FMES na Nyani Ngabu hawakosei kabisa!
Waafrika ndo tulivyo!
Ila mkuu, kwa nini tuwapigie kura watu wasiotaka kutoka madarakani?
Vipi kuhusu watu kama Maalim Seif, tangu 1995 anagombea yeye tu?
Siku akishinda ataweza kutoka madarakani kwa hiari kweli?
Hii ya Kalamu hata mimi imenikata maini kabisa pamoja na mapenzi yangu kwa Salim. Yaani huyu bwana hutakuja kumsikia akinyanyua mdomo kabisa kuhusu uozo wote unaendelea. Sasa wakati mwingine tunashindwa kujua convictions zake ni zipi na kama hatujui convictions zake anatukwaza sana sisi wapenzi wake kumtetea mbele ya vichwa kama akina FMES!
Hata hivyo nafikiri huyu mzee wetu walishamjeruhi sana na sidhani kama anaweza kuuzika tena na kukabili mashambulizi ya wanasiasa wa leo TZ.
Ni wangapi wako tayari kumsupport Salimu kama akiwa tayari kutaka kugombea? Nani atakuwa tayari kumsupport na kujibu mashambulizi...
Anaweza kuhimili, si unaona McCain baada ya 2000 amerudi tena, sema swali la kujiuliza wananchi tuko tayari kumchagua na kumpitisha?
Kwenye hili la kuzungumzia ufisadi anajua mwenyewe kwa nini yuko kimya kuna watu kadhaa ambao I have always admired them naona wamekaa kimya tangu hili sakata la ufisadi limeanza.
On the other hand wakizungumza tutasema wanataka cheap political attention na tutaanza kuuliza walikuwa wapi siku za nyuma and blah blah...
Dah kwa kweli hili hata mie huwa linanishangaza sana..ingawaje wana demokrasia na maendeleo wamekuwa wakijaribu kuonyesha mfano bora wa demokrasia lakini vyama vingine vya upinzani wamekuwa wakienda tofauti kabisa na demokrasia wanayoihubiri majukwaani..hivi jamani kwa mfano ktk CUF ama TLP..ina maana hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kugombea urais ukiacha bwana profesa haruna/maalim seif na muheshimiwa lyatonga?? Sijui.. lakini kwa tafakari yangu naona hapa kuna tatizo kubwa..tena saana tu..otherwise pengine ndio mfumo uliopo kwenye katiba husika..kwamba mtu agombee mpaka ashinde..mtizamo wangu tu...
Biography of Dr. Salim Ahmed Salim
Dr. Salim Ahmed Salim

The President who never became.
Thats sound like a cute title of the Book. Mkumbo unasemaje?
The President who never became.
Thats sound like a cute title of the Book. Mkumbo unasemaje?
Swali kubwa ni je Salim ana future ndani ya CCM kama anataka kuliongoza Taifa letu?
CCM wakituletea huyu 2010 mbona nitawapenda!!, kama hawataweza kumwambia Vasco da Gama aachie usukani, basi angalau wamsimamishe Visiwani Zanzibar. just a wish Tena kama hawataki, heri utaratibu wa mgombea binafsi ungeharakishwa, hapo watanzania tunakamata huyu tunaunganisha na Dr.Slaa, bonge la timu ya ushindi halafu uone kama TZ haitabadilika,au sio jamani?
Mkuu Gamba,
Heshima mbele, tatizo sio CV za viongozi wetu, isipokuwa tatizo ni CV za sisi wananchi wapiga kura, Salim ana CV nzito lakini tatizo ni kwamba urais hauamuliwi na CV peke yake, kwa bahati mbaya pamoja na CV yake kuwa nzito, alishindwa kwenye uchaguzi wa mgombea wa rais wa CCM,
Sasa kama Muungwana tu alimshinda kule CCM, je atawezaje kupambana na kina Freeman, na Lipumba? Na je akikutana na Dr. Slaa sio ndio itakuwa mauti kabisa kwetu CCM! Pole pole ndugu, urais ni pamoja na kushinda uchaguzi,
Salim ni kweli ana CV nzito, na pia ametuweka kwenye ramani ya Dunia politically, lakini tatizo hakuwa na political base nyumbani, kuanzia visiwani mpaka Bara, sasa uongozi wa kubebwa kama wake ulimalizwa na siasa za vyama vingi!
Otherwise, ni kweli CV yake ni nzito sana!
Ni wangapi wako tayari kumsupport Salimu kama akiwa tayari kutaka kugombea? Nani atakuwa tayari kumsupport na kujibu mashambulizi...