka tuonekane tunajua diplomasia. Nionyeshe wapi nimesema hivyo. To the contrary nimekuuliza utateteaje interests za Tanzania katika jumuiya, una mkakati gani, hujajibu.
Nimekuuliza pros and cons za East African Federation kwa Tanzania. Hujajibu.
Una majibu?
kwa hili mkuu sina cha kukuomba msamaha,
Sijakuombwa uombe msamaha, unajishtukia.
ninasema hivi Kenya ndio waliovunja Jumuiya in the first place na sasa ndio machampion wa kuundwa kwa haraka haraka Jumuiya mpya na hasa One Currency na Federation,
Lugha yako haijakaa kujenga jumuiya, bali kuzuia. Unataka Jumuiya au hutaki? Utaweza kututajia pros and cons? Utaweza kututajia mkakati wako kuhakikisha watanzania hawapunjwi? Utaweza vipi kuwahakikishia Watanzania kwamba hutalipuka bungeni na kusababisha embarassment huku ukijifikiria unawatetea wananchi?
ninasema kwa haya mtu yoyote mwenye akili timamu ni lazima ashituke, sasa na wao kwa sababu wanajua tunao wananchi kama wewe ambao wako tayari kuuuza nchi kwa maneno ya kuheshimu Diplomasia,
Ni mtu mwenye akili ndogo tu anayeweza kuona diplomasia kama weakness. Wenye upeo wanajua maana ya "mental jujitsu" za diplomasia ni nini.
ndio maana wanakuja kwa kasi ya ajabu sana, ninasema hapana!
Hizi kauli za ku dismiss diplomasia wakati unaenda kwenye chombo cha kidiplomasia ndizo zinahalalisha wanaosema wewe ni intellectual pigmy na hapa unapotaka kwenda si saizi yako.
- Otherwise, nitajibu maswali ambayo yana valid arguments muhimu kwa wananchi na Taifa, ukiona sikujibu ujue halina mshiko!
William.
Nimekuuliza open ended questions ambayo kama wewe una mkakati unapata uwanja wa kujimwaya. Tupe makakti wako.