Who is Salim Ahmed Salim?

mimi ya 2010 haina maandalizi sana, BTW under the sun the impossibles can be possible.

Zitto Kabwe for President 2015, umri sijui utakuwa umetosha?
 
Nashangaa kuona propaganda za 2005 zinarudiwa, eti SAS ni mwarabu hawezi kutawala, mi nasema hii ni kupotosha mada.

Laso mnauliza ameifanyia nini nchi kimaendeleo, let me point out that hii ndo sababu moja kubwa wenzetu hata watu wa Ethiopia ambao walikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo na bado wana vita na Eritrea, wameanza kutupita!

Natumia huu mfano kwa sababu nimeona ni jinsi gani Ethiopia ilivyoamua kuwa karibisha wenzao wa nje, hata wale ambao walikataa kuchukua tena uraia wa Ethiopia yaani diaspora. Waliwafungulia milango na kuwakaribisha na ndio wanaoleta maendeleo! Sasa sisi tunanza kuleta longolongo eti kafanya nini?

Hivi mnajua umuhimu wa SAS kutupatia
1. Credibility

2. Siasa aliyofanya yeye haikuwa na takrima au mtandao au upuuzi mwingine tuliouona ulisababisha Tanzania kuwa stuck with the current lame president.

3. new perspective on a number of issue including nation building. Change from the same old, same old.

Rejecting a man like him is our loss not his!
 
mimi ya 2010 haina maandalizi sana, BTW under the sun the impossibles can be possible.

Zitto Kabwe for President 2015, umri sijui utakuwa umetosha?

Mama umri hautakuwa kuwa umetosha. Tufikiri hii ya 2010, naona kama kuna ka mwanga hivi.
Jana nilikuwa katika moja ya miadi yangu hapa New York katika ziara yangu. Nikajikuta ninaandika bila kufikiri kwa kina maneno haya katika notebook yangu.

'suluhisho sio CCM kutoka madarakani, bali ni kubadili mfumo wa uendeshaji wa nchi. CCM haiwezi kubadili mfumo huo hivyo inabidi ikae pembeni ili chama chama kingine chenye mawazo, fikra na mwono mpya kiweze kubadili mfumo. Chama hicho ni CHADEMA. CHADEMA nayo haiwezi peke yake, lazima ishirikiane na vyama vingine, Asasi za Kijamii na Watanzania wengine wenye nia njema na nchi yetu'

Sijui kisera fikra hii ya bila kufikiri kwa dhati ina maana gani. Lakini nimeipenda kweli. Si kweli hili? Wana JF
 
Mama umri hautakuwa kuwa umetosha. Tufikiri hii ya 2010, naona kama kuna ka mwanga hivi.
Jana nilikuwa katika moja ya miadi yangu hapa New York katika ziara yangu. Nikajikuta ninaandika bila kufikiri kwa kina maneno haya katika notebook yangu.

'suluhisho sio CCM kutoka madarakani, bali ni kubadili mfumo wa uendeshaji wa nchi. CCM haiwezi kubadili mfumo huo hivyo inabidi ikae pembeni ili chama chama kingine chenye mawazo, fikra na mwono mpya kiweze kubadili mfumo. Chama hicho ni CHADEMA. CHADEMA nayo haiwezi peke yake, lazima ishirikiane na vyama vingine, Asasi za Kijamii na Watanzania wengine wenye nia njema na nchi yetu'

Sijui kisera fikra hii ya bila kufikiri kwa dhati ina maana gani. Lakini nimeipenda kweli. Si kweli hili? Wana JF

I think you have put your finger on the essence, tatizo si CCM per say bali mfumo, lakini naomba uelewe kuwa mabadiliko yoyote ni lazima ihusishe CCM pia, hata kama wao ndio watakuwa opposition and minority.

Ni pamoja tu ndiyo tunawezak uleta mabadiliko ya kweli. Nadhani ungeanzisha separate thread because I am interested in discussing this.
 
