Hapo ndipo tatizo lako kutokukubali imani linapojionesha.Ikiwa unajua suala la mungu ni la imani,sasa wewe unayetaka uthibitisho na unasema kuamini hakuhitaji uthibitisho unakuwa na maana gani? ndiyo maana nasema wewe hukubaliani na imani ila unakataa.
Tatizo lako huwezi kufuatilia argument.
Katika imani kuna imani potofu na imani sahihi.
Nikisema kwamba nakuja nyumbani kwako, naamini upo nyumbani, nikafika nikakukuta hupo, imani yangu kwamba ulikuwapo nyumbani, kwa wakati ule ilipokuwa imani, ilikuwa ni imani potofu.
Nikisema kwamba nakuja nyumbani kwako, naamini upo nyumbani, nikafika nyumbani nikakukuta upo nyumbani unanikaribisha, imani yangu kwamba ulikuwapo nyumbani, kwa wakati ule ambao ilikuwa imani, ilikuwa imani sahihi.
Kufika kwako na kufahamu kwamba upo au haupo kutathibitisha imani yangu kama ilikuwa sahihi au potofu.
Nikifika na kuthibitisha kama upo nyumbani, natoka kwenye imani, naingia kwenye ujuzi, kwa sababu nimethibitisha.
Imani kabla ya uthibitisho haijahakikiwa, ni kama kubashiri tu bila uhakika. Kubashiri bila uhakika kunaweza kuwa sawa au kusiwe sawa hata kama habari haina mushkeli kama wa contradiction.
Habari ikiwa na mushkeli wa contradiction, mushkeli unaonesha kuna kitu hakipo sawa, kuna uongo hapo.
Sasa kwa nini nikubali imani, ama imani iliyo na mushkeli wa contradiction ama iliyo na mushkeli wa contradiction wakati kuna njia ya kufanya ili kuthibitisha imani hiyo?
Kwa nini niseme tu "nje mvua inanyesha" kwa imani nikiwa ndani ya nyumba isiyo na mawasiliano yoyote na nje wakati naweza kufungua mlango nikaangalia kama nje mvua inanyesha?
Kwa nini nikubali kuishia kwenye imani wakati naweza kuchunguza na kuthibitisha?