'Who created God' is an Illogical Question!

'Who created God' is an Illogical Question!

Hayo ni maelezo niliyokupa baada ya wewe kutetea hoja yako ya kwa nini Mungu alimuumba shetani.Nami nikasema kama Mungu alimuumba shetani huenda akawa hana upendo(asingemuumba mwaribifu wa wanadamu) au hana ujuzi wa kujua jambo kabla halijatokea(hakujua kama Shetani atakuja kuasi na kuleta madhara makubwa).

Sasa hapo ukubali tu kuwa Mungu hana sifa za kiungu(upendo wote & ujuzi wote) na kwa maana hiyo hakuna Mungu mwenye sifa hizo zaidi ya hii Miungu uchwara kama miti, miamba, miungu mtu, n.k.
Kama unapinga uwepo wa Mungu, maana yake unakuwa disqualified kutumia kazi zake au uwepo wake kujustfy kutokuwepo kwake. Tafuta njia nyingine ya kuprove kutokuwepo kwake bila kumuhusisha yeye kwenye inputs zako.
 
Fact:

Hakuna aliyethibitisha kwamba Mungu yupo mpaka sasa.
Wewe mwenyewe ni Uthibitisho wa Uwepo wa Mungu.
Dunia inayokuzunguka na Universe yote Ni ushahidi wa Uwepo wa Mungu. Take time to explore nature achana na hizo outdated traditional logics na contradiction. Jifunze kidogo Modal Logics
 
Mwanzo kabisa nilisema kwanini tunajiuliza kama Mungu yupo?
Kwanini hatujiulizi kama Ziwa Victoria lipo?......jibu ni kwasababu Ziwa Victoria lipo na Mungu ni nadharia tu, siyo kweli.
Kwa ambaye hajaliona ziwa Victoria,atauliza uwepo wake,hata kama lipo lakini hajaliona.Ikiwa umeona unyao wa simba,japo hujamuona huyo simba,utajuwa eneo hili lina simba.
Unapoona dunia na vilivyomo,ni kwa mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayeshindwa kuelewa kama lazima atakuwako aliyeyafanya hayo,na hakuna aliyefanya hayo ila Mungu tu.
Uwepo wa Mungu,hautaji darubini,uko ndani ya mwili wa mwandamu,jinsi ulivyoumbwa na mwili unavyofanyakazi.Ambapo wanasayansi wanakiri,usagaji wa chakula,kwenye mwili wa mwanadamu,kama wangeweza kutengeza mashine,kama mwili unavyosaga chakula,machine hiyo ingechukuwa dunia nzima kwa ukubwa wake.
Hakika ni mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayesema hakuna Mungu.
 
Mungu hayupo. Huyu Mungu mjuzi wa yote mwenye upendo wote na nguvu zote hayupo.

Angekuwepo dunia isingekuwa na maovu. Angeumba dunia ambayo maovu hayawezekani kuwepo.
Kwa hyo kuwepo kwa mouvu ni sababu moja wapo ya kusema mungu hayupo..??
 
Kwa ambaye hajaliona ziwa Victoria,atauliza uwepo wake,hata kama lipo lakini hajaliona.Ikiwa umeona unyao wa simba,japo hujamuona huyo simba,utajuwa eneo hili lina simba.
Unapoona dunia na vilivyomo,ni kwa mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayeshindwa kuelewa kama lazima atakuwako aliyeyafanya hayo,na hakuna aliyefanya hayo ila Mungu tu.
Uwepo wa Mungu,hautaji darubini,uko ndani ya mwili wa mwandamu,jinsi ulivyoumbwa na mwili unavyofanyakazi.Ambapo wanasayansi wanakiri,usagaji wa chakula,kwenye mwili wa mwanadamu,kama wangeweza kutengeza mashine,kama mwili unavyosaga chakula,machine hiyo ingechukuwa dunia nzima kwa ukubwa wake.
Hakika ni mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayesema hakuna Mungu.
Kama umeuona unyayo wa simba utasema ni sima kwa kuwa unamjua na nyayo zake unazijua
Hivo kama umeona traces za Mungu lazima kwanza umjue huyo Mungu yukoje
 
Kama unapinga uwepo wa Mungu, maana yake unakuwa disqualified kutumia kazi zake au uwepo wake kujustfy kutokuwepo kwake. Tafuta njia nyingine ya kuprove kutokuwepo kwake bila kumuhusisha yeye kwenye inputs zako.
Hivi mkuu ngoja nikuulize

Mfano
Mimi hapa iceman nikisema leo kuwa huko juu sana angani kuna kuna viti vya dhahabu vingi sana. Na ntakwambia kuwa watu wenye matendo mema wakifa huwa wanaenda kukaa huko.

Je kwakuwa siwezi kuthibitisha kama vipo uta nipinga mimi!!?
Au utakubali kwakuwa wewe huwezo kuthibitsha kama kweli viti hivo havipo!!?
 
Kwanza alianza binadamu kuwako,ndio binadamu akaanzisha sayansi.Bila kuwako binadamu,kusingekuwako na sayansi.Vipi mwenye akili timamu,ataisifu sayansi kabla ya kumsifu aliyefanya sayansi ikawepo.
Kwa wasioamini Mungu husifu matokeo,badala ya kusifu aliyesababisha hayo matokeo.
Binadamu ndio kasababisha kuwepo sayansi,na je ni nani aliyesabisha binadamu kuweko?Na hivyo anavyofanyia sayansi binadamu,kama nyota,mwezi,jua nk.,ni nani aliyesababisha viwepo?Hakuna mwingine ila ni Mungu.
 
Hujathibitisha kwa ithibati,isiokinzana kwa pande zote mbili za hadhira,zinazokinzana kama Mungu hayupo.
Unaweza kuthibitisha hivyo hivyo kwamba Mungu yupo?

"Kuthibitisha kwa ithibati" ndiyo maana yake nini kama si kurudia neno moja mara mbili kwa namna tofauti?

Idea ya Mungu wenu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kufanyika wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya haileti kujipinga yenyewe kwa yenyewe.
 
Lete uthibitisho,kama mabaya yanaletwa na Mungu.
 
Sasa mkuu nduo uzuri wa sayansi kuwa kitu kina semwa kwa calculations na kinakuja kugundulika kuwa ni kweli. Uwepo wa Mungu umesemwa miaka zaid ya 1000 hata trace zake tuu hazipatikani.
Na suala la vitabu vya Mungu ndii tatizo kabisa, vitabu hivo ni vya watu kama wewe walikaa wakafikiria waka viandika so hata wewe unakuwa decived mkuu, kufikiria Mungu alikuwa ana ongea na mfanyabishara mmoja huko saudi Arabia, au mzee mmoja huko Israel.
Nakuelewa lakini naomba kutofautiana na wewe kuhusu vitabu.
Mfano mdogo tu Mungu Miaka zaidi ya 3000 iliyopita kupitia watu unaowaona hawafai tena AYUBU ambaye hakuna ushahidi wowote kama alikuwa Muisrael Alimwambia Vitu Viwili vya Msingi
1: Mwanga Aliimba unatembea 2: Giza liko stationary (does not move) Imeichukua dunia miaka yote hiyo hadi Newton mwaka 1675 kugundua hilo, Cha ajabu Credit zitaishia kwa newton au galileo au NASA wakati hajagundua kitu kipya ni kitu ambacho Mungu alikisema na Akasema Amekiumba yeye.

Ndio maana anasema "MPUMBAVU ANASEMA MOYONI MWAKE HAKUNA MUNGU"
Mjinga yeye anachukua hatua kuangalia kazi anazosema ni zake na kuona kama kuna uhalisia wa anachokisema. Mfano alisema anashikilia malimwengu kwa nguvu zake, Leo 2015 anakuja jamaa anagundua DARK ENERGY that holds the universe and it is Impractical to be by chance, na wanakubaliana hadi wanasayansi wasioamini uwepo wa Mungu kuwa kuna kitu kingine intelligent, with knowledge, creative power behind this fine-turning and energy balance. Mungu anasema na alisema miaka zaidi ya 4000 iliyopita ni yeye na hajawahi kubalisha, Ukimfikisha hapa mtu anaitwa KIRANGA anakwambia sio kazima awe Mungu, Ukimuomba alternative yeye anadhani ni nani au nini ili tukijadili tuone uhalali wake. Dunia ni Duara linaloelewa Mungu kasema ameiumba hivyo miaka miingi zaidi ya 3000 iliyopita sisi tunajua na Science imethibitisha lakini wapo watu duniani wana chama chao ambacho kiongozi ni ELOUTIONIST yaani kuonyesha ubishi tu wanasema Dunia Ni Kama Meza. Sasa Dunia lazima iwe na watu wenye kufikiri wanavyotaka ili maisha yaende.
Ila MUNGU YUPO, PROOF ni KAZI ZAKE.

