Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Unapoenda kwenye maduka ya simu ya Kariakoo hasa Yale ya mtaa wa Msimbazi. Yanaotazama shule za Uhuru. Jambo la kuzingatia ni kuwa kuna maduka mengi hapo yamejaa wezi na matapeli. Ambao wanatumia loophole za kisheria. Kuibia watu bila woga na polisi hawawezi kukusaidia

Nimeandika hili baada ya kupata experience na nilipofika polisi msimbazi. Ndio nikashangaa sheria zilivyo na why, Hawa wezi wa Kariakoo wanatamba mchana kweupe.

Iko namna hii asilimia 80 ya viduka vinavyouza simu hapo kwanza kabisa. Hawatumii mashine za efd. Wana vitabu vyao vya risiti za kienyeji. Na TRA Kariakoo wanawajua wote. Na jamaa bado wanadunda..

Sasa ikitokea wamekuuzia simu hapo. Mfano unaweza uziwa Samsung ambayo ndani pengine ni Itel au Tecno. Ukistuka Tu mgogoro unaanzia kwa risiti Kiduka kimoja na kina vitabu vya risiti kibao vya majina tofauti

Ikitokea umewabana wakupe risiti ya efd. Ukiwafikisha polisi na kesi ya simu feki. Kwa mujibu wa sheria polisi hawana mamlaka ya kusema simu hii ni feki. Unatakiwa uende Ubungo TBS ndio waseme hii simu ni feki. Otherwise kesi ya kukupa risiti ambazo sio za TRA inabidi uende TRA. Na sio polisi

Sasa hizi loophole za mara nenda TBS mara nenda TRA ndo zinazowafanya. Wajiachie mchana kweupe..
TRA wanacheza nao polisi Msimbazi wanacheza nao..

Matokeo yake watu wengi mno wa ndani na nje wanapigwa maeneo hayo kila siku

Utapeli mkubwa unaofanyika hapo ni huu
1. Simu used kuuziwa kama mpya.

2. Simu brand tofauti Kwa cover ndani mashine simu ingine
Mfano Samsung kwa nje mashine ndani TECNO unaweza kukuta nje LG au Sony Ndani Itel.

3. Simu kwenye cover ni 4g ndani ni 3g au 2g.

4. Utapeli wa kuambiwa tutakurudishia hela yako ukiwastukia.. halafu inaanza njoo kesho njoo kesho...


Ukweli watu wengi wanatapeliwa na serikali ni kama haina msaada kabisa

Nimejiuliza why Polisi wasiwe na vitengo maalum vya kutambua vifaa vya electronics? Vitu kama simu ni Ku Google Tu IMEI no
Je polisi hawawezi hadi TBS Ubungo?

Na Why TBS why wasiwe na ofisi Kariakoo? Kariakoo ni asilimia 90 ya simu za Tanzania zinatoka hapo na zinauzwa Tanzania yote. Watu wa mikoani wanakuja kukusanya. Na wafanyabiashara wa nchi jirani pia. Comoros, Zambia, Malawi n.k, Wanakuja Kariakoo kukusanya

Wangapi watakuwa wanaibiwa na hawapati msaada wa polisi au taasisi yoyote?

Sheria zibadilishwe kuwalinda wanunuzi. Polisi wawe na maaafisa wa TRA na TBS, Hasa pale msimbazi Polisi..

Opereshen maalum ifanyike kusafisha Kariakoo na wafanya biashara hawa matapeli
Mimi naweza kufikisha miaka 10 sijaenda Kariakoo
So ...
 
Mnakumbuka K alivyoanza na mkwara pale alipokua naibu waziri?
Funga mageti funguo weka kule. Mkulu akaona labda hili jembe. Duh. Alipoonjeshwa na mdada wa kipare na kujua kupanda ndege bure, akaanza kutongoza kila mrembo aliye kwenye chati.
Sasa hivi hata kwenye malumbano ya baiskeli simuoni.
Ameshajua mtu mwenye pesa si mwenzake
mh ni mpare??? mbona nasikia ni Kisa-lawe bora arudi Iga-Lula na humu yumo
nimecheka sana ulipokumbusha mageti ya Dr Mwaka kufungwa
 
mh ni mpare??? mbona nasikia ni Kisa-lawe bora arudi Iga-Lula na humu yumo
nimecheka sana ulipokumbusha mageti ya Dr Mwaka kufungwa
Yuko mpare pia.
Kama umeoa usiguse mchepuko wa kipare....
 
Nikiwaga kariakooo natembea na ule usemi wa navy seal special force nanukuu"heads down eyes open" kuna wale watoto(washikaji wanafanyaga bisness yao kuita wateja kwa style ya kupiga makofi makutano ya ddc na wanyama hoteL ,nawaaangaliaga nasemaaaaa hiiiiiiiiiiiiiiiiiii "heads down eyes open" tunaishi nao
 
Kuna mengi yanasononesha kwenye hii nchi polisi vituo vyote Tanzania nzima kumejaa rushwa lakini serikali ni kama vile haioni huu mchezo
Mchezo wanauona sana tuu sema hawaathiriki nao directly ingekuwa ni issues za kupata shavu la kisiasa wangekuja fasta.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa, kuna kisa kingine ngoja nikiweke hapa, kuna jamaa mmoja alinunua iphone kwenye duka fulani K/koo pia na risiti kapewa kila kitu sasa ile simu ametumia kitambo tu sasa hivi juzi juzi kapigiwa simu na polisi kuwa anatuhumiwa kwa kununua simu ya wizi.

Jamaa akawauliza ni nani huyo anasema hii ni simu yake polisi hawana cha kusema, sasa kesi imeenda hadi jamaa akawaambia polisi twendenj niwapeleke dukani sasa cha ajabu walivyofika K/koo walikuta lile duka limefungwa jamaa mwenye iPhone akijaribu kumcheki mwenye duka haeleweki sasa kumbe jamaa mwenye iPhone akagundua kuna mchezo mchafu unaendelea kati ya muuza duka na polisi.

Wito wangu kuweni makini sana na hawa wauza simu haka kamchezo sio powa kabisa watu wanalizwa wengi sana.
Ndiyo maana tangia nianze kununua simu Dar sijawahi kununua simu Kariakoo, huwa naendaga maduka ya Posta....
 
"Sheria zibadilishwe kuwalinda wanunuzi. Polisi wawe na maaafisa wa TRA na TBS, Hasa pale msimbazi Polisi..

Opereshen maalum ifanyike kusafisha kkoo na wafanya biashara hawa matapeli"


Nimependa hii conclusion yako ya kibabe sana. Solution ni hiyo tu na si vinginevyo.
Hii inatokea sana kwa nchi za mabeberu, maduak yanavamiwa na polisi na kushirikiana na taasisi za serikali za watimiaji (consumers) lakini ni baada ya uchunguzi wa kina na kesi kibao za malalamiko kutoka kwa vyama vya consumers
Na hapo ndio Polisi wana act kwa ushahidi huo

Sidhani hata hiki chama cha kuwalinda walaji (consumer protection) kinafanya kazi, hiki ndo kinatakiwa kifuatilie issue kama hizo kuanzia ubora wa bidhaa zinazouzwa madukani na kushughulikia malalamiko kama hayo.
Wazugaji hao wakibongo
Lakini hii process ya kushataki ni ndefu mno hata kwenye nchi za mabebberu
Hebu angali hapo chini, hii kwa UK
Na hamna kipengele kinasema nenda kashtaki Polisi
Na unaambiwa usiwe zwazwa unaenda macho juu vya mteremko
NA UNAAMBIWA KAMA UNAPENDA KUNUNUA VYA MTEREMKO, UNAVUNJA SHERIA ZA NCHI


 
Hivyo ndio nimesema tumezoea tu kwenda polisi na mashtaka ya kipuuzi kama haya ndio maana hawajishughulishi mpaka ulete vielelezo

Muda umepita sana bado mna akili ya kizamani, Kama huna ushahidi kuwa hiyo ni simu feki, unapoteza muda wa polisi

Na si kazi ya polisi kuchunguza hiyo simu kuwa ni feki. Ni mamlaka ya viwango tu ndio kazi yao. Polisi wanahusika only kwenye hela za bandia tu.

Mpaka TBS wathibitishe kuwa hilo duka linauza simu feki ndio watahusika. hii ndivyo ilivyo hata Uk, US, Europe ptopote.
Shida elimu haitolewi na mamlaka mbalimbali juu ya maswala yanayozihusu na namna ya kuanzia pale shida inapotokea.
 
kwangu mie wezi wenye leseni ya kuibia wananchi hapa tz ni WABUNGE wetu woote kwa ujumla wao!
 
Nimenunua Samsung Galaxy S8+, nje ya box imeandikwa 64GB Duos ila nilipoiwasha simu na kuanza kuitumia nikakuta ni128GB Single Line 😏🤔🙈
Duh ila mkuu bana simu ya bei kubwa hivyo unaenda kununua Kkoo aisee🤔,pole na hukujaribu kuiwasha hapo hapo dukani? Vipi pia hawakukubadilishia ulivorudi??
 
TsRA Walipofungia simu zote feki kumbe makufuli yote yaliisha.
Simu feki zipo zimezagaa na TsRA haina macho wala meno kuzidhibiti hzo simu.
 
hv unachukuaje smu bila kuitest? yaan kabis unaona hz ni font za tecno afu we unaamini hii ni samsung...
..
 
Taratibu mjukuu, niko Darkabla ya uhuru
Sasa km ww ni kibabu... kariakoo unatafuta nn wkt wapo watoto na wajukuu wa kuwatuma??hapo nimekuelewa...maana napishanaga na vibabu town,ujaiuliza mjn wanafanya nn?
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa, kuna kisa kingine ngoja nikiweke hapa, kuna jamaa mmoja alinunua iphone kwenye duka fulani K/koo pia na risiti kapewa kila kitu sasa ile simu ametumia kitambo tu sasa hivi juzi juzi kapigiwa simu na polisi kuwa anatuhumiwa kwa kununua simu ya wizi.

Jamaa akawauliza ni nani huyo anasema hii ni simu yake polisi hawana cha kusema, sasa kesi imeenda hadi jamaa akawaambia polisi twendenj niwapeleke dukani sasa cha ajabu walivyofika K/koo walikuta lile duka limefungwa jamaa mwenye iPhone akijaribu kumcheki mwenye duka haeleweki sasa kumbe jamaa mwenye iPhone akagundua kuna mchezo mchafu unaendelea kati ya muuza duka na polisi.

Wito wangu kuweni makini sana na hawa wauza simu haka kamchezo sio powa kabisa watu wanalizwa wengi sana.
Sad
 
Back
Top Bottom