Jamani na mimi nilishapigwa hapohapo maduka yanayotizamana na Shule ya Uhuru nikawaonesha risiti ya Jina la Duka wakanikatalia kabisa.
Hawa wauzaji wao wana simu aina nyingi sasa mm nikaletewa aina mojawapo inaitwa Bundy kwa manjonjo na promotion ya kupewa fulana na Betri wakadai niwape 250,000/
Wanapenda kukaa kwenye Noah kwenye choo cha kulipia kule Samora baada ya Clock Tower tumebishana wakashuka hadi 175,000/ fulana na Betri wananinyang'anya eti wanatangazia.
Jamani nusu saa hamna kitu simu haina Network, kwa vile nina risiti iliyoelekeza kuwa wapo Plot na Block mitaa ya Uhuru nikaipata, Boss akaniruka nikajua nimepigwa.
Baada ya mwezi nikawaona tena wapo Dodoma mitaa ya Nyerere square, wakanivaa na uongo wao basi kwa hasira nikawakoromea na kuwaonesha kimeo chao cha Bundy tena imekufa kabisa,
wakaniomba msamaha wakalala kona na mm nikawaambia bora wafungashe naifuata risiti nikawakamate.
Nashangaa mpaka leo bado wanaziuza tu na hawakamatwi na Noah yao ya kijivu T ??? CBV
nitaomba ruksa yenu nikipata picha niwaweke hadharani hapa
Jamani simu tununue maduka ambayo unaweza hata kuirudisha ukabadilishiwa