WhatsApp yawakaba koo waongo, sasa kuumbuka!

WhatsApp yawakaba koo waongo, sasa kuumbuka!

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,832
Reaction score
63,321
Kuanzia sasa longo longo ya kwamba sikuupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kudai kuwa ujumbe haujafika utakuwa unaongopa mchana kweupe.
whatsapp.jpg

safe_image.php

  • Huduma hiyo inapatikana kupitia Whatsapp katika simu zote za mkononi zenye uwezo wa kuitumia
  • Tick ya kijivu ina maana kuwa ujumbe umetumwa, tick mbili za kijivu zina maana ujumbe umemfikia mlengwa, na tick mbili za blue zina maana kuwa mlengwa ameusoma ujumbe uliotumwa
  • Ukibonyeza na kushikilia ujumbe uliotuma inatokea Pressing and holding an individual message shows the Message Info option
  • Ukibofya utaona muda kamili ambao ujumbe huo ulisomwa
  • Maoni kuhusu mabadiliko hayo yamepokelewa tofauti katika mitandao ya kijamii, wapo ambao hawajafurahishwa
Whatsapp haijatoa sababu za kufanya mabadiliko hayo ambayo yamewakera baadhi ya watumiaji.

Kuanzia jana huduma hiyo inayomilikiwa na Facebook- itakuwa ikionyesha tick mbili za rangi ya blue upande wa chini kulia katika kila ujumbe unaotuma kubainisha kuwa umesomwa.


Na ukibofya ujumbe wenyewe utaona muda kamili ambao mlengwa alifungua na kuusoma ujumbe husika.Mia

Chanzo:Taarifanews
 
Aaaalaaa... Kumbe, unajua kuanzia juzi naona jumbe zinakuwa na tick 2 za blue, nikawa najiuliza zina maana gani? Basi nikakosa jibu, asante mkuu Mia..

Kama mimi, tangu juzi najiuliza mbona naona rangi rangi tena....kumbeeeeeeee.....
 
Mi mwenyewe jana nomeona hii aisee nikawa hata sielewi maana yake nikatamani niwaulize nliokuwa nachat nao nikaamua nikapuuzia...kumbe
 
mark zugerberg anaendelea kuboresha
 
Hata isomwe hadi iwe nyeusi... mwendo ni uleule tu... "msg sijapata" hahahaaaaa
 
Back
Top Bottom