Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Unapoenda kwenye maduka ya simu ya Kariakoo hasa Yale ya mtaa wa Msimbazi. Yanaotazama shule za Uhuru. Jambo la kuzingatia ni kuwa kuna maduka mengi hapo yamejaa wezi na matapeli. Ambao wanatumia loophole za kisheria. Kuibia watu bila woga na polisi hawawezi kukusaidia

Nimeandika hili baada ya kupata experience na nilipofika polisi msimbazi. Ndio nikashangaa sheria zilivyo na why, Hawa wezi wa Kariakoo wanatamba mchana kweupe.

Iko namna hii asilimia 80 ya viduka vinavyouza simu hapo kwanza kabisa. Hawatumii mashine za efd. Wana vitabu vyao vya risiti za kienyeji. Na TRA Kariakoo wanawajua wote. Na jamaa bado wanadunda..

Sasa ikitokea wamekuuzia simu hapo. Mfano unaweza uziwa Samsung ambayo ndani pengine ni Itel au Tecno. Ukistuka Tu mgogoro unaanzia kwa risiti Kiduka kimoja na kina vitabu vya risiti kibao vya majina tofauti

Ikitokea umewabana wakupe risiti ya efd. Ukiwafikisha polisi na kesi ya simu feki. Kwa mujibu wa sheria polisi hawana mamlaka ya kusema simu hii ni feki. Unatakiwa uende Ubungo TBS ndio waseme hii simu ni feki. Otherwise kesi ya kukupa risiti ambazo sio za TRA inabidi uende TRA. Na sio polisi

Sasa hizi loophole za mara nenda TBS mara nenda TRA ndo zinazowafanya. Wajiachie mchana kweupe..
TRA wanacheza nao polisi Msimbazi wanacheza nao..

Matokeo yake watu wengi mno wa ndani na nje wanapigwa maeneo hayo kila siku

Utapeli mkubwa unaofanyika hapo ni huu
1. Simu used kuuziwa kama mpya.

2. Simu brand tofauti Kwa cover ndani mashine simu ingine
Mfano Samsung kwa nje mashine ndani TECNO unaweza kukuta nje LG au Sony Ndani Itel.

3. Simu kwenye cover ni 4g ndani ni 3g au 2g.

4. Utapeli wa kuambiwa tutakurudishia hela yako ukiwastukia.. halafu inaanza njoo kesho njoo kesho...


Ukweli watu wengi wanatapeliwa na serikali ni kama haina msaada kabisa

Nimejiuliza why Polisi wasiwe na vitengo maalum vya kutambua vifaa vya electronics? Vitu kama simu ni Ku Google Tu IMEI no
Je polisi hawawezi hadi TBS Ubungo?

Na Why TBS why wasiwe na ofisi Kariakoo? Kariakoo ni asilimia 90 ya simu za Tanzania zinatoka hapo na zinauzwa Tanzania yote. Watu wa mikoani wanakuja kukusanya. Na wafanyabiashara wa nchi jirani pia. Comoros, Zambia, Malawi n.k, Wanakuja Kariakoo kukusanya

Wangapi watakuwa wanaibiwa na hawapati msaada wa polisi au taasisi yoyote?

Sheria zibadilishwe kuwalinda wanunuzi. Polisi wawe na maaafisa wa TRA na TBS, Hasa pale msimbazi Polisi..

Opereshen maalum ifanyike kusafisha Kariakoo na wafanya biashara hawa matapeli
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa, kuna kisa kingine ngoja nikiweke hapa, kuna jamaa mmoja alinunua iphone kwenye duka fulani K/koo pia na risiti kapewa kila kitu sasa ile simu ametumia kitambo tu sasa hivi juzi juzi kapigiwa simu na polisi kuwa anatuhumiwa kwa kununua simu ya wizi.

Jamaa akawauliza ni nani huyo anasema hii ni simu yake polisi hawana cha kusema, sasa kesi imeenda hadi jamaa akawaambia polisi twendenj niwapeleke dukani sasa cha ajabu walivyofika K/koo walikuta lile duka limefungwa jamaa mwenye iPhone akijaribu kumcheki mwenye duka haeleweki sasa kumbe jamaa mwenye iPhone akagundua kuna mchezo mchafu unaendelea kati ya muuza duka na polisi.

Wito wangu kuweni makini sana na hawa wauza simu haka kamchezo sio powa kabisa watu wanalizwa wengi sana.
 
Duuh nje Samsung ndani Itel ??aki ya nani dunia hii🙄🙄 ila kkoo mimi naonaga wenye maduka wote wajanja janja tu sasa sijui tuwe tunanunua wapi vitu.
Au unataka Simu ya 4g kumbe ni 3g
Unakuja kugundua ushafika home
Ujue umeliwa hapo..wataaanza kukuzungusha
Kusema ubadili ...njoo kesho subiri mzigo unakuja..ukienda polisi ndo kabisa wanakushangaa..
 
Kwa brand kama LG au Sony wakikuwekea
Ndani itel huwezi jua kama sio mjanja

Ni wezi sana sana hapo kkoo na polisi wanajua kila kitu
Jamani na watu wengi shopping zetu ni huko, hadi watu wa nchi jirani ; itakua tuna mavitu feki kibao na hatujui dah. Ina siyo fair mwambie mnunuzi this is fake na price yake iko pungufu ama og na price iko juu achague mwenyewe kulingana na mfuko wake🙄🤔
 
Jamani na mimi nilishapigwa hapohapo maduka yanayotizamana na Shule ya Uhuru nikawaonesha risiti ya Jina la Duka wakanikatalia kabisa.

Hawa wauzaji wao wana simu aina nyingi sasa mm nikaletewa aina mojawapo inaitwa Bundy kwa manjonjo na promotion ya kupewa fulana na Betri wakadai niwape 250,000/

Wanapenda kukaa kwenye Noah kwenye choo cha kulipia kule Samora baada ya Clock Tower tumebishana wakashuka hadi 175,000/ fulana na Betri wananinyang'anya eti wanatangazia.
Jamani nusu saa hamna kitu simu haina Network, kwa vile nina risiti iliyoelekeza kuwa wapo Plot na Block mitaa ya Uhuru nikaipata, Boss akaniruka nikajua nimepigwa.

Baada ya mwezi nikawaona tena wapo Dodoma mitaa ya Nyerere square, wakanivaa na uongo wao basi kwa hasira nikawakoromea na kuwaonesha kimeo chao cha Bundy tena imekufa kabisa,
wakaniomba msamaha wakalala kona na mm nikawaambia bora wafungashe naifuata risiti nikawakamate.

Nashangaa mpaka leo bado wanaziuza tu na hawakamatwi na Noah yao ya kijivu T ??? CBV
nitaomba ruksa yenu nikipata picha niwaweke hadharani hapa
Jamani simu tununue maduka ambayo unaweza hata kuirudisha ukabadilishiwa
 
Back
Top Bottom