ANaruka na kuuliza swali, Naomba ushahidi Mungu Yupo?
 
Unajuaje hilo?

Kila wanaosema Mungu hayupo wakitoa ushahidi mpya, wanaosema Mungu yupo wanaweza kukanusha kwa kuweka "Deus ex Machina".

Mfano, kuna watu walisema radi ni ushahidi kwamba Mungu yupo, ni hasira ya Mungu. Wanasayansi walipokuja na kuonesha kwamba radi ni umeme tu, wanaoamini Mungu wakasema umeme huo unatokana na Mungu.

Kwa njia hii, hususan kwa sababu wanaosema Mungu yupo wanasema haonekani wala kupimika, tutafikiaje muafaka?

Kuamini Mungu yupo si kama kuamini jua litatoka kesho.

Jua lina track record ya kuonekana kila siki likichomoza, Mungu hana track record ya kuonekana kwa njia ambayo inaweza kuthibitishwa hata siku moja.

Jua halina contradiction. Nikisema "jua litachomoza kesho" kauli hiyo haileti contradiction, haijiping yenyewe. Nikisema "Kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, lakini akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana" kauli hiyo ina contradiction.

Utafananishaje kuamini kitu ambacho hakina contradiction na kuamini kitu chenye contradiction?
Nimesema itafika muda ambao itajulikana au kuthibitika kuwepo au kutokuwepo kwa mungu,na ndiyo maana huwa kuna msemo wa bora uamini halafu usimkute kuliko kutokuamini na ukamkuta.

Ina maana kinachoendelea hapa kati ni sababu na dalili zenye kufanya kuamini uwepo wa mungu. Ndiyo maana nikasema sawa na kuamini kuchomoza kwa jua kesho na ukasubiri ifike hiyo kesho ili ndiyo ijulikane ukweli wa kuchomoza ama kutochomoza kwa jus.

Sasa sijajua tatizo lako lipo wapi hapo? unaposema watu hawawezi kuthibitisha huwa una maanisha nini?
 
Mkuu mi hata nikikukuta kwenye chumba cha upasuaji na ikawa we ndo oparetor mwenyewe sitakubali unihudumie especially kwa ujinga uliouonyesha hapa... ! Hivi hata historia ya medicine unaifahamu kweli ?! Unajua tumetoka wapi kweli ?! Unafahamu for just 500 years kuna maendeleo mengi sana yamefanyika katika field nzima ya medicine kuliko dini ?! Na kama wanasayansi wangetegemea kila kitu kutoka kwa mungu unadhani tungekuwa hapa leo? Its a shame.. !
Kwa hyo na wewe huamini uwepo wa mungu.??
 
Wasioamini Mungu ili hoja zao,ziwe na nguvu,lazima wamtegemee Mungu.Hawana pa kushika,kwa vile hoja zao wanakinzana. Wasioamini Mungu wako makundi 17,wkiwa katika set 7,zinazokinzana,kwa kupingana,mikwamo isio na kikomo,yenye kujikwamisha yenyewe.
Issue siyo watu hawataki kumwamini Mungu, bali wanataka ushahidi wa uwepo wa Mungu.
 
Mkuu mi hata nikikukuta kwenye chumba cha upasuaji na ikawa we ndo oparetor mwenyewe sitakubali unihudumie especially kwa ujinga uliouonyesha hapa... ! Hivi hata historia ya medicine unaifahamu kweli ?! Unajua tumetoka wapi kweli ?! Unafahamu for just 500 years kuna maendeleo mengi sana yamefanyika katika field nzima ya medicine kuliko dini ?! Na kama wanasayansi wangetegemea kila kitu kutoka kwa mungu unadhani tungekuwa hapa leo? Its a shame.. !
Theists ni wahuni sana, wanatumia facts za science kudai eti ni kazi za Mungu.

Tangu lini wameanza kutumia medical field kama njia ya kujiponya? hawa si waliaminishwa wakiugua waende kwenye mabanda ya ibada kufanyiwa maombi? mbona wakiugua wanakuja mahosipitalini? ama upako wa kuponya umepungua?
 
mkuu rudi ukasome biology ya form four.. !
Usiwaze sana, hawa ni wale waliofaulu kwa njia ya political standardization.Wanafikiri Evolution ni rahisi na haraka kama kusonga ugali.
 
Kama unapinga uwepo wa Mungu, maana yake unakuwa disqualified kutumia kazi zake au uwepo wake kujustfy kutokuwepo kwake. Tafuta njia nyingine ya kuprove kutokuwepo kwake bila kumuhusisha yeye kwenye inputs zako.
Hayo maelezo yako umeyatoa wapi? ni kwa mujibu wa nani? unajua kuwa ninichokitaka ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu?
 
Hivi kwanini wanyama kuuliwa na kufanywa kitoweo huwa ni jambo la kawaida tofauti na akiuliwa binaadamu?

Nani aliyeweka mfumo wa aina hii kuwa binaadamu ana haki ya kuishi kuliko mnyama?
 
Nimesema itafika muda ambao itajulikana au kuthibitika kuwepo au kutokuwepo kwa mungu,na ndiyo maana huwa kuna msemo wa bora uamini halafu usimkute kuliko kutokuamini na ukamkuta.

Ina maana kinachoendelea hapa kati ni sababu na dalili zenye kufanya kuamini uwepo wa mungu. Ndiyo maana nikasema sawa na kuamini kuchomoza kwa jua kesho na ukasubiri ifike hiyo kesho ili ndiyo ijulikane ukweli wa kuchomoza ama kutochomoza kwa jus.

Sasa sijajua tatizo lako lipo wapi hapo? unaposema watu hawawezi kuthibitisha huwa una maanisha nini?
Utajuaje kwamba kitu kitatokea muda ujao ikiwa hata kuondoa contradiction iliyooneshwa katika kitu hicho leo huwezi?

Unawezaje kusema pembetatu ambayo ni duara pia hapohapo ipo katika Euclidean geometry na itathibitishwa siku za mbeleni ikiwa leo hii ukiulizwa pembetatu hiyo ambayo pia ni duara ina nyuzi 180 au 360 huwezi kujibu?
 
Kwa ambaye hajaliona ziwa Victoria,atauliza uwepo wake,hata kama lipo lakini hajaliona.Ikiwa umeona unyao wa simba,japo hujamuona huyo simba,utajuwa eneo hili lina simba.
Unapoona dunia na vilivyomo,ni kwa mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayeshindwa kuelewa kama lazima atakuwako aliyeyafanya hayo,na hakuna aliyefanya hayo ila Mungu tu.
Uwepo wa Mungu,hautaji darubini,uko ndani ya mwili wa mwandamu,jinsi ulivyoumbwa na mwili unavyofanyakazi.Ambapo wanasayansi wanakiri,usagaji wa chakula,kwenye mwili wa mwanadamu,kama wangeweza kutengeza mashine,kama mwili unavyosaga chakula,machine hiyo ingechukuwa dunia nzima kwa ukubwa wake.
Hakika ni mwenye uelewa mdogo tu,ndio anayesema hakuna Mungu.
Kuna ushahidi gani kwamba Mungu ndiye aliyeumba dunia?

Kwani ni lazima kila kitu kiwe kimeumbwa? kama jibu ni ndiyo, nani aliyemuumba Mungu?

Sayansi bado haijafika ukomo, kusema mashine inaweza kuwa kubwa kama dunia siyo kwamba ndio mwisho wake.Zamani zilikuwepo zana kubwa sana kiumbo kama Camera, simu n.k, lakini leo vinaundwa kwa size ndogo na imara zaidi.
 
Hivi kwanini wanyama kuuliwa na kufanywa kitoweo huwa ni jambo la kawaida tofauti na akiuliwa binaadamu?

Nani aliyeweka mfumo wa aina hii kuwa binaadamu ana haki ya kuishi kuliko mnyama?
Dini zinasema kuwa binadamu aliumbwa kwa udongo, je ni material yepi yaliyotumika kuumba wanyama wengine?
 
Back
Top Bottom