Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Uzi mzuri Sana!!

Hasa kwa Waha wa Kigoma.... Ushamba mwingi sana
Thubutu kuna muha katoa 1M kariakoo kajaza vyombo kwenye Fuso kaondoka,
Mwenye duka ndo anaanza kupaniki,mzigo umeshaondoka
 
Wewe ndio washamba wenyewe
China plaza kuna maduka mengi tu yanauza used kama mpya..
Na unaweza pigwa hata humo China plaza

Kwa taarifa yako wenye maduka mengi hapo Kkoo walifungua branch humo China plaza
Unajiona unajua kumbe hujui
Naona yupo sawa
Kariakoo kuna watu kati wengi sana(winga)

Ila China Plaza hawawaruhusu Mawinga
 
Wewe uliuziwa aina simu aina ya Bundy uliyemquote naye aliuziwa simu aina ya Vituz halafu unaniambia nitembee kuliko kukaa kijijini, kama watu mliotembea mnaweza kununua simu aina yq Bundy na Vituz na baadaye mkasema mmeibiwa si bora hata huyo bundi anayeshinda kwenye miti?
ni vijijini tu ndio hakuna machinga, Rais karuhusu hawa jamaa watapakae popote na wao wana Ofisi na magari ya kusambaza bidhaa za aina zozote, nakushangaa wewe hujawahi kupigwa changa la macho, hata kura kina Lissu wamekubali changa la macho sembuse CDM wametulia ndio maana nikasema karibu Kkoo Bundy wapo, ingawa na mm sikuitumia nachangamsha jukwaa bado nina kitochi x-tigi
 
Ina maana ni sawa na kinachoendelea kule gerezani?..maana stori tunazopata ni kuwa unaibiwa kifaa cha gari alafu unaenda kukinunua kule na maisha yanaendelea kama kawaida tu.
Au pale mnadani jirani tu na kituo cha msimbazi
 
Tahadhari na wizi huu. Aina za simu ambazo wanaziuza hata hazieleweki. Kuna simu zinaitwa VITU na K-mouse. Wanawatumia mabinti kufanya uhalifu huo. Ukinasa tu umeumia. Bei zao ni shilingi 250,000 lakini huwa zinapoa kwa makubaliano. Wanadanganya kwamba wanafanya promotion na pia wanakuahidi kupata zawadi ya T-Shirt. Utaambiwa uchague kikaratasi ambacho kimeandikwa aina ya zawadi utakayopewa. Nilinasa kwa zile aina ya VITU lakini walivyorudi na K-mouse niligoogle na kugundua nini nilikuwa kinaendelea. Wanapendelea kukaa maeneo yaliyo karibu na benki na wapo tayari kukusubiri utoe fedha ya malipo. Pia wanakubali malipo ya fedha kwa njia ya mitandao. Tahadhari kabla ya hatari.
Ni kweli kabisa hawa mabint hata ukiwakatalia bado wanakufuata nyuma kwa maneno mazuri sasa wenzetu wanatubishia naona hii biashara ni vijijini tu haipo tupo hapa kuhabarishana dunia inavyoenda sio mtu aingizwe mjini wakati JF ipo
cc @Majaribu2013
 
Ni kweli kabisa hawa mabint hata ukiwakatalia bado wanakufuata nyuma kwa maneno mazuri sasa wenzetu wanatubishia naona hii biashara ni vijijini tu haipo
tupo hapa kuhabarishana dunia inavyoenda sio mtu aingizwe mjini wakati JF ipo
Kuna siku nimeona wamepaki pale external wapo na kipaza sauti na Noah au siyo hao?!
 
Umakini ulio utumia ukajua ni simu fake ulishwandaje kutumia umakin huohuo hapohapo dukani ulipo inunua kabla hujaondoka? Au huwa hawaruhusu kukagua?
 
Naona yupo sawa
Kariakoo kuna watu krrrrrati wengi sana(winga)

Ila China Plaza hawawaruhusu Mawinga
Huyu anazingua yeye anaenda kununua simu chini ya mwamvuli anasema kariakoo mbaya hata akienda dubai atapigwa tu maana anapenda rahisi
 
Dawa ni kudeal na huyo tapeli,namfuatilia mpka anapoishi halafu badae atawapa majibu matapeli wenzake hakuna kwenda police
 
Hivyo ndio nimesema tumezoea tu kwenda polisi na mashtaka ya kipuuzi kama haya ndio maana hawajishughulishi mpaka ulete vielelezo

Muda umepita sana bado mna akili ya kizamani, Kama huna ushahidi kuwa hiyo ni simu feki, unapoteza muda wa polisi

Na si kazi ya polisi kuchunguza hiyo simu kuwa ni feki. Ni mamlaka ya viwango tu ndio kazi yao. Polisi wanahusika only kwenye hela za bandia tu.

Mpaka TBS wathibitishe kuwa hilo duka linauza simu feki ndio watahusika. hii ndivyo ilivyo hata Uk, US, Europe popote.

Na Tbs hahusiki na simu feki, ni FCC bro (fair competition commission)
 
Hapo lazima pawepo na ushirika Kati ya maduka hayo na baadhi ya watendaji wa kutatua kero za wananchi
 
Nina miaka 13 tokea mpaka android imenikuta kwenye idara ya vitu vya mawasiliano.usipende kuaminisha watu kupaka mavi hapo kariakoo,taaluma yangu kubwa ni mawasiliano.
Karakoo ni sehemu ya vijana na wafanya biashara wanao fanya biashara kwa mitaji midogo,pili vitu vingi unavoviona ni wewe ukitaka copy unapata kwa kuwa wafanya biashara wa mambo haya wanataalamu kuendana na mtu hana taka nini.!
Simu kutoka south africa,dubai,hong kong,walio kuja nazo toka nje ya nchi na kuwapa watu wauze ufikisha pale kwa kuwa ni rahisi kuhuzika haraka.
Tokea nimekaa kariakoo nimeweza kumili iphone 2g,3g,3gs,4,4s,5,5s,6,6s,7,7s,8,8s,x,xr,xs max na kwa bahati na simu nyingi ambazo mtu itamchukua mda kupata kwa kuwa maduka makubwa ni bei.
Maduka yapo mazuri watu wapo wazuri ni wewe tu
Na kariakoo ndio imezalisha vijana mnao waona wameenda pembeni sijui mwenge,sijui wapi kuanzisha viduka hata posta lakini bizaa wanatoa huku kariakoo
mkuu umeongea vizuri vipi kuhusu tuhuma za mtoa uzi unalizungumziaje hilo?
 
Kuna raia wana akili kuliko hata maaskari tuliowapa dhamana ya kutulinda sisi pamoja na mali zao.
 
Kuna siku nimeona wamepaki pale external wapo na kipaza sauti na Noah au siyo hao?!
Ndio hao Mkuu kuna wavulana km watatu na wasichana watatu mmoja wa hao mabint anabakia kwenye siti ya mbele ya abiria, na dereva wao wanajiunga kupromote hizo bidhaa.

sasa hujui km utauziwa simu ya bundi ila unaletewa vikaratasi ujaribu bahati yako, na kucheza ni bure au buku, unaweza ambulia vocha au betri lkn nyingi ni simu, ukishinda huwezi jua ila wanakupeleka kwenye Noah unasikia huyu Bingwa kashinda nipe simu nimuelekeze .....................
ukigutuka unakuta unapewa Warrant na mawasiliano yao kabisa TRACE .....Co Ltd Kariakoo sasa nenda kadai fidia hakuna mtu. wewe waache iko siku wataingia tena choo sio chao, maana siku hiyo walikimbia
 
Ndio hao Mkuu kuna wavulana km watatu na wasichana watatu mmoja wa hao mabint anabakia kwenye siti ya mbele ya abiria, na dereva wao wanajiunga kupromote hizo bidhaa.
sasa hujui km utauziwa simu ya bundi ila unaletewa vikaratasi ujaribu bahati yako, na kucheza ni bure au buku, unaweza ambulia vocha au betri lkn nyingi ni simu, ukishinda huwezi jua ila wanakupeleka kwenye Noah unasikia huyu Bingwa kashinda nipe simu nimuelekeze .....................
ukigutuka unakuta unapewa Warrant na mawasiliano yao kabisa TRACE .....Co Ltd Kariakoo sasa nenda kadai fidia hakuna mtu. wewe waache iko siku wataingia tena choo sio chao, maana siku hiyo walikimbia
Basi itakuwa wamepiga watu wengi sana
 
Back
Top Bottom