'suluhisho sio CCM kutoka madarakani, bali ni kubadili mfumo wa uendeshaji wa nchi. CCM haiwezi kubadili mfumo huo hivyo inabidi ikae pembeni ili chama chama kingine chenye mawazo, fikra na mwono mpya kiweze kubadili mfumo. Chama hicho ni CHADEMA. CHADEMA nayo haiwezi peke yake, lazima ishirikiane na vyama vingine, Asasi za Kijamii na Watanzania wengine wenye nia njema na nchi yetu'

Sijui kisera fikra hii ya bila kufikiri kwa dhati ina maana gani. Lakini nimeipenda kweli. Si kweli hili? Wana JF


Hiyo naikubali mwanangu, hivi chadema hadi muda huu mmejiandaaje kutafuta kura 2010? je mna mabalozi na watendaji kata wangapi Tanzania nzima ambao ndio watakuwa shina la kumomonyoa sisiemu 2010? Je mmeshapata wanachama wapya wangapi tangu 2005?

Bila hivyo kuing'oa sisiemu itakuwa ngumu sana. Hako kamwanga ulikokaona ni kazuri sana ila kanahitaji nguvu ya ziada. Hongera sana kwa hilo.

Nina maswali ya ziada:

Je chadema mko tayari kumsupport mgombea yeyote yule kutoka upinzani (sio mwana chadema)kwa kiti cha urais au lazima awe mwana chadema?

Je chadema mko tayari kumsupport mgombea binafsi ambaye atakuwa competent kuliko mgombea wa chama chenu kwenye kiti cha urais?
 
Zitto...

Katika ulichoandika jana hapo kina ukweli mkubwa sana.

a. Kwanza, binafsi naamini suluhisho si tu kuiondoa CCM madarakani bila kuhakikisha kitu kingine better kinaingia. Hatuwezi kubadilisha CCM kwa chama kingine chochote ambacho si bora kuliko. Itakuwa ni kuruka mkojo....

b. Chama hicho kingine lazima kijithibitishe kuwa ni bora kuliko. Kinaweza kujithibitisha hivyo kwa sera na fikra zake zilizo bora lakini zaidi kwa kuonesha utendaji ulio bora zaidi, uwazi zaidi, uwajibikaji zaidi na zaidi ya yote, ioneshe kweli inaunua maisha ya watu wake (hata kama ni kwenye kakijiji kamoja).

c. Katika kuitakia nchi mema mtu asifungwe na Chama chake na awe tayari kushirikiana na wale wote wanaotaka kuleta mabadiliko ya kweli na yaliyobora. Katika kufanya hivyo basi ipo haja ya kuwashirikisha wale wote ambao wanaonesha nia hiyo na wanaangalau rekodi ya kufanya hivyo.

d. Mabadiliko ya kweli hata hivyo hayawezekani hadi pale mtu wa kijijini aweze kuona kuwa CCM haiko kwa faida yake. Lakini kama juzi Iringa CCM wamevuna wanachama wapya 700 baada ya kuambiwa Ufisadi na CCM haviendani, ni kwa kiasi gani tunaweza kuwashawishi watu kama hawa kurudisha kadi hizo.

e. Hata hivyo kundi kubwa linalohitaji kushawishiwa si walio kwenye vyama kwa sababu kwa hesabu za haraka haraka wanachama wa vyama vya siasa ni kama robo tu ya wapiga kura wote. HIvyo, ni wale wasio na vyama na wasiobeba kadi ambao kwa kweli wanahitaji kushawishiwa. Tutawashawishi vipi?

Ni hapo tunapoangalia mambo haya na mengine ndio naamini tunaweza kwa kweli kuona kama 2010 kuna mwanga au bado kuna utando wa giza.
 
Salim Ahmed Salim
The President delayed

...anaweza kuwa drafted na Watanzania wanaomwona aweza kuwa Rais mzuri kwa Taifa letu....... Draft Salim, 2010.

Salim-Slaa ticket kinda possible!!!!!! Tuendelee kujadili

Zitto Kabwe, Mheshimiwa Mbunge;

Kwa taadhima na unyenyekevu mkuu nashukuru kwa huduma yako.

Kambi ya upinzani na mwamko mzima wa mageuzi ukuelewe vipi unapo mpaka mafuta mtu wa CCM hadharani kama anaweza kuwa Rais? Tuswalishe kujitoa kwako katika huo mwamko?

Waliokuja nyuma na uongozi kama wako wakina Mrema, Marando na wengine wengi mpaka leo hawajaweza kufuta muhuri uliopigwa mgongoni mwao unaosema 'Kachero wa CCM.' Na kina Lamwai na Nyakyoma wakadhihirisha.

Kujitoa kwako kwenye mageuzi kumetukuka kweli?
 
Zitto Kabwe, Mheshimiwa Mbunge;

Kwa taadhima na unyenyekevu mkuu nashukuru kwa huduma yako.

Kambi ya upinzani na mwamko mzima wa mageuzi ukuelewe vipi unapo mpaka mafuta mtu wa CCM hadharani kama anaweza kuwa Rais? Tuswalishe kujitoa kwako katika huo mwamko?

Waliokuja nyuma na uongozi kama wako wakina Mrema, Marando na wengine wengi mpaka leo hawajaweza kufuta muhuri uliopigwa mgongoni mwao unaosema 'Kachero wa CCM.' Na kina Lamwai na Nyakyoma wakadhihirisha.

Kujitoa kwako kwenye mageuzi kumetukuka kweli?


Heeee, nampaka mtu wa CCM mafuta? Kasumba gani tena hii.... Mimi ninamzungumzia Mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza na ndio maana hata ticket nimesema Salim-Slaa. Hebu tuondokane na mawazo mgando. Haya ni majadiliano ya kifikra. Yapo juu ya vyama. Na hapa ninashiriki mijadala kama Zitto na sio kama kiongozi wa CHADEMA. Jamani si ni lazima niwe na jukwaa la kusema kwa uhuru bila kupewa lebel ya chama changu? au?

'tumwangalie mtu, sio kwa kadi ya chama cha siasa alichonacho, bali kwa mchango wake katika Taifa letu' This is another nice quote enhee, paraphrasing Martin Luther King in ... I have the Dream....
 
Mkandara,

..sijahoji uwezo wa Salim Salim ktk masuala ya diplomasia na siasa za kimataifa.

..kinachonikwaza mimi ni kwamba Salim Salim hana rekodi inayopimika ya kushughulikia matatizo ya wananchi wa kawaida. pia hana rekodi ya kupimika ya kushughulikia matatizo ya kiuchumi.

..kuhusu Tazara kuna mambo mengi sana yaliyopelekea kupatikana kwa mradi ule.

..hivi una uhakika kwamba bila Salim Salim wachina wasingetupa msaada wa reli?

..Kuhusu Salim Salim kuwa Mjamaa, which i doubt, hizi siyo zama za Itikadi. Kama ni Maraisi Wajamaa tulishakuwa nao, tena wakereketwa kuliko huyo Salim Salim.

..Tatizo langu na Salim Salim ni kwamba sioni kama ana interest na siasa za ndani za Tanzania, other than seeking the country's highest office. kama Salim angekuwa na interest na siasa za ndani basi baada ya kushindwa Uraisi angetafuta jimbo akagombee ubunge.

NB:

..niliwahi kuonya zama zile kwamba Kikwete hatatufaa. nasikitika kwamba utabiri huo unaelekea kuwa kweli.

Rafiki yangu Joka,

Je ni nani ambaye tunamfahamu ambaye anapimika?
 
Kama kawaida tunaanza kucheza mdundiko lakini katika mduara!

HIvi tunahitaji kiongozi mwenye cheti na sifa kibao za kitaaluma au

  • tunahitaji kiongozi mwenye uwezo na ushawishi mkubwa kulizindua Taifa letu katika kufufua shughuli za maendeleo?
  • kiongozi ambaye ataweka maslahi ya Taifa na wananchi kwanza,
  • kiongozi ambaye atasimamia kwa dhati ujenzi wa Taifa,
  • kiongozi ambaye atakuwa mstari wa mbele kujenga utii wa sheria, kuboresha utu na kuimarisha uchapakazi na uwajibikaji,
  • kiongozi ambaye atahamasisha wananchi wa kila hali na mali,
  • kiongozi ambaye atakuwa makini katika kazi zake, kulilinda Taifa lake, kutumia vizuri na kwa manufaa rasilimali za Taifa,
  • kiongozi ambaye si mtawala au mangimeza, bali ni shujaa na mchapa kazi ambaye katika uongozi wake, taswira ya Mtanzania kwa mtanzania mwenyewe itakuwa taswira yenye maendeleo, iliyo na afya, yenye uwezo wa kujitegemea na yenye uwezo wa kuingia uwanja wa kimataifa wa kiushindani katika ubunifu na maarifa,
  • kiongozi ambaye atakuwa ni mwadilifu, mwenye hekima, busara na kufuata haki,
  • kiongozi ambaye atakuwa mwepesi kusikiliza ushauri, kusikiliza vilio, mwenye uwezo wa kukiri kupotea au kufanya kosa,
  • kiongozi ambaye atafanya kazi na kuonyesha dhati kuwa ana Uhuru wa kuongoza na si kufanya kazi ili kuridhisha kundi au tabaka moja katika jamii
Hivi vyeti, utitiri wa qualification pekee hauna maan akama mtu huyu anayetaka kuwa Rais na Kiongozi wa Taifa letu hata kuwa japo 50% ya hivyo vigezo nilivyoviweka hapo juu.
 
Siasa za kweli na safi , siasa za maendeleo na mwelekeo ni zile mtu unamoa mtu sifa kama unaona anafaa bila ya kujali Chama chake .Hizi ndiyo siasa endelevu na pevu.m

Zitto kasema maoni yake na labda ana imani kwamba Salim angaliweza ama anaweza .Kusema kaunga mkono CCM ni mgando mkubwa na uelewa finyu ndiyo haya ya CCM kuua Nchi kisa Chama chetu .Mpen mtu haki yake kama mna imani naye si lazima awe katika Chama chenu .

Pamoja na hayo mimi nampinga kwa nguvu zote Salim hawezi tena sasa na hata kabla asingaliweza .Kama nilivyo mpinga JK kabla kwamba hatawezi na sasa nasena hawezi .
 
Lemme assume kind of a maximo role for 2010

a list of MASHUJAA WETU aka National team players(call it Taifa Stars?)/as opposed to a list of shame/, a bit of fairness clubs are cosidered

1.salim-independent
2.slaa-chadema
3.mwakyembe-ccm
4.zitto-chadema
5.lipumba-cuf
6.lisu-chadema
7.mbatia-nccr
8.kilango-ccm
9.kijobisimba-independent
10.haji duni-cuf
11.rose migiro-if back from UN

others
12.kitila-chadema
13.mvungi-nccr
14.ananilea nkya-free?
15.ntungilei-tlp
16-kahangwa-nccr
18.a lady plz
19.shein-ccm(kama continuity ni dawa)

20. kocha mchezaji(waridi)
huyu nitamliplace mkinipatia another a strong lady

the list will continue if i get to know the real names of footballers in JF club, and will be uptodated according to the names i find mentioned in here
Please criticize a name/list by genuine reason
 
Yaleyaleeeeeee mada imesha haribika kabisa sasa .

Hakijaharibika kitu,
Mimi naona mada ndio kwanza inakua, au mwenzetu target yako ni ipi hasa ambayo unaona kwamba mada ilenge hapo tu. hapa tunajadili kiongozi,viongozi, uongozi, freely and fairly
 
Siasa za kweli na safi , siasa za maendeleo na mwelekeo ni zile mtu unamoa mtu sifa kama unaona anafaa bila ya kujali Chama chake .Hizi ndiyo siasa endelevu na pevu.Zitto kasema maoni yake na labda ana imani kwamba Salim angaliweza ama anaweza .Kusema kaunga mkono CCM ni mgando mkubwa na uelewa finyu ndiyo haya ya CCM kuua Nchi kisa Chama chetu .Mpen mtu haki yake kama mna imani naye si lazima awe katika Chama chenu .

Pamoja na hayo mimi nampinga kwa nguvu zote Salim hawezi tena sasa na hata kabla asingaliweza .Kama nilivyo mpinga JK kabla kwamba hatawezi na sasa nasena hawezi .

nakuunga mkono lunyungu.

na ndo maana nchi kama marekani bush anapingwa na wafuasi wa republican na wanakosoa sera zake na baadhi ya misimamo yake, lakini hapa kwetu utasikia wanasema "chama kwanza mtu baadae", so hata kama mtu ni mzigo wenyewe wanamchagua tu....
 
hivi ukimsimamisha Salim kama mgombea wa CCM amid maskendo yote haya ya ufisadi na kwa upande wa upinzani wakaungana na kumpitisha Slaa kuwa mgombea wao mnadhani mchuano unaweza kuwa vipi?

DK Salim kama angekuwa msafi angekemea maovu wanayoyafanya CCM kama kina Najib Balala, Raila Odinga na wapigania haki wengine wa kenya walivyoweza kumpinga kibaki wakiwa ndani ya serikali...lakini yeye kanyamaza kimyaa kama vile haoni nini kinaendelea nchini, halafu anataka akichaguliwa kugombea urais aibuke kama vile yeye ni msafi...kwangu nasema NO.
 
Thanks Guys kwa kukata issues za uongozi hapa. Lakini Ukweli unabakia pale pale siasa ni mchezo ambao rafu zake hukera. Siasa huweza kuibua watu usiowategemea na kuwadumaza watu usiotegemea.

Kwa siasa za Tanzania sasa hivi Salim ku qualify kuwa rais ni ndoto unless Tanzania mazingira ya ya kampeni na mitandao na rushwa vikome. fanya utafiti utagundua kuwa kuanzia serikali za mitaa, wabunge na hata Rais kuchaguliwa kwao si sera zao madhubuti bali ilitegemea walikata kiasi gani. Ufisadi umezidi pale ambapo kuchaguliwa kwako inategemea How much mfisadi you are.

Viongozi madhubuti hawachaguliwi. kumbukeni kauli ya Kingunge wakati wa uchaguzi wa CCM. ALISEMA HAKUWA TAYARI KUTOA RUSHWA LILI ACHAGULIWE. Je Salim how keen is he in corruption? Pili viongozi walio wengi siasa ni proffession ya mkato kupata mali kwa chee and easy.

Salim ana CV nzuri, lakini wakati wake umeisha jamani. he is too old now. mwacheni apumzike sasa. Tangu akiwa na miaka 19 tu sijui 22 tayari balozi. Je ina maana alikuwa na udiplomasia kiasi gani kupata ubalozi? wakati wengine miaka 22 tuko form 2 wkati huo!!! sometimes BAHATI NAYO.

Of course kwa salim alikuww anamwakilisha FAVOURS ZA BABA YAKE! vIONGOZI MADHUBUTI TUTAWAPATA SIKU WATANZANIA WAKING'AMUA KWA THITHIEM BOMU!na miungu wadogo eti kwa sababu ilitoka na TANU na ASAP vyama vilivyoleta uhuru wa TZ.(Hata Jongwe alileta uhuru zimbabwe lakin sasa hivi ahafi!!!) WAPINZANI WACHUKUE NCHI THEN KUANZANIA HAPO MAMABO YATAKUWA mswano SIO KULAMBANALAMBANA!